JOSEPHINE MGAZA AGOMBEA VITI MAALUM TANGA

July 21, 2015

Mgombe ubunge viti maalumu mkoa Wa  Tanga.
Wanawake ni nguzo ya maendeleo.
 ………………………..
DHAMIRA YANGU
1. Kuwaunganisha wanawake wote Wa mkoa Wa tanga
2. Kujenga jumuiya imara ya UWT. 3. Kusaidia na kuboresha
maisha ya wanawake Wa makundi     
    mbalimbali
4. Kuwa mtetezi na mwakilishi Wa wanawake katika masuala
ya kijamii na kiuchumi.
5. Kusaidia uanzishwaji Wa miradi ya kiuchumi ili
kupambana na umasikini.
6. Nitakuwa mtumishi wenu
na sio kiongozi. Nichague Mimi nikawatumikie kwa manufaa ya wanawake    
     Wa mkoa Wa
Tanga.
Daima wanawake ni nguzo ya  jamii.
** Chagua Josephine Mgaza***
 MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA 9 WA WAKE WA MARAIS KUHUSU KANSA HUKO NAIROBI.

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA 9 WA WAKE WA MARAIS KUHUSU KANSA HUKO NAIROBI.

July 21, 2015


1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta huko Nairobi kuhudhuria  mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume tarehe 20.7.2015.
PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa nchi za Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyetta (hayupo pichani) tarehe 20.7.2015.
4
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na wake wa Marais kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Kenya ukiimbwa.
5
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa amesimama na baadhi ya wake wa Marais wa Afrika wakati wimbo wa Mataifa ya Afrika ukiimbwa. Kushoto kwa Rais Kenyatta ni Mkewe Mama Margret Kenyatta akifuatiwa na Mke wa Rais wa Namibia Mama Monica Geingos, Mama Salma Kikwete na mwisho ni Mama Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wa Niger.
6
Baadhi ya Wake wa Marais wa Nchi za Afrika wakishiriki kumvisha mkanda maalum kwa kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Hiari kwenye Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika. Wanaomvisha mkanda huo kwa niaba ya wake wa Marais ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa ‘Forum of African First Ladies against Cervical, Breast and Prostate Cancer, Mama Dkt. Lalla Mahammadou wa Niger, Mama Monica Geingos wa Namibia, Mama Mary Ayen Mayardit wa Sudan Kusini. Mama Salma Kikwete na Mwisho ni Mama Mathato Mosisili wa Lesotho.
2
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Afrika wakifuatilia kwa makini sherehe za ufunguzi.
     7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi wa Forum of African First Ladies Against Cervical, Breast and Prostate cancer mara baada ya viongozi hao kutembelea Hospitali ya HH Aga Khan jijini Nairobi tarehe 20.7.2015.

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA KILICHOJENGWA NA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL.

July 21, 2015

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.
DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.


‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

July 21, 2015
IMG_9354
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
IMG_9341
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
IMG_9348 IMG_9317
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.