Waziri Mkuu awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

December 21, 2014

index
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili jijini Doha, Qatar jana usiku (Jumamosi, Desemba 20, 2014) kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza leo.
Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia fursa za kiuchumi na miradi mikubwa inayoweza kuzinufaisha nchi hizo na nje ya mipaka yake kwenye Ghuba ya Arabuni (Arabian Gulf) na bara la Afrika.
Vile vile Waziri Mkuu anatarajiwa kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta za uchimbaji gesi na mafuta, usindikaji mazao, uvuvi na mifugo, ajira na uendelezaji miundombinu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. Vilevile atakutana na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa nchi hii. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.
Vilevile Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Atatembelea pia Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.
Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali na wakuu wa taasisi za TPSF na TPDC.
Rais Kikwete atunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi

Rais Kikwete atunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi

December 21, 2014

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha D92A3118 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha D92A3178 
Rais Kikwete akitunuku Kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha Jeshi huko Monduli Mkoani Arusha leo.Jumla ya maafisa 171 walitunukiwa kamisheni wakati wa hafla hiyo.
(picha na Freddy Maro).
MAAFISA WA POLISI WATAKIWA KUDUMISHA NIDHAMU

MAAFISA WA POLISI WATAKIWA KUDUMISHA NIDHAMU

December 21, 2014

indexNa Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.
Maafisa, Wakaguzi,  na Askari wa Jeshi la Polisi hapa nchini, wametakiwa kudunisha nidhamu wakati wote, kutenda haki kwa kila mmoja na kuwaheshimu wananchi wa rika zote bila ya kujali dini, rangi ama itikadi zao kisiasa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, SACP Ali Lugendo, wakati akizungumza na Wanafunzi wa Mafunzo ya Uofisa (Mrakibu Msaidiizi wa Polisi) na wale wa cheti na Stashahadi ya Sayansi ya Polisi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kamanda Lugendo amesema kuwa pamoja na kufundisha masomo ya sheria na haki za binadamu, lakini kazi kubwa inayofanywa na chuo chake ni kusisitiza nidhamu kwa kila afisa na askari wanaofika chuoni hapo.
Amesema kuwa nidhamu ni somo la kwanza analofundishwa askari anapokuwa katika mafunzo ya awali kwenye chuo cha Polisi Moshi kwani amesema nidhamu ni msingi wa kwanza kwa majeshi yote duniani.
“Hakuna Jeshi lolote duniani, likiwemo Jeshi letu la Polisi hapa nchini ambalo haliendeshi kwa misingi ya nidhamu”. Alisema Kamanda Lugendo na kuongeza kuwa bila nidhamu hakuna Jjeshi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Nidhamu kwenye chuo cha Polisi Dar es Salaam (Dar es Salaam Police Academy) SSP Mussa Loyd, aliwataka Maafisa hao kuwa kioo cha jamii na kuwatendea haki wananchi  bila ya upendeleo wakati wote wanapokuwa kazini katika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa, mbali ya kuzuia vitendo vya kuhalifu, kushuku, kupeleleza na kuwakamata watuhumiwa, lakini kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha kuwa kila Askari anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila ya ubaguzi ama kumuonea mmoja wao.
“tunachotakiwa kufanya sisi Polisi ni kutenda haki kwa kila mmoja bila ya kujali dini, kabila, rangi ama itikadi ya mwananchi kisiyasa maana sisi hatuna chama”. Alisema Loyd.