HUMPHREY POLEPOLE AMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUSIMAMIA RASIRIMALI ZA TAIFA

HUMPHREY POLEPOLE AMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUSIMAMIA RASIRIMALI ZA TAIFA

June 15, 2017
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Picha na Said Khamis
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.
          Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.
          Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi HAMPHREY POLEPOLE, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa.
          POLEPOLE amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais MAGUFULI hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi.
          Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema kilichofanywa na Rais MAGUFULI ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini.
          Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na Mmliki wa Kampuni ya Barrick Gold Cooparation  kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa mara watakachokubaliana baada ya mazungumzo na Tanzania.
SIMBA YAENDELEZA VURUGU ZA USAJILI,SASA ZAMU YA MTIBWA SUGAR KUIBOMOA

SIMBA YAENDELEZA VURUGU ZA USAJILI,SASA ZAMU YA MTIBWA SUGAR KUIBOMOA

June 15, 2017
IMG-20170615-WA0058-640x427

Kiungo kiraka wa Mtibwa Sugar Ally Shomari amemalizana na uingozi wa Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
1
Shomari ana uwezo wa kucheza namba mbili, saba, sita kama kiungo mkabaji lakini nane. Pia anaweza kucheza 11 au 10.
Muda wowote kuanzia sasa Ally Shomari atatambulishwa, amekuwa mchezaji wa saba kusainishwa mkataba na Simba baada ya Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili, Aishi Manula, John Bocco, Shomary Kapombe na Emmanuel Mseja.
SAMSUNG WAJA NA PROMOSHENI YA NUNUA SAJILI NA USHINDE

SAMSUNG WAJA NA PROMOSHENI YA NUNUA SAJILI NA USHINDE

June 15, 2017
unnamed
Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo Samsung (Kushoto) akiwaonyesha  waandishi wa habari stika mbili zinazolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Katikati  ni, Meneja wa Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe,  akifatiwa na meneja bidhaa wa Samsung Bw Elias Mushi, Meneja wa Phyramid consumers Karen Babu na Lulu Chiza Mkurugenzi wa masoko Phyramid consumers.
1
Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo Samsung (Kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni yao mpya ya Nunua sajili na Ushinde inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Katikati  ni, Meneja wa Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe,  akifatiwa na meneja bidhaa wa Samsung Bw Elias Mushi na Meneja wa Phyramid consumers Karen Babu
2
Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo Samsung (Kushoto) akiwaonyesha  waandishi wa habari bidhaa zinazohusishwa katika kampeni yao mpya ya ‘Nunua sajili na Ushinde’ inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Kulia  ni, Meneja wa Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe.
…………………………..
Samsung wazindua stika mbili za kupambana na bidhaa feki
Samsung wazindua stika mbili kwa utambuzi wa bidhaa Halisi
Samsung waungana na Pyramid consumers kukuza soko Tanzania
Dar es salaam, June 2017. Samsung Tanzania wameanzisha mfumo wa kuweka stika mbili katika bidhaa zao kwa ajili ya utambuzi wa bidhaa zao halisi pamoja na kupambana na bidhaa feki nchini. Sambamba na mkakati huo Samsung piawameanzisha Kampeni ya ‘Nunua Sajili na Ushinde’. Kampenihiyo ya mwezi mzima inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini itaanza tarehe 16 ya mwezi juni katika  mikoa yote ya Tanzania, na itaambatana na promosheni kabambe inayotarajiwa  kuwazawadia mamilioni ya watanzania  watakao nunua bidhaa halisi za Samsungkama vile TV, Friji, Microwave, mashine ya kufulia pamoja na Viyoyozi.
 “Ukizingatia bidhaa feki zina hatarisha afya za watumiaji, mahitaji ya bidhaa bora na halisi yanaongezeka kwa kasi kila kukicha. Samsung tumeendelea kufanya jitihada zaidi katika kukidhi matakwa ya  wateja wetu ulimwenguni pamoja na Tanzania kwa ujumla. Samsung Tanzania inaamini kwamba kampeni ya ‘Nunua, Sajili, Na Ushinde’ itaongeza uzoefu mpya na uelewa  kwa wateja wetu wa dar es salaam na mikoani pia juu ya utambuzi wa bidhaa feki zisizo kuwa za Samsung” alisema Meneja Bidhaa kutoka Samsung, Bw. Elias Mushi.
Akiongeleakuhusumkakati huo mpya Bw Mushi alisema ‘tumeongeza alama mpya kwenye bidhaa zetu ambazo ni stika mbili zitakazo wasaidia wateja kutambua bidhaa feki sokoni, Bidhaa za Samsung zitakuwa na stika mbili, stika msambazaji na stika inayotambulisha bidhaa halisi ya Samsung. Kampeni ya ‘Nunua Sajili na Ushinde’ itakua ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa wateja wetu ambayo itawapa taarifa za bidhaa zetu zinazoenda sambamba na mahitaji ya matumizi yao.

