January 19, 2014

NYOTA WATATU COASTAL UNION WAPATA ULAJI OMAN, NI NYOSSO, SANTO NA DANNY LYANGA

WACHEZAJI watatu wa timu ya soka ya Coastal Union ya Tanga, beki Juma Nyosso, kiungo Jerry Santo na mshambuliaji Danny Lyanga wanatakiwa na klabu ya Al Musannaa ya Ligi Kuu ya Oman, imefahamika.
Habari ambazo BIN ZUBEIRimezipata mjini hapa zimesema kwamba klabu hiyo imekwishakutana na
Jerry Santo kulia akiwa na Salum Esry jana kabla ya chakula cha usiku
Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ kwa mazungumzo juu ya nyota hao.
Hata hivyo, habari zaidi zinasema makubaliano hayajafikiwa kutokana na Coastal kusema Musannaa imetoa ofa ndogo ya kuwanunua nyota wake hao. Inaelezwa, kiungo Mkenya, Jerry Santo anatakiwa pia klabu ya Fanja, ambayo hadi sasa ina mgeni mmoja tu kikosini mwake, Cisse wa Senegal. 
Jana tena Aurora alikuwa ana kikao na uongozi wa Musannaa hata akashindwa kuhudhuria mwaliko wa chakula cha usiku, ambao Coastal walipewa na mwanachama wa timu hiyo anayeishi hapa, Salum Esry.
Aurora hakuwa wazi sana alipoulizwa leo asubuhi kuhusu maendeleo ya mazungumzo hayo, lakini Ofisa Habari wa Coastal, Hafidh Kido alisema dili hilo bao halijaiva.

MAWAZIRI WAPYA HAWA HAPA: WAPO MIGIRO, JUMA NKAMIA ,MWIGULU NCHEMBA NA JENISTA MHAGAMA

January 19, 2014
Sunday, January 19, 2014
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.akitangaza baraza la mwaziri leo.

  •   Hakuna Mabadiliko Ofisi ya Rais
  • Ofisi ya Makamu Wa Rais - Naibu Waziri Kitwanga amehamishwa na nafasi yake imejazwa na Mhe. Ali Mwalimu
  • Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu Wizara ya Fedha (Sera). Aliyekuwa nafasi hiyo sasa ni Waziri Kamili
  • Uchumi na Mapato sasa anatoka Janet Mbene na inajazwa na Adam Malima
January 19, 2014

NDOA YA MBUNGE ALIYEOLEWA NA "KISERENGETI BOY" NI BALAA TUPU ... MBUNGE AMNG'ANG'ANIA KIJANA LIVE


 Rose Rosweeter Kasikila (60).

Dar es Salaam, Tanzania. Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Michael Christian (26). Rosweeter Kasikila (60) aliyeolewa na kinda wa miaka 26, Michael Christian, amegoma kutoa vyeti vya shule vya kijana huyo na kumtaka arejee nyumbani ili waendelee kuishi kama wanandoa.


Msimamo wa mbunge huyo umekuja baada ya kinda huyo kutumia kila mbinu akitaka arejeshewe vyeti vyake halisi vya shule ambavyo vimeshikiliwa na mbunge huyo kama njia ya kumshinikiza warudiane.

Habari zinasema kuwa taarifa ya ndoa hiyo iliyofungwa kwa siri na kuibua gumzo nchini, mara baada ya kuripotiwa na gazeti la Tanzania Daima, ndugu, marafiki na majirani  wa mbunge huyo walimtaka aivunje  na kurejesha kila kitu cha kinda huyo ili kuepukana na aibu Zaidi mbele ya jamii.

“Mbunge huyo ni mama yangu, tuliposikia habari za ndoa yake na huyo kijana, sisi kama familia tulishtushwa na kuhuzunika sana.  Tulikubaliana naye kwenye vikao vya familia avunje ndoa  hiyo na amrejeshee kijana huyo kila kitu, lakini hadi sasa amekaidi na ninasikia anafanya kila awezalo kutaka warudiane na kijana huyo,” amedokeza mmoja wa familia.