LEO SIKU YA WAMAMA DUNIANI NIMETEMBELEA HOSPITAL 3 TEMEKE,AMANA,MWANANYAMALA KWENYE ODI ZA WAZAZI

May 11, 2014


Mkurugenzi Mtendaji wa Wanawaketunaweza Ltd Mrs Zeenat Singh leo hii
tar 11/5/2014 ambapo ni siku ya Mama Duniani, Mkurugenzi Mtendaji
ametembelea hospital tatu za jijini Dar es Salaam ili kuwafariji na
kuwapa moyo wazazi "Wakina-Mama" na kuwazawadia sabuni za kufulia.

Ziara ilianzia Temeke Hospital akiwepo Mkurugenzi Mtendaji, Katibu

John Tall na mpiga picha Rodgers na kuanza katika wodi ya Wazazi na
tulipokelewa na Shamim Kanju na tulipewa data kuwa jumla ya watoto 32 walizaliwa toka saa 6 usiku mpaka asubuhi ya leo ikiwa 13 Wanawake na 19 Wanaume.

Tukafika Ilala hospitali ya Amana nako tukapokelewa na Getrude Massawe
  na kupewa data watoto 94 walizaliwa ikiwa 44 Wanawake na 50 Wanaume na ziara yetu ikaishia Mwananyamala Hospital na tukapokelewa na  Tuswege Mwamwanja na hapo pia tuka tembelea wodi ya wazazi na kupewa
data kuwa watoto 28 wamezaliwa ikiwa ni 12 Wanawake na 16 Wanaume. 


hii inaleta jumla ya watoto 154 waliozaliwa kutoka saa 6 usiku mpaka saa 1 asubuhi "Wanawake 69 na Wanaume 85"

Kwa kweli mimi kama Mkurugenzi Mtendaji nikiwa na timu yangu tunapenda
  kutoa shukran zetu za dhati kwa uongozi wote wa Hospital tulizotembelea na kile kidogo tulichokuwa nacho tumeweza gawana na Wazizi tuliowafikia kama picha zinavyojieleza.


 tunaiomba jamii kutupia jicho kwa Wanawake kwani tukiwezeshwa tunaweza... kwa habari na mawasiliano pitia www.wanawaketunaweza.com



MGOMBEA URAIS WA SIMBA SPORT CLUB AFUNIKA MITAA YA DAR LEO ALIPOKWENDA KUCHUKUA FOMU YA URAIS WA TIMU HIYO ONA HAPA LIVE!!

May 11, 2014
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MAMIA ya wanachama wa Simba SC mchana wa leo walimsindikiza mwanachama mwenzao, Evans Elieza Aveva kwenda kuchukua fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi ujao Juni 29, mwaka huu.

Wanachama hao walimlaki Aveva barabara ya Lumumba na kumsindikiza kwa maandamano hadi makao makuu ya klabu, wakipitia barabara ya Uhuru na baadaye Msimbazi, yalipo makao makuu ya klabu yao.

Hata hivyo, wahusika wa makao makuu ya klabu walilazimika kuuzuia msafara huo na kumruhusu Aveva aingie na mtu mmoja tu kwenda kuchukua fomu, Saidi Tuliy, ambaye naye alichukua fomu ya kugombea Ujumbe.
Pointi tatu; Aveva akionyesha vidole vitatu wakati wa maandamano kumaanisha sera yake ni ushindi
Mimi ndiye rais wenu; Aveva akiwaonyesha alama dole tupu wanachama wa SImba SC wakati wa maandamano
Umati uliomsindikiza Aveva kuchukua fomu
Aveva akionyesha kadi yake ya uanachama, kulia ni Said Tuliy
Aveva akikabidhiwa fomu yake ya kugombe Urais

Alipoingia alitoa kadi yake ya uanachama kujitambulisha kwa mtoa fomu, kisha kukabidhi ada na kupewa fomu yake kabla ya kuondoka kwa maandamano mazito.
 
Wakati wa maandamano wanachama walikuwa wakisukuma gari ya Aveva kuanzia Lumumba hadi makao makuu na mgombea huyo alikuwa akionyesha ishara ya vidole vitatu, akimaanisha sera yake ni pointi tatu- maana yake ushindi.
Na alipofika makao makuu wanachama ambao walikuwa hapo wakimsubiri nao walimlaki kwa shangwe, wakisema; “Huyu ndiye rais wetu,”.
 
Kwa ujumla mapokezi ya Aveva yanaweza kuwakatisha tamaa watu wengine kujitokeza kuwania nafasi hiyo, kwani Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Usajili ameonekana kuungwa mkono na watu wengi.
Ni mtu mmoja tu hadi sasa ambaye tayari amechukua fomu ya Urais mbali na Aveva, ambaye ni Andrew Tupa, lakini habari zinasema mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo,  Michael Richard Wambura naye atachukua fomu ya nafasi hiyo kesho.
 