UBA Bank Tanzania yaingiza sokoni Kadi zake Mpya za Mastercard

June 15, 2017
 Mkuu wa kitengo cha malipo ya kiditali wa bank ya UBA Tanzania, Mr. Priscussy Kessy akiongea na baadhi ya wafanyakazi na wateja wa benki hio wakati wa uzinduzi wa Kadi za Mastercard zitakazoanza kutolewa kwa wateja wa UBA Bank Tanzania.
 Mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Tanzania, Mr Peter Makau akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kwa wateja wa bank hiyo ya UBA Tanzania
 Mkurugenzi Mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (kushoto) akikata utepe na mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Mr Peter Makau (kulia) kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kutoka Benki ya UBA Tanzania.
 Mkurugenzi mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa bank ya UBA Tanzania Mr Peter Makau (wa pili kushoto)wakikata keki kuashiria uzinduzi wa huduma hio ya kadi za mastercard ya bank ya UBA Bank uzinduzi uliofanyika leo katika tawi la benki hio lililopo barabara ya Pugu
 Mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya UBA Tanzania, Mr Jitendra Kumar Bhardwayi akizungumzia ujio wa mastercard ya UBA Bank ambayo amesema itamsaidia katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kumrahisishia shughuli zake za kibiashara
 Baadhi ya wafanyakazi wa UBA bank Tanzania wakifurahi mara baada ya uzinduzi huo wa kadi za Mastercard za UBA Bank.
Wafanyakazi wa benki ya UBA wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kadi za mastercard kutoka benki ya UBA leo

RC MAKONDA ATAJA MAMBO MAKUU MANNE KUKABILIANA NA UHALIFU JIJINI DAR ES SALAAM

June 15, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda
  
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Jana June 14, 2017 wakati wa Hafla ya kukabidhiwa magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuyatengeneza aliyataja mambo manne ambayo ameamua kuyafanya ili kuliongezea nguvu Jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu.Mambo hayo ni Kama ifuatavyo:

1. Ameamua Kufanya mchakato wa kutafuta Bastola 500, Radio Call, Baiskeli 500 pamoja na Pikipiki 200 ambazo tayari zipo bandarini kwa ajili ya Askari watakaokuwa wanafanya Doria kwa Matembezi, Watakaotumia Baiskeli, Pikipiki na Magari ili kukabiliana na uhalifu katika Jiji la Dar es salaa. Alisema kuwa kuhusu swala la magari tayari amekabidhiwa magari 26 mabovu kwa ajili ya matengenezo ambayo yapo safarini kuelekea Manispaa ya Moshi kwa ajili ya matengenezo. Hakuna gharama ya matengenezo itakayotolewa na serikali bali wadau wamejitolea kutengeneza Pasina malipo.

2. Kufunga Kamera kwenye vituo 20 vya Polisi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata taarifa ili kuondoa usumbufu na mianya ya Rushwa, Kuweka kompyuta 8 kwenye kila kituo katika vituo 20, kuzindua utaratibu wa wahalifu kupigwa picha pindi wanapoingia kituoni na taarifa zao kuwekwa kwenye mfumo wa kompyuta ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu hao. Mambo yote hayo yatafanyika kwa minajili ya kuondoa Mianya yote ya Rushwa dhidi ya wahalifu na Askari wa Jeshi la Polisi.

