MKIKITA WAMLAKI KWA SHANGWE MFILIPINO MTAALAMU WA MASOKO

October 20, 2017
 Mtaalamu wa masuala ya Masoko kutoka Ufilipino, Dk.Wenfredo Muni akikabidhiwa zawadi ya maua na Meneja Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Neema Fredrick wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam  jioni hii. Aliyevaa fulana ya njano ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na Mdau Haji Mohamed. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk Muni akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth akimsalimia Dk. Muni
 Waziri wa zamani wa Afya, Dk. Rashid Seif akisalimiana na Dk. Muni
 Dk. Rashid Seif akikumbatiana kwa fura na Dk. Muni wakati wa mapokezi
 D. MUni akifurahia zawadi ya shada la maua

‘HALMASHAURI ZIMUUNGE MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA VITANDA VYA KUJIFUNGULIA’, DKT NCHIMBI.

October 20, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akifungua moja kati ya vitanda 14 vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
 Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa vitanda vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Aisharose Mattembe akizungumza na wauguzi, madaktari na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) mkoa wa Singida kabla hajakabidhi vitanda 14 alivyopewa na Rais Magufuli ili avifikishe kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Emmanuel Kimario akimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia vitanda vya kujifungulia ili kupunguza uhaba wa vitanda kwa Mkoa was Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaidiana na wataalamu wa afya pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Aisharose Mattembe kufunga moja kati ya vitanda 14 vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Halmashauri saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kununua vitanda kumi kwa ajili ya akina mama kujifungulia ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli za kuboresha afya ya mama na mtoto.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo mapema leo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupokea vitanda vya kujifungulia 14, magodoro 20 na mashuka 50 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 121 kutoka kwa Rais Magufuli.

Dkt Nchimbi amesema halmashauri zinatakiwa kuiga mfano wa Rais Magufuli anayojali afya kwa ajili ya wananchi hivyo wanapaswa kutenga kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu kwa ajili ya kununua vitanda hivyo kwa mwaka huu wa fedha.

“Tumezoea kupokea tu na tumepokea sana vifaa tiba kutoka kwa rais wetu mpendwa Magufuli, hebu tujifunze upendo wake kwa wananchi, hivyo naagiza kila halmashauri inunue vitanda kumi vya kujifungulia nadani ya mwaka huu wa fedha”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Amengeza kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya kwakuwa kuna huduma bora zaidi huku akiwataka wakunga wa jadi wawasaidie wajawazito kufika katika vituo hivyo.

Aidha Dkt Nchimbi amemshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Singida Aisharose Mattembe aliaminiwa na Rais Magufuli na kumtuma kufikisha vitanda hivyo Mkoani Singida huku akimtaka kuanzisha tunzo ya wakunga watakaosaidia kufikisha akina mama wajawazito katika vituo vya kutolea huduma za afya.
IAWRT yavitaka vyombo vya habari nchini kuwa na sera ya jinsia

IAWRT yavitaka vyombo vya habari nchini kuwa na sera ya jinsia

October 20, 2017
Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) imevitaka vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi katika vyombo hivyo. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa IAWRT nchini, Rose Mwalimu katika mafunzo yaliyotolewa na chama hicho kwa waandishi wa habari wa vituo vya runinga, redio na mtandaoni kuhusu sera ya jinsia katika vituo vyao vya kazi. Mwalimu alisema katika kusaidia kuwepo na sera ya jinsia wameandaa mafunzo hayo ambayo yanalenga kusaidia kukuza sera ya jinsia katika maeneo ya kazi kwa wanahabari jambo ambalo litasaidia kuboresha vipindi vinavyorushwa kwani hata uandaaji wake utakuwa unahusisha jinsia zote. Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) nchini, Rose Mwalimu akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoandaliwa na chama hicho. "Haya mafunzo ya leo ni njia mojawapo ya kukuza sera ya ujinsia katika vyombo vya habari, utekelezaji wake huwa ni katika kutafuta watu ambao ni watangazaji ambao wao ndiyo watakuwa kama wasimamizi ambapo kupitia wao watatengeza vipindi ambavyo vitakidhi sera ya jinsia inavyotaka ili na wengine waige, "Lengo ni kuwa na vipindi bora na sio tu vipindi bora lakini vipindi bora ambavyo vitakuwa na tija katika jamii ... tatizo wafanyakazi wengi hawajui haya madhara kama hakuna utekelezaji wa sera ya jinsia, madhara yapo kwa namna mbili, kwa wafanyakazi wao wenyewe na kwa wasikilizaji na watazamani, kwako kutokuwa na sera kama hushirikihi hizi jinsi mbili hata huo uhuru wa kupeana habari unakuwa haupo," alisema Mwalimu. Alisema kuwa takwimu za utafiti walioufanya mwaka 2014 zinaonyesha kuwa ni vyombo vya habari vichache ambavyo vina sera ya jinsia hivyo hata uwiano wa madaraka katika vyombo hivyo unakuwa upande mmoja wa wanaume. “Utakuta hata vyombo vya habari wakurugenzi na wahariri wakuu ni wanaume sasa wanawake wapo wapo na wanafanya nini?, wanawake wengi watangazaji wanapewa habari zinazowahusu wao wenyewe lakini hawashirikishwi vya kutosha katika habari za maendeleo," alisema Mwalimu.
Gladness Munuo akiwasilisha mada mbalimbali katika mafunzo kwa wanahabari kuhusu sera ya jinsia.
Baadhi waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sera ya jinsia.
Washiriki katika picha ya pamoja.

