ESRF YAKUTANISHA WANAZUONI KUANDAA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TANZANIA

ESRF YAKUTANISHA WANAZUONI KUANDAA RIPOTI YA MAENDELEO YA BINADAMU TANZANIA

June 13, 2016
MAANDALIZI ya Ripoti ya pili ya Maendeleo ya Binadamu (THDR) inayotarajiwa kuzinduliwa Juni 2017 yamefikia katika ngazi ya mwisho ya ukusanyaji wa maoni ya kitaalamu katika mada mbalimbali zinazojadiliwa katika ripoti hiyo.

Maandalizi hayo yanayowezeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na wadau wengine yanafanyika kwa mfumo wa warsha ya siku mbili jijini Dar es salaam, jana Jumatatu na

Katika warsha hiyo ya rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya uhariri, inajadiliwa na wanazuoni kupitia mada 11 ambazo zitakuwapo katika taarifa hiyo ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.

Warsha hiyo ya siku mbili itatoa msingi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini kwa kuangalia Sera ya hifadhi ya jamii katika muktadha wa mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa jana baada ya ufunguzi wa kongamano hilo uliofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida ni usambazaji wa maji kwa kuangalia sera, fedha na upatikanaji wake; elimu; sera ya jamii na mabadiliko ya kiuchumi; na hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akifungua warsha ya siku mbili iliyowakutanisha wanazuoni kuandaa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es Salaam. (Picha na Modewjiblog)

Akifungua kongamano hilo Dkt. Kida aliwataka wadau wote kutambua kwamba kazi wanayoifanya ni ya muhimu sana kwa taifa kwani imekuwa chanzo cha upangaji wa mipango ya maendeleo na namna inavyostahili kuwa.

Alisema mpango wa pili wa maendeleo nchini kuelekea uchumi wa kati umechukua fikra na falsafa nyingi kutoka katika taarifa ya Maendeleo ya Binadamu iliyofanyiwa mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka 2015.

Mpango wa maendeleo wa pili wa miaka mitano uliozinduliwa wiki iliyopita umetumia vionjo vingi kutoka katika ripoti iliyopita na hivyo ni vyema wadau wakachangia mada hizo na kuzipa uhai mkubwa zaidi kwa manufaa ya Ripoti ijayo alisema Dkt. Kida.

Aidha aliwataka wahusika wote kuwa karibu na ESRF wakati wa uandishi wa mwisho ya ripoti hiyo baada ya kumalizika kwa kongamano hilo.
Mtafiti mwandamizi mshiriki na Mshauri wa kiufundi wa mradi wa THDR, Marc Wuyts akizungumzia mada ya uhusiano wa sera ya jamii na mabadiliko ya kiuchumi katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea jijini Dar esSalaam.

Akizungumza uhusiano wa sera ya jamii na mabadiliko ya kiuchumi (Situating Social Policy in social economic transformation: A conceptual Framework) Mtafiti mwandamizi mshiriki na Mshauri wa kiufundi wa mradi wa THDR, Marc Wuyts alisema iko haja ya kutambua kwamba mabadiliko ya kiuchumi yatafanikiwa kwa kuongeza ufanisi na tija ya kiuchumi kabla ya kugawa manufaa yake kuimarisha huduma za kijamii.

Alisema kukosekana kwa maunganisho na kuanza kutekeleza sera za jamii na kusahau misingi ya kuinua uchumi, ndio uliokwamisha siasa za Ujamaa na kujitegemea za Rais Julius Nyerere.

Alisema ipo haja kubwa ya kutambua muunganiko na kipi kinafaa kuanza kwanza ili kufanikisha maendeleo na ustawi wa binadamu na kutahadharisha kwamba tafiti yoyote ambayo haitazingatia ukuaji wa uchumi kwanza hayatapeleka taifa hili katika uchumi wa kati.

Alisema utekelezaji wa mpango wa Mkukuta utafanikiwa ikiwa kutaangaliwa namna ya kuunganisha mpango huo na sera ya maendeleo ya kupeleka taifa katika uchumi wa kati.

