TIGO YAMWAGA SIMU JANJA ZA TEKNO R6 KWA WASHINDI WA DROO YA NYAKANYAKA BONUS

April 06, 2018


 Mtaalam wa huduma na bidhaa wa mtandao wa tigo tanzania baraka hamza akiongea na waandishi wa habari mkoani morogoro wakati wa hafla ya kukabidhi simu aina za tekno r6 kwa washindi wa promosheni ya tigo nyakanyaka bonas, ambapo wateja 672 wa tigo wamejishindia simu hizo zenye uwezo wa 4g.


Mmoja wa washindi wa nyakanyaka bonus mwl justina Mathew jaka akikabidhiwa zawadi ya simu na meneja wa tigo kanda ya kati-pwani patricia sempinge katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya tigo huduma kwa wateja mkoani morogoro. Wateja 672 wa tigo wamejishindia simu za tecno r6 zenye uwezo wa 4g.


Meneja Mauzo Tigo Mkoa Wa Morogoro Abbas Abdraman Akikabidhi Zawadi Ya Simu Ya Tecno R6 Kwa Samson Baada Ya Kuwa Mojawapo Ya Washindi 672 Katika Promosheni Ya Tigo Nyaka Nyaka Bonas.

Mojawapo Ya Washindi 672 Wa Droo Ya Nyakanyaka Bonas Farida Yussuph(Katikati) Akipokea Zawadi Ya Simu Aina Ya Tecno R6 Kutoka Kwa Meneja Wa Tigo Kanda Ya Kati-Pwani Patricia Sempinge(Kushoto) Wakati Wa Hafla Iliyofanyika Katika Ofisi Ya Tigo Huduma Kwa Wateja Mkoani Morogoro.

Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza (Kulia) Na Abbas Abdraman Meneja Mauzo Tigo Mkoa Wa Morogoro (Kushoto) Wakikabidhi Zawadi Ya Simu Tecno R6 Kwa Mojawapo Ya Washindi 672 Wa Promotion Ya Tigo Nyakanyaka Petrocia Makongera (Katikati) Katika Hafla Iliyofanyika Katika Ofisi Ya Tigo Huduma Kwa Wateja Mkoani Morogoro


Meneja Wa Tigo Kanda Ya Kati-Pwani Patricia Sempinge Pamoja Na Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza (Kulia) Akikabidhi Zawadi Ya Simu Ya Tecno R6 Kwa Mojawapo Ya Washindi Wa Promosheni Ya Nyakanyaka Bonasi, Japhet Mbonea Mkoani Morogoro.

Mkazi Wa Morogoro Henry Msemwa Akipokea Zawadi Ya Simu Aina Ya Tekno R6 Kutoka Kwa Mtaalam Wa Huduma Na Bidhaa Wa Mtandao Wa Tigo Tanzania Baraka Hamza Mara Baada Ya Kuwa Moja Wa Washindi Wa Droo Ya Nyakanyaka Bonas


Baadhi ya washindi wa promotion ya nyakanyaka bonus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tigo katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya tigo huduma kwa wateja mkoani morogoro. Wateja 672 wa tigo wamejishindia simu za tecno r6 zenye uwezo wa 4g.

INUKA KUTUMIA MILIONI 40 KUTOA ELIMU YA MAGONJWA YA KIFUA KIKUU KWENYE MIKOA YA KILIMANJARO NA TANGA

April 06, 2018
MTANDAO wa Maendeleo ya Wanawake,Watoto na Elimu nchini (INUKA) umeanza kutoa elimu ya magonjwa ya kifua kikuu,saratani ya matiti na tezi dume kwa wakazi wa vijijini na shule kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Mtandao huo,David Msuya wakati akizungumza na Tanga Raha Blog ambapo alisema wametenga sh. milioni 40 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwenye kuendesha mafunzo ya magonjwa hayo kwenye vijiji vilivyopo wilayani nane za mikoa hiyo miwili.

Msuya alisema kuwa lengo la kuendesha mafunzo hayo kwa wakazi wa vijijini ni kutokana na ukweli kwamba jamii inayoishi katika maeneohayo ni vigumu kufikiwa na mafunzo mbalimbali nahivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa kupata elimu kama hizo.

