SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA TAASISI YA UTSS (UNDER THE SAME SUN) LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA TAASISI YA UTSS (UNDER THE SAME SUN) LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

June 13, 2017
unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (kushoto) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (katikati) pale ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Vicky Ntetema
2
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (kushoto) pale ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
3
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the same Sun) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Ndg. Peter Ash (wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Vicky Ntetema (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BULEMBO AMALIZA ZIARA KATIKA WILAYA 47 ZA MIKOA SABA, JOTO LAKE LASABABISHA CHADEMA 376 KUTIMKIA CCM

June 13, 2017
Na Bashir Nkoromo
Hatimaye Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za mikoa hiyo.
Katika ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10, 2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili, ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.
Alhaj Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.
Hata hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.
Katika ziara hiyo, Alhaj Bulembo pia pamoja na mambo mengine ya kuhimiza ujenzi na uimarishaji Chama na Jumuia zake, alikuwa na ajenda za kufafanua kuhusu mabadiliko yaliyowaacha nje badhi ya waliokuwa Mabalozi na pia kufafanua kwa kina umuhimu wa Mabalozi wapya waliopatikana sasa na wale waliobaki kutokana na mabadiliko hayo ndani ya Chama.
Alhaj Bulembo kwenye vikao vya ndani kwenye ziara hiyo alipata fursa za kuwapiga msasa, kwa kuwapa darasa zito Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika Wilaya husika, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia zote za Chama, Mabalozi na Watendaji wote wa serikali.
Mara kadhaa alisisitiza umuhimu wa madiwani kuwa karibu na viongozi wa Chama hasa mabalozi, ikiwa ni pamoja na kuwatambua kwa karibu hadi kwa majina na kujenga mahusiano ya kawaida kwa lengo la kukuza ukaribu baina yao na viongozi hao, siyo tu wa kichama bali hadi wa kifamilia.
Katika hali ambayo haikuwa ikitarajiwa,  katika wilaya karibu zote alizofika, ilionekana dhahiri kwamba madiwani karibu wote walikuwa hawana mahusiano ya kawaida na mabalozi, hali hii ilijidhihirisha pale Alhaj Bulembo alipokuwa akiwasimamisha madiwani na kumuuliza kila mmoja alivyoshiriki kwenye uchaguzi wa mabalozi, idadi ya mashina na majina ya mabalozi katika kata zao.
Madiwani wengi walijikuta wengine hawajui hata idadiya mashina katika kata zao, na pia walishindwa kutaja idadi ya mabalozi kwenye eneo lao, na kutaja majina ya mabalozi ndiyo ilikuwa kazi kubwa. Diwani alijikuta akitaja balozi mmoja au wawili tu, kata nzima.
“Mnajua lengo la mahusiano haya, ni kukirahisisha Chama kupata kura kwa urahisi wakati wa uchaguzi, kwa sababu ninyi madiwani mkiwa mmeshajenga mahusiano na Wenyeviti wenu wa mitaa na mabalozi hakutakuwa na kazi ngumu ya kutafuta kura, na lazima mtambue kuwa Mabalozi ndiyo siri kubwa ambayo hufanikisha ushindi wa CCM katika chaguzi”, anasema Bulembo kwa nyakati tofauti.
Mbali na darasa alilokuwa akitoa kwenye vikao hivyo, katika ziara hiyo amewesha CCM kujizolea wanachama wapya 376 ambao walikihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM, wakiwemo waliokuwa viongozi wa Chadema katika vitongoji na Vijiji na aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Baada ya Makala hiyo fupi yafuatayo ni matukio katika picha katika ziara ya mwisho wa ziara hiyo ambayo Bulembo aliifanya jana katika Wilaya za Mbogwe na Geita mkoani Geita.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mbogwemkoani Geita, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mbalozi na Watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo, jana, Juni 10, 2017.
 Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadi kutoka kwa mmoja wa wanachama sita wa Chadema, waliotangaza kutahmia CCM wakati wa kikao hicho.

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA MKUU WA JKU NA MKUU WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

June 13, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad  kuwa   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU )  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu wao Wapya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Halotel yashusha Neema kwa wateja wake

June 13, 2017
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko Kinondoni Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mr Nguyen Van Son, amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma za kampuni hiyo, wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa watanzania ambao hadi sasa zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano, tayari wamejiunga na mtandao huo na wanafurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.

