HARUSI YA MISS MILIKA BINAGI NA BWANA SAMWELI CHACHA WA TARIME MKOANI MARA YAFANA.

March 19, 2016
Kushoto ni Bwana Harusi JOHN SAMWEL CHACHA akiwa pamoja na Bibi Harusi Milika Daniel Binagi, katika hafla ya harusi yao iliyofanyika Juzi Alhamisi Machi 17,2016 Rebu, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Picha Zaidi BONYEZA HAPA
Mkuu wa MKoa wa Morogoro afunga kikao kazi cha 11 cha maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Mkoani Morogoro.

Mkuu wa MKoa wa Morogoro afunga kikao kazi cha 11 cha maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Mkoani Morogoro.

March 19, 2016

oll1
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiongea na maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe(wa tatu kutoka kulia) kufunga kikao cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika Mkoani Morogoro.Wengine pichani  ni Mwenyekiti  mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw.Assah Mwambene(wa kwanza kulia),Kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ikulu Bw.Gerson Msigwa(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa chama cha maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali(TAGCO) Bw.Innocent Mungi.(wa pili kulia).
oll2
: Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe wakati alipokuwa akifunga kikao cha 11 cha maafisa hao mkoani Morogoro.
oll3
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe akiongea  na maafisa habari na mawasiliano wa Serikali  wakati akifunga kikao kazi cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika mkoani Morogoro.
oll4
Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw,Kebwe Steven Kebwe(wane kutoka kushoto waliokaa) mara baada ya kumaliza kikao kazi mkoani Morogoro.
oll5
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe akiongea  na maafisa habari na mawasiliano wa Serikali  wakati akifunga kikao kazi cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika mkoani Morogoro.

Washindi wa promosheni ya Kwea Pipa kwenda Barcelona watangazwa

March 19, 2016

 Mshindi wa  wa Promosheni ya kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu Jamal Othman mkazi wa Lushoto, Tanga akikabidhiwa mfano wa hundi toka kwa Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta na Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam Media, Mgope Kiwanga katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Tigo Makumbusho jijini Dar es salaam.


Mshindi wa  wa Promosheni ya Kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu Ismail Salim mkazi wa Dar es salaam akikabidhiwa mfano wa hundi toka kwa Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta na Meneja wa idara ya michezo Azam Media Baruan Muhuza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Tigo Makumbusho jijini Dar es salaam.


Washindi wa  wa Promosheni ya Kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Tigo na Azam Media  katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Tigo Makumbusho jijini Dar es salaam.







Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa washindi wawili wa wa Promosheni ya  Kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu



Waandishi wa habari  wakichukua matukio wakati wa kutangaza Washindi wa  wa Promosheni ya Kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu 
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

RC PAUL MAKONDA AZUNGUMZA NA WENYEVITI NA MAOFISA WATENDAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM UKUMBI WA MWALIMU NYERERE LEO

March 19, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mambo mbalimbali hasu suala la usafi wa mazingira.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania, Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.
 Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)
Maofisa Watendaji na Wenyeviti wa Manispaa ya Kinondoni wakipiga makofi kwenye mkutano huo.
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI

March 19, 2016
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.
Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.
TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).
Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.

Tanzanias happy with implementation speed of the proposed construction of the Tanzania-Uganda crude oil pipeline

