RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA

November 21, 2014



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa .Mohamed Janabi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita..Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tenahospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri.
Picha na  Freddy Maro

 WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI.....STORI KAMILI IKO APA

WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI.....STORI KAMILI IKO APA

November 21, 2014

Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.
Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie kupitia mlango mdogo wa dharura huku wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman Abba amesema walilazimika kuzuia mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata taarifa kwamba kuna majambazi walipanga kuvamia Bunge hilo.Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia Bungeni, Wabunge wawili walipoteza fahamu katika vurugu hizo

WAIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA MASHARTI YA LESENI UFUNGUAJI WA MAKAMPUNI

November 21, 2014
baadhi wa wahitimu wakiwa kwenye maandamano kuingia ukumbi



WAHITIMU wa mafunzo chuo cha Ufundi  Ustadi (Veta) Tanga wameitaka Serikali kulegeza masharti ya leseni kufungua kampuni lengo likiwa ni kuweza kujiajiri ili ujuzi wao usiwe wa mifukoni na makabatini.

Wakizungumza wakati wa mahafali ya 38 chuoni hapo jana, wahitimu hao wamesema kwa sasa ni vigumu kupata ajira Serikalini na hivyo kutaka ujuzi wao kuweza kuutumilia kwa kufungua makampuni yao na kuweza kuisaidia Serikali katika kutoa ajira.

Wamesema kufanya hivyo kutawawezesha kutoa ajira kwa wengine wasio na kazi jambo ambalo litasaidia kupunguza vijana wasio na kazi mitaani pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya na waporaji wa kutumia nguvu.

“Tuko na furaha ya kuhitimu kozi zetu ila changamoto kubwa iko katika kupata ajira iwe serikalini ama taasisi binafsi----hii ni kutokana na kuwa na wasomi wengi wasio na kazi” alisema Devid Elias

“Jambo zuri ambalo Serikali inatakiwa kufanya hasa sisi ambao tumetokea katika vyuo ni kutulegezea masharti ya upatikanaji wa leseni za kampuni----itakuwa msaada kwetu na vijana wasio na kazi”alisema Elias

Kwa upande wake mhitimu wa kunyoosha bodi za magari, Rose John, amewataka wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari kuacha kukata tamaa na badala yake wajiunge na vyuo vya ufundi.

Alisema kuna wanafunzi wengi ambao humaliza elimu ya sekondari wamekuwa wakikata tamaa ya masomo na kusahau kuwa viko vyuo vya ufundi ambavyo vinaweza kuwatoa kimaisha kama vilivyo vyuo vyengine.

“Tatizo hasa liko kwa wazazi mtoto anapoamaliza naona ndio mwisho wa masomo na kumuingiza katika biashara au kumuacha akipotea---wanasahu kuwa viko vyuo vya ufundi” alisema Rose

Aliwataka wazazi kukumbuka kuwa vyuo vya ufundi vinaweza kuwabadilisha watoto wao katika maisha yao mbeleni pamoja na ya kwao na hivyo kutambua kuwa elimu na ujuzi sio wa shuleni peke yake.

Aliwakumbusha kuwa kumuacha mtoto wakati yuko na elimu ya kiwango cha chini ni jambo la hatari linaloweza kuwatumbukiza katika magenge ya kihuni pamoja na biashara haramu za uuzaji unga na uvutaji bangi.
chanzo:Kumekucha Blog
Sentensi 5 za Adebayor kuhusu kumfukuza kwake mama yake na kumtelekeza