Alisema kuwa jamii inayoishi vijijini itanufaika na elimu hiyo kwa kujengewa uwezo wa uelewa wa maambukizi ya magonjwa hayo na kuchukua tahadhali ya kujikinga nayo na hivyo kupunguza ongezeko la kifua kikuu,saratani ya matiti na tezi dume.

Mratibu huyo alisema kuwa lengo la kuendesha mafunzo hayo kwa jamii za vijijini na wanafunzi wa sekondari ni kuinusuru jamii hiyo ambayo ambayo imekuwa na
tatizo la elimu ya magonjwa hayo kutokana na kutofikiwa na wataalamu kwa urahisi na kwa wakati.

Hata hivyo alisema pamoja na serikali kujikita kwenye uhamasishaji wa masuala mbalimbali yanayohusu afya kupitia vyombo vya habari lakini jamii ya vijijini imekuwa vigumu kufikiwa kutokana na mazingira ya ufikaji wa taarifa hizo.

Msuya alizitaja Wilaya hizo ambazo zitanufaika na mafunzo hayo kuwa ni Handeni,Kilindi, Mkinga na Pangani kwa upande wa Mkoa wa Tanga naWilaya nyingine nne za Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa upande mwingine mratibu huyo alichukua nafasi hiyo kuwaomba wahisani kutoka mashirika na taasisi mbalimbali kusaidia gharama za utoaji wa elimu hiyo na kwamba kufanya hivyo licha ya kuisaidia serikali lakini pia watakuwa wameinusuru jamii na tatizo la kuathirika kwa magonjwahayo.

“UDHAMINI WA LIGI YA KIKAPU MKOA TANGA WAIPASUA KICHWA TRBA

April 06, 2018
CHAMA cha Mpira wa Kikapu Mkoani Tanga (TRBA) kimeanza kusaka wadhamini ambao watafanikisha michuano ya ligi ya mkoa itakayoanza hivi karibuni Jijini Tanga ikishiriki timu kutoka wilaya mbalimbali.

Hayo yalibainishwa na Katibu Msaidizi wa Chama hicho, Patrick Semindu wakati akizungumza na Tanga Raha Blog ambapo alisema wameamua kufanya hivyo mapema ili kuweza kufanikisha malengo yao ya kuchezwa mashindano hayo.

Alisema pia kutokana na kuwepo kwa changamoto kamati ya ufundi na utendaji itakutana mwishoni mwa wiki hii kuweza kuweka mipango itakayosaidia kupatikana udhamini ambao utasaidia kuendesha mashindano hayo.

“Kikao hicho kitakuwa na agenda mbalimbali ikiwemo kuidhinisha tarehe ya kuanza mashindano hayo na namna yatakayoendeshwa lakini mpaka sasa hakuna mdhamini yoyote aliyekwisha kujitokeza kama tukikosa tutaendesha ligi kupitia ada za timu shiriki “Alisema

Hata hivyo alisema lengo la kufanya hivyo iwapo wadhamini watakosekana ni kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa namna yoyote ile na bingwa wa mkoa aweze kupatikana.

TAFITI ZINAONESHA NI MUHIMU KUWEKEZA KATIKA UFUNDI STADI KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA-DKT MMARI

April 06, 2018

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya REPOA Dk.Donald Mmari amesema kuna sababu ya kuwekeza zaidi katika kutoa elimu ya ufundi stadi nchini kwa lengo la kupika watalaamu wa fani mbalimbali ambao watashiriki kufanya kazi zenye tija na kuleta ushindani kimataifa.

Dk.Mmari ametoa kauli hiyo wakati akielezea changamoto ambazo wamezibaini kwenye warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na REPOA kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Amesema wadau walioko kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina mambo mengi kwa maslahi mapana ya nchi yetu na katika mjadala huo wamebaini bado kunachangamoto ambazo ni vema zikafanyiwa kazi ili kufikia malengo ya ujenzi wa viwanda na kuwa na bidhaa zenye ushindani katika soko la kimataifa.

