ALPHONCE FELIX NA JACKLINE SAKILU WASHINDI WA TIGO NGORONGORO MARATHON

April 21, 2014
Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio ambaye aliyemwakilisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Tigo Ngorongoro zilizofanyika jana Aprili 19, 2014 kuanzia Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu akiongea machache wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zawadi zao. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola.
Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio (kushoto) na Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) wakimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 22 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:03:59. Mbio hizo za Tigo Ngorongoro zilifanyika jana Aprili 19, 2014 kwa kuanzia geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu. Tigo ndiyo walikuwa ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo,
Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) akimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:03:59.
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Riadha Tanzania, akitoa zawadi kwa Fabian Joseph aliyeshika nafasi ya nne,
Mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya ZARA ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo akitoa zawadi kwa mshindi wa saba kwa upande wa wanawake.
Washindi wa Mbio za Tigo Ngorongoro upande wa wanawake wakiwa wamejipanga kusubiri zawadi zawadi zao… kutoka kulia mshindi wa kwanza Jackline Sakilu, Nathalina Elisante, Marry Naali, Failuna Abdi na Flora Yuda.
Wanariadha wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza mbio katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwachomoka wenzake.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akimaliza kwa furaha.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo kulipoanzia kwa mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
Mshindi wa kwanza wa mbio za makampuni akifurahia mara baada ya kumaliza.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu ya Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika Mbio za Tigo Ngorongoro.Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog..

TAMASHA LA PASAKA LATIKISA UWANJA WA TAIFA

April 21, 2014




 Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana kwenye u8wanja wa Taifa akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo na kuwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa katiba mpya akisema uamuzi mtautoa nyini ni serikali gani mnaiihitaji iwe moja, Tatu au Mbili nyinyi ndiyo mtaamua na sisi tutakipitisha kile mlichokiamua, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Angela Kairuki.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana.
 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama
 Mwimbaji wa ijini kutoka nchini Uingereza Dayo Bello akiimba na mkewe Ruth Tobi wakati wa tamasha la pakasa kwenye uwanja wa Taifa jana.

 Mwimbaji Jesca BM naye alipagawisha mashabiki
 Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake jukwaani
 Umati uliojitokeza  katika tamasha hilo.
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka akirejea kuketi huku akizungumza na Richard Kasesela na Alex Msama katikati.
 Upendo Kilahiro akiimba jukwaani na kundi la Victoria Singers.
 Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia mwanamuziki Kekeletse Phoofolo hayupo ichani wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani.
Ikafika zamu ya Upendo Nkone
Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo kazi moja tu burudani .
Rose Muhando na kundi lake wakipagawisha kwenye tamasha la Pasaka jana katika uwanja wa Taifa.

MZEE WA MIAKA 61 AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ILEJE MBEYA

April 21, 2014

Gari ya wagonjwa toka Ileje ikiingia Hospitali ya rufaq Mbeya  
Majirani wakimuhudumia majeruhi
NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya- Mbeya Yetu Blog.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.

Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka nazo.

Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.

Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha kikatili.

Kamanda Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.

MMH..CHADEMA...TAALUMA SI KIGEZO KIKUBWA CHA KUPATA UBUNGE...JE NI SAHIHI?!

April 21, 2014

1) Godbless Jonathan Lema -- Diploma
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
 4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six

