ZAIDI BILIONI 126 HUPATIKANI KUTOKANA NA ZAO LA UFUTA MKOA WA LINDI
WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAWAZIRI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza Kikao Kazi cha Mawaziri kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kikao Kazi cha Mawaziri wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kikao hicho kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Mei 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)HISTORIA MPYA MIUNDOMBINU YA KIMKAKATI KUANDIKWA
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limeridhia na kuidhinisha zaidi ya shilingi trilioni 3.5 kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Bajeti hiyo pamoja na mambo mengine inatarajiwa kuweka historia nchini ambapo barabara kuu na za mikoa zenye urefu wa kilometa 2,035 zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha Lami na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo mbalimbali.
Akijibu hoja za wabunge wakati wa majumuisho ya bajeti ya Wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kwa dhati kuifungua nchi kiuchumi kupitia miundombinu ya kimkakati inayosimamiwa na Wizara kwa upande wa Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi.
Prof. Mbarawa amezitaja barabara 7 zenye urefu wa kilometa 2,035 zitakazojengwa kwa utaratibu wa EPC + F kuwa ni barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435), barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (Simiyu) (km 339) na barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijochini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 460).
Miradi mingine ni barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa Junction (km 453.42), barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175), barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (km 218), barabara ya mchepuo ya Uyole – Songwe yenye urefu wa kilometa 48.9 pamoja na barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81).
Aidha, barabara ya Express way kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro ambayo ujenzi wake unashirikisha sekta binafsi itajengwa huku miradi ya mabasi ya mwendo kasi ya DART na daraja la Jangwani vikitengewa Bilioni 2.2.`
Kwa upande wa Sekta ya Uchukuzi shilingi Trilioni 1.13 zinatarajiwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ikiwemo vipande vipya vya Dodoma hadi Kigoma, Uvinza hadi Burundi na DRC.
Ununuzi na utengenezaji wa ndege nne utakaogharimu takriban shilingi bilioni 300 utatekelezwa ukiwa ni mkakati wa kuendelea kuifufua ATCL ili kulifanya shirika hilo kuwa na tija na kuchagiza uchumi nchini.
Profesa Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha huduma za usafiri wa anga, utabiri wa hali ya hewa na usafiri kwa njia ya maji zinakuwa salama na za uhakika.
Jumla ya wabunge 75 wamechangia katika bajeti hiyo ambapo kati ya hao 67 kwa kuongea na nane kwa maandishi. Na hatimaye bunge kupitisha kifungu kwa kifungu Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
SAMIA LEGAL AID YAZINDULIWA MANYARA, HUDUMA ITATOLEWA SIKU KUMI.
Na John Walter-Manyara
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Paulina Gekul amewataka wananchi kutumia Huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign), kupata haki zao na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Naibu Waziri Gekul ametoa wito huo leo mei 23,2023 mjini Babati wakati akizindua kampeni hiyo kwa Mkoa wa Manyara, itakayotolewa bure kwa wananchi wote kwa siku kumi katika wilaya tano za mkoa huo.
Amesema kampeni hiyo inayosimamiwa na serikali kupitia wizara ya Katiba na Sheria, itasadia kuimarisha mfumo wa utoaji Huduma za msaada wa kisheria kuanzia Serikali Kuu Hadi Serikali za Mitaa.
Pia, Gekul amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya Vijiji, kuweka mfumo mzuri wa kushighilikia changamoto za kisheria zitakazoibuliwa wakati wa kampeni hiyo.
Aidha amesema wataalamu wa sheria kutoka wizara ya Katiba na Sheria watakuwepo katika wilaya zote tano za mkoa wa Manyara kwenye majimbo Saba kuwasikiliza wananchi kuanzia ngazi ya kata na kutoa elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu Sheria.
Kampeni hiyo inayotekelezwa chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la Legal Services Facility (LSF) na mashirika mengine, imepewa jina la Samia, ili kuenzi mchango wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika kutokomeza vitendo vya ukatili hasa kwa kina mama, watoto na makundi Maalum na kutoa nafasi ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi wote.
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Manyara Kheri James ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mbulu, amesema mkoa upo tayari kutoa ushirikiano ili wananchi waweze kupata huduma hiyo muhimu. Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Pater Toima amempongeza na kumshukuru Rais kwa kuwakumbuka wanyonge wanaokosa haki zao kwa kutokujua sheria.
NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA UWAJIBAKAJI UNAOZINGATIA SHERIA SEKTA YA ARDHI
Na Munir Shemweta, WANMM
Naibu waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema watumishi wa sekta ya ardhi nchini wanao wajibu katika utendaji kazi na dhana nzima ya kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia sheria.
