MTOTO AUAWA KIKATILI NA MUUAJI AJIKATA UUME WAKE NA KUULA KAMA KITOWEO
KILIMANJARO mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Francis Fortunatus mwenye umri wa miaka (9) ameuwawa kikatili kwa kukatwakatwa na mapanga kichwani huku mtuhumiwa aliyetenda kosa hilo akijikata uume wake na kisha kufariki dunia. Tukio hilo la kusikitisha limetokea wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 1:00 asubuhi julai 18 mwaka huu katika eneo la marangu kata ya marangu mashariki, jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akielezea mazingira ya tukio hilo la kusikitisha kamanda Boaz, alisema kuwa mtoto huyo akiwa njiani akielekea shuleni gafla alivamiwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Laurance Flavian (20) na kuanza kumkatakata kwa mapanga kichwa bila sababu yeyote na kusababisha kifo cha mtoto huyo papohapo.
Boaz alisema mara baada ya mtuhumiwa huyo kuona kuwa amesababisha mauaji alichukua panga alilo tumia kumkatakata mtoto huyo na kuamua kujikata uume wake mwenyewe.
MANGULA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CAPP JIJINI DAR ES SALAAM
Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akimkaribisha Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan kwenye ofisi Ndogo za CCM Lumumba.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip akiwa kwenye mazungumzo na Katibu
Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan kwenye ofisi
ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam,Julai 18,2014.
Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akiagana na Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan
Makamu
Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akiagana na Balozi wa
Sudani nchini Tanzania Dk.Yassir Mohamed Ali nje ya Ofisi Ndogo za CCM
Lumumba ambapo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) alikuwa na mazungumzo na
Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan.
(Picha na Adam Mzee wa CCM Blog)
WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS-MAZINGIRA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA NIDA
Picha
ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali yanavyotiririshwa toka katika
kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge
akiangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na maji yenye
kemikali yanayotiririshwa na kiwanda cha NIDA. Anayemfuatia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC Bonaventura Baya, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete.
Jengo la kiwanda cha NIDA likionekana kwa nje
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge
akiongea na Menejimenti ya kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA
Textiles kuhu kiwanda hicho kinavyoharibu mazingira kwa kutiririsha maji
yenye kemikali katika mto kibangu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith
Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake aliyoifanya
katika kiwanda cha NIDA textiles jijini Dar es Salaam
…………………………………………………
Rai imetolewa kwa wawekezaji wote
Nchini kuhakikisha wanajali na kutunza Mazingira.Hayo yamesemwa jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Binilith
Mahenge wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza
nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela katika kata ya Kigogo jijini
Dar es Saalam.
Kiwanda hicho ambacho
kinalalamikiwa na wananchi kuwa kinatiririsha maji machafu yenye
kemikali katika mto kibangu uliopo pembeni ya kiwanda hiko ambako
wananchi wanalima mbogamboga kando yamto huo na wanatumia kula pia
wanauza ili kujipatia kipato pasipo kujali athari zilizopo kwenye maji
hayo yenye kemikali.
Akiongea na Menejimenti ya kiwanda
hiko Dkt. Mahenge baada ya kutemebelea mto huo na kujionea maji
yalivyoathiriwa na kemikali zitokazo kiwandani, aliitaka Menejimenti ya
kiwanda hiko kuacha mara moja kutiririsha maji yenye kemikali katika mto
kibangu na hivyo basi kuchukua hatua za kitaalamu ili kuondoa kemikali
zilizopo kwenye maji hayo.
Akiongea kwa niaba ya Menejimenti
ya Kiwanda Afisa Utawala Mohammed Olewo aliahidi kwamba watafanyia kazi
maagizo ya Waziri kwa ufasaha na wanaahidi watarekebisha makosa yote
yaliyotokea pia watadumisha na kutunza mazingira.
Ziara hiyo ni moja ya ziara za
Waziri anazofanya kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
kwa ajili ya kukagua utunzaji wa mazingira.
RAIS AFUTARISHA WANANCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (wa nne kulia) akijumuika na waislamu na Viongozi katika swala ya
Magharibi katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu kabla ya futari
aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (katikati) akijumuika na Viongozi katika futari aliyowaandalia
wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana katika viwanja vya Ofisi ya
Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi
wa Mkoa wa Kusini Unguja kwa pamoja wakijumuika katika fuitari
iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji
Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Naibu
Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na MIchezo Bihindi Hamadi Khamis (wa
pili kulia) akijumuika na Viongozi wengine katika futari iliyoandaliwa
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali
Mohamed Shein kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Ukumbi wa
Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini jana.
Akinamama wa Mkoa wa Kusini Unguja wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini jana.
Akinamama wa Mkoa wa Kusini Unguja wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini jana.
