MKUU WA MKOA WA TANGA MWANTUM MAHIZA AWASIMAMISHA KAZI WAFANYAKAZI WATANO WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA.

December 05, 2015


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akizungumza kwenye Majumuisho ya Ziara yake na amewasimamisha kazi watendaji watano wa idara ya ardhi na mipango miji kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kufanya uchunguzi kutokana na utendaji mbovu wa kazi.
.
Baadhi ya wakuu wa Wilaya na wakuu wa Idara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
                                    
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdulah Lutavi akizungumza wakati wa Majumuisho ya Ziara ya Mkuu wa Mkoa aliyofanya Jiji la Tanga.

 Wawakilishi wa Bandari ya Tanga wakiwa makini wakati wa kikao hicho.

                                     Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa.
Dkt.Mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya Bombo Asha Mahita akizungumza wakati wa Majumuisho

                                      
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga kushoto ni Kamanda wa Poilisi Mkoa wa Tanga Zubeir Mwombeji.

WATENDAJI WA TAMISEMI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KUHUSU USAFI, UJENZI HOLELA, WANAOFANYA BIASHARA MAENEO YA DART

December 05, 2015

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa ofisi hiyo leo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dares Salaam , ambapo lengo kuu lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Afya -TAMISEMI ,Dkt .Deo Mutasiwa .
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakimsilikiza Katibu Mkuu wa ofisi ambaye hayupo pichani.

Na Magreth Kinabo – maelezo
SERIKALI imewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kwa uadilifu weledi wa taaluma zao na kufuata sheria zilizopo katika kusimimia suala la usafi wa mazingira, likiwemo la kudhibiti biashara holela, gereji bubu,uegeshaji wa magari holela.

Pamoja na hayo wasimamie, upigaji holela wa muziki katika vilabu, baa na kumbi zaidi ya saa zilizopangwa na kuzuia bodaboda zinazosafirisha abiria hadi maeneo ya miji katikati, pia kuzuia ujenzi holela.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa ofisi hiyo katika mkutano wa kikazi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu lilikuwa ni kutoa maelekezo ya utendaji kazi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

Akizungumzia kuhusu suala la usafi wa mazingira kufuatia ziara iliyofanyika hivi karibuni imeonekana kuwa na changamoto mbalimbali alisema;
“Kazi zetu haziendi vizuri kwa sababu hatusimamii sheria zilizopo ndio kumekuwa na malalamiko katika utendaji wa kazi zetu, mfano katika suala la gharama za usimamizi wa usafi wa mazingira ni kubwa . Lakini kinachofanyika ni kweli kinalinganishwa na gharama hizi?” alihoji Katibu Mkuu huyo.

Akitolea mifano gharama zinazotumika katika suala hilo, kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/2015 alisema kwa upande wa manispaa ya Kindondoni wanatumia Sh. bilioni 2.6, Ilala ni Sh. bilioni 2.6, wakati Temeke wanatumia Sh. bilioni 1.2 .

“Kilichobainika ni kwamba mikataba ya watu wanaojishughulisha na usimamizi wa usafi wa mazingira ni ya mwaka mmoja na wanaopewa mikataba hiyo ni watu ambao hawana uwezo wa kutosha wa kutekeleza jukumu hilo.

“ Ama watu wasio na uwezo ama mnaofahamiana nao. Au kampuni zenye mahusiano na baadhi ya watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa au wenye uhusiano na viongozi wenu, Jiepusheni na kuwapa watu hawa kwa sababu kutokana na hali hiyo hamtaweza kukabiliana nao. Kama kuna kiongozi ambaye mmepatia nafasi hii lazima athibitishe kuwa na uwezo. Na kama pia ni miongoni mwenu hakikisheni kuwa ni mtu mwenye uwezo. Kazi zetu haziendi vizuri kwa sababu ya nasaba au viongozi wenu,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo, huku akisema lazima wabadilike na kuangalia kama hawana uwezo wajitoe au wafukuzwe.