5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level  
6) Simon Peter Msigwa - -- O level,  
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education,
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM  
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)  
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary,  
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL  
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV  
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM  
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University  
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated  
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping  
17) Said Amour Afri --- Primary school  
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level  
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine  
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM  
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree  
22) John John Mnyika --- CV not updated  
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT  
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated
Msitari mwekundu kwa Uongozi wa juu nchini kama Ubunge unatakiwa uwe juu ya Advance diploma, Hili la Ubunge kwa chadema ni kama vile Mheshimiwa slaa alivyotangaza Kirahisi kuhalalisha gongo kwa lengo la kuvuna kura za wanywa gongo eti atakuza uchumi kupitia watengeneza gongo na wanywaji! Kasahau kwamba gongo hata kama sio sumu ila inaweza kutengeneza genge la wavivu kufanya kazi, Hawajali taaluma na wanazidi kujitetea na kutangaza kwamba elimu sio kigezo cha lazima kwenye uongozi kwani wasomi wa ccm wamechemsha tangu Uhuru!. 
Ukweli ni kwamba ukiondoa wabunge wasomi wachache wa chadema wengine ni wapiga kelele tu Bungeni wanafanya kuonekana tu kwamba wanaongea lakini ni wabunge wasio na mtazamo wambali wanaona mwisho wa pua zao tu. 
Taifa zima linapaswa kuamua sasa Kukataa kuongozwa na waigizaji wa Darasa la saba, na lazima tusitumie maneno rahisi kujenga jamii isiyothamini elimu Kama tunavyoaminishwa na wanasiasa rahisi hawa ambao kwasasa wanaonekana kivutio kwa wasiosoma kama akina afande sere, JB, Ray, Mzeemajuto ambao lengo lao kusaka ubunge nikuongeza umaarufu wao ila hawana vission yeyote kwa Watanzania. 
Bungeni sio sehemu ya kuenda kufanya sanaa, Bungeni sio kwenda Kuchekesha Bali nikuenda kuwawakilisha watu milioni karibia hamsini sasa ambao asilimia 80 wanaishi katika umasikini wakutupwa, acha mwanamziki afanye kazi ya mziki, muigizaji aigize, mchekeshaji achekeshe nasio kukimbilia mambo mazito ya kitaifa kwa umaarufu rahisi walionao. 
Tujiulize swali Tunajenga Taifa gani kwa kuongoza na Darasa la 7 au wasanii?  Hivi mzee majuto anataka aende Bungeni Kufanya nini kama sio dharau kwa Bunge letu?  Mtu kama Lema au Sugu Ufahamu wake unaweza kulitoa taifa letu toka katika umasikini? au ndio tunazidi kuongeza migogoro katika jamii?  
Tusitumie Kigezo rahisi Eti wasomi wameshindwa basi kilamtu awe kiongozi katika jamii, angalia ukweli Hivi mtu kama zitto au J Mnyika anaposimama bungeni unaweza kufananisha na sugu au Lema. 
Taifa lolote lililoanza kupoteza Muelekeo linaanza kukumbatia wasio soma na wahuni kama akina lema na sugu na hii ni dalili mbaya Lazima Tujitambue na Tutambue athari za mfumo huu unaojongea Taratibu, Tusipokuwa makini Tutafanya kosakubwa sana kwa kuongozwa na Dicteta ambae kichwa chake ni sifuri kabisa. 
Chadema Kama chama Mbadala talajali wa CCM, jitahidini kutujengea viongozi Bora, shawishini wasomi wagombee nafasi kubwa kama ubunge na msiangalie umaarufu wa mtu kwasababu baadaye mkipewa nchi mawaziri watabaki kunywa gongo, kuvuta bangi, kufanya maigizo, na kuimba bongo flever tu badala yakuwa serious kujenga Uchumi. 
Wabunge ambao ni darasa la saba je wanajiendeleza kielimu au ndio wamebweteka wakijua chadema Hakuhitaji wasomi? au nadharia yenu ya kuogopa umaarufu wao ndio bado itawapa nafasi ya kugombea ubunge tena 2015?, Tuleteeni akina Mnyika, akina mdee, akina zitto wengi2015 nasio kutujazia watu waliokimbia umande eti wanaweza kwakuwa wapiga kelele wasiojua hata uelekeo. Uchaguzi wa 2015 lazima Uwe uchaguzi utakaotuletea wasomi vijana wengi bungeni, Sugu, Lema, Majimarefu, Murugo, wote jiandaeni kugombea labda udiwani na hata baadhi yenu udiwani pia hauwafai gombeeni serikali za mtaa mwakani.

PICHA YA SIKU ONA WATU NA MAPENZI YAO HAO LIVE!!!!!!!!!!!!!!

