SPIKA WA BUNGE, NAIBU SPIKA WAKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA

SPIKA WA BUNGE, NAIBU SPIKA WAKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA

November 07, 2016
duga1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke aliyemtembelea mapema leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine waliyozungumza Balozi huyo alimpa Mhe Spika pole kufuatia Kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta .
duga2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  (kushoto) akimsikiliza  Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke  wakati akizungumza naye Ofisini kwake Mjini Dodoma.
duga3
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimueleza jambo  Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke aliyemtembelea mapema leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
duga4
  Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke aliyemtembelea mapema leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
duga5
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza  Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke  wakati akizungumza naye Ofisini kwake Mjini Dodoma.
duga6
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana kwa dharura kujadili kuhusu hoja ya kuahirisha Bunge kufuatia kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa Marehemu Samwel Sitta ambapo Kikao hicho kiliridhia Bunge liahirishwe ili Waheshimiwa Wabunge wapate muda wa kuomboleza kufuatia Msiba huo.
   
           Picha na Ofisi ya Bunge.

BENKI YA TWIGA YATOKA KIFUNGONI ITAANZA KUTOA HUDUMA ZAKE KESHO

November 07, 2016
Gavana wa Benki Kuu. Profesa Beno Ndulu.


Na Dotto Mwaibale

BENKI ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga)ambayo ilikuwa imefungwa kwa muda na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itaanza kufanya kazi baada ya mchakato wa kuifanyia tathmini ya kifedha kukamilika.
 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana benki hiyo itaanza kutoa baadhi huduma za kibenki kwa umma kuanzia kesho Novemba 8, 2016. 

"Kwa mamlaka iliyopewa kisheria kupitia kifungu namba 58(2) (a) na (b) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu inapenda kuutarifu umma kwamba zoezi la tathmini ya hali ya kifedha ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) limekamilika; kwa mantiki hiyo, Twiga itaanza kutoa baadhi huduma za kibenki kwa umma kuanzia Jumanne tarehe 8 Novemba 2016" ilisema taarifa hiyo. 
Huduma hizo ni pamoja na ukusanyaji wa marejesho ya mikopo ya wateja. Meneja Msimamizi wa benki hiyo atawajulisha wateja huduma zitakazotolewa na taratibu za kuzingatia. 

Benki Kuu ipo katika mchakato wa kupitia na kuchambua njia mbadala za kutatua tatizo la mtaji linaloikabili Twiga Bancorp. 
Njia inayopewa kipaumbele ni kutafuta mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya, mchakato utakaowahitaji kuchambua hali halisi ya taarifa za hesabu za Twiga (due diligence). 

Zoezi hilo linatarajiwa kuchukua takribani wiki tatu na litakapokamilika, Benki Kuu itaingia makubaliano na wawekezaji wapya kuhakikisha wanaingiza mtaji unaohitajika haraka iwezekanavyo ili shughuli za kawaida za kibenki ziweze kuendelea.

Benki ya Twiga itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu hadi hapo utaratibu wa kuwamilikisha wawekezaji wapya utakapokamilika. 

Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuiweka Twiga Bancorp Ltd chini ya usimamizi wake kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016 kutoka na upungufu mkubwa wa mtaji unaoikabili.

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha ilieleza taarifa hiyo. 


MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA KITUO CHA HUDUMA SHIRIKISHI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

November 07, 2016
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure, hii leo.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pact Tanzania
Viongozi mbalimbali
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza na wanahabari ambapo amesema kituo hicho kitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Sekour Toure
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka maafisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na askari polisi kitengo cha dawati la jinsia, kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati akifungua kituo cha huduma Shirikishi dhidi ya Ukatili wa kijinsia na watoto cha One Stop Centre kilichojengwa na taasisi ya Pact Tanzania kwa ufadhiri wa watu wa Marekani, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Amesema hatua za kukabiliana na ukatili wa kijinsia zinapaswa kuchukuliwa mapema badala ya kusubiri utokee katika jamii ambapo amesema watakaokuwa wakipatikana na hatia za kujihusisha na ukatili wa aina hiyo watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sekour Toure, Dkt.Leonard Subi, amesema kituo hicho kitajumuisha watumishi mbalimbali ikiwemo polisi, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kinjinsia ambavyo bado vimeshamiri mkoani Mwanza.

Amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba, wananchi 238 mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za ukatili wa kijinsia katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya na kati ya hao 77 ni ukatili wa watoto. Kituo hicho tayari kimehudumia watu wazima 30 waliolengwa na ukatili wa kijinsia huku watoto wakiwa ni 67.

Naye Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi milioni 80 ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa na mafunzo ambapo kinakuwa kituo cha nane nchini miongoni mwa vituo vya One Stop Centre.
DKT. POSSI AIPONGEZA UNESCO KUPUNGUA KWA UKATILI DHIDI YA ALBINO

DKT. POSSI AIPONGEZA UNESCO KUPUNGUA KWA UKATILI DHIDI YA ALBINO

November 07, 2016
Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu watu wenye ualbino pamoja na kufanya tathmini jinsi wananchi walivyo na uelewa kuhusu watu hao.

Dk. Possi ameyasema hayo katika mkutano wa kuelezea tathmini ambayo imefanywa na UNESCO kwa wananchi wa wilaya nne ambazo tathmini ilifanyika na kusema kuwa ni jambo zuri ambalo limesaidia kuonyesha hali jinsi ilivyo na ni njia gani ambayo serikali inaweza kutumia ili kumaliza vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino.

"Watu wenye ualbino wamekuwa wakiteseka kwa kipindi kirefu, wanakosa nafasi ya kusoma, kufanya biashara na mambo mengi yanawakabili, watu wa mashirika sio suluhisho ni jamii yenyewe, watu wengi bado hawana elimu ya kutosha kuhusu ualbino,

"Inabidi ifike hatua watu wenye ualbino waishi sawa na watu wengine na serikali imekuwa ikifanya jitihada kumaliza vitendo hivyo lakini inabidi jamii itambue hili sio jukumu la serikali peke yake ni muhimu kila mmoja akashiriki kuvitokomeza vitendo vya ukatili, UNESCO imetuonyesha njia ya kuiwezesha serikali kufanikisha nia yake," alisema Dkt. Possi.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi kutoa hotuba kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Kwa upande wa UNESCO kupitia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema UNESCO imnatambua kila mwanadamu ana haki ya kuishi kama binadamu wengine na kupitia utafiti wao ambao uliambatana na kutoa elimu wanaamini kuwa ni muda wa jamii kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya kikatili kwa maalbino.

"UNESCO imeamua kujihusisha sana na hili jambo na kujitahidi kutoa elimu kwa jamii, tumeanza kulifanyia kazi jambo hili la kikatili kwa maalbino na mashambulizi ambayo wamekuwa wanakutana nayo sababu ya imani za kishirikina ambazo ni kinyume na haki za kibinadamu,

"Utafiti huu utaweza kusidia kumaliza vitendo vya kikatili kwa watu wenye ualbino, kila mtu ana haki za kimsingi na hilo ndilo ambalo UNESCO inalisimamia, na katika kufanikisha hili kila mtu katika jamii kwa nafasi yake ana wajibu wa kushiriki kumaliza vitendo hivi, ni lazima kushirikiana kumaliza jambo hili," alisema Rodrigues.

Tathmini hiyo imefanyika katika wilaya nne ambazo ni Misungwi na Sengerema kwa Mwanza, Msalala iliyopo Shinyanga na Bariadi mkoani Simiyu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza katika mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akitoa neno kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kiongozi mkuu wa tathmini hiyo, Dkt. Nandera Mhando akiainisha mambo muhimu yaliyobainika kwenye tathmini wakati mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt akitoa maoni kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp.
Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp akizungumza jambo kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr. Qasim Sufi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifafanua jambo kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni Sehemu ya washiriki wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwemo wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.



Mshehereshaji wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism), Mathias Herman akiendesha mjadala kwa washiriki katika mkutano huo uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt (wa pili kushoto), Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr. Qasim Sufi wakati wakijiandaa na zoezi la picha ya pamoja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.