Aliongeza kwamba katika suala hilo kumekuwa na migongano ya watumishi wa halmashauri ambao wanatakiwa kufanya kazi kama timu; mfano maafisa afya, mazingira na usafishaji, lakini akasema wanaonana kama maadui.

“ Hawa wangepaswa kufanya kazi kwa kushirikiana ,lakini ni maadui kwa sababu ya maslahi … hili ni lenu wakurugenzi kwani hata watoto wako wakisambaratika ni lazima huwaketishe chini ili mambo yaende, asiyekubali unamwajibisha,” alisema.

Sagini alisema watendaji hao , wote ni wadau wa usafi, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, hivyo aliwataka wapeane mikono katika kikao hicho, ambapo walifanya hivyo ikiwa ni hatua ya kuonesha ushirikiano.

Pia alisema watu wanaosafirisha bidhaa za vyakula kwa kutumia majani ya migomba au matenga wasiruhusiwe kufanya hivyo wapewa muda wa wiki moja au mbili kutumia utaratibu mwingine.
Aliwataka pia watendaji mbalimbali wa TAMISEMI kuwa na ushirikishwaji katika ngazi za chini kwenye halmashauri kwa kuwa haliko vizuri.

Sagini alisema ni vizuri kukawekwa mfumo wa TAMISEMI wa kushirikisha ngazi za chini kama ilivyo kwa mjumbe wa nyumba kumi kwenye masuala ya vyama.

“ Ni lazima tuingie katika mfumo huu wa kuwa na watendaji wa kaya 30 ambao watakuwa chini ya TAMISEMI . Suala hili lina faida ya ulinzi na usalama na kuwatambua wageni… tunaangalia jinsi ya kulitekeleza,” alisema.

Aliwataka wakurugenzi wasikae maofisini kwenye madawati bali watembelee maeneo mbalimbali ili kutatua kero za wananchi na kuangalia mipangilio ya miji na majiji.

Katika suala hilo la usafi wa mazingira alisema mtu mwenye uwezo wa kusafisha jiji liwe safi apewe nafasi huku akisisitiza suala la kushirikisha sekta binafsi ni muhimu katika mambo mbalimbali likiwemo la ujengaji wa maegesho ya magari, ambapo sasa yanahitajika kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka(DART).

“ Kwenye eneo hili la DART lazima mbadilike tunataka barabara za DART ziwe nyeupe yaani watu wasifanye biashara,” alisisitiza huku akitaka kuanzia Jumatatu wiki ijayo yatekelezwe.

Aliwataka watu wanaohusika na vyombo vya usafiri na usafirishaji kutovunja sheria, akatolea mfano boda boda.

SKYLIGHT BAND WAENDELEA KUWASHA MOTO WA NGUVU NDANI YA ESCAPE ONE USIKOSE LEO

December 05, 2015
Waimbaji wa Bendi ya Skylight pamoja na mashabiki wa bendi hiyo wakiendelea kuzirudi katika kiota cha Escape One Jijini Dar es Salaam na leo sio siku ya kukosa maana utakosa vitu vizuri kutoka katika bendi hiyo
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Kasongo Junior na Natasha wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Sasa ukafika muda wa waimbaji wa bendi ya Skylight kuonesha maujuzi yao uku JOniko akiendelea kuchana mistari.
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya Skylight.
Mwimbaji wa Band ya Skylight, Bijal Valentine akishusha mistari ya kufa mtu mbele ya mashabiki wao waliofika kwenye kiota Cha Escape One huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni Leah, Suzy na Sony Masamba.
Sam Mapenzi(kushoto) akiimba pamoja na Natasha (kulia) moja ya nyimbo zinazobamba hapa nchini huku Meneja wa bendi hiyo akifurahia kwa kupiga makofi baada ya Natasha kurudi tena katika bendi hiyo.
Sony Masamba akichana mistari na mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuzirudi huku Sam Mapenzi na Kasongo Junior wakimsikindiza kwa miondoko ya aina yake. Hakika hii sio ya kukosa leo Jumapili njoo wewe na umpedaye upateraha ya nguvu kutoka katika bendu hiyo.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni.
Mashabiki wakiendelea kujimwaga na burudani ya Skylight Band kiota cha Escape One.
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza‬ kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam
Sasa ikafika muda wa kuzungusha mduara hakika ukikosa leo utakuwa umekosa vitu vizuri.
Kifaa kipya cha Bandi ya Skylight, Leah (katikati) akitoa burudani ya nguvu mbele ya mashabiki wao huku akisindikizwa na waimbaji wenzake Sony Masamba (kushoto) pamoja na Suzy.
Sony Masamba akichana mistari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku Leah pamoja na Suzy wakimsindikiza kwa kuzirudi mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani).
Hakika Skylight band inawagusa sana mashabiki wao maana...... sasa na wewe njoo leo ujionee mwenyewe mambo yanavyokuwa.
Mashabiki wakitweta jasho na sebene la Skylight Band.
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakicheza kwa kuwaonesha style ya nyimbo yao ili waendane nao wanapokuwa wanacheza nyimbo za bendi hiyo.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOWASILI AFRIKA YA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOWASILI AFRIKA YA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA.