Kumekuwa na dhana kwamba utekelezaji wa sera zinazonyanyua hifadhi ya jamii kunaimarisha uchumi lakini huwezi kutumia ambacho hujakizalisha.
Profesa Flora Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es salaam akizungumzia upatikanaji wa maji, usambazaji, gharama na sera zake wakati wa kujali vipengele muhimu katika taarifa ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017 katika warsha ya siku mbili inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu huyo alisema kwa kufanya kitendo hicho unakuwa unakwamisha maendeleo ya kiuchumi kwa kuwa umetumia ambacho hujakizalisha.

Imani kuwa elementi zilizomo katika hifadhi ya jamii zinachochea ukuaji wa uchumi, ndio kisa kilichuokwamisha siasa ya ujamaa.

Mtaalamu huyo anaamini katika mada yake kwamba ujamaa ulijali zaidi kuwaweka watu katika hali bora na kusahau kushughulika na masuala ya kiuchumi na hivyo kuikwamisha siasa hiyo.

Alisema ustawi wa jamii kama usipoangaliwa hukwamisha ukuaji wa kiuchumi.

Mtaalamu mwingine Profesa Flora Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es salaam alizungumzia upatikanaji wa maji, usambazaji, gharama na sera zake (Water Provision in Tanzania- Access Financing and Policy Trends).
Profesa wa Elimu na Menejimenti yake, kutoka Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Herme Mosha akichambua kipengele cha elimu katika kuendeleza maarifa nchini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili iliyowakutanisha wanazuoni kuandaa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es Salaam.

Katika mada yake alisema kwamba bado kuna tatizo kubwa la utumiaji wa maji katika usafi na pia matumizi ya vyoo. Alisema japokuwa kumekuwepo na maendeleo katika matumizi ya vyoo, asilimia 11.5 hawana vyoo kabisa.

Aidha alitaja mikoa ya Mara, Arusha na Manyara kuongoza kwa kutokuwa na vyoo huku akisema wastani asilimia 7.5 hawana vyoo na Mara ikiongoza katika kundi hilo.

Mikoa yote hiyo ni ya wafugaji labda tabia zao za kuhamahama na mifugo yao zinachangia. Pia profesa huyo alisema kwamba matumizi ya maji unaweza kuona kama yapo ya kutosha kwa kuangalia suala la uoshaji mikono.

Alisema watu hawaoshi mikono kwa maji na sabuni na mkoa wa Dare s salaam unaongoza sana katika hilokwa wastani wa asilimia 21 huku maeneo mengine yakiwa katika wastani wa 7 hadi 9. Alisema upatikanaji wa maji ni muhimu katika kuonesha maendeleo ya binadamu.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wakiwasilisha maoni yao katika warsha ya rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya uhariri, inayojadiliwa na wanazuoni hao kupitia mada 11 ambazo zitakuwapo katika taarifa ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.

Naye Profesa wa Elimu na Menejimenti yake, kutoka Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Herme Mosha, akichambua elimu katika kuendeleza maarifa alizungumzia tatizo la hesabu nchini na kutaka juhudi za makusudi kuchukuliwa kukabiliana nalo kwani maendeleo ya rasilimali watu katika stadi ni muhimu sana kufikia uchumi wa kati.

Alipongeza serikali kwa kuweka uwiano mzuri wa jinsia katika shule na pia ongezeko la fedha kwa ajili ya maabara na uboreshaji wa elimu nchini.

Aidha amesema kwamba maamuzi ya makusudi ya serikali kurejesha vyuo vya kufunza stadi badala ya kuwa vyuo vikuu utasaidia kuwepo kwa wataalamu wanaostahili katika kufanikisha mapinduzi ya viwanda.

Mwenyekiti wa warsha hiyo ya siku mbili Prof. Amon Mbelle akitoa mwongozo wakati wa kupitia na kufanyia maboresho rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya uhariri wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanazuoni wanaoshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kupitia na kufanya maboresho katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanazuoni wanaoshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kupitia na kufanya maboresho kwenye Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es Salaam.
MADAWATI YALIYOKAMILIKA YAKABIDHIWE MASHULENI KWA MAANDISHI