Buku ya Sokabet yampa milioni 2 fundi magari

October 20, 2017


Na Mwandishi Wetu
MKAZI wa Mikumi mkoani Morogoro, Frank Chodaus amekuwa ni mmoja wa wanaonufaika na mchezo wa kubashiri matokeo kutoka kampuni ya Sokabet baada ya kujishindia shilingi milioni 2 baada ya kubashiri kwa kutumia shilingi 1000 tu.

Ndani ya tovuti ya kampuni hiyo ya Sokabet kila wiki huwa kuna kipengele kinachowawezesha washiriki kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kubashiri matokeo kwa shilingi elfu moja tu, ambapo ndipo huko Frank aliponufaika.

Akizungumza juu ya ushindi huo mratibu wa Kampuni ya Sokabet, Franko Ruhinda alisema mshindi huyo alipatikana wikiendi iliyopita baada ya kupatia michezo 11 kati ya 13 ambayo alitakiwa kupatia kwenye kipengele hizo cha Jackpot.

“Unajua kama ambavyo tumekuwa tukishauri watu kuendelea kujiunga na kushiriki katika Sokabet, ndani ya muda mfupi wanaweza kujiingizia mamilioni kwa kuweka fedha kidogo tu katika ubashiri wao, ushindi wa Frank ni mfano tu wengi wanaojishindia ndani ya tovuti yetu,” alisema Franko.

Alipowasiliana na mwandishi wa habari hii, mshindi huyo alisema ilikuwa ni furaha kwake kupata fedha hizo kwa kuwa hakutegemea lakini ni jambo muhimu kwa kuwa fedha hizo zimemwezesha kutatua matatizo yake mengi.

Akifafanua zaidi alisema: “Mimi ni fundi magari na nimekuwa nikishiriki sana katika michezo hii ya kubet, sasa Sokabet ilivyoanzishwa kwanza sikujiunga kwa kuwa nilikuwa sijapata elimu vizuri, baada ya kufatilia magazeti ndipo nikawajua vizuri na kujiandikisha.

Nilipojiandikisha nikaanza kubet mdogomdogo, mwanzoni sikupata, lakini kila wiki nimekuwa nikibet katika vipengele tofauti kikiwemo kipengele cha Jackpot.

“Sasa wiki iliyopita, nilibet kama kawaida kwa buku (Sh 1,000), baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu, sikufuatilia majibu kwa kuwa mechi nyingi ziliisha usiku wa Jumamosi.

“Kawaida huwa nikibet kama hivyo nasubiri kuona kama nitapata ujumbe, nikiona sijapata dnipo nafungua akaunti yangu ya kubet na kuangalia nilipokosea,

“Sasa Jumapili nikashtukia nikipata ujumbe kuwa nimeshinda shilingi milioni 2, ilikuwa furaha kubwa kwangu kwa kuwa sikutegemea na unajua wakati mwingine hivi vitu ni bahati.”

Aliongeza kwa kusema haya: “Hicho kipengele mtu anatakiwa kupatia michezo 13 ambapo kama ningefanikiwa hivyo maana yake ningepata milioni mia, na kama ningepatia michezo 12 ningepata milioni tano, ila mimi nilipatia michezo 11.”

Kuhusu matumizi ya fedha hizo, fundi huyo ambaye ana umri wa miaka 25 alisema zilimsaidia katika matumizi yake lakini ataendelea kubet kwa kuwa anaamini anayo nafasi nyingine ya kupata mzigo mkubwa zaidi ya alioupata mwanzo.