[PICHA ZOTE NA RAMADHAN OTHMAN<IKULU]
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ANGELLAH KAIRUKI AKIFANYA MAJUMUISHO YA WIZARA YAKE ALIYOIFANYA WIKI HII
Mkurugenzi
mkuu wa kituo cha haki za binadamu Hellen Kijo Bi. Simba(LHRC) (kulia)
akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria baada ya
kutembelea Taasisi zinazoshughulikia msaada wa kisheria jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiongea na
wanahabari(hawapo pichani) kutoa maelezo ya majumisho ya ziara yake ya
siku tano ya kuzitembelea Taasisi zinazotoa Huduma ya Msaada wa Kishria
Mkoani Dar es Salaam.
Picha na Rose Masaka-MAELEZO.
WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU JIMBONI KWAKE NACHINGWEA LEO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha
Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza
kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu
2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze
Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya
Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na
kuzinduliwa. Picha zote na Felix Mwagara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Mwaka 2014, Rachel Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru
uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia Wilaya ya Nachingwea. Wapili
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo ambaye ndio
aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi
wa Nyumba ya Mganga katika Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru
ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya
Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa
katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo
itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji)
akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Regina Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya
maji baada ya kufungua mradi wa maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya
ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwa
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu
2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze
Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo
ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya
kukabidhi Bajaj kwa walemavu na Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata
mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli za maendeleo
katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo
wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria
Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya”
utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya
maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea. Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na zote na Felix Mwagara.
*MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBO LA CHALINZE, SASA NI ZAMU YA JESHI LA POLISI
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa
polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na
wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali
kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha
vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali
yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya
ulizni na usalama wa raia na mali zao.
Pamoja
na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu
pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi
vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya shilingi
milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich
Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye
kituo kikuu cha polisi Chalinze.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi
mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na
mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la
Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S.
Magomi.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili
kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na
jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya
kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Kamanda
wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa
akitoa shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara
baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa ituo cha
polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa
shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa
akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la
kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.
Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.
Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.
Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wanafunzi
wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua
ujenzi wa shule hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi
wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze
Bw. Ahmed Nasser.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya
shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser
mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.
Diwani
wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbune
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la
polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo.
MKUU WA WILAYA JORDAN RUGIMBANA VITAMBULISHO KINONDONI
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Jordan Rugimbana leo amezindua rasmi utoaji wa Vitambulisho
vya Taifa kwa wananchi Wilaya ya Kinondoni, na kuwa mtu wa kwanza
kupokea kitambulisho chake mbali na kuwakabidhi wananchi 22 Vitambulisho
vyao kutoka Kata ya Saranga mtaa wa Matangini.
Hapa anamkabidhi mmoja wa wananchi
Bi. Chiku Issa Waziri kitambulisho cha Taifa, akishuhudiwa na Maafisa
Usajili katika Wilaya Bw. Dickson Mbanga Weiss na Bw. Abdulrahman Muya
(1505)
Mkuu wa Wilala ya Kinondoni
akiwasili leo katika Kata ya Saranga Mbezi tayari kuzindua zoezi la
utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Kata ya Saranga, Mbezi
Dar-es-salaam (1462)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan
Rugimbana akikabidhiwa Kitambulisho chake na Afisa Usajili Wilaya ya
Kinondoni Ndugu Abdulrahman Muya baada ya kukamilisha hatua za mwisho za
uhakiki leo Kata ya Saranga Mbezi Dar-es-salaam. Kushoto ni Bw. Dickson
Mbanga Weiss Afisa Usajili Kinondoni. (1470)
Mmoja wa wananchi wa Kata ya
Saranga akiongozwa na Afisa Usajili wa NIDA kukamilisha hatua za mwisho
za kuhakiki taarifa zake kabla ya kukabidhiwa kitambulisho chake leo,
Kata ya Saranga Mbezi.(1505)
ZIARA YA WAZIRI WA FEDHA, MHE. SAADA MKUYA KATIKA MANISPAA ZA ILALA, KINONDONI NA TEMEKE.
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Stima Kabikile (katikati)
akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) wakati
alipofanya ziara yake ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Kinondoni
na Temeke kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na utendaji
kazi wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha
namna ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya (kulia) Ilala akimsomea
taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na mikakati yake ya kufikia
malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe. Waziri wa Fedha Bi. Saada
Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Temeke na
Kinondoni.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo
yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano
na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo
yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano
na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akiongozana na viongozi wa Manispaa
ya Kinondoni wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa
hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi
za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni
wananchi. katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Bw. Yusuph Mwenda
na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kulia) akisalimiana na
Waziri waFedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) mara alipowasili katika ofisi
za Manispaa hiyo kwa ziara ya kikazi katika jana kwaajili ya kupata
taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo zikiwemo njia wanazotumia kukusanya
kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya
ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni
wananchi.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia) akihutubia mkutano huku akisisitiza
juu ya kujikita zaidi katika kutumia TEHAMA katika kukusanya kodi za
majengo kama njia rahisi inayomrahisishia mlipaji kodi kuweza kulipa
kodi zake katika vituo vya huduma.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akipitia moja ya taarifa alizopewa na
uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni wakati alipofanya ziara yake
ya siku moja ofisi hapo.
