MBUNGE MUSSA WA JIMBO LA TANGA AWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

December 29, 2016


Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake  na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata mafanikio.
Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema licha ya kushiriki huo lakini pia wakulima watambue katika kipindi hiki wanapaswa kutayarisha mashamba yao ili kuweza kulima kilimo cha kisasa chenye tija.
Aidha pia aliwataka kuhakikisha wanawajibika kusafisha maeneo yao ili yaweze kuwa na muonekana mzuri ili waweze kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokana na kuwepo kwa hali hiyo.
 “Lakini pia ni niwatake halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasafisha maeneo yao kwa kuondoa takataka “Alisema Mbunge Mussa.
Sanjari na hilo Mbunge huyo pia aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye Jimbo lake kuhakikisha wanaongeza bidhii kwenye masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao
 “Niwaambie wanafunzi wakati wanapokuwa shuleni acheni masuala ya michezo badala yake hakiksheni mnazingatia elimu kwani ndio mkombozi mkubwa kwenye maisha yenu ya sasa na baadae “Alisema.

TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA

December 29, 2016
Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao.
Kwa zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu yao katika wodi yao iliyopo Hospitalini hapo Muhimbili. Katika tukio hilo, Mo Dewji Foundation waliweza kutoa vitu mbalimbali kama zawadi kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho. 
Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na unga wa ngano, sabuni za kunawia mikono, sabuni za kuogea, doti za khanga, mafuta ya kupikia na vitu vingine vingi. Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amewatakia kila lakheri watoto na wazazi wa kituo hicho katika kuingia mwaka mpya ambapo pia aliwahakikishia wafanyakazi wa kituo hicho kuwa taasisi yao itaendelea kusaidia kituo hicho.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akimkabidhi Mwalimu Leonard ambaye ni mwalimu anayetoa elimu kwa watoto wenye kansa wanaopatikana kituoni hapo.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akikabidhi zawadi hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha TLM
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho, pamoja na baadhi ya watoto hao wa TLM.
Mratibu wa Miradi wa MO DEWJI Foundation, Catherine Decker akiwa pamoja na watoto wa TLM, wakati wa tukio hilo la kuwafariji watoto pamoja na kutoa zawadi.
Mwalimu Leonard wa TLM akiwa na mmoja wa watoto wa kituo hicho wakati wa tukio hilo la kutoa zawadi.
Jengo la TLM

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

December 29, 2016


1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
8
Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na  kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.
Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.
”Unapotokea msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee”
Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.
Kwa upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016

TAMWA WAPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA MAKUNDI MAALUM YALIYOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2015 MANISPAA YA IRINGA

December 29, 2016
Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
Na Fredy Mgunda,iringa
MAKUNDI maalumu yanayohusisha vijana, walemavu na wanawake wa mjini Iringa walioingia katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakitoa masikitiko yao ya namna vyombo vya habari vilivyowapa nafasi finyu katika mchakato huo.

Makundi hayo yalikuwa yakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo iliyofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

Dora Nziku anatoa malalamiko yake kwa kuvilaumu vyombo vya habari mkoani iringa kwa kutowapa nafasi wanawake,walemavu hata wale wasio na kipato kwa kuwa waandishi wengi walikuwa wanajali maslai kuliko ukubwa wa habari
“Naona kama wanawake tuliathiriwa zaidi katika mchakato huo kwani habari zetu hazikupata nafasi kama ilivyo kwa wagombea wengine hasa wanawake,” alisema Diwani wa Viti Maalumu Iringa Mjini, Dora Nziku (CCM).

Nziku alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanahabari kuomba hela kwa wagombea na viongozi wa kisiasa ili waweze kutoa habari zao.

“Pamoja na kuwapa hela wakati mwingine habari hizo hazitoki na mimi ni mmoja wa wahanga wa hilo, nimewahi kuita wanahabari, wakaniomba hela lakini hawakutoa habari zangu na nadhani hazikutoka kwasababu mimi ni mwanamke,” alisema diwani huyo bila kutaja wanahabari hao.

Naye Agusta Mtemi aliyekuwa mgombea udiwani viti maalumu mjini Iringa (CCM) alisema katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda kwa kura 266 wagombea wenzake zaidi ya 10 lakini katika mazingira tata alionekana kama mshindi namba mbili na kukosa nafasi ya kuwawakilishi wanawake wenzake katika Baraza la Madiwani la Jimbo la Iringa Mjini.

Naye Imelta Mhanga kijana aliyegombea udiwani viti maalumu (CHADEMA) mjini Iringa alilaumu mchakato ndani ya chama akisema unawanyima uhuru wa kuongea na vyombo vya habari hasa wanapofanyiwa figisufigisu.

“Ndani ya taasisi kuna vitisho, kwamba shughuli za chama ni siri ya chama, hazitakiwi kutoka nje. Kwahiyo tunaogopa kukutana na wanahabari,” alisema huku akipinga kwamba wanahabari wanataka fedha mara zote ili kutoa habari zao.

Kwa upande wake, Selekti Sinyagwa ambaye ni mlemavu wa miguu aliyegombea udiwani viti maalumu ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) alisema; “kwa kweli walemavu tunabaguliwa sana katika mchakato wa kupata viongozi, jambo hili linatufanya tujione kama ni jamii tofauti na jamii tunayoishi nayo.”

Afisa Miradi wa TAMWA, Reonida Kanyuma alisema taasisi hiyo iliangalia namna makundi hayo yalivyoripotiwa katika vyombo vya habari ili kwa kushirikiana na wadau waje na suluhisho litakaloondoa tofauti zilizopo.

“Tulifanya ufuatiliaji katika mchakato huo, na kuona jinsi wanawake, walemavu na vijana walivyoripotiwa katika vyombo hivyo vya habari ikilinganishwa na wagombea wanaume katika nafasi za udiwani, ubunge na urais waliopewa nafasi,” alisema.

Alisema kwa kuwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine, vyombo vya habari havipaswi kuwabagua wagombea kwa kuangalia udhaifu wao au mfumo dume na badala yake vitoe fursa sawa kwa kuzingatia uwezo na dhamira waliyonayo katika kuwatumikia watu wengine.


“Ni matarajio ya TAMWA na wadau wote wa maendeleo kwamba sekta ya habari itatenda haki kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote katika chaguzi zijazo,” alisema.