March 19, 2016
By Sultani Kipingo
Tanzanians are happy with the implementation speed of the proposed construction of the Tanzania-Uganda crude oil pipeline which is expected to start in August this year, and will be completed in 2019. 
Many of those interviewed expressed gratitude to President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and his Tanzanian counterpart Dr. John Pombe Joseph Magufuli for initiating the 4-billion-U.S. dollar oil pipeline project that is expected to hasten socio-economic development between the two nations.
“We are overwhelmed by the rapidity of the project considering only two weeks have  passed since  Presidents Museveni and Dr. Magufuli  jointly approved the project when they met in Arusha. 
“It is unbelievable to note that officials from both sides have this week signed the agreement and come August the construction work takes off”, said Ms Natala Kimaro of Moshi. 
Amani Abdallah of Tanga  said that the 1,403-kilometer pipeline that will link oil fields in Uganda’s Lake Albert, Hoima region to Tanga port in Tanzania is testimony to true East African integration spirit, hoping more such projects would be initiated. 
The construction of the crude oil pipeline will be carried out by three oil firms–UK’s Tullow Oil PLC, France’s Total E&P and China’s Cnooc. Once completed, the pipeline is expected to transport up to 200,000 barrels per day passing through a number of Tanzanian regions from the Indian Ocean port of Tanga to Uganda. 
The construction will lead to installations of 200km of permanent new roads and corresponding bridges, and upgrades to 150km of existing roads, opening up regional integration in the energy sub-sector. 
 Tanzanians are also happy that that the crude oil pipeline project will also increase foreign Direct Investment  by more than 50 percent per annum, let alone creating over 15,000 jobs.
Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli announces the crude oil pipeline project to reporters after his meeting with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit 
"The project will be implemented at Dr. Magufuli's  speed" jokes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda when confirming  the project to reporters after talks with his host President Dr. John Pombe Joseph Magufuli on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit. 
Tanzania's Minister for Energy and Minerals  Prof. Sospeter Muhongo (second left) and Uganda's Minister for Energy and Minerals Development Engineer  Irene Muloni ( wa tatu right), with the Managing Director of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) Dr. James Mataragio  (left) and the General Manager of  Total E&P Uganda, Mr Adewale Fayemi (second right) sign the crude oil pipeline project implementation plan in Arusha on March 17, 2016. Seated extreme right is Permanent Secretary Ministry of  Energy and Minerals Development of Uganda Dkt. Kabagambe Kaliisa 
Map of the proposed crude oil pipeline project

BREAKING NEWS SUKARI KUTOKA NCHINI BRAZILI ,INDIA YAKAMATWA TANGA

March 19, 2016
KAMANDA WA POLISI MKOANI TANGA,KAMISHNA MSAIDIZI WA JESHI LA POLISI,LEONARD PAULO AKIANGALIA SHEHENA YA SUKARI ILIYOKAMATWA IKITOKEA VISIWANI ZANZIBAR INAYOTOKA NCHINI BRAZILI NA INDIA IKIINGIZWA BILA KULIPIWA USHURU

MKUU WA MKOA WA TANGA,MARTINI SHIGELLA AKINYAJUA JUU SUKARI ILIYOKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA KUSHRIKIANA NA TRA ILIYOINGIZWA NCHINI KWA NJIA ZA PANYA IKITOKEA NCHINI INDIA NA BRAZILI




UTEUZI WA MKAPA UNATIA MATUMAINI - BAN KI MOON

March 19, 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, taarifa yake kuhusu ziara yake aliyoifanya hivi karibuni nchi Burundi. Katika taarifa yake ameelezea kutiwa matumaini na uteuzi wa Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa kuwa Mwezeshaji wa majadiliano ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana Ijumaa uliojadili kuhusu Burundi. Aliyeketi nyuma ya Balozi, ni Bw. Khamis Abdallah Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi, Bw. Alain Amic Nyamitwe naye akielezea hali ya mambo na jitihada mbalimbali ambazo serikali ya Burudi imekuwa ikichukua katika kurejesha hali ya amani na utulivu.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika mkutano wao wa Ijumaa ambapo baada ya kupokea taarifa kuhusu Burundi, waliendelea na kikao chao cha ndani.

Na Mwandishi Maalum, New York

Wakati Mwezeshaji wa majadiliano kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa ameanza mchakato wa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema, uteuzi wa Benjamin Mkapa unatia matumaini.

Ban Ki Moon ametoa kauli hiyo jana Ijumaa, wakati alipokuwa akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, taarifa kuhusu ziara yake aliyoifanya nchini Burundi mwezi uliopitia.

“ Uteuzi uliofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kumteua Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa mwezeshaji wa majadiliano kuhusu Burundi ni maendeleo yanayotia moyo”. Amesema Ban Ki Moon.

Na Kuongeza, ni lazima Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika, Jumuiya na Umoja wa Mataifa kusaidia utalamu wa hali ya juu wa usuluhishi ambao Burundi unahitaji. Akielezea zaidi kuhusu ziara aliyoifanya nchi Burundi ziara iliyomwezesha kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Kisiasa akiwamo Rais wa Nchi hiyo Bw. Piere NKurunzia. Ban Ki Moon, amesema hakuna njia mbadala zaidi ya mazungumzo ya kisiasa ambapo pande zinazopingana zitakaa katika meza ya mazungumzo.

Akasema, wakati wa ziara hiyo iliyofuatia baada ya wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama kufaya ziara yao, alitoa wito kwa wadau wa pande zote kutorejea kule walikotoka akimaanisha vita vilivyosababisha vifo vya wananchi wengi wa nchi hiyo kabla ya kupatika kwa Mkataba wa Amani wa Arusha ( The Arusha Agreement).