April 21, 2014

BREAKIN NEWZZ:- MKUU WA WILAYA AFARIKI DUNIA JANA MUHIMBILI!!

April 21, 2014



Mheshimiwa Moshi Chang'a DC wa kalambo amefariki Dunia jana Mchana kwenye Hospital ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa Matibabu. DC Chang'a alianzia kazi yake ya Ukuu wa Wilaya ya Mbeya na Baadae Tabora.- Source JF Blog

TANESCO NJOMBE WANASA WEZI WA NYAYA ZA UMEME KITUO CHA MKOA HUO

April 21, 2014



 HAWA NDIO VIJANA WAnaotuhumiwa kuHUSIKA NA WIZI WA NYAYA ZA UMEME MJINI NJOMBE na Mmoja ametokomea kusikojulikana
Na Gabriel Kilamlya  Njombe

Shirika la Umeme Tanesco Wilaya ya Njombe Leo Limefanikiwa Kuwanasa Watu Wawili Waliokutwa Wakiiba Nyaya za Umeme Katika Kituo cha Kusambazia Umeme Yaani Power Station Mjini Njombe Huku Wawili Wakihusika Katika Tuhuma Tofauti Ikiwemo Ya Kununua Nyaya Hizo na Mmoja Kushindwa Kuwajibika Kama Mlinzi wa Zamu.

Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nne Asubuhi Huko Katika Mtaa wa Uzunguni Kwenye Kituo Hicho cha Umeme Yaani Power Station Ambapo Vijana Wawili Wamekatwa na Mmoja Ametokomea Kusiko Julikana Wakati Wa Msako Huo.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwafikisha Kwenye  Kituo cha Polisi Mjini Njombe Msimamizi wa Shirika la Umeme Wilaya ya Njombe Bwana Renatus Henerico Amesema Kuwa Wizi wa Nyaya Hizo Ulianza Tangu Wiki Iliyopita Lakini Kutokana na Kuweka Mtego wa Kuwanasa Wezi Hao Leo Zoezi Hilo Limefanikiwa.

Bwana Renatus Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa ni Pamoja na Justin Kyando Mwenye Umri wa Miaka 17 Mkazi Wa Ramadhani Mjini Njombe,Gehazi Kilumbe Mwenye Umri wa Miaka 18 Ambaye naye ni Mkazi wa Mtaa Huo wa Ramadhani,Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Nyaya Hizo Pamoja na Anna Mhenga Ambaye Alikuwa Mlinzi wa Zamu Katika Lindo Hilo.

Aidha Amemtaja Castory Mligo Kuwa Ametoroka wakati Wa
Tukio Hilo na Kwamba Miongoni Mwa Vijana Hao Wawili Walikuwa Wafanyakazi wa Mkataba Mfupi Katika Shirika Hilo Yaani S.T.E Ambapo Baada ya Mkataba Wao Kuisha Wakaanza Kujihusisha na Matukio Hayo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Nyaya Hizo Zilizo Ibiwa Hadi Sasa Zinagharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 60 Kwani Walianza Kuiba Tangu Siku Nyingi.
 
Blog hii Imefanikiwa Kuzungumza na Mmoja wa Watuhumiwa Hao Anayefahamika Kwa Jina la Justin Kyando Ambaye Amesema Kuwa Wamekuwa Wakiiba  Nyaya Hizo na Kuziuza Kwa Mfanyabiashara Huyo Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Vyuma Chakavu Katika Mtaa wa Msichoke Mkabala na Chuo Kikuu cha Amani Mjini Njombe.

Bwana Christian Mlelwa ni Mkuu wa Ulinzi Katika Kampuni Ya Jirani Security Group Yenye Makao Makuu Yake Jijini Dar es Salaam Ambaye Amesema Amekuwa Akimuomba

Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kumuongezea Walinzi Hususani Katika Eneo Hilo la Power Station Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kwani Eneo Hilo ni Kubwa Zaidi.

HATIMAE MSEMAJI WA P-SQUARE AONGEA KUHUSU TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI

April 21, 2014

Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.

ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA NJOMBE AWATAKA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA KUWA NA HOFU YA MUNGU

April 21, 2014
Na Prosper  Mfugale, Njombe
Askofu Wa Jimbo Katholiki La Njombe Alfred Maluma Amewataka Wajumbe Wa Bunge Maalumlu La Katiba Kutangulizi Hofu Ya Mungu Katika Kuijadili Na Kuichambua Rasimu Ya Katiba Mpya Ili Taifa Liweze Kupata Katiba Bora Itakayowafaa Watanzania.
Ameyasema Hayo Kwenye Misa Ya Mkesha Wa Pasaka  Katika Kanisa  Katoliki Jimbo La Njombe Wakati Akihubiri Injili Maalumu Ya Mkesha Huo.
Askofu Maluma Amesema Takribani Miaka Hamsini Ya Uhuru Taifa La Tanzania Limekuwa Likipokea Wageni Mbalimbali  Kufuatia Hali Ya Amani Ambayo Imetokana Na Muungano Imara Ulioanzishwa Na Waasisi Wa Taifa Hilo
Amesema Watanzania Hawana Budi Kuendelea Kuliombea Bunge Maalumu La Katiba Ili   Katiba Bora Ipatikanae Ambayo Italeta Haki Na Demokrasia Kwa Watanzania Wote Nasio Wachache.
 Pia Ametumia Fursa Hiyo Ya Mkesha Kumshukuru Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Kwa Kuamua Kuwaruhusu Watanzania Kuunda Katiba Mpya Ya Kisheria Ambayo Itatea Haki Na Demokraia Kwa Wote

Katika Hatua Nyingine Amesema Anashangazwa Na Kitendo Cha Baadhi Ya Wajumbe Wa Bunge Maalumu Wa Bunge La Katiba Kutumia Bunge Hilo Kwa Kufanya Mizaha Badala Ya Kujadili Rasimu Kama Walivo Tumwa Kuwawakilisha Watazania Waliobaki Na Kuongeza Kuwa Iwapo Muungano Utavunjika Heshima Ya Taifa Hilo Haitakuwepo Na Kwamba Taifa Hilo Halita Tawalika Kama Ilivyo Sasa
PROFESA KABUDI AWASHA MOTO KATIBA MPYA

PROFESA KABUDI AWASHA MOTO KATIBA MPYA

April 21, 2014
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akifafanua jambo. Picha na Maktaba 
********
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amejibu baadhi ya hoja za watu wanaopendekeza muundo wa serikali mbili na kusema Serikali ya Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka serikali tatu mwaka 1984.”
Aidha, amewashangaa wanaolibeza jina la Tanganyika kutumika serikalini kwa madai kuwa jina hilo siyo haramu kwa kuwa limo ndani ya Katiba ya sasa.

Alisema kuwa wakati huo madai ya serikali tatu yalitolewa na Zanzibar na kusimamiwa na Rais aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.
“Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza la Wawakilishi, Brigedia Mstaafu Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa Waziri Kiongozi), alikuwa akiongea kwa sauti nzito, kama ulikuwa ukimsikiliza, unasema muungano haupo,” alisema Profesa Kabudi na kueleza kuwa Fakhi alisema: “Zanzibar siyo koloni la Tanganyika.”
Alikuwa akichangia hotuba katika Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika mjini Zanzibar jana. Alieleza kwamba mjadala wa sasa wa muungano siyo mkali kama uliokuwepo mwaka 1983 na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla mzungumzaji kumaliza hotuba yake.
Katika maelezo yake, Profesa Kabudi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa Fakhi alikuwa haongei kama mtu baki, bali aliagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lugha ilikuwa ni kali,” alisema.
Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema kuwa masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unawezekana kuwa muungano unatunyima fursa moja ua mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao, lakini wahakikishe wanawahudumia wananchi,” alisema.
Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka CCM, wakiwamo Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu ya Katiba Mpya.
Kikwete pamoja na wajumbe hao kwa nyakati tofauti, walisema kuwa Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba haionyeshi uhalisia wa matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu muundo wa muungano.