Ametaja moja ya changamoto ambao wameijadili ni uhaba wa wataalam katika nyanja mbalimbali na hiyo inatokana na kutowekeza zaidi kwenye elimu ya Ufundi stadi ambayo inaandaa vijana kujiajiri na kuwa watalaamu wazuri."Tumekubaliana na kutoa mapendekezo kuwa ili tuingie kwenye ushindani ipo haja ya kuhakikisha watanzania wanaalindaliwa katika elimu na ujuzi unaohusu masuala ya ufundi.

"Ni vema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta za umma na binafsi kuwekeza zaidi katika kuwajengea uwezo wananchi ambao utawafanya washiriki kikamilifu katika kufanya kazi kwenye viwanda,"amesema Dk.Mmari.Amefafanua nchi nyingi ambazo zimeendelea na zenye uwezo wa kuhimili ushindani kwenye soko la kimataifa msingi wake mkubwa wamewekeza katika elimu, ujuzi na utalaam.

"Hivyo ili kushindana nao lazima Tanzania nayo ikawekeza katika elimu, ujuzi na utaalamu kwa kuandaaa vijana watakaokuwa na ujuzi.Tumekubaliana yale ambayo tumeyaona kama changamato tumeweka na mapendekezo yetu na tumekubaliana Serikali iyapate na ikiwezekana kuyafanyia kazi,"amesem Dk.Mmari.

Amesisitiza ni vema nchi ikawekeza zaidi kwenye kujenga vyuo vya VETA ambavyo jukumu litakuwa kuandaa watalaam na kwamba kuna wakati iliingia kasumba ya kuwa na vyuo vikuu vingi ili wanaohitimu wawe na Shahada lakini elimu hiyo haina ujuzi na matokeo yake kunaibuka changamoto ya uhaba wa watalaamu.

Kwa upande wa Mlkuregenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural  Association (TAHA)  Jacqueline Mkindi amesema pamoja na kujadili mambo mengi kwenye warsha hiyo wamegundua ujuzi kwenye maeneo ya viwandani bado tatizo kubwa.Amesema ipo haja ya kuhakikisha wanaandaliwa watalaamu wenye ujuzi unaokubalika kimataifa kwa lengo la kuwa na bidhaa zenye ushindani na kufafanua jukumu ambalo TAHA wanafanya ni kuwaandaa vijana kujiajiri kwa kuwapatia mafunzo yenye ujuzi.

"TAHA tumebaini kuna tatizo la uhaba wa watalaam, kwa mfano kwetu inapofika kipindi cha kuchanganya mbegu maabara lazima utakuta wanaofanya kazi hiyo ni watalaamu kutoka nje."Sababu kubwa ni kwamba kwetu hawapo.Hivyo wakati nchi inajipanga kwenye ujenzi wa viwanda ni vema ikaenda sambamba na kuandaa watalaam ili kuondoa changamoto iliyopo,"amesema Mkindi.

Ameongeza cha msingi ni kuweka uratibu mzuri utakaosaidia vijana kuwajengea uwezo utakaosadia kuondoa changamoto ya uhaba wa watalaamu katika fani mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini, REPOA, Dk. Donald Mmari akizungumza wakati wa kufunga Warsha ya siku mbili kwa watafiti iliyoandaliwa na tasisi yake juu ya kwanini ushindani ni muhimu kuelekea uchumi wa Viwanda.

Mlkuregenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Asspciation (TAHA) Jacqueline Mkindi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo walipjadili nafasi ya kilimo katika uchumi wa Viwanda.

Mratibu na Mtafiti wa Warsha hiyo kutoka Repoa, Dk. Blandina Kilama akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo wakati alipokuwa akiongoza meza ya majadiliano.

Mtafiti Kutoka Repoa, Dk. Lucas Katera akizungumza jambo kaatika mjadala wa Nishati kuelekea Uchumi wa Viwanda wakati wa Warsha ya siku Mbili ya Watafiti iliyoandaliwa na Repoa.

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya siku mbili kwa watafiti juu ya kwanini ushindani ni Muhimu kuelekea Uchumi wa Viwanda wakifatilia mada kwa makini.
WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI WATAKIWA KUJITATHIMINI

WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI WATAKIWA KUJITATHIMINI

April 06, 2018


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lililofanyika mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), akizungumza na wajumbe wa baraza hilo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya sekta hiyo katika kikao cha baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora akiwasilisha rasimu ya bajeti na mpango wa utekelezaji wa sekta hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika mkoani Morogoro.