Sentensi 5 za Adebayor kuhusu kumfukuza kwake mama yake na kumtelekeza

November 21, 2014
Adebayor-and-mum
Mapema leo asubuhi ilitoka habari kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Togo kumfukuza mama yake kwenye moja ya nyumba zake huko nchini Togo kutokana na kutokuwa na maelewano na mazuri na mama yake huku zikitoka taarifa kwamba kisa cha yote haya ni tuhuma za uchawi.
Masaa kadhaa baada ya habari hiyo kusambaa kwenye mitandao, Emmanuel Adebayor amekanusha kumfukuza mama yake kwenye nyumba kwa sababu ya alidhani anampiga misumari.
Dada yake Adebayor Maggie alikaririwa kupitia radio ya Peace FM kwamba mshambuliaji huyo amegoma kumhudumia mama yake na hajaonana nae kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mama yake ameripotiwa kuuza mifuko, makufuri na bidhaa nyingine ili aweze kuisadia familia yao.
Hata hivyo mshambuliaji huyo anayelipwa £101,000 kwa wiki amekanusha madai hayo ya dada yake kwamba amemtelekeza mama yake.
Adebayor, nae kwa upande wake alitafutwa na Peace FM, alisema: ‘Sijawahi kumfukuza mama yangu kwenye nyumba yangu. Aliamua kuondoka mwenyewe.
‘Nawezaje kuwa na mawasiliano na mama yangu ikiwa yeye anamwambia kila mtu kwamba sitoendelea mbele kwenye kazi yangy, hivyo nimeamua kuwa mwenyewe nifanye mambo yangu.
‘Inabidi waache kuongea kuongea, na waache kunifanyia uchawi, waniache peke yangu.
‘Nimemnunulia nyumba ya $1.2m huyo mtu anayejiita dada yangu. Unaweza kuamini huyo dada alienda kuipangisha hiyo nyumba bila kunifahamisha? – Alimaliza Adebayor
YANGA KUANZA MAZOEZI NOVEMBA 24 BAADA YA MAPUMZIKO YA WIKI MBILI.

YANGA KUANZA MAZOEZI NOVEMBA 24 BAADA YA MAPUMZIKO YA WIKI MBILI.

November 21, 2014
TIMU ya Dar es Salaam Young Africans inatarajia kuanza mazoezi Novemba 24 mwaka huu baada ya kuwa na mapumziko ya wiki mbili.
Maandalizi hayo yatakuwa ni kujiandaa na  mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC katikati ya mwezi Disemba mwaka huu.

Kocha mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo alitoa mapumziko hayo kwa wachezaji wake, kufuatia baadhi ya wachezaji kuitwa na timu zao za Taifa kwa ajili ya mechi za kalenda ya FIFA na wengine kujiandaa na michuano ya Challenge Afrika Mashariki na Kati.

Wachezaji wa Young Africans walioitwa timu za Taifa ni (Tanzania), Deo Munish "Dida", Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa (Rwanda) Haruna Niyonzima, (Uganda) Hamis Kizza.

Aidha kocha Maximo pamoja na wachezaji kutoka nchini Brazil kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" wako nchini Brazil kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi ya mechi za mzunguko wa nane.

Kocha msaidizi Leonardo Neiva amebakia nchini Tanzania, ambapo kwa sasa anaandaa programu ambayo itatumika kuanzia Novemba 24, 2014 pindi kikosi kitakapoanza tena maandalizi ya kujiandaa na michezo itakayofuata.

Wachezaj wote wanatarjiwa kuripoti Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa kumalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC. 
 chanzo:blog ya http://www.youngafricans.co.tz

TFF YAKUSANYA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 12 DAR

November 21, 2014


Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.


Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.


IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MASHINDANO TFF, BONIFACE WAMBURA

WAWILI WATAFUTWA NA POLISI TANGA KWA TUHUMA ZA KUMUUWA MTOTO WA JAMII YA WAFUGAJI WILAYANI KILINDI.

November 21, 2014
JESHI la polisi Wilayani Kilindi Mkoani Tanga linawatafuta watu wawili kwa tuhuma za kumuuwa mtoto wa jamii ya wafugaji, Said Omar (19) na kisha  maiti yake kuitundika juu ya mti wa mkunazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Fresser Kashai, alisema tukio hilo lilitokea juzi sa 1 usiku katika bonde la Kimbe kijiji cha Nyadigwa tarafa ya Kibirashi.