"Tunahitaji nidhamu na miongozo mbalimbali ili kutoa hiduma stahiki kwa watanzania.
Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleio ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema hayo tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi.
Aidha, amesema mwajiri naye anao wajibu wa kuweka mazingira mazuri mahali pa kazi sambamba na kuwaheshimu watumishi na kuwaendeleza ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela, Naibu Waziri Pinda alisema mpango wa urasimishaji unafikia kikomo mwaka huu wa 2023 na makazi holela yanaendelea kushamiri huku miji ikikua kwa kasi.
Kwa mujibu wa Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, kazi ya Baraza la Wafanyakazi ni kutumia mkutano huo wa Baraza kuishauri serikali juu ya mkakati mpya wa kuondoa makazi holela.
Amelitaka Baraza la Wafanyakazi kujadili kwa kina makadirio ya mipango ya matumizi kwa mwaka 2023/2024 na kuweka mipango inayotekelezeka.
Pamoja na mambo mengine ametaka kuwekwa mikakati madhubuti kwenye masuala ya makusanyo ya kodi ya ardhi ambapo amesema wizara imekusanya bil 129 sawa asilimia 51.6 ya lengo jambo alilolieleza halikubalikia.
Ameelekeza kila mkoa kuongeza kasi ya makusanyo ili kutimiza lengo lililowekwa na kuchukua hatua kwa wadaiwa wote sugu kutokana na muda wa msamaha wa rais kupita.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa kikoa cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara yake tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma.
RAIS DKT. SAMIA AMWAPISHA JAJI (Mst.) TEEMBA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAADILI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, (Kushoto) akimwapisha Mhe. Jaji (Mst.) Rose Teemba (Mwenye suti ya kijivu) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma tarehe 23.5.2023.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi,(hayuko pichani) akiongoza kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa waheshimiwa majaji wa Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu chamwino, jijini Dodoma tarehe 23. 5.2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,(wa pili kushoto), Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri (wa tatu kushoto) na Jaji. Sivangilwa Mwangesi, Kamishna wa Maadili wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa majaji wa Rufani, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili na watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria Ikulu, Chamwino jijini Dodoma tarehe 23.5.2023.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemwapisha Jaji (Mst.) Rose Teemba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma tarehe 23.5.2023.
Mhe. Rais alimteua Jaji Teemba tangu tarehe 24.4.2023 kwa mujibu wa kifungu cha 26(1) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 kinachoeleza kuwa Baraza la Maadili litakuwa na wajumbe watatu watakaoteuliwa na Rais, miongoni mwao akiwemo aliyeteuliwa kutoka miongoni mwa watu wenye wadhifa au wamewahi kuwa na wadhifa wa Jaji wa Mahakama Kuu.
Aidha, kifungu hicho cha 26(3) kinasema kuwa Rais, atateua mmojawapo wa Wajumbe wa Baraza kuwa Mwenyekiti.
Katika hafla hiyo, Mhe. Rais ameeleza kuwa hana mashaka na uzoefu katika utendaji kazi wa Jaji Teemba.
“Jaji Sivangilwa Mwangesi, Kamishna wa Maadili akisha maliza kazi yake anakuleteeni nyinyi Baraza la maadili, ichambueni vizuri na kutuletea mapendekezo yenu,” amesema na kuongeza kuwa, “Tuna matatizo makubwa kwenyey eneo la uadilifu katika utawala, shughulikieni.”
Kazi kubwa ya Baraza la Maadili ni kufanya uchunguzi wa kina wa malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya viongozi wa umma waliotajwa katika kifungu cha 4 cha Sheria hiyo.
Aidha, uchunguzi huo hutanguliwa na uchunguzi wa awali ambao kwa mujibu wa kifungu cha 18(2)(c) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, hufanywa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Jaji mstaafu Teemba anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Ibrahim Mipawa aliyemaliza muda wake, akiongoza Baraza hilo tangu Agosti 16, 2019 alipoteuliwa kushika wadhifa huo.
Jaji mstaafu Teemba anakuwa Mwenyekiti wa tano wa Baraza la Maadili toka kuanzishwa kwake akitanguliwa na Jaji mstaafu Damian Lubuva, Jaji mstaafu Hamis Msumi, Jaji mstaafu Januari Msofe na Jaji mstaafu Ibrahim Mipawa.
ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA STADI ZA KAZI NI MUHIMU KWA KUANDAA NGUVU KAZI YENYE UJUZI – MHE. KATAMBI