“Tunafarijika sana kwa namna ambavyo Watanzania wameendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa jamii hii, ni faraja kubwa kwetu kwamba katika kipindi hiki kifupi tumepata mafanikio makubwa na bado tunaendelea kupata wateja wanaojiunga na mtandao wetu siku hadi siku,” Jambo hili linatufanya tusilale tufikilie ni namna gani tunapaswa kuendelea kukizi mahitaji yao.

“Kuzinduliwa kwa kampeni hii itakuwa ni sehemu ya sisi kusogea karibu na wateja wetu, kuwahudumia pamoja na kuwasikiliza ni nini wanahitaji kutoka kwetu,” Tunaamini kabisa kwamba kuwa karibu na wateja wetu tutajenga mtandao bora kabisa utakao kuwa na huduma zinazolenga maisha halisi ya Watanzania.

Aidha Naibu Mkurugenzi huyo alitaarifu kuwa, Kampuni hiyo imeanza utaratibu wa kuwa na vifurushi Maalumu kulingana na maeneo na mahitaji ya wateja husika, Huku akitolea mfano wa kuwa na vifurushi maalumu kwa wateja wa Mtandao huo wa Zanzibar ambao wameanzishiwa kifurushi maalumu cha ZANZIBAR YETU, ambacho kwa watumiaji wa Halotel wataweza kuongea bure siku za mwisho wa wiki kwa shilingi 1000 pamoja na vifurushi vingine, Kwa wateja wapya wa mikoa ya Mbeya, Manyara, Pwani, Arusha, Kilimanjaro na Mara, Mkoa huo wanaweza kupata dakika 60 za kupiga simu bure ndani ya mtandao kila wanapoweka muda wa maongezi kwa siku 30 baada ya kusajili . 
 
Pamoja na Ofa ya Kiboko yao ambayo inapatika katika baadhi ya minara ya 3G ya mtandao huo.Naibu Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa, licha ya kuboresha na kutoa huduma zinazowalenga Watanzania, kampuni hiyo pia imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha Mawasiliano na ubora wa Mtandao huo ambapo hivi karibuni mtandao huo ulitangaza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 200 kwa ajiri ya kuboresha ubora wa sauti na kasi ya intaneti, huku wakitarajia kuwekeza zaidi katika mwaka ujao wa fedha. 

Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Salim Selemani, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao. Pamoja nae katika picha ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Frank Mwakyoma na waendesha pikipiki wa kituo cha makumbusho.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Simon Mkumbo, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son, akitoa maelekezo namna ya kupata huduma za mtandao huo kwa baadhi wa wafanyabiashara wa nguo katika stendi ya Makumbusho mara baada ya kujiunga na mtandao huo, Kampuni hiyo imezindua huduma ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na mtandao huo pamoja na wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja wa mtandao huo.

KLABU YA GYMKHANA DAR ES SALAAM KUADHIMISHA MIAKA 100 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

June 13, 2017
Klabu ya Gymkhana Dar es salaam inayojihusisha na michezo ya aina mbalimbali imejipanga kusherehekea kutimiza miaka 100 kwa staili ya tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916.

Katika kuadhimisha tukio hilo la kihistoria, Klabu hiyo imeandaa idadi ya michezo mbalimbali itakayosindikiza maadhimisho hayo ambapo michezo hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 03 Julai, 2017 na kuhitimishwa tarehe 08 Julai kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bw. Walter Chipeta.

Miongoni michezo iliyopangwa kufanyika katika kuadhimisha miaka 100 ya klabu hayo ni pamoja na Gofu, Tenisi, Skwashi, Soka, Kriketi, mchezo wa kuogelea na mingine mingi ambayo kwa ujumla itawahusisha wanachama na wasio wanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta alisema, “Maadhimisho ya miaka 100 ni tukio la kihistoria kwa ajili ya klabu yetu na tumejipanga kusheherekea shughuli hii kupitia michezo mbalimbali ambayo itaanza rasmi tarehe 03 Julai na kilele chake kuwa tarehe 8 Julai.”

Chipeta alisema klabu hiyo inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kushiriki kwenye maadhimisho hayo na kusisitiza kwamba washiriki watafurahia na kuburudika.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ndio wadhamini rasmi wa maadhimisho ya miaka 100 ya Gymkhana Ndg. Itandula Gambalagi alisema, “Tunajisikia fahari kuhusishwa na klabu kubwa kama hii na kwenye tukio la kihistoria kama hili la kuikumbuka klabu hii kongwe. Aliongeza kuwa tukio hilo litatoa fursa kwa NHC kujitangaza zaidi na kukutana na wateja wake muhimu katika mazingira tulivu ya kijamii.”