Alisema watu waliofanya kitendo hicho waliichukua maiti ya mtoto huyo na kuining’iniza juu ya mkunazi  kisha kutokomea kusikojulikana na hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi pamoja na  kuwasaka wauaji  hao.

“Tunaendelea kuwasaka waliohusika na taarifa za awali ni kuwa wamekimbilia milimani na wamekuwa wakirejea majumbani kwao nyakati za usiku----tuna uhakika tutawatia mbaroni” alisema na kuongeza

“Kitendo ambacho wamekifanya ni cha kikatili na hakikubaliki katika jamii---tutahakikisha tunawatia mikononi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria” alisema Kashai

Akizungumzia kuhusu jamii kuishi kwa maelewano na kushirikiana kwa kila jambo, kamanda Kashai aliwataka wafugaji na wakulima kuwa na utaratibu wa kukutana kila baada ya mwezi mmoja kuzungumza changamoto wanazokabiliana nazo.

Alisema jamii  hizo zinapaswa kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kujadili na kuzungumza changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo  jambo ambalo litasaidia kuondosha vitisho vya uhasama.

“Haya matukio ya ugomvi ugomvi wa wakulima na wafugaji tatizo ni kuwa hakuna utaratibu wa kukutana na kujadili mambo yawahusuyo hasa mashamba na mifugo” alisema

“Kama kungelikuwa na utaratibu huo katu tusingelisikia ugomvi pande mbili hizi popote katika ardhi yetu ya Tanzania---hivyo natoa ushauri Serikali za vijiji kuandaa mikutano hiyo nasi kama polisi tutaibariki” alisema Kashai

Kamanda Kashai alisema mikutano hiyo polisi kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya usalama vitashirikiana na wakulima na wafugaji kuandaa mikutano hiyo lengo likiwa ni kuleta mahusiano mema pande mbili hizo.

PICHA TANO ZA WAKINA MAMA WAKIUZA BIDHAA ZAO KWENYE SOKO LA SONI WILAYANI LUSHOTO LEO

November 21, 2014
 Wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga mji mdogo wa Soni halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Tanga wakipanga bidhaa zao kusubiri wateja.
 Wafanyabiashara wa mboga mboga na matunda mji mdogo wa Soni halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Tanga wakiwa katika ujasiriamali. Wanawaker kama hawa wanastahili kuwezeshwa ili kujikamua kimaisha na kuacha kuwa wategemezi wa wanaume.

Kama ambavyo wanaonekana wakichakarika ili mradi tu wasiwe wakaaji na walinzi wa majumba wakati uwezo wa kufanya kazi wako na hata kama na mtoto mgongoni, hii ni kwa sababu kufanya kazi na utakuja taka kufanya kazi nguvu zimekuishia.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA LISHE NA VIRUTUBISHO (ICN2) ROME ITALIA, PAPA FRANCIS AUNGURUMA

November 21, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014.
 Papa Francis, akihutubia wakati wa mkutano huo....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Balozi Wilfred Ngirwa (kulia).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kulia) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy. 
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho. 
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. 
*********************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA KUHUSU LISHE NA VIRUTUBISHO JIJINI ROME, ITALIA NOVEMBA 21, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Novemba 19, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la 
Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome Italia. 

Mkutano huu umefanyika ikiwa ni miaka 22 baada ya mkutano wa kwanza maarufu kwa jina la ICN1 kufanyika katika jiji la Rome na kuazimia kuwa, upo umuhimu wa kuhakikisha binadamu wanapata Lishe bora yenye virutubisho ili kusadia kujenga afya ya binadamu duniani. Mkutano huu wa pili pia umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi wa Kudumu wa Italia katika Umoja wa Mataifa Gianni Ghisi aliyesoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Italia Giorgio Napolitano ambapo alifafanua kuwa Rome inawakaribisha wawakilishi wan chi mbalimbali na kwamba inatamani kuona mkutano huu unatoka na majibu ya tatizo la lishe duni kwa watu wa mataifa mbalimbali. 