MADAWATI YALIYOKAMILIKA YAKABIDHIWE MASHULENI KWA MAANDISHI

June 13, 2016


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezitaka halmashauri zote kuzikabidhi shule madawati yote ya likamilika kwa maandishi ili kuepuka udanganyifu na madawati hewa
Hayo ameyasema leo katika ziara yake ya kikazi halmashauri ya Busokelo wilaya ya Rungwe kukagua kazi ya utengenezaji wa madawati katka halmashauri
Amewashukuru wananchi, wadau na viongozi wa ngazi zote katika halmashauri zote Mkoa wa mbeya kwa namna walivyohamasika kuchangia utengenezaji wa madawati na anaamini Mkoa wa Mbeya itatekelezwa agizo la kukamilisha madawati ifikapo tarehe 39 juni ila kwa ajili ya kujiwekea sawa Mkoa umejieleza malengo ya kukamilisha tarehe 20 na kuna kila dalili zoezi hilo litakamilika kama ilivyopangwa

Amewataka viongozi wa halmashauri na watendaji kuyakabidhi madawati yote yaliyokamika kwa maandishi ili kudhibiti taarifa za madawati hewa kuficha ukweli na baadaye ibainike bado kuna upungufu. Naomba mkabidhi kwa kurejea taarifa ya upungufu kwa kila shule na si vinginevy 
Elimu ya udereva wa kujihami yawafikia madereva wa TBL Arusha na Moshi

Elimu ya udereva wa kujihami yawafikia madereva wa TBL Arusha na Moshi

June 13, 2016

VIK1 
Katika kuhakikisha  madereva wanaosambaza bidhaa za kampuni wanafanya kazi zao kwa ufanisi,kampuni ya TBL Group imeandaa mafunzo maalumu kwa madereva kutoka viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Moshi,Mbeya na Mwanza.
Mafunzo hao ambayo yamemalizikia mkoani Arusha yaliendeshwa na mkufunzi wa madereva kutoka kampuni ya CFAO Motors,Hubert Kubo ambaye amewapatia madereva hao elimu  ya udereva wa kujihami ikiwemo utunzaji wa vifaa wanavyoviendesha.
Baadhi ya madereva waliohudhuria mafunzo hayo walishukuru mwajiri wao kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali kuhusiana na kazi yao ambayo walidai yanawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi na kuwa na  uwezo wa kukabili changamoto mbalimbali za kikazi kwa urahisi.
VIK2 
Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha
VIK3 
Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha
VIK4 VIK5 VIK6

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELEA VITUO VYA AFYA MKOA WA KASKAZINI

June 13, 2016

Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na viongozi wa Chama na Serikali alipowasili Chaani Masingini kukagua kituo cha Afya cha kijiji hicho kufuatia mwaliko wa Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul- latif.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Kaskazi ‘A’ Hassan Ali Kombo na Daktari dhamana wa Wilaya hiyo Rahma Abdalla Maisra wakati akikitembelea kituo cha Afya cha Chaani Masingini.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatana na viongozi wa Jimbo la Chaani wakiangalia tanuri la kuchomea taka za kituo cha Afya cha Chaani Masingini alipotembelea kituo hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif akimkaribisha Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kuzungumza na wananchi waliofika kituo cha Afya cha Chaani Masingi ambacho kinahitaji matengenezo makubwa.
Waziri Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Donge na Kamati Kiongozi ya Jimbo hilo katika Kituo cha Afya cha Donge Wilaya Kaskazini B.
Mkuu wa kituo cha Afya Donge vijibweni Miza Ali Ussi akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho kujua changamoto zinazowakabili.
Mwakilishi wa Jimbo la Donge Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza katika mkutano huo (kulia kwake) ni Mkuu wa kituo cha Afya Donge Miza Ali Ussi. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR

Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amezitaka Kamati Kiongozi za Majibo kusimamia kikamilifu vituo vyao vya  Afya na kuhakikisha majukumu waliyopangiwa wanayatekeleza kikamilifu  ili kuimarisha huduma katika vituo hivyo.

Alisema Serikali imebadili mfumo katika kusimamia vituo vya afya kwa kuvipeleka moja kwa moja kwa jamii kusaidia huduma ndogo ndogo huku Serikali kuu  ikibakia na jukumu lake la msingi la  kuvipatia vifaa vya matibabu, dawa na mishahara ya wafanyakazi. 

Waziri Mahmoud Thabit Kombo alieleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya Afya vya Mkoa wa Kaskazini Unguja kujua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa vituo hivyo katika kutoa huduma bora.

