MAMBO MUHIMU KUMI UNAYOPASWA KUMWAMBIA MPENZI WAKO KILA SIKU

February 04, 2015
Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu marafiki zetu.
1. Nakupenda: Ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.
2. Nilikuwa nakuwaza: Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja.Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?: Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.

4. Unga mkono maamuzi mazuri ya mpenzi wako: Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingineupande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha uhusiano wenu.
5. Mwambie mpenzi wako kuwa Umependeza: Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.


6. Samahani ni neno zuri kwa mpenzi wako: Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.


7. Hakuna kama wewe: Mpenzi wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye ni bora na hakuna kama yeye.


8. Napenda mawazo yako Picha: StudioMwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona anaakili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.


9. NakuheshimuKama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.


10. Napingana na hilo: Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila kitu na hakuna mwanamke anayetakakuzaa watoto na mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya kila mmoja. 


Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wakomtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.11. Usiku mwemaTunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka bahari, hivyo hakuna kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’ mwema.Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana,

MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

February 04, 2015

DSC_0100

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari  (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king’amuziki kipya cha  DStv HD  leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.
Akizungumza  na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam,  Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.
Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.
“Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu  hivyo ni wakati wa kuchangamkia  ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
DSC_0239
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king’amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.
Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.
 King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.
Kwa upande wake,  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu  aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa  DStv,  kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh  39,000/ tu.
DSC_0140
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king’amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati ambapo  bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara  ya kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa,  siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.
“Huduma za DStv  siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu.  Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo… Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.
DSC_0194
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king’amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/  kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/  ambayo pia ni ofa. Ving’amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.
Katika hatua nyingine, DStv  wamezindua huduma mpya  kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv  kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’,  Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet,  na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.
Akielezea, juu ya huduma hiyo,  Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama  Tablet na kisha kujisajili kupitia ‘App’   kwa kujisajili kwa kuandika  ‘DStv Now’.
Aidha, Ronald  Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya  DStv Now  ni kwa wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.
Pia  kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti  ya DStv.com
DSC_0209
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving’amuzi vya DStv kupitia akaunti zao.
DSC_0225
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now “application” inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop)  unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com
DSC_0228
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.
DSC_0247
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king’amuzi kipya cha DStv HD.

Wateja wa Airtel kushinda gari Moja Kila Siku

February 04, 2015

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Levi Nyakundi (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Beatrice Singano Mallya (kulia) wakionyesha kipeperushi wakati wakizindua rasmi  promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapowateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kushinda kila siku gari  moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyoulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Levi Nyakundi (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Beatrice Singano Mallya (kushoto) wakionyesha baadhi magari yatakayoshindaniwa wakizindua rasmi  promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari  moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mwendesha pikipiki akinyesha umahiri wake kunogesha wa uzinduzi  wa promosheni ya 'Airtel Yatosha Zaidi' ambapo wateja watakaojiunga na bando la yatosha watapata nafasi ya kujishindia kila siku gari  moja aina ya Toyota IST. Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
********
Airtel Tanzania leo imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya AirtelYatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
 
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. Nia yetu kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.
 
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi “Aliongeza Nyakundi
 
Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi.  hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku.
 
Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza  Mallya
 
Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au  kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima.
 
Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake.

DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA MKOANI TABORA

February 04, 2015

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sikonge mkoani Tabora wakati alipopita kukagua barabara za mkoa huo. Dkt. Magufuli aliwaahidi wananchi hao wa Sikonge kuwa Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mpanda-Tabora kupitia Sikonge yenye zaidi ya kilomita 359 itakayofadhili na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Sikonge mara baada ya kuwahutubia.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila kushoto akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kabla ya kuhutubia mkutano kwa wananchi wa Tabora. Waziri Magufuli aliwaeleza wananchi kuwa Wizara ya Ujenzi itawasimamia kikamilifu Wakandarasi wanaojenga barabara katika mkoa huo na kuhakikisha miradi yote inakwisha kwa wakati.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Tabora kuhusu ujenzi barabara za mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisalimiana na wananchi mara baada ya mkutano wake alioufanya Tabora mjini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila akihutubia wananchi katika mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Col.Ngemela Eslom Lubinga akimuonesha Waziri wa Ujenzi ramani ya Wilaya ya Mlele katika sehemu linapojengwa daraja la Kavuu lenye urefu wa mita 84 litakalounganisha Kijiji cha Kibaoni na makao makuu ya Wilaya hiyo Inyonga.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Inyonga Wilayani Mlele ambapo barabara ya Mpanda-Tabora itapita.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Col.Ngemela Eslom Lubinga mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya Mkuu huyo wa wilaya inayojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Wilayani Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Tabora mara baada ya kukugua mradi wa barabara ya Sikonge-Tabora.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI JIJINI DAR

February 04, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha viongozi wa dini cha mashauriano kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari jana. Kulia ni ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ,Alhad Salum Musa.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Asha Rose Migiro katika mkutano wa mashauriano wa viongozi wa dini uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam jana. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini baada ya kuzungumza katika mkutano wao wa mashauriano uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini mara baada ya umalizika kwa kikao chao kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari jana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA UJERUMANI ATEMBELEA KANISA KUU LA KILUTHERI LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

February 04, 2015

 Muonekano wa Kanisa la Azania Front
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (kulia), akimkaribisha Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipofika kutembela kanisa hilo Dar es Salaam leo jioni.
 Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck akisalimiana na Mama Anna Mkapa baada ya kuwasili kanisani hapo.
 Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck (katikati), akisaini baada ya kufika kanisani hapo.
 Wanakwaya wakitumbuiza.