Katika siku ya ufunguzi pia hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon iliwasilishwa pamoja na uzoefu wa masuala ya Lishe kutoka Italia ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia Paolo Gentiloni aliwasilisha hotuba yake huku akiwakaribisha washiriki wa mkutano huu wa ICN2 katika jiji la Rome na kufafanua kuhusu matarajio ya Italia katika mkutano wa sasa ukilinganisha na ule uliofanyika miaka 22 iliyopita.

Akiwasilisha taarifa ya Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wa Maendeleo ambao wamekuwa wakichangia katika sekta za Afya na Kilimo na akafafanua kuwa Tanzania imepiga hatua tangu ICN1 na sasa inahitaji kuona mkutano huu unatoka na maamuzi yanayotekelezeka ili kuwasaidia wananchi wa mataifa mbalimbali hasa watoto na akina mama wajawazito kuwa na uhakika wa lishe bora yenye virutubisho.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo vingi vilitokana na lishe duni na kwamba serikali ya Tanzania inaendelea kulipatia msukumo suala la lishe na virutubisho kwa wananchi wenye uhitaji ili kujenga taifa lenye afya na lenye watu wenye uwezo wa kusaidia nguvu zao katika kuleta maendeleo.

Akizungumza siku ya pili ya Mkutano huo Baba Mtakatifu Fransis alisema haki ya chakula bora si tu kuwa imetolewa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu bali pia ni haki inayoashiria utu na ambayo haipaswi kutolewa kama zawadi kwa wanadamu. 

Papa Fransis aliendelea kusema kuwa, katika dunia ya sasa masuala ya chakula, lishe na mazingira yametokea kuwaunganisha binadamu wa mataifa yote sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma na akazitaka serikali za dunia kuhakikisha zinapunguza utupaji wa vyakula sambamba na kuongeza mikakati ya kuhakikisha kila mwanadamu anapata lishe bora.

ICN2 inatazama pia kuhakikisha kuwa nchi zinakuwa na mikakati ya kupunguza utapiamlo na kwamba chakula kinachopatikana kiwe kile kilichoboreshwa ama kuongezewa virutubisho ili kusaidia jamii zinazokabiliwa na matatizo kama utapiamlo kuepukana nayo 
na hivyo kuwa na kizazi chenye afya bora na chenye uwezo wa kutumika katika uzalishaji ama katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Margareth Chan, Mkurugenzi wa WHO aliueleza mkutano huo kuwa suala la lishe ni mhimili katika kufanya jamii inayoweza kukabiliana na magonjwa huku pia Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva akifafanua kuwa, shirika lake linautumia mkutano huu unaoshirikisha nchi 172 kutoa mwongozo kwa dunia kuhusu jambo hili muhimu katika maisha na hasa sasa ambapo tunaelekea kukamilika kwa Malengo ya Milenia na kuanza malengo mapya.

Katika mkutano huo, licha ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Tanzania pia iliwakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid pamoja na Waziri wa Mifugo Dkt. Titus Kamani sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim. 

Sambamba na kuhudhuria mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi Italia na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa sambamba na kukutana na Mkurugenzi wa FAO ambaye alionesha furaha yake kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepitia na kuahidi ushirikiano zaidi katika masuala ya Kilimo. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais na ujumbe wake umeondoka kurejea nyumbani Tanzania tayari kuendelea na shughuli nyingine za Kitaifa leo Ijumaa Novemba 21, 2014.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
                       Rome, Italia
                 Novemba 21, 2014

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI WA HABARI WA NEW HABARI 2006 LTD, MAREHEMU INOCENT MUNYUKU

November 21, 2014


Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
 Mwakilishi wa klabu ya Yanga, Said Motisha akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya klabu yake ambapo alitoa ubani wa sh. laki tano.
 Motisha akikabidhi ubani wa sh. laki tano.
 Mmoja wa watu waliosoma na marehemu Munyuku akitia salama za rambirambi ambapo walitoa sh. laki tatu.
  Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.
 Mwakilishi wa familia, Mkuchika akitoa neno la shukrani.
 Rashid Kejo akitoa salama za rambirambi.
 Mwakilishi wa Uhuru Publishers akitoa salama za rambirambi na ubani wa sh. laki mbili.
 Waombolezaji wakielekea katika gari kwa ajili ya safari ya Morogoro kwa mazishi ya marehemu Inocent Munyuku.