3. Kuhakikisha Jeshi la Polisi linaondoa biashara zote haramu na Bandari Bubu zilizopo katika Jiji la Dar es salaam ikiwemo kubaini maduka yote yanayouza vifaa vya magari na utambuzi wa mahali wanaponunua vifaa hivyo lengo ikiwa ni kubaini na kukomesha wizi wa vifaa vya magari unaofanyika katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam.

4. Kufunga kamera za barabarani ili kubaini utovu wa nidhamu unaofanywa na madereva na kurahisisha upatikanaji haraka wa taarifa za uvunjaji wa sheria barabarani badala ya askari kukimbizana na madereva wanaovunja sheria, Kuhakikisha Plate Namba za magari yote zinaingia kwenye mfumo huo ambapo kama gari ikifanya jambo baya barabarani iwe rahisi kukamatwa badala ya askari kuanza kulikimbiza. Jambo hili litasaidia baadhi ya wamiliki wa magari kuacha kuazimisha magari kwa watu wasiokuwa na leseni pia litaongeza nidhamu ya madereva wawapo barabarani.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA LEO BUNGENI MJINI DODOMA

June 15, 2017
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akijibu Maswali Bungeni mjini Dodoma Juni 15, 2017. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenya Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma, Juni 15, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu wa Bunge, Dkt, Thomas Kashililah, Mbunge wa Igunga, Dkt.  Dalaly Kafumu na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja wa Bunge mjini Dodoma Juni 15, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitea na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 15, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwenye jengo la Utawala la Bunge Juni 15, 2017.

WATUMIAJI WA JUMIA TRAVEL KWENYE SIMU WAONGOZEKA KWA 33%

June 15, 2017

Na Jumia Travel

 JUMIA Travel kwa kushirikiana na Google wameachia matokeo ya utafiti kuhusu maendeleo ya programu za mtandaoni (Progressive Web App - PWA) kwa kulinganisha na matumizi ya programu za kawaida za Android na IOS.

Ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba kufuatia uimarishwaji kwenye vipengele vyote vya PWA, kampuni imeweka wazi kwamba kumekuwa na ongezeko la watumiaji wapya kwa 33% ukilinganisha na tovuti ya simu iliyopita. Pia kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba kutokana na maboresho mapya kwenye PWA yameonyesha idadi ya watumiaji imeizidi ile programu ya awali kwa zaidi ya mara 12 na inazidi kukua, wakati nusu ya idadi ya watumiaji waliokuwa wanatembelea mtandao na kuondoka imepungua.      

Timu ya Jumia imeitengeza upya tovuti yake ya kwenye simu za mkononi kwa kutumia teknolojia za PWA na matokeo ya utafiti huu yameonyesha mafanikio mapya yaliyojieonyesha hususani katika nyanja za uhifadhiji wa nafasi, ukaachi wa chaji wa betr na matumizi ya data ya intaneti. Uunganishwaji wa mfumo wa PWA kwenye tovuti ya Jumia kwenye simu umechochea matokeo mazuri zaidi kwa watumiaji, kuongezeka kwa watumiaji na hasa, kupungua kwa kiwango cha wasiokuwa wakitumia mtandao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy amesema kuwa, “Tunafanya kazi kwenye soko lililotawaliwa kwa kiasi kikubwa na watumiaji wa simu, kwa hiyo tunalenga kuleta teknolojia ya kisasa kabisa inayolenga kutumika kwenye masoko yote hata maeneo ambayo kasi ya intaneti ina changamoto.”

Ameendelea kwa kusema kuwa lengo la kampuni ni kuiinua teknolojia na kuendelea kuwekeza kwenye rasilimali



zitakazowaletea matokeo mazuri watumiaji, “Afrika ni soko ambalo linatumia simu kwa kiasi kikubwa, ndiyo kwanza tunaanza, na tunaamini kwa kuwatengenezea mazingira mazuri na rafiki ya matumizi ya simu ni jitihada kubwa katika kuyatimiza mahitaji ya wateja wetu.”

Naye kwa upande wake Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee ameongozea kuwa, “Matokeo ya utafiti huu uliofanywa na Google kwa kushirikiana nasi ni ishara nzuri kwetu kuonyesha kwa namna gani tunavyokuwa hususani katika maboresho ya huduma zetu. Ukizingatia kwamba watumiaji wa simu za mkononi mpaka hivi sasa Tanzania wapo zaidi ya milioni 40, ambayo ni sawa na ueneaji wa asilimia 83. Matumizi hayo kwa kiasi kikubwa yamechochewa na ueneaji wa intaneti ambao umekua na kufikia asilimia 19.86 kwa mwaka 2016 kutokea asilimia 17.26 mwaka 2015 nchi nzima kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).”
 
“Ripoti inasema kwamba mtandao wa Jumia Travel kwenye simu za mkononi umeongezeka kuwa na watumiaji kwa 33%, idadi ya watumiaji wanaoutembelea na kuondoka imepungua kwa 50%, idadi ya watumiaji imeongezeka mara 12 ukilinganisha na ya wale wa Android na IOS, inatumia kiwango cha data mara tano chini zaidi, kiwango cha data kinachotumika katika kufanya miamala ni mara mbili chini zaidi, wakati nafasi inayohitajika kuihifadhi kwenye simu imepungua kwa mara 25 chini zaidi na pia ni rahisi zaidi kufanya maboresho ya mara kwa mara. Hivyo basi, takwimu zote hizi ni dhahiri kwamba maboresho ya kurahisisha huduma zetu hayana kikomo na Google wamelidhihirisha hilo kupitia ripoti yao ya kitaalamu zaidi juu ya programu yetu,” alihitimisha Bi. Dharsee.    

Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Data (IDC) inaonyesha kwamba Afrika kiwango cha uingizwaji wa simu za mkononi kimeongezeka kwa kasi kwenye kila robo ya mwaka, na soko linatarajiwa kuongezeka maradufu, na hivyo kuchangia thelethi moja ya simu zote zinazosafirishwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2017. Hii itazidi kuimarisha zaidi idadi ya wateja wanaopendelea kufanya manunuzi kwa njia ya simu. Pia ni tahadhari zaidi kwa wadau wa sekta ya biashara mtandaoni kuendana na mpango mkakati wa kutumia simu zaidi katika kuendesha shughuli zao.

“MILIONI 10 ZINAHITAJIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA MBIO ZA MAGARI MKOANI TANGA “

June 15, 2017
CHAMA cha mbio za magari mkoani Tanga (Tanga Motors Sports Club (TMSC) kimesema kinahitaji milioni 10 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Tanga Rally 2017 yanayo tarajiwa kufanyika  Julai 8 mpaka 9 mwaka huu mjini hapa.

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Awadhi Bafadhili
  alisema mashindano hayo msimu huu yatashirikisha washiriki kutoka nchini mbalimbali ikiwemo Kenya na Tanzania ili kuweza kumpata bingwa

Alisema hivi sasa wanachokifanya ni kuangalia kama kutakuwa na

uwezekano wa kubadilisha njia kutoka Pongwe na Muheza kutokana na kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo inaweza kuwa kikwazo cha kushindwa kufikia malengo yao.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema  katika mashindano hayo msimu huu
  kunatazamiwa kuwa na madereva maarufu ambao wanafanya vizuri mkoani Tanga, Ally Kiraka,Ashu Barbosa,Utu Nizimal,Ottu Nirmal,Twalib Khatibu,Anthony John, Naeel Asher na Said Baghzah ambao ni tishio kwa mchezo huo.

Alisema licha ya madereva hao lakini wengine ambao wataungana nao ni
  kutoka mikoa ya Arusha,Moshi,Dar,Iringa na Morogoro ambao ni Mzee Gerald Miller,Ahmed Huwell,Sameer Nahdi, Dharam Pandya,Sunny Birdi,Jamil Khan na Isaac Taylor ambao uwepo wao umepelekea mashindano hayo kuonekana yatakuwa na ushindani mkubwa.

