April 07, 2014
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.  Bernard K. Membe (Mb) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje na Usalama, Bi. Catherine Ashton wakiweka saini  Mkataba wa Kubadilishana Maharamia wanaokamatwa Bahari Kuu. Mkataba huo ulisainiwa mjini Brussels, Ubelgiji hivi karibuni. Mhe. Membe alifwatana  na  ujumbe wa Rais kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Afrika unaofanyika mjini Brussels.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard K. Membe (Mb.) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya wa Mambo ya Nje  na Usalama, Bi. Catherine Ashton wakipeana mkono mara baada ya kusaini mkataba huo.Picha Kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
April 07, 2014

Ballo mwimbaji taarab afariki dunia

140407134217 ballo taarab 304x171 bbc nocredit 1ee21
Mwimbaji maarufu wa taarabu nchini Kenya Muhammad Khamis Bhallo amefariki dunia katika mji wa Mombasa nchini Kenya .
Marehemu Bhallo ambae amefia nyumbani kwake akiwa na umri wa zaidi miaka sitini, kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo hali ambayo ilimlazimu kwenda nchini India mara kadhaa kwa ajili ya matibabu.
April 07, 2014
MAAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBALI NCHINI RWANDA YALIYOADHIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO MAUAJI YALIYOFANYIKA MWAKA 1994 -2014 IMETIMIZA MIAKA ISHIRINI  YANAYOITWA KWIBUKA 20

BAADHI YA WAGENI WALIOFIKA WAKIOMBA

WAGENI WALIOHUDHURIA  DR .SALIM AHMED SALIM  JENERAL ULIMWENGU

WAGENI WALIOFIKA KWENYE MAADHIMIUSHO HAYO

WAGENI WALIOFIKA KWENYE MAADHIMIUSHO HAYO
April 07, 2014

SHOW ROOM YA MAGARI YATEKETEA KWA MOTO MWENGE DAR


 Duka la Magari (showroom) iliyokuwa karibu na eneo la Mlimani City barabara ya Samnujoma jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto na kusababisha hasara ambayo bado haijafahamika, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika.Magari yakiwa yameteketea kwa moto.
Hapa moto ulikuwa ndiyo umeanza kuwaka kabla ya kuanza kuunguza magari.
April 07, 2014

WIZARA YA FEDHA YAWEKA WAZI JINSI ITAKAVYOTEKELEZA MATOKEO MAKUBWA SASA 'BRN'

Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
*************************************************
April 07, 2014

MH. MWANDOSYA AONGOZA MAADHIMISHO YA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA JIJINI DAR


Maandamano yakiwa yameanza kuelekea ukumbi wa Mlimani City
Mmoja ya Waandamaji wa siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda ikiwa imetimia Miaka 20 akiwa amebeba Mwenge Maalum kwa ajili ya Maadhimisho.
April 07, 2014

KINANA, NAPE KUTUA KIGOMA KESHO ASUBUHI


NA BASHIR NKOROMO, KIGOMA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kutua Kigoma kesho, kuanza ziara ya siku tano mkoani hapa.
Ratiba iliyotolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Mohamed Nyawenga, inaonyesha kuwa mapokezi ya Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma, uliopo eneo la Kipampa, Ujiji yatafanyika kuanzia saa 3.00 asubuhi na kumalizika saa 4.00 asubuhi.
Kulingana na ratiba hiyo, baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Kinana ataenda Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma, ambako atafanya shughuli kadhaa ikiwemo kusaini kitabu cha wageni na kupokea taarifa ya Chama, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya mkoa na baadaye kufungua mradi wa maduka.
Baada ya kupumzika  kati ya saa 6. 00 hadi saa 7. 00 mchana, Kinana ataondoka na msafara wake kwa njia ya boti kupitia ziwa Tanganyika, kwenda Hifadhi ya Taifa ya Gombe ambako atatembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kufahamu changamoto na mafanikio zilizopo kwenye rasilimali hiyo ya nchi.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa, Aprili 9, 2014, Kinana atakwenda wilaya ya Kasulu ambako baada ya kusaini kitabu wilayani na kuzungumza na katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya hiyo, atafanya shughuli kadhaa katika Kata mbalimbali.


Kinana anaaza ziara hiyo, baada ya juzi kumaliza nyingine ya siku sita katika mkoa wa Rukwa, ambako katika ziara hiyo alikagua uhai wa chama, utekelezaji wa ilani na Chama na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia za kuzitatua pale zilizpojitokeza.
Wakati huohuo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pia anatarajiwa kutua mkoani Kigoma, kesho asubuhi, kuungana na Kinana kwenye ziara hiyo.

Nape anaungana na Kinana baada ya kumaliza shughuli pevu ya kuratibu kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze. Kampeni hizo zilimalizika juzi na uchaguzi wake kufanyika jana ambapo CCM imeibuka kidedea kwa kuzoa kura nyingi.

Kutokana na theNkoromo Blog kupata fursa ya kuwepo Kigoma, itakuwa ikijitahidi kuwahabarisha hasa kwa picha matukio yatakayoambana na ziara hiyo ya Kinana.