Kihistoria Aveva ni Simba damu ambaye amekuwa akiisaidia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni miongoni mwa waasisi wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S.), ambalo limekuwa na msaada mkubwa wa kifedha katika klabu hiyo.
Hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, lakini amekwishaongoza kwa mafanikio Kamati kadhaa, ikiwemo ya Usajili mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambayo ilifanya kazi nzuri ya kuibua vipaji kama vya akina Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Gabriel, Juma Kaseja, Yahya Akilimali, Said Maulid ‘SMG’, Suleiman Matola na wengine wengi.

JK atembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani cha Dangote, Nigeria

May 11, 2014

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj AlikoDangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote  wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote  wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote  wakati akizungushwa kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei , 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye machimbo ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme  wa kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na  mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda  cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei 9, 2014. 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na  mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda  cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na  mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda  cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei , 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika mfuko wa saruji alipotembelea kiwanda cha saruji chaDangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela Mei  9, 2014
JWTZ lashiriki Mkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa

JWTZ lashiriki Mkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa

May 11, 2014
image 
Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.
image (1) 
Ujumbe wa Tanzania (waliovaa sare za kijani), kutokakushoto Kanali Martin BusungunaLuteniKanali Joseph Bakariwakati wa mkutano.
image (2) 
Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.
image (3) 
Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano.
Na LuteniKanali Juma Sipe (PA, Marekani).
JWTZ limeshirikiMkutano wa Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the International Military Sports Council -CISM) uliofanyikaMjini Quito, EquadoAmerica ya Kusinikuanziatarehe 05-09 Mei, 2014.
Mkutano huo ulijadilina kuendelea kusikiliza na ushiriki wa majeshi katika Michezo ya Kimataifa chini ya Kauli mbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki kupitia Michezo (Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika kutumia michezo kama chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa duniani. Badala ya kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua migogoro.
Moja ya mambo yaliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo wa nchi za Afrika ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana na kukosekana fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika na kutoona umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo.
Aidha, Mkutano ulimchagua Rais mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka Bahrain na Kanali Dorah Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika.
Ushiriki wa Tanzania na utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa miaka kadha sasa. Kwa mfano,katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika Paramaribo, Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni Kanali) alitunukiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa kwa “Twalipo Youth Sports Foundation” (twalipo soccer academy.blogspot. com) nchini Tanzania.
Katika mkutano huojumla ya wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa Baraza hilo. Tanzania iliwakilishwa na Kanali MartinBusungu, Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na LuteniKanali Joseph Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.
Mkutano huo wa mwaka hutanguliwa na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya, AsianaAmerika) ambako masuala ya michezo ya Majeshi yanayogusa mabara husika hujadiliwa.
Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya ushirikiano Kusini mwa Afrika nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda na Zambia.
Kwa uelewa zaidi tafadhali tembelea wavuti www.cismmilsport.org

MAUAJI YA KUTISHA,MTOTO AUA WAZAZI WAKE WAWILI,ACHOMA MOTO NYUMBA.

May 11, 2014


Na Dixon Busagaga,Hai.
WANANDOA wawili wameuawa kinyama baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusuf Njau (32),  anayheaminika kuwa ni mtotoi wa wanandoa hao, kuwacharanga kwa shoka kisha kuchoma moto nyumba  yao na kutokomeakusiko julikana.
 
Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Masama-Roo,  Kata ya Machame Mashariki,
wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kijana huyo kuchukua uamuzi huo ambao unadhaniwa ni sababu za ugomvi wa kifamilia.

Wal;iouawa wametambulika kwa majina ya Shahidu Njau(60) ambaye  ni baba yake mzazi wa motto huyo na  Minae Swai (57) ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo ambao kwa pamoja waliuawa baada ya kupigwa na shoka katika maeneo mbalimbali ya mwili.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai alisema walipofika katika eneo la tukio baada ya kusikia ukunga, walikuta watu wakizima moto huku mwili wa Mama yake muuaji uliocharangwa na mapanga kila mahali ukiwa chini.

Alisema kuwa wakati kijana huyo akiendelea kutenda unyama huo, alitokea baba yake mzazi, Mzee Shaidu  aliyekuja kuingilia kati ugomvi wa Mama na mwanae lakini naye alikatwa kichwani.

Swali alisema Mwili wa Baba ulikutwa ukiwa pembeni wa mwili wa Mama ukiwa umekatwa kichwani na ubongo kufumuliwa lakini hata hivyo alikuwa bado hajafa.

Alisema walimchukua kwa nia ya kuokoa uhai wake lakini muda mfupi baada ya kutoka kwenye eneo la tukio wakiwa katika kituo cha mafuta maeneo ya kwa Sadala Shaidu alipoteza maisha.

"Tulikuta mwili wa Baba ukiwa pembeni nao ukiwa umejeruhiwa vibaya kichwani, ubongo ulikuwa pembeni, tulimchukua kumpeleka Hospitali lakini tulipofika kwa Sadala alipoteza maisha," alisema Swai

Taarifa kutoka katika kijiji hicho zilisema muuaji, Yusuf Njau, ambaye amewahi kujifunza ngumi akiwa Dar es salaam amewahi kuwatishia Uhai baadhi ya ndugu zake zaidi ya mara mbili.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Halfani Swai alisema kuwa kijana huyo ambaye ni morofi sana aliwahi kutishia kuwaua Shangazi na Baba mdogo.


"Muuaji aliwahi kuwatishia shangazi yake na Baba mdogo,amewahi kujifunza Ngumi na ni mkorofi sana kijijini kwake," alisema Swai.


Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa huyo katika tukio la kutishia kuuwa shangazi na Baba Mdogo alikatwa na kuachiwa.

Alisema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Hai ambapo juhudi za kumsaka Muuaji anayedaiwa kuonekana akiranda
kijijini hapo zinaendelea.

 

Kwa upande mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga alisema tukio hilo ni kinyama na kuwataka wananchi kuwa na subira huku akitahadharisha raia kuchukua hatua mikononi. Makunga aliwataka Wananchi kuwaachia watu wa usalama kuchukua hatua huku akitahadharisha kuhusu jaribio la wananchi kuchukua hatua mikononi kuwa inaweza kuleta madhara zaidi.
Wakati huo miili ya marehemu imezikwa jana mchana majira ya saa 7, kwenye makaburi ya Nyumbani, katika kijiji cha Masama Roo, Tarafa ya Masama, |Kata ya Machame Mashariki, wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.


Mwisho.

BREAKING NEWS:BALOZI WA MALAWI NCHINI AFARIKI DUNIA.

May 11, 2014

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Balozi Gomile-Chidyaonga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mwaka 2011, alikuwa Naibu Balozi wa nchi hiyo Uingereza alifikwa na mauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Balozi Gomile-Chidyaonga ndiye aliyefanikisha ujio wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) ambayo Mei 4 mwaka huu ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars jijini Mbeya.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Balozi Gomile-Chidyaonga, Ubalozi wa Malawi nchini na Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYANI NZEGA, AFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYANI NZEGA, AFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA

May 11, 2014

1 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala wakishiriki katika ujenzi wa jengo la mapokezi OPD la hospitali ya wilaya ya Nzega wakati katibu mkuu huyo alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo katika ziara yake anayoendelea nayo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali inayoshirikisha pia wananchi, pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzipatia au kuzitafutia majawabu, Ndugu Abdulrahman Kinana pia anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi katika ziara hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NZEGA-TABORA) 1a 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nzega leo jioni. 2 

Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akielekeza jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa jengo la OPD katika hospitali ya wilaya ya Nzega, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa. 2a 

Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Nzega leo jioni. 3 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Nzega Dr. Emanuel Mihayo  wakati alipowasili katika eneo ambalo mradi wa ujenzi wa jengo la OPD la hospitali hiyo unaendelea, Kulia ni Mnganga mkuu msaidizi wa hositali hiyo Dr. Amos Petro

  3a 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Nzega. 4 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi ya CCM katika kata ya Nkiniziwa wilayani Nzega leo.  5 

Ujenzi wa  jengo la Hospitali ya wilaya ya Nzega ukiendelea. 6 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akichangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofizi ya CCM kata ya Nkiniziwa, kulia ni mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala akipokea michango mbalimbali. 7Mjumbe wa mkutano mkuuu wa CCM Ndugu Hussein Bashe akimkumbatia mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala mara baada ya kupokea mchango wa fedha taslimu shilingi laki tano kutoka kwa Hussein Bashe kwa ajili ya ujenzi wa ofizi hiyo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia. 10 Mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala akimpongeza Mjumbe wa mkutano mkuuu wa CCM Ndugu Hussein Bashe mara baada ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Nkiniziwa, katikati ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 13 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha nne  shule ya sekondari ya Kampala  Amos Kashindye, mara baada ya kuitembelea shule hiyo na kukagua maabara ya sayansi na fizikia katika shule hiyo. 15 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika mji wa Ndala. 16 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua vikundi vya ngoma. 17 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua moja ya barabara zinazojengwa mjini Nzega kwa kiwango cha lami, kushoto  kwake ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mh. Fatma Mwasa Mkuu wa mkoa wa Tabora. 18 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza moja wa wachimbaji wadogowadogo wa madini kutoka wilayani Nzega Samson Mabula wakati alipotoa malalamiko kwa niaba ya wachimabji wenzake. 19 

Mh. Khamis Kigwangala mbunge wa jimbo la Nzega akiwahutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nzega leo. 20 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM ndugu Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi kwwa viongozi wa kata  pikipiki kwa ajili ya watendaji wa chama cha Mapinduzi. 21 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa vijana.