DKT MWANJELWA: TUMIENI USHIRIKA KUPIGA VITA ADUI NJAA, UJINGA, MARADHI NA UMASKINI

October 20, 2017
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akiangalia sehemu ya bidhaa za chakula zilizosindikwa kutoka katika Vikundi vilivyoanzishwa chini ya  Ushirika wa Akiba na Mikopo wa TANESCO (TANESCO - SACCOS) katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani DodomaNaibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akinunua dagaa walioongezwa thamani kutoka kwa kina Mama wa MWACIWOTE SACCOS ya  Jijini Mwanza. SACCOS hiyo imeundwa na kina Mama Waalimu wa Shule za Msingi na SekondariMgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akipa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Ngome SACCOS Brigedia Jenerali Charo Hussein Yateri namna ambavyo inajiendesha kwa mafanikio makubwa ikiwa na Wanachama zaidi ya 12,500 nchini katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani DodomaMgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akipa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa TANESCO SACCOS Bibi Somoe Ismail namna ambavyo inajiendesha kwa mafanikio makubwa ikiwa na Wanachama zaidi ya 5,612 nchini kote katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa amewataka Washiriki wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), kuvitumia Vyama hivyo kama silaha ya kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo ya kweli.
Dkt. Mary Mwanjelwa ambaye ndiye mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha Uanzishwaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo amesema hakuna ubishi kuwa mafanikio yaliyopatikana kupitia Vyama hivyo yanadhihirisha kuwa ni njia madhubuti ya Wananchi katika kupambana na adui njaa, ujinga, maradhi na umaskini.
Dkt. Mwanjelwa amekaririwa akisema “Nimetembelea mabanda kadhaa ya Vyama vya Akiba na Mikopo kutoka Taasisi za Umma kama Ngome SACCOS, TANESCO SACCOS, Bandali SACCOS, wameniambia kiasi cha mitaji waliyonayo ni unazungumzia mabilioni ya Shilingi za Kizanzania, ambapo Wanachama wanakopeshana kwa riba nafuu na kwa muda mzuri”
“Jambo hilo linatia moyo na niwaombe Viongozi na ninyi Wanachama ambao mmejiunga kwenye Vyama vya Akiba na Mikopo kuwahamasisha wengine kujiunga na Vyama vya Akiba na Mikopo ili tuongeze wigo wa idadi kubwa ya Watanzania”. Amekaririwa Naibu Waziri.
“Na kama Watanzania wengi watajiunga basi tutakuwa na nafasi kubwa kama Taifa kupambana na maadui hawa watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini”. Amekaririwa Naibu Waziri Dkt. Mwanjelwa.
Aidha, Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameuagiza Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Bwana Tito Haule, kuhakikisha anaitumia nafasi ya kuelimisha umma kuhusu faida na uzuri wa USHIRIKA kupitia Vyama vya Kuweka na Kukopa kama ndiyo silaha ya kupeleka mbele maendeleo ya Ushirika nchi.
“Mrajis elimu kwa Umma ni jambo la muhim sana, hata kama mnafanya mambo mazuri lakini kama Wananchi hawatafahamu kuhusu faida na mambo mazuri yanayohusu kujiunga na Vyama vya Akiba na Mikopo itakuwa ni kazi bure, fanyeni kila linalowezekana ili kuwaelimisha Watanzania”.
Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa USHIRIKA pia ni njia ya kuongeza tija na uzalishaji katika mazao ya kilimo na kwa njia hiyo, uzalisahaji wa mazao ya kilimo kwa ajili ya viwanda vya kati na vikubwa unaweza kuongezeka kwa kutumia Vyama vya Akiba na Mikopo.
“Msisahau kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia katika kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa viwanda na Watanzania wengi wanaojihusisha na Sekta ya Kilimo ni zaidi ya asilimia 75 kwa maana hiyo, Vyama vya Akiba na Mikopo pia vitumike katika kuongeza tija na uzalishaji wa malighafi za viwanda vya usindikaji vidogo, vya kati na vikubwa”. Amemalizia Dkt. Mary Mwanjelwa.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) yalianza rasmi jana tarehe 18 Oktoba na yanafikia kilele leo tarehe 19 Oktoba, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Mjini Dodoma.

DC MTATURU AFUNGUA MKUTANO JUU YA MAOMBI YA KUREKEBISHA BEI ZA HUDUMA YA MAJI WILAYANI MANYONI

October 20, 2017

Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua  wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Baadhi ya wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wakifatilia Mkutano
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua  wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira. (Picha Zote Na Mathias Canal)