Katibu wa baraza la wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Vendeline Massawe, akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa baraza kwa kumchagua kushika nafasi hiyo mara baada ya katibu wa zamani kupata uhamisho, Mkoani Morogoro.

Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), pamoja na viongozi wengine wakishiriki kuimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha baraza la wafanyakazi, Mkoani Morogoro.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi mara baada ya kufungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika Mkoani Morogoro.

…………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi kujitathimini yale waliyoazimia kutekeleza kwa mwaka wa Fedha 2017/18 kama yamefikia lengo ili kuweza kusaidia kuboresha utendaji na kutafutia ufumbuzi masuala ambayo yanakwamisha ufanisi wa kazi na kuwezesha mazingira wezeshi kwa wafanyakazi.

Prof. Mbarawa amesema hayo mkoani Morogoro, wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi ambapo pamoja na mambo mengime amesisitiza umuhimu wa baraza hilo katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi wenye tija, staha na upendo.

“Ni matarajio yangu kuwa kila mjumbe kwa nafasi aliyonayo katika baraza hili atatumia fursa hii kutoa michango ya mawazo ili iweze kuwa mwongozo mzuri wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, ametoa wito kwa wajumbe hao kuhakikisha kuwa Wizara inashiriki kikamilifu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwajengea watanzania miundombinu bora na imara ili kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda na hivyo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya kuifanya nchi yetu iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Profesa Mbarawa, amewataka wajumbe hao kujadili kwa kina Rasimu ya Bajeti na Mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Prof. Mbarawa, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi ya Wizara, Idara na Taasisi za Umma kuhusu usimamizi wa rasilimali watu, utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi na weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma.

Ameongeza majukumu mengine kuwa ni kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi; kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi; maslahi ya Wanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi.
ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKOA WA KASKAZINI PEMBA

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKOA WA KASKAZINI PEMBA

April 06, 2018


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mjasiriamali wa kazi za sanaa za mikono katika ufukwe wa Nungwi Ndugu Rabinson Mungule wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua miradi ya CCM ikiwa sehemu ya kuhamasisha Chama Cha Mapinduzi kujitegemea kwa kutumia rasilimali zake katika mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia urembo wa wanawake unaouzwa katika fukwe za Nungwi Ndugu Rabinson Mungule wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua miradi ya CCM ikiwa sehemu ya kuhamasisha Chama Cha Mapinduzi kujitegemea kwa kutumia rasilimali zake katika mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Zamani Mambo ya Ndani ya Nchi, Ali Ameir Mohammed, alipomtembelea nyumbani kwake, Kichaviani, Jimbo la Donge, Makamu wa Rais alikuwa kwenye ziara katika mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa sehemu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amesikitishwa sana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika machimbo ya mchanga Donge.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara Visiwani Unguja na leo alikuwa na ziara katika mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Rais amesema hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa mazingira yasiendelee kuharibiwa.

Makamu wa Rais pia amewataka Viongozi wote wa CCM kuhakikisha kuwa Chama kinajitegemea kwenye maeneo yao, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kukagua shughuli za kiuchumi za CCM katika ufukwe wa Nungwi ikiwa sehemu ya ziara yake aliyoifanya kwenye mkoa wa Kaskazini Unguja.

Makamu wa Rais pia alifungua ofisi mbili za CCM moja ikiwa ya jimbo la Donge na nyingine ikiwa Ofisi ya CCM mkoa wa Kaskazini ambapo inahistoria ya kipekee kutokana na kuwekwa jiwe la msingi mwaka 1986 na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA KILA KIJIJI KUTENGA ENEO LA UHIFADHI WA MISITU, ATOA SIKU 7 KWA TFS KUWASILISHA MPANGO WA UVUNAJI

April 06, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.


                Na Hamza Temba, WMU, Kishapu, Shinyanga


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga maeneo katika kila kijiji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ikiwa ni pamoja na vijiji hivyo kuunda kanuni na taratibu zao wenyewe za kusimamia maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika mkoani humo kuanzia Aprili 03 mwaka huu.