“ Nilitoa wito kwa pande zinazopinga na wananchi wa Burudi kutorejea kule walikotoka na waonyeshe dhamira ya dhati ya kukaa katika meza ya mazugumzo yatakayokuwa jumuishi na umoja wa kisiasa kwa kuwa hiyo ndiyo njia sahihi na pekee ya kutatua mgogoro wao “. Akasisitiza Ban Ki Moon.

Ban Ki Moon ameeleza zaidi kuwa aliwaeleza viongozi wa Burundi kwamba kusainiwa kwa Mkataba wa Arusha Agosti 2000 uliotokana mahasimu kukaa meza moja na kukaa katika meza na kukubaliana kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe pia ulifungua ukurasa mpya wa maridhiano na kushirikiano wa kuijenga nchi yao.

Akabanisha kuwa Rais wa Burundi wakati wa mazungumzo yao aliahidi kutekeleza mambao kadhaa yakiwako ya kuwaachia huru wafungwa wakiwamo viongozi wa upinzani, kutoa uhuru kwa vyombo vya habari pamoja na kusitisha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji ya holela.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizugumza kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ameliambia Baraza Kuu la Usalama kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, kama Mwenyekiti wa EAC, anaamini kwa dhati kabisa kwamba hali ya kisiasa nchini Burundi inaishughulisha siyo tu Ukanda wa Afrika ya Mshariki, bali pia Jumuiya ya Kimataifa.

“ Hali ya Kisiasa inaishughulisha EAC na Jumuiya ya Kimataifa, siyo kwa sababu Burundi ni mwanachama wa EAC, lakini ni kutokana na ukweli kwamba athari za mgogoro wa Burundi zinaweza kutuathiri sisi sote ”. Akasema Balozi Manongi kwa niaba ya EAC.

Na kuongeza ni kwa kulitambua hilo ndiyo maana EAC inaendelea na juhudi zake za kutafuta suluhu ya kudumu nchini Burundi, na kwamba inakaribisha juhudi zinazofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa za kushirikiana na Burundi na Kanda ya Afrika Mashariki.

“Sisi kama Jumuiya ya Afrika Mashariki tunaomba juhudi hizi tunazozikaribisha ziende sawia na hatua za kuboresha na kusaidia mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya watu wa Burundi, ikiwani pamoja na kuisaidia kuimarisha mifumo na Taasisi zake za kiutawala.” Amesisitiza Balozi Manongi.

Msemaji huyo wa EAC akabinisha kwa kusema , hapana shaka pana mambo mengi yanayochangia uwepo wa hali tete ya kisiasa nchini Burundi. Mambo anayosema yanapashwa kujadiliwa wa uwazi na katika ujumla wake. Na kwamba EAC inawashukuru wale wote ambao wamekuwa wakiunga mkono jitihada zinazofanywa na EAC.

Akizungumzai kuhusu utezi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya Burundi akimsaidia Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Balozi Manongi amesema, EAC imetiwa na inashukuru kwa kauli za kutia moyo za kuukubali uteuzi wa Rais mstaafu Mkapa.

Akasema katika juhudi zake za kuisaidia Burundi na watu wake alizofanya wakati wa mchakato wa Amani wa Arusha. Mkapa alisema yafuatayo “ Suluhu endelevu kuhusu mgogoro wa Burundi unatakiwa kutoka ndani ya majadiliano ambayo wadau wote wenye dhamana kuhusu Burundi watashiriki kwa uhuru. Suluhu endelevu inatakiwa kumilikiwa na kuheshimiwa na washiriki wote wa mchakato wa kutafuta amani. Shinikizo kutoka nje haiwezi kuleta suluhu ya kudumu”

Balozi Manongi akabanisha kwamba maneno hayo aliyoyasema Rais Mstaafu wakati huo bado yana matinki na uzito katika mazingira na hali ya sasa ya Burundi.

Na kuongeza , inatia moyo kuwa Rais Mstaafu Mkapa amekwisha anza ziara za awali za kuwatembelea viongozi na wadau mbalimbali ndani ya EAC kwa lengo la kuhakikisha kwamba viongozi na wahusika wote wanakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu dhamana mpya aliyokabidhiwa. Na amewahakikishia viongozi wa EAC dhamira yake, kujituma kwake, uwazi na ujumuishi katika utekelezaji wa dhamana hiyo.

“Rais Mstaafu Mkapa anahitaji uungwaji mkono wa dhati na ushirikiano kutoka pande zote nchini Burundi, katika EAC na katika Jumuiya ya Kimataifa” akasisitiza Balozi Manongi.