……………………………………………………………………….
Na Rose Masaka.
WAZIRI
wa Fedha Bi. Saada Mkuya amefanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya za
Mkoa wa Dar es Salaam ili kupata taarifa za makusanyo ya kodi za
majengo ikiwa ni eneo moja kati ya maeneo sita ambayo yamepewa
kipaumbele katika suala la ukusanyaji wa kodi kama vile eneo la kilimo
na miundombinu.
Bi.
Saada Mkuya amesema kuwa aliahidi kufanya ziara hiyo katika kikao
kilichofanyika wiki iliyopita baada ya kurudisha zoezi la ukusanyaji wa
kodi za majengo katika Serikali za Mitaa ili kuona kinachoendelea,
kupata uhalisia na changamoto zinazowakabili watendaji wote wa Manispaa
ya Ilala, Kinondoni naTemeke.
“Tumerudisha makusanyo ya kodi za majengo kwenye mitaa kwasababu ni rahisi na wanajua nyumba zote” alisema Bi. Mkuya.
Kodi
ya majengo imekuwa ni moja ya chanzo kikubwa kinachotegemewa na
Halmashauri za wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam. Serikali iliona
hili mnamo mwaka 2013 na kuteua chanzo hiki kuwa mfano katika mpango
wake wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Kwa
upande wake Mweka hazina wa Wilaya ya Ilala Bw. Stima Kabikile amesema
kuwa Halmashauri ya Illala kupitia kitengo chake cha uthamini kwa
kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa wamejiwekea malengo ya
kuyatambua majengo 10,000 ambayo hayakuwepo katika jedwali la awali kwa
kutumia njia rahisi ya haraka ya uthamini.
“Tumeweza
kubaini na kuongeza idadi ya majengo 6,820 kati ya 10,000 tuliyokadiria
yenye thamani ya Shilingi bilioni 989.6 yenye tozo ya kiasi cha
shilingi trilioni 1.5 na kuweka kwenye mfumo tayari kwa malipo”. Alisema
Bw. kabikile.
Mtaalamu
wa kodi za majengo Wilaya ya Ilala Bw. Joseph Kawiche amesema kuwa kila
mmiliki wa nyumba hulipa kutokana na asilimia zake ingawa kuna baadhi
ya watu ambao hawajaona umuhimu wa suala hili na kuwa wanafichiana
majina,kwa hiyo wameona ni vizuri kutumia njia mbadala ya picha ili
kuwabaibni wanaokwepa kulipa kodi.
Kwa
upande wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Wilaya hiyo Bw.
Yusuph Mwenda amesema kuwa ameona umuhimu mkubwa wa kutumia Serikali za
Mitaa na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti ili
kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu kulipa kodi za majengo.
“Wenyeviti
wa mitaa 171,watendaji wa Kata 34 na Watendaji wa Mitaa 171 wanashiriki
na kuainisha majengo yaliyoachwa wakati wa uthamini”. Alisema Mwenda.
Mkurugenzi
wa wilaya ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa jumla ya
Shilingi bilioni 1.1 zimekwishakusanywa katika majengo 3123,aidha
majengo 3120 yaliyobakia yenye wigo wa kodi bilioni 1.4 yao katika hatua
nzuri ya ulipaji.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke amesema kuwa
Halmashauri imekusanya kiasi cha shilingi milioni 165.7 kutokana na
majengo ambayo awali hayakuwepo katika daftari la majengo ambapo mapato
yanatarajiwa kuongezeka kwa hali ya juu katika mwaka huu wa fedha baada
ya majengo yote 10,000 kuthaminiwa.
Baadhi
ya changamoto zinazozikabili Wilaya hizo ni pamoja na waraka wa msamaha
wa kulipa kodi ya majengo wakati sheria ipo kimya wakati wanamiliki
majengo ya makazi,kupangishana biashara ambao raia na wanajeshi
wastaafu wanao,pia shule binafsi kudai kutoa huduma wakati ada zao zipo
juu, hivyo Manispaa zote tatu zimetoa wito kwa wananchi wa Tanzania
kulipa kodi kwa hiari na Serikali iweke wazi sheria za misamaha kama
zipo.
Subscribe to:
Posts (Atom)