February 25, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amewasili nchini China kwa ziara

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  akipokelewa na mwenyeji wake Mhe. wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China mara baada ya kuwasili kwenye  Wizara ya Mambo ya Nje ya China
 Mhe. Membe na Mhe. Wang Yi katika picha ya pamoja.
  Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Wang Yi mara baada ya kupokelewa.
February 25, 2014

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATEMBELEA MRADI WA MAJIKO SANIFU NA KUZURU KABURI LA SOKOINE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange juu ya kusafisha na kuyafanya maji kuwa salama, wakati alipotembelea sehemu ya karakana hiyo inayotumia umeme wa nguvu za jua (Solor Power Energe).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Kisioki Moitiko kuhusu utengenezaji wa majiko hayo, wakati alipotembelea kwenye karakana hiyo leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoin wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu alipokua katika ziara ya kikazi Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

BILIONI 2.4 ZAHITAJIKA UKARABATI WA MIUNDOMBINU SHULE YA SEKONDARI TANGA SCHOOL

February 25, 2014

            (Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake)
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
JUMLA ya sh. Bilioni 2.4 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari ya Tanga School iliyopo mkoani Tanga kutokana na uchakavu ilionao baadhi ya majengo kwenye shule hiyo.

Shule hiyo inahitaji ukarabati wa miundombinu iliyokuwepo tokea mwaka 1967 ikiwemo madarasa,maabara,karakana, maktaba, mabweni,bwalo na zahanati ambazo ukarabati huo utaifanya kuonekana na muonekano mpya.


Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema maeneo mengine yanayohitajika ukarabati ni viwanja vya michezo,nyumba za walimu ,Jengo la Utawala,Chumba cha Kompyuta na duka na Mgahawa wa shule pamoja na gari la shule.

WAZIRI MUKANGARA MGENI RASMI KILIMANJARO MARATHON

February 25, 2014
Mhe. Dk. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi.

Aggrey Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo alisema jana kwamba Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake. 
Aggrey Marealle
“Uwepo wa waziri ni ishara ya uungaji mkono tukio hili na ameeleza kufurahishwa kwake na maandalizi ya hali ya juu ya Kilimanjaro Marathon. Dk. Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle.

Marealle aliongeza kwamba baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum  wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema “mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Waandaaji John Addison wa Wild Frontiers, Mwesiga Kyaruzi wa Executive Solutions na Debbie Harrison
Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu.  Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.
February 25, 2014

MABALOZI WAJITAMBULISHA KWA RAIS Dk.Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Zambia  nchini Tanzania Bi, Judith Kangoma Kajimpanga aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais jana mchana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A5438 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi  waZambia  nchini Tanzania B,i Judith Kangoma Kajimpanga aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais jana mchana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A5473 
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Oman nchini Tanzania Soud Ali Mohamed aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais jana mchana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
February 25, 2014

WAZIRI MKUU NA MATUKIO YA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Bunge Maalum la Katiba nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Februari 25, 2014. Kutoka kushoto ni Abdallh Sharia  Ameir, Riziki Said Lulida na  Jerome Dismas Bwausi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A0605 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Bunge Maalum la Katiba nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Februari 25, 2014. Kutoka kushoto ni Abdallh Sharia  Ameir, Riziki Said Lulida na  Jerome Dismas Bwausi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
February 25, 2014
Pikipiki aina ya Hero Dawn yazinduliwa Tanzania
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa aina mpya ya Pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn Bw. Subhash Patel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Pikipiki hizo zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Astarc Group leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Astarc Group Bw.Salil Musale na kulia ni Mkurugenzi wa Astarc Group Africa Bw. Sameer Musale.Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Astarc Group wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya Pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn leo jijini Dar es Salaam.  Astarc3 
Bw. Subhash Patel ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Pikipiki mpya aina ya Hero Dawn akijaribu moja ya pikipiki aina ya Hero Karizma inayotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Astarc Group
Mkurugenzi wa Astarc Group Africa Bw. Sameer Musale akitoa historia fupi ya kampuni ya Astarc ambayo ni watengenezaji na wasambazajiwa pikipiki aina ya Hero ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Astarc6 
Baadhi ya wananchi wakijibu maswali mbalimbali kuhusu pikipiki aina ya Hero Dawn wakati wa uzinduzi wa pikipiki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
February 25, 2014

MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA MBEYA

Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
 
Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
February 25, 2014

MTEMVU ACHANGIA SH.IL. MOJA VICOBAYA MASHINE YA MAJI TEMEKE

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani) akilakiwa na wanachama wa Masdhine ya Maji Vicoba alipowasili kwa ajili ya sherehe ya kuitunisha mfuko wa Vicoba hiyo iliyopo Temeke, Dar es Salaam. Mtemvu alichangia sh. mil. 1. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mtemvu akimkabidhi Agnes Mangula cheti cha kuhitimu mafunzo ya uwezeshaji wa mpango wa VICOBA wakati wa hafla hiyo
Mwanachama Novatus Sambi akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
February 25, 2014

VIJANA KUANDALIWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII

IMG_2040
Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi akichangia wakati wa majadiliano ya awali jinsi ya kuendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla.
Na Genofeva Matemu (MAELEZO)
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd imeadhimia kuanzisha programu ya kuendeleza maendeleo ya jamii kwa kutumia vijana waliopo katika ajira mbalimbali kwa kuwajengea uwezo utakaowawezesha kuleta maendeleo katika jamii yao.
Hayo yameafikiwa wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel alipokutana kwa ajili ya majadiliano ya awali na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla pamoja na Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
February 25, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Februari 25, 2014

22 WAITWA TAIFA STARS KUIKABILI NAMIBIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).

Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.

Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.
February 25, 2014

FAINALI YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA KUFANYIKA JUMAPILI HII MBEYA


Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania[TBL] Kanda ya nyanda za juu kusini, Claud Chawene amesema lengo kuu la mashindano hayo kuwa ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika utayarishaji na uchomaji wa nyama choma.

Afisa habari TBL makao makuu Michael Machellah 

Baadhi ya waandishi wa habari



HOTEL YA MIKUYU ENEO AMBALO MKUTANO WA TBL ULIFANYIKIA


Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imefanikiwa kuwapata washiriki kumi waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano la nyama choma Mkoa wa Mbeya.

Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika Machi 2 Jumapili mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi  Ruanda Nzovwe.

Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania[TBL] Kanda ya nyanda za juu kusini, Claud Chawene amesema lengo kuu la mashindano hayo kuwa ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika utayarishaji na uchomaji wa nyama choma.

Chamwene ameyabainisha hayo alipokuwa anaongea na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Hoteli ya Mkuyu iliyopo Ilomba Jijini Mbeya ambapo awali washiriki walipatiwa mafunzo na wakufunzi mbali mbali ili kuyafanya mashindano hayo kuwa na ubora.