Aidha pia alisema mpaka sasa tayari wafadhili watatu wameonyesha nia
  ya kusapoti mashindano hayo ambayo ni Kiwanda cha Unga cha Pembe na Mkwawa Power Drinking water cha Mkoani Iringa na Mkwabi Super Market.

Akizungumzia changamoto ambazo wanakumbana nazo wakati wa mashindano
  hayo alisema mojawapo ni kitendo cha madereva wa pikipiki na baiskeli maarufu kama bodaboda kukatiza barabarani wakati wa mashindano hayobila taarifa jambo ambalo ni hatari.

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma zake kwa umma

June 15, 2017
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.


DC KASESELA AKESHA KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA SITA USIKU MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI

June 15, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa nyakavangala uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa Juhudi za kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo alilosimama  Mkuu huyo wa Wilaya.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane

Kasesela alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa likiendelea

"Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku"alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa na subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao kwa kuwa wameshaukaria mahali ulipo.

"Ungalia tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo tumebakiza sehemu ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia toka siku ya jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu ili tutoe mwili wake ukiwa salama" alisema Kasesela

Haya yamemkuta mchimbaji mwenzenu hivyo nawataka kuwa makini wakati wa uchimbaji wa madini katika mgodi huu wa nyakavangala la sivyo mgodi huu utafungwa sio muda.

Lakini mwili wa Vaspa Nyenza umepatikana saa 7 na dakika 50 usiku na  msafara kuelekea mortuary umeanza na Mazishi kufanyika Kijiji cha Itengulinyi Ifunda kesho asubuhi kuanzia saa 3 au 4 hivi

Kwa upande wake Chief inspector Mayunga Ngele aliwataka wachimbaji wote kutochimba tena kwenye mashimo yaliyozuiliwa ili kuepusha ajali mbalimbali hapo mgodini kwa kuwa hata huyo marehemu na wenzake walishakatwa kuchimba katika shimo hilo ambalo lilikuwa kwenye hali mbaya ya kuanguka.

"Tamaa ndio zimemponza huyu marehemu maana tuliwakataza lakini mwenyewe waliingia kinyemela kwa lengo la kwenda kuchimba kwa wizi kwenye shimo lilokataliwa ndio maana yamewakuta hayo kama wangekuwa wameusikia ushauri wetu basi tusingefika hapa tulipo usiku huu "alisema inspector Ngele

Naye Thomas masuka mmiliki wa mgodi wa Nyakavangala alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha kila kitu kianda kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali na kuahidi kuwa gharama za kuuokoa mwili hadi kuufikisha kwako ni kwake na ndugu hawatalipia pesa yoyote ile.

"Kuanzia kutokea kwa kifo chake,uokoaji na kuusafirisha mwili wa marehemu huyu gharama zote nitazilipa mimi kama mmiliki wa mgodi huu kwa mujibu wa sheria za madini hata angekuwa Mwananchi wa kigoma,Mwanza, Mbeya, Bukoba na sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania basi ni wajibu wangu kuhakikisha mwili wa marehemu unafika mali pake kwa usalama unaotakiwa" alisema Masuka

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC) NA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM (DIT) WASAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO(MoU)

June 15, 2017
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(wa tatu kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(wa pili kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili. MoU imejikita kwenye ushirikiano wa Utafiti,  Taaluma, kubadilishana wataalamu, ziara za kitaaluma kwa wanafunzi.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakibadilishana mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 

Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) akizungumza jambo baada ya taasisi hiyo na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)kuweka saini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha,kushoto ni Dk Richard Massika.

RC MAKONDA AKABIDHIWA MAGARI 26 YA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA KUYATENGENEZA

June 15, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akikagua gwaride wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilless B. Muroto akisoma taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Baadhi ya magari Mabovu yaliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe ally Happi (Kushoto) wakijadili jambo mara baada ya kumalizika hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiyakagua magari mabovu aliyokabidhiwa kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiyakagua magari mabovu aliyokabidhiwa kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilless B. Muroto akitoa maelezo ya magari hayo mabovu mbele ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe Paul C. Makonda wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare makori, na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo mara baada ya hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam