*BREAKING NEEEEZZZ!!!! MILIPULO KADHAA YAUA NA KUJERUHI MJINI MOMBASA

May 04, 2014

 Mlipuko kadhaa imetokea mjini Mombasa nchini Kenya, ambapo imedaiwa walipuaji wamelipua sehemu tatu tofauti.
Akizungumza kutoa taarifa za tukio hilo Kamishna wa kaunti ya mombasa Nelson Marwa, amesema kuwa waliotekeleza shambulizi hilo huenda wametoroka wakitumia piki piki.

Aidha amesema kuwa watu 3 wamefariki kutokana shambulizi hilo la guruneti, huku mlipuko mwingine ukishuhudiwa katika eneo la Nyali Reef, lakini hakuna majeruhi.

Ikumbukwe kuwa shambulizi hili linajiri siku chache tu baada ya mlipuko mwingine kushuhudiwa jijini Nairobi katika kituo cha polisi cha Pangani ambapo watu 4 wakiwemo maafisa 2 wa polisi walifariki.

Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa polisi  tayari wameanza kuwasaka washukiwa wa matukio hayo.
Repoti kutoka Shirika la Msalaba mwekundu, inasema kuwa waliofariki ni watu watstu akiwamo mwanamke mmoja na wanaume wawili.

Wwalijeruhiwa 25,kwa sasa waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na xray na ukaguzi mwengne.vioñgozi wa kaunti wa msa wamefika.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwa eneo la tukio.
Majeruhi.....akihudumiwa.
Majeruhi....
Majeruhi...
Mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo.

RIDHIWANI AMPONGEZA DIAMOND PLATINUMZ KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK, SOMA UJUMBE HAPA

May 04, 2014

Kwanza Hongera sana kwa kushinda Kili Awards.Hii ni zawadi nzuri unayoweza kupata baada ya Jitihada,Kujituma, na Burudani nzuri kwa washabiki wako.Mungu akujalie mema zaidi ya hapo.Hongera sana Platnumz.

BREAKING NEWS TFF YAONGEZA TIMU LIGI KUU SASA ZAFIKA TIMU 16

May 04, 2014
TIMU 16 LIGI KUU MSIMU WA 2015/2016
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.

Mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.

Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.

Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.


BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)