Wengine waliotoa taarifa zao kuhusu hali ya Burundi alikuwa ni Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Prince Zeid Raad Hussein, Mwenyekiti wa Burundi Configuration Balozi Jurg Lauber na Bw. Alain Amic Nyamitwe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Burundi.

JOPO LA NGAZI YA JUU KUHUSU UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI LAZINDULIWA

March 19, 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon (katikati) akiwa na wenyeviti wenza wa Jopo a ngazi ya juu kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Jopo siku ya uzinduzi wa Jopo hilo uliofanyika sambamba na mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake (CSW) unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa
Wenyeviti -Wenza wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, Rais wa Costa Rica, Mhe. Luis Guillerma Solis na Mkurugenzi Mtendaji wa IKEA Switzerland Bi. Simona Scarpaleggia wakibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi, mara baada ya kundi hilo kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mapema wiki hii. Mmoja wa wajumbe wa Jopo ambao idadi yao ni 21 ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu. Ban Ki Moon ameunda Jopo hilo ili limpatie maoni na mapendekezo kuhusu uwezeshwaji wa mwanamke kupitia utekelezaji wa Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Na Mwandishi Maalum, New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezindua Jopo la Nganzi ya Juu ambalo ameliunda kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekeo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Jopo hilo ambalo linaundwa na viongozi na wataalamu wa kada mbalimbali linaongozwa na WenyeViti -Wenza ambao ni Rais wa Costa Rika, Mhe. Luis Guillerma Solis na Bi. Simona Scarpaleggia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa IKEA Switzerland.

Wajumbe wa Jopo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, Mkuu wa Banki ya Dunia, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha ( IMF) Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Mkurugenzi Mtendaji wa UN- WOMEN, wapo pia Maprofessa na wataalamu wa uchumi, watafiti, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi kutoka serikalini, wataalamu wa masuala ya jinsia na fursa sawa na wafanyabiashara. Kwa pamoja jopo hilo linakuwa na wajumbe 21.

Mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jopo hilo, Marchi 15 sambamba na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake. Wenyeviti- wenza walianza ratiba ya kukutanana na Wenyeviti wa Makundi ya Kikanda ya Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa madhamuni ya kupata ushauri na mawazo yao ya awali kuhusu mapendekezo ya nini Jopo hilo linatakiwa kuzingatia katika utafiti wake na hatimaye kile kitakachoingizwa kwenye andiko lao.

Mwenyekiti wa Kundi la nchi za Afrika, kwa mwezi Marchi, Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongini mwa wenyeviti waliokutana na wenye-viti wenza wa Jopo, ambapo aliwasilisha baadhi ya maeneo ambayo Afrika inaamini kwamba yakiendelea kutiliwa mkazo yatachagiza kasi ya kuwainua wanawake kiuchumi.

Baadhi ya maeneo hayo ni fursa ya wanawake kupata elimu pamoja na elimu ya juu, upatikanaji wa mitaji na mikopo, nafasi za uongozi zikiwamo za kisiasa, umiliki wa mali na haki ya kumiliki ardhi, afya ya uzazi na uzazi wa mpango na salama, kuondokana na umaskini na affirmative action na fursa za kupata misaada na ushauri wa kisheria.

Balozi Manongi amewaeleza wenye-vita wenza wa Jopo kuwa mapendekezo anayowasilisha kwa niaba ya nchi za Afrika si mpya kwani yanaendelea kufanyiwa kazi na serikali mbaliambali. Lakini ni Imani ya Afrika kwamba kama yakiendelea kupewa msukumo unaostahili pamoja na mengine yatakayokuwa yanawasilishwa kwa Jopo bila shaka kasi ya uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi itakuwa kubwa zaidi.

Jukumu la Jopo hilo la Uwezeshwaji wa Wanawake kiuchumi pamoja na mambo mengine ni kutoa mapendekezo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya uwezeshwaji wa wanawake kupitia utekelezaji wa Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu kwa kuboresha matokeo ya kiuchumi kwa wanawake, kupaisha uongozi wa wanawake katika kusukuma mbele ajenda 2030 ambayo ni jumuishi, endelevu na inayojali mazingira.

Vile vile Jopo litatakiwa kutoa mapendekezo ambayo watendaji na watoa maamuzi serikalini, katika sekta binafasi, Taasisi za Umoja wa Mataifa, na wadau wengine wataweza kuyafanyia kazi. Ripoti ya kwanza Jopo inatarajiwa kuwasilishwa mwezi Septemba 2016.