December 05, 2015

SAM1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Picha na OMR
SAM2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni  Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya. Picha na OMR
SAM3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe)  akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM7 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa  Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM8 
Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na OMR
SAM9 
Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na OMR
SAM10 
Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na OMR

MKURUGENZI MKUU NHC AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MIKOPO YA NYUMBA KONGAMANO LA WAHANDISI

December 05, 2015

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kwenye kongamano la 28 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (Institution of Engineers Tanzania – IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha na mikopo ya nyumba katika kuimarisha sekta ya ujenzi wa nyumba endelevu za gharama nafuu nchini. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere. IET ni Taasisi inayojitegemea iliyoundwa mwaka 1977, ikiwa na lengo la kuimarisha fani ya Uhandisi hapa nchini. Taasisi hii tayari ina jumla ya wanachama 3,000 kutoka katika sekta mbalimbali hapa nchini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kwenye kongamano la 28 la taasisi ya Wakandarasi Nchini (IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha katika kuimarisha sekta ya ujenzi wa nyumba endelevu za gharama nafuu nchini. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kwenye kongamano la 28 la taasisi ya Wakandarasi Nchini (IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha katika kuimarisha sekta ya ujenzi wa nyumba endelevu za gharama nafuu nchini. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.
Washiriki wa kongamano la 28 la Taasisi ya Wakandarasi Nchini (IET) juu ya mchango wa Wahandisi katika kujenga Mazingira Endelevu kwenye ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini Kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam linafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere.
 Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kwakiwa katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa NHC
  Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kwakiwa katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa NHC
 Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kwakiwa katika banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa NHC
TAMISEMI YAENDELEA KUHAMASISHA SUALA LA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.

TAMISEMI YAENDELEA KUHAMASISHA SUALA LA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.

December 05, 2015

MZ1 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wakiwasili eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
MZ2 
Baadhi ya wahudumu wakiendelea na usafi eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa huku Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakikagua na kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
MZ3 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli Majuto akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
MZ4 
Vijana wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika mazingira ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji.
MZ5 
Kijana Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
MZ6 
Msafara wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba wakishuhudia moja ya shimo la maji mchafu ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa afya ya wananchi wanaofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam au wale watakaotumia samaki hao kama hawatakuwa wameandaliwa katika hali ya usafi na salama. Lengo ni wananchi wengi wanaofika sokoni hapo ni kununua samaki waweze kuwauzia watu wasoweza kufika sokoni hapo na wengine kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani.
MZ7 
Mama lishe Zainabu Hamad anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula katika soko la Feri zoni 4 kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni hapo kwa lengo la kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya wananchi wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
MZ8 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko la Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha ya uchafu uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda hawachukui tahadhari yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo wanauza matunda aina ya mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi kuyazonga zonga matunda hayo kitu ambacho ni hatari kwa suala la usalama wa afya ya malaji.
MZ9 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akijionea wafanyabiashara wadogo walivyovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam huku mafundi wakiendelea na kazi ya kupaka rangi.
MZ11 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la Kariakoo jijini Dar esa salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)