 Mwili wa marehemu Munyuku ukiingizwa katika gari tayari kwa safari ya kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa marehemu Inocent Munyuku.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hospitali ya Lugalo wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, marehemu Inocent Munyuku.
 Mwandishi wa gazeti la Jamhuri, Alfred Lucas (kushoto) na Limonga Justine Limonga wa Radio Uhuru.
 Waombolezaji.
 Msanifu Mkuu wa Kurasa wa gazeti la Tanzania Daima, Emily Maya akimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda.
Mkurugenzi wa Global Publisher, Eric Shigongo akiteta jambo na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda.

 Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa heshima za mwisho. Kushoto Mwandishi wa habari wa gazeti la Hoja, Iche Mang'enya akitoa heshima za mwisho.

MAKUBWA HAYA......WAZAZI WA MISS TANZANIA 2014 WAIBUKA KUDAI CHAO

November 21, 2014

Wazazi wa Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania  iwape maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa hadi sasa wako njiapanda.
 
Kauli hiyo ya  Eva na Deus Kamazima imekuja siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam.
Wakizungumza nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.
Walisema kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.
“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti.
Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika.
“Sijapewa taji wala zawadi , lakini kitendo cha kupewa kiti cha umalkia nimeridhika,” alisema  Lilian.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema kuwa ni kweli bado hawajamkabidhi fedha na zawadi  kwa kuwa kuna taratibu za kiofisi bado zinafanyika.
“Ni kweli, tulimwambia atuachie akaunti yake kwa kuwa kuna taratibu zinafanyika, tutamwekea pesa na kuhusu zawadi huyo alirithi taji, hakuwa mshindi wa kwanza, lazima mwelewe,” alisema Lundega.
 
edited by fredy mgunda

MKUU WA MKOA MPYA WA DODOMA CHIKU GALAWA AFUNGUA WARSHA YA KUPINGA RUSHWA YA NGONO KATI YA MABOSI NA WATENDAJI WA CHINI

November 21, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifafanua jambo wakati alipokuwa
akifungua Semina ya siku moja ya kutafuta namna ya kukabiliana na
Rashwa mbalimbali ikiwemo ya Ngono kati ya viongozi na watendaji wa
chini iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania Jaji Engera Kileo
akizungumza katika semina hiyo.
Shekh Husen Kuzungu akifafanua jambo wakati akichangia mada kwenye
semina ya kutafuta namna ya kutokomeza Rushwa ya Ngono iliyoandaliwa
na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania  (TAWJA) iliyofanyika Dodoma.
Mahakaimu, Wabunge, na wakuu wa vyombo vya Dora wakifuatilia jambo
wakati mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifungua Semina kuhusu
namna ya kukabiliana na tatizo la Rushwa ya Ngono linaloendelea
kushamili kati ya wenye vyeo na wasio na vyeo, iliyoandaliwa na Chama
cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)
Wajumbe waliohudhuria warsha ya kutafuta namna ya kukomesha Rushwa ya
ngono maofisini kati ya mabosi watendaji wa chini ikiwemo vyuoni na
mashuleni iliyoandaliwa na chama cha majaji wanawake Tanzania (TAWJA) iliyofanyika Dodoma
Majaji, mahakimu, viongozi wa Dini na viongozi wa vyombo vya Dora
waliohudhuria semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu mpya
wa mokoa wa Dodoma Chiku Galawa.