 Askofu Malasusa na Rais wa Ujerumani, Gauck wakiteta jambo.
Rais Gauck akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo pamoja na waumini. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
 Mkuu wa Wilaya ya Wete hayuko tayari kufanya kazi na asasi za kiraia zenye mlengo wa siasa

Mkuu wa Wilaya ya Wete hayuko tayari kufanya kazi na asasi za kiraia zenye mlengo wa siasa

February 04, 2015
ime
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Hassan Khatib Hassan kuwa  Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -Pemba  .
Mkuu wa Wilaya ya Wete Hassan Khatib Hassan amesema kuwa hatakuwa tayari kufanya kazi na asasi za kiraia ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwa mlengwa wa chama cha siasa kwani hazitakuwa na mwelekeo mzuri .
Akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Mtabwe waliofika  Ofisini kwake kujitabulisha , amesema kuwa siasa ni sumu ya mafanikio ya Jumuiya na kwamba Jumuiya nyingi zimekuwa zikishindwa kufikia malengo yake kutokana na Viongozi kuzihusisha na masuala ya kisiasa .
Aidha Mkuu wa Wilaya ameelezea kusikitishwa na kitendo cha uharibifu wa mazingira katika Jimbo hilo hasa vitendo vya ukataji wa miti na kuitaka Jumuiya hiyo kuhakikisha kuwa maeneo ya wazi ambayo yameathirika kwa kukatwa miti ovyo yanarejeshwa katika hadhi yake kwa kupandwa miti
Amefahamishwa  kuwa asasi ya kiraia zina nafasi kubwa katika kufanikisha udhibiti wa uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya Tabianchi iwapo zitakuwa tayari kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka.
Amesema kuwa katika kufanikisha suala la uhifadhi na udhibiti wa uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji ovyo wa miti asasi za kiraia zinatakiwa kuwa mstari wambele kuwaelimisha wananchi athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayotokea siku hadi siku. . Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza haja kwa Jumuiya hiyo kukaa pampja na asasi nyingine ambazo zinafanya kazi sawa na Jumuiya hiyo ili kuondoa suala la migongano katika utendaji wa kazi zao .
“Tunatambua kwamba asasi za kiraia zinanafasi kubwa katika kudhibiti suala la yharibifu wa mazingira na mafanikio zaidi yatapatikana iwapo mtakuwa tayari kushirikiana na Jumuiya nyingine ambazo zina malengo sawa na ya Jumuiya yenu ” alifahamisha .
Naye Diwani wa Wadi ya Mtambwe Hamad Mjaka  Bakar amesema kuwa lengo Jumiya hiyo ni kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira pamoja na kutafuta njia muafaka za  kutatua kero zianazo wakabili wananchi wa Jimbo hilo  .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo hilo Said Massoud amesema kuwa uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokea katika Jimbo hilo ni ukataji ovyo wa miti pamoja na  uvuvi wa chaza wa kutumia vijembe .
Amesema kuwa uvuvi wa aina hii umekuwa ukichangia sana matendo ya uharibifu wa mazingira na kuongeza kwamba Jumuiya tayari inaendelea na kampeni zake za utoaji wa elimu kwa wananchi ili kudhibiti vitendo hivyo .
“Vitendo hivi ni lazima tukiri kwamba vipo katika Jimbo letu la Mtambwe na hasa  vya ukataji miti ovyo pamoja uvuvi wa chaza kwa kutumia vijenmb vidogo vidogo na hili tunaendelea kupambana nalo na muda mfupi wananchi wataepukana nalo ” alieleza.
Hivyo Jumuiya hiyo imeiomba Serikali kuweka msukumo katika kufanikisha kuyadhibiti matendo hayo kwa kuwahakikisha kwamba wanaosafirisha miti mibichi wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria .
WAZIRI JUMA NKAMIA AWATAKA WAMILIKIWA WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI JUMA NKAMIA AWATAKA WAMILIKIWA WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO

February 04, 2015

unnamed1
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
unnamed2 
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
unnamed3Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo unnamed4Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng’ong’o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma unnamed6 
Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
unnamed7 
Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
unnamed8 
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
unnamed9 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze uwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini. Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia alisema kuwa serikali inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari. “Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia Aidha alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika. Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria . Hata hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote. Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa.