DC ASIA APIGA MARUFUKU WILAYA YA KILOLO KUTOA WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI

September 07, 2017
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa katika moja ya shule za msingi wilayani kilolo akiwa amefika kaunagalia hali ya mitihani inaendeshwani na usalama wake upoje 
 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanafuzi waliohitimu elimu ya shule ya msingi katika shule ya msingi Boma la ng'ombe wilaya kilolo mkoani Iringa 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani iringa watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamemalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza uchumi wa taifa.

Akizungumza wakati wa kuangalia amani ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema sasa imefika mwisho wa wilaya hiyo kuwa soko la wafanyakazi wa ndani.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka iringa kilolo sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawakamata na kuwafungulia kesi serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Abdallah

Abdallah aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka shule watoto waliofaulu kinyume cha hapo wazazi watachukulia hatua kali.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubari hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Abdallah

Aidha Abdallah aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo.
“Acheni kuwavulia chupi wanaume mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu kama mimi ambavyo leo hiii nimekuwa kiongozi wenu kwa kwasababu nilikataa kuvua chupi nikiwa na umri kama wenu ndio maana leo hii nipo hapa”alisema Abdallah

Aidha Abdallah aliwapongeza walimu wa shule za msingi za wilaya ya kilolo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri wilaya ya kilolo kupitia elimu.

“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu wa wilaya hii kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika wilaya yangu ya kilolo na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Abdallah

Kwa upande wake diwani wa kata ya boma la ng’ombe Anderson Mdeke alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba shuleni limekuwa sugu hivyo wameanza kuridhibiti na limepungua kwa kiasi kikubwa.

“Kwa kweli tatizo la mimba kwenye shule za kata yangu ya lipo na tumeanza kutafutia ufumbuzi ili kulikosesa kabisa ili watoto wetu wasome bila kuwa na buguza” alisema Mdeke

Naye mwalimu wa shule ya msingi Mwanzala Grace Magawa alikiri kuwepo kuwepo kwa mimba za utotoni katika  baadhi ya shule za msingi za wilaya ya kilolo kutokana mazingira yanayowakabili baadhi ya wanafunzi ndio husababisha mimba za utoto.


“Mwanafunzi akirudi nyumbani anawakuta wazazi wake washakunywa pombe na hawana habari ya kuulizia maendeleo ya mtoto wake hivyo mtoto anaamua kufanya anachotaka kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi wake au walezi wake” alisema Magawa

DC MSHAMA AAGIZA WAKURUGENZI KUHAKIKISHA WANAFUATILIA WATUMISHI WA AFYA WALIOAJIRIWA NA MFUKO WA PEPFAR KUPITIA THPS MKOANI PWANI

September 07, 2017
Mkuu wa Wilaya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). Mkuu wa Wilaya Kibaha Assumpter Mshama alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Maggid Mwanga akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
Mkurugenzi wa THPS Dk. Mbatia akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo na kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everist Ndikilo
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi Dk. Beatrice (RMO PWANI) iliyotolewa na wafanyakazi wa THPC kutokana na mchango wake katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi pamoja na cheti Batuli Mituro ya Muuguzi bora kutoka kituo cha Ikwiriri HC katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akipatiwa maelezo juu ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kina kutoka kwa mtaalamu wa THPS.
Mgeni rasmi Assumpter Mshama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa THPS

MBUNGE AITAKA TBS KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO

September 07, 2017
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba akizungumza wakati akifungua semina kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani Muheza inayofanyika kwa wiki nzima ambayo aliiandaa lengo kubwa likiwa kuwawezesha kuzitengenezea ubora bidhaa
zao wanazozalisha.



Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba katikati akifuatilia kwa umakioni mafunzo hayo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba wa kwanza kulia akifuatilia kwa umakini semina hiyo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba akifuatilia namna ya utengenezaji wa sabuni za maji kushoto ni Katibu wake
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba kulia akiangalia namna sabuni ya maji inavyotengenezwa wakati wa semina hiyo
Baadhi wataalamu wakichanganya sabuni ya maji
Wajariamali wilayani Muheza wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Mbunge huyo
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafikia wajasiriamali wadogo wadogo nchini kwa kufungua ofisi zao kwenye ngazi za wilaya na mikoa ili kuwasaidia kuepukana na hasara wanazoipata kutokana na bidhaa zao kutokukidhi viwango.

Uwepo wao katika maeneo hayo utasaidia wajasiriamali hao kuweza
  kutengeneza bidhaa bora ambazo zitawawezesha kuweza kuingia kwenye soko la ushindani ili kupata mafanikio.

Ushauri huo ulitolewa  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga
  kupitia (Chadema), Yosepher Komba  wakati akifungua semina kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani Muheza inayofanyika kwa wiki nzima ambayo aliiandaa lengo kubwa likiwa kuwawezesha kuzitengenezea ubora bidhaa
zao wanazozalisha.

Alisema mara nyingi wajasiriamali wamekuwa wakikumbana na changamoto
  ya bidhaa zao kuambiwa hazijakidhi viwango hivyo iwapo TBS watashuka chini kwa wananchi hususani wajasiriamali itasaidia kuondokana na adha za namna hiyo.

“Ukiangalia wajasiriamali hasa wa maeneo ya vijijini wamekuwa

wakikumbana na changamoto nyingi hasa mara baada ya kuzalisha bidhaa zao au kuzitengeneza wanapokuwa wakizipelekea sokoni wanaambiwa hazina ubora hivyo TBS tumieni nafasi hiyo kuwafikia wananchi hao “Alisema

Aidha pia aliwataka wajasiriamali kuhakikisha wanapozitengeneza bidhaa
  zao ni lazima kuzipeleka kwenye shirika la viwango ili kuweza kupimwa ubora zilizonazo badala ya kuziingiza sokoni.

“Lakini kwa watengenezaji wa sabuni za maji msije mkatafuta soko kwa
  kuchukua maji mengi kuweka wakati wa uzalishaji wake hivyo ni kuharibu ubora wa bidhaa yako badala yake muweni wabunifu “Alisema.

Akiwa akizungumza mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Gerald Nyaisa
  ambaye ni mkulima wa mbogamboga wilayani Muheza alisema wataumia mafunzo hayo ili kuweza kuongeza thamani ya bidhaa zao wanazozalisha .

Alisema umuhimu wa semina hiyo hasa kwa wajasiriamali ni muhimu
  kutokana na uwepo wa sera ya Tanzania ya Viwanda ambayo inawagusa wakulima kwa asilimia kubwa katika harakati za kukuza uchumi.

“Lakini pia nitoe wito kwa vijana waweze kujikita kwenye kilimo na
  ujasiriamali badala ya kuendelea kukaa vijiweni ambako wanapoteza muda mwingi ambao wangeweza kuutumia katika uzalishaji “Alisema.

Mafunzo hayo yalihusisha vikundi nane vya wajasiriamali kutokana
  maeneo mbalimbali wilayani humo ambavyo ni Muinuano Group,Wamama Wajasiriamali,New Muheza Investment, Bodaboda,Uvumilivu, Harakati Vicoba
Group Mshikamano Juu na Kikundi kipya cha genge Mzee.

JOE FALTER ACHAGULIWA KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA JUMIA TRAVEL

September 07, 2017
KAMPUNI inayojishughulisha na huduma za hoteli na tiketi za ndege kwa njia ya mtandao barani Afrika, Jumia Travel imemtangaza Bw. Joe Falter (pichani) kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu mpya akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Paul Midy ambaye amechaguliwa kushika wadhifa mkubwa zaidi kwenye makampuni ya Jumia. Bw. Falter ambaye pia ni mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni dada ya Jumia Food, amechukua majukumu hayo ikiwa ni jitihada za kuimarisha zaidi shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo.

TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM

September 07, 2017


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.
Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera,  kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe. Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji, kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye bwawa hili, alisisitiza.
Mkuu huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“ Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw. Shekimweri.


Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Mtandao wa Jinsia watoa tuzo kwa Halmashauri za Kisarawe na Kishapu

Mtandao wa Jinsia watoa tuzo kwa Halmashauri za Kisarawe na Kishapu

September 07, 2017
 
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule ( wa pili kushoto) akimpongeza Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kulia) kwenye Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akipongeza. 
Burudani kutoka kwa msanii Misoji Mkwabi (wa kwanza kushoto) kwenye Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.[/caption] MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imetoa tuzo, kuzitambua na kuzipongeza halmashauri za wilaya ya Kishapu na Kisarawe baada ya kutenga sehemu ya bajeti zao kwa ajili ya kujali huduma za wanawake na watoto. Halmashauri ya Kishapu tayari imetenga shilingi milioni 279.5 katika mwaka wa fedha 2017/18 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba maalumu 33 vinavyotumiwa na wasichana shuleni kwa ajili ya kujistili wawapo katika siku zao. Kwa upande wa Halmashauri ya Kisarawe imepewa tuzo kwa ajili ya kufanikiwa kuwawezesha wanawake katika wilaya hiyo, ambapo imetenga asilimia 5 ya mapato yao na kuzitumia katika kuwawezesha akinamama. Tuzo za halmashauri hizo mbili zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akizinduwa rasmi Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Ofisa Elimu Msingi wilayani Kishapu, inakiri kuwepo na changamoto ya watoto wa kike kukosa maeneo ya kujisitili wawapo shuleni na kuingia katika siku zao. Halmashauri ya Kishapu imeanza kuchukua hatua kwa kujenga vyumba maalumu shuleni kwa kushirikisha nguvu za wananchi ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike. Taarifa kutoka Kituo cha taarifa na maarifa Kata ya Songwa, zinaeleza kuwa wanafunzi wa kike katika shule za msingi na sekondari wilayani Kishapu hupoteza siku 40 za masomo kwa kila mwaka kutokana na shule nyingi wilayani humo kutokuwa na vyumba maalumu vya kujihifadhi pale wanapokuwa katika siku zao.    
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi ya akinamama. 
Deo Temba (kushoto) akizungumza jambo na mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia) na mmoja wa waalikwa katika Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. 
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kulia) akiteta jambo na Mama Getrude Mongela. 
Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017 wakifurahiya jambo na Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuzinduwa tamasha hilo.___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com