Alisema huduma ya matengenezo madogo madogo, kulipia umeme na maji, kuviwekea uzio na ulinzi  sasa vipo chini ya  Kamati Kiongozi za Majimbo ambazo zinaundwa na Wabunge, Wawakilishi, Madiwani, Masheha na Mkuu wa kituo cha Afya husika.

Aliongeza kuwa hivi sasa Serikali haitoa kipaumbele kujenga vituo vipya vya Afya bali inaelekeza nguvu zake kuviimarisha vituo viliopo kwa kushirikiana na mradi wa ORIO na Milele pamoja na Kamati Kiongozi za Majimbo.

Aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Chaani kwamba kituo chao cha Afya cha Chaani Masingini, ambacho kimesitisha kutoa huduma kwa miaka mitano kutokana na kuwa kibovu, kitaanza kufanyiwa matengenezo makubwa hivi karibuni kupitia Mradi wa ORIO.

Waziri wa Afya aliwataka viongozi na wafanyakazi wa sekta ya Afya kuwapa ushirikiano wa karibu wakunga wa jadi ambao wanatoa mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua.

Alisema wakunga wa jadi bado wanaendelea kuaminiwa na wanachi wengi, hasa sehemu za vijijini, kutokana na huduma nzuri wanazotoa kwa wateja wao na ameshauri wapatiwe vitambulisho maalum  ili waweze kutambulika.

Aidha alisema Zanzibar imepata sifa kubwa mbele ya Jamii ya Kimataifa katika kupambana na Malaria na maradhi mengine yaliyokuwa yakiwasumbua wananchi, lakini hali sio nzuri katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga hivyo ametaka juhudi zaidi ifanywe kukabiliana na tatizo hilo.

Akinamama wa Jimbo la Chaani walimueleza Waziri wa Afya kuwa wanapendelea zaidi kujifungua kwa wakunga wa jadi kutokana na kauli zisizoridhisha kutoka kwa wakunga wa vituo vya Afya wanapokwenda kujifungua.

Walishauri kutolewa elimu ya ukarimu na upole kwa wakunga wa vituo vya afya ili kuwajengea imani wajawazito kwenda kujifungulia kwa wingi katika vituo hivyo.

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba yupo tayari kutoa kila msaada unaotakiwa ili kuona huduma za Afya katika Jimbo hilo zinaimarika.

Waziri wa Afya alitembelea vituo vya Afya vya Chaani Masingini, Chaani Kikobweni na Kituo cha Afya   Donge.

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

June 13, 2016

Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli (katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo leo asubuhi mjini Dodoma.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Wabunge wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AGAWA FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NA KUJIONEA MABASI YA MWENDO KASI

June 13, 2016

index 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa
watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shughuli hiyo maalum ya kukabidhi furati na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum, Jangwani jijini Dar es salaam.( Picna na OMR)
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwaleakitoa neno la shukrani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya shughuli ya kukabidhi futari na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum kukamilika.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es salaam ambayo kwa kiasi kikubwa yamerahisisha usafiri na kutaka wananchi kuyatunza mabasi hayo.

KAMERA YA GLOBU YA JAMII NA TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BARABARA YA MBEYA TUNDUMA....

June 13, 2016

Pichani ni Muonekano wa Barabara ya kutoka Mbeya kuelekea Tunduma mpaka Mkoani Rukwa, na hiki ni Kipande Kidogo cha Njia panda ya Mlowo Mbozi Mkoani Songwe kama ambavyo kinaonekana katika Taswira ni chenye Kumeremeta.
Hiki pia ni kipande Kidogo cha Barabara hiyo ya Mbeya Tunduma na hapa pia ni Njia panda ya kuelekea Vwawa ni mara baada ya kutoka Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.
Baadhi ya Wafanya Bishara Wa Kuza Matunda Wakiwa katika Kilinge chao Cha kufanyia Biashara Zao eneo la Mpemba Wilayani Momba..
Wataalamu wa kuendesha Gari Ng'ombe wakiwa Sambamba na Gari lao Kando kando ya Barabara hiyo..
Gari Ng'ombe likianza Safari ya kuchanja Mbuga...
Baadhi ya Wakazi wa Eneo la Mlowo Mbozi wakiwa Wamekaa Kando Kando ya Barabara hiyo bira kuwa na Hofu Ya Kuogopa Magari.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAPISHWA NA KUPOKELEWA MAKAO MAKUU YA WIZARA.

June 13, 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.