Katika kufanikisha zoezi hilo ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuchagua mikoa 10 ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo ikiwemo mikoa ya Shinyanga na Tabora ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu.

Ameugiza pia we uongozi huo wa TFS kuweka mpango wa uhifadhi wa misitu ya asili katika maeneo hayo kwa kushirikiana na vijiji kupanga maeneo yanayostahili kuhifadhiwa sambamba na kuwapa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa maeneo hayo.

Wakati huo huo Dk. Kigwangalla ametoa siku saba kwa uongozi huo wa Wakala wa Huduma za Misitu kuwasilisha kwake mpango wa tathmini ya uvunaji wa mazao ya misitu wa nchi nzima kwa kuzingatia kiasi cha rasilimali misitu kilichopo na kiwango halisi kitakachotakiwa kuvunwa ambacho hakitazidi robo ya rasilimali iliyopo.

"Hatuwezi kuendelea tu kutoa vibali vya kuvuna misitu hatujui tunavuna wapi, tuna rasilimali kiasi gani, wavune kiasi gani, hapana, mnitengenezee mpango laa sivyo nitasitisha uvunaji, nikisema nasitisha uvunaji nitapeleka waraka kwa Wakuu wa Mikoa, na nina uhakika kwa nguvu walinayo hawashindwi kuzuia uvunaji.


"Kwahiyo TFS nawapa siku saba mniletee mpango wa tathmini ya namna ambavyo tuna rasilimali kwenye kila mkoa, tujue mkoa flani una miti cubic mita kadhaa ya mbao kadhaa, ya kuni kadhaa, ya mkaa kadhaa na kwa mwaka huu tutaruhusu wavune kwenye msitu fulani kiasi kadhaa, twende kisayansi, sio Meneja wa TFS anakaa Wilayani anatoa vibali watu wanaenda kuvuna,".

Dk. Kigwangalla amesema takwimu za uharibifu wa misitu hapa nchini zinatisha jambo ambalo likiachwa liendelee bila kuchukua hatua nchi itageuka kuwa jangwa.

"Kwa mwaka tunakata miti kwa mahitaji mbalimbali kati ya ekari 800,000 na 1,200,000.
Ili kurejesha walau nusu ya miti tunayokata kwa mwaka tunahitaji kupanda miti 3,000,000 kwa mwaka mfululizo kwa miaka 17 ili kufidia kiasi cha uharibifu tunachofanya kwa nusu mwaka" alisema Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ezekiel Mwakalukwa ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alisema kumekuwepo na jitihada za kuandaa programu kubwa za kitaifa za uhifadhi wa mazingira katika maeneo mahususi yaliyoonekana kuzidiwa na tatizo la uharibifu wa mazingira.

Alitaja Programu hizo kuwa ni Hifadhi Ardhi Dodoma (HADO), Hifadhi Ardhi Shinyanga (HASHI), na Hifadhi Mazingira Iringa (HIMA).

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack alisema mkoa wake kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Tabora umeanza kuchukua hatua za kurejesha uoto wa asili katika maeneo yao ikiwemo kuanzisha utaratibu wa kugawa miche ya miti kwa kila kaya pamoja na kuimarisha kamati za uhifadhi wa mazingira.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Taboba, Aggrey Mwanri alisema ushirikiano huo ni muhimu kwani utawezesha kukabiliana na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo kwa kuweka mikakati ya pamoja wa kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga jana.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiteta jambo wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho hayo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakiwasalimu wananchi wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ezekiel Mwakalukwa ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa maelezo kuhusu maadhimisho hayo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakielekea eneo la tukio la kupanda miti wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki kucheza ngoma wakati wa maadhimisho hayo.

RAIS DKT. MAGUFULI AELEKEA MKOANI MANYARA LEO

April 06, 2018


Picha zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Marubani wa Ndege ya abiria ya ATCL wakati akielekea kupanda ndege hiyo kuelekea mkoani Kilimanjaro na badae mkoani Manyara kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kitaifa mkoani humo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ndege hiyo ya abiria ya Shirika la Ndege la ATCL kuelekea mkoani Kilimanjaro na baadae mkoani Manyara. PICHA NA IKULU