Licha ya NHC kuwa wadhamini rasmi wa shughuli hiyo, Klabu ya Gymkhana pia ilitoa shukrani kwa wadhamini wengine wa mashindano hayo ambao ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.

Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana ikiwa ni kituo au sehemu ya kukuza michezo, kwa miaka mingi imekuwa ni chombo muhimu kinachowaunganisha watu kupitia michezo na shughuli mbalimbali za kijamii.

Pia, imekuwa ikiendesha michezo ya watoto na watu wenye ulemavu ambao pia wanapata fursa ya kushiriki michezo kama tenisi na Skwashi. Hii ni klabu ambayo inapokea watu wote wanaopenda kuwa sehemu ya jumuiya ya wapenda michezo na kuwa sehemu ya maadhimisho haya ya kihistoria ili kuendelea kukuza michezo mbalimbali.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa Julai 08. Katikati ni Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael na kushoto ni Mratibu wa Masoko na Matukio Levina George.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kushoto)  akiwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na dhamira ya klabu hiyo ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916. Klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08 katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria. Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi.
Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na udhamini wa mashindano yatakayosindikiza maadhimisho ya miaka 100 ya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana tangu ilipoanzishwa mwaka 1916. Katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria, klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano hayo. Wadhamini wengine wa mashindano hayo ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akisalimiana na Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.

TAASISI ZA KIBENKI ZATAKIWA KUBORESHA MIFUMO YAO YA KIUTENDAJI

June 13, 2017

Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano (kushoto)akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Benki ya TPB,kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu TPB,Sabasaba Moshingi ,ambapo ofisi hiyo  mpya ipo katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.


Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akizindua jiwe la msingi katika benki ya TPB iliyopo eneo la Mwanjelwa.


Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindanoakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la ofisi ya benki ya TPB Mwanjelwa.
Afisa Mtendaji Mkuu TPB  SabaSaba Moshingi ,kushoto akimkabidhi ripoti ya Mwaka Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya jengo la Tpb Mwanjelwa jijini Mbeya.
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akionesha kadi maalum aliyokabidhiwa na benki ya TPB mara baada ya kuzindua jengo hilo la ofisi eneo la mwanjelwa jijini Mbeya.
Meza kuu  katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa TPB.

Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa

June 13, 2017


Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.

Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake.

Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.
Mshindi wa Sh Milioni 20 katikati Amani Kabuku, akisaidiwa kushika 'maburungutu' yake ya fedha baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.

Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo.

“Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,” Alisema Kabuku. Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kutumia fursa ya uwapo wa mchezo wa bahati nasibu ya Biko ili washinde zawadi nono kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kwa ushindi wa papo kwa hapo, ambapo bahati nasibu yao ikichezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

“Baada ya kuingiza namba ya kampuni kinachofuata ni kuweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi, huku wale wanaocheza mara nyingi wakiwa na nafasi kubwa ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili, ambapo Jumapili hii mshindi mwingine wa Sh Milioni 20 akitarajiwa kupatikana katika droo kubwa,” Alisema Heaven.

Kwa mwezi Mei pekee, bahati nasibu ya Biko imeweza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake wa papo kwa hapo pamoja na wale walioibuka na droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, huku wakiamini kuwa uwapo wa mchezo wao wa kubahatisha ukiwa ni njia ya kukuza uchumi kwa washiriki wao na Watanzania kwa ujumla, huku pia ukiwa ni mchezo rahisi kuliko michezo mingine yoyote inayofanyika nchini Tanzania.
MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 13, 2017.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 13, 2017.

June 13, 2017
unnamed
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Juni 13, 2017
1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angeline Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
2
NaibuWaziri waAfya ,Maendeleo yaJ amii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017
3
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akifuatilia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Suzan Kolimba hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
4
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
6
Waziri waNchiOfisiya Waziri MkuuSera ,Bunge,Kazi,Vijana,AjiranaWatuwenyeUlemavuMhe.JenistaMhagamaakizungumzajambonaMbungewaMtamaMhe.NapeNnauyekatikakikao cha 46 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Juni 13, 2017.
WIZARA YA ARDHI WAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TATHMINI YA ULIPAJI WA KODI YA PANGO LA ARDHI NA MALIPO YAKE KWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI

WIZARA YA ARDHI WAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TATHMINI YA ULIPAJI WA KODI YA PANGO LA ARDHI NA MALIPO YAKE KWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI

June 13, 2017
unnamed
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Bw,Hezekiely Kitilya akiwa katika mkutano na waandishi wa habari akizungumzia tathmini ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na Malipo yake yanavyoweza ufanyika kwa mfumo mpya wa kielektroniki leo mjini Dodoma.
1
Afisa Ardhi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo Bi.Jane Kapongo akifafanua jambo kwa waandishi wahabari (hawapopichani) juu ya Hati za Kimila kutumika kama dhama na katika Taasisi za Kifedha Nchini leo Mjini Dodoma.
2
MsajiliwaHatikutokaWizarayaArdhi,NyumbanaMaendeleoyaMakaziBw.GeofreyMauyaakizungumzanawaandishiwahabarijuuyataratibumbalimbalizahatinajinsiyakuzipatakatikamkutanonawaandishiwahabariMjini Dodoma.
3
KamishnaMsaidiziwaArdhi Kanda ya Kati Bw,HezekielyKitilyaakisisitizajambokwawaandishiwajuuyatathminiyaulipajikodiyapango la ardhina Malipo yake yanavyoweza kufanyika kwa mfumompyawakielektronikileomjini Dodoma.
PichanaDaudiManongi,MAELEZO,DODOMA.
MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017

June 13, 2017
unnamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika kuanzia tarehe 14-23 Juni,2017 yenye kauli mbiu “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma,Vijana washirikishwe kuleta mabadiliko Barani Afrika”.Kulia kwake ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi,Susan Mlawi.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari leo Mjini Dodoma.
Picha na DaudiManongi,MAELEZO,DODOMA
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA WOTE

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA WOTE

June 13, 2017
unnamed 1 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na wakuu wa mikoa wote katika kikao kilichohudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 13, 2017
PICHA NA IKULU
WAANDISHI WAPEWA ELIMU JUU YA MATONE YA VITAMIN A

WAANDISHI WAPEWA ELIMU JUU YA MATONE YA VITAMIN A

June 13, 2017
unnamed
Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Asha Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamin A watoto wenye umri wa miaka miwili hadi mitano katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
1
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika kazi za vikundi kupanga mikakati ya kuihamasisha jamii kuitikia kampeni ya kuwapatia watoto matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
2
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Nasra Manzi akiwasilisha kazi ya kukundi chake katika mkutano wa kuwaelimisha waandishi kuhusu matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
Picha na Makame Mshenga.
…………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Asha Hassan amesema Zanzibar bado ipo nyuma katika kiwango cha Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kuwapatia matone ya Vitamn A watoto wenye umri kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano.
Bi. Asha alieleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamen A watoto wenye umri huo lililoanza tarehe 1 Juni ambalo linategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi huu kwa awamu ya kwanza mwaka huu na awamu ya pili itafanyika mwezi Disemba.
Alisema Zanzibar hadi hivi sasa imefikia asilimia 82 katika  mpango huo wakati kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya  Ulimwenguni ni asilimia 95.
Alizitaja Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi ndizo zenye asilimia ndogo zaidi chini ya asilimia 70 wakati Wilaya ya Kati inaongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 95.
Alisema Kitengo kimeanzisha utaratibu wa kuwafuata wazazi wanaoishi mbali na vituo vya afya ili kuwapatia watoto  matone ya Vitamin A lakini baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi mashirikiano.
Aliwasisitiza wazazi kufanya juhudi kuhakikisha watoto wao wanapata matone hayo kwa vile ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizo ya maradhi ikiwemo kuharisha na kutoona vizuri.
Afisa Kitengo cha Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ali Saidi alisema kumekuwa na dhana potofu  kwa wananchi hasa wanaoishi mjini kwamba watoto wao hawahitaji matone ya Vitamin A kwa vile wanakula vizuri lakini dhana hiyo sio sahihi.
Alisema utafiti uliofanywa na Kitengo hicho unaonyesha kwamba watoto  wenye hali nzuri ya Vitamin A  Zanzibar ni asilimia 12 na asilimia 88 iliyobaki wanaupungufu.
Aliwatoa wasi wasi wazazi kuwa hata wale wachache wenye Vitamin A vya kutosha mwilini wanapopewa matone hayo hayana madhara yoyote na wanaweza kutumia. 
Washiriki wa mkutano huo walikishauri Kitengo cha Lishe kuongeza kutoa elimu kwa wazazi kwani baadhi yao bado hawajaelewa umuhimu wa matone ya Vitamin A na wengine wanadhani kuwa matone hayo ni sawa na chanjo jambo ambalo sio sahihi.    
RC GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA KUBORESHA UTALII MKOANI ARUSHA

RC GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA KUBORESHA UTALII MKOANI ARUSHA

June 13, 2017
unnamed
*RC Gambo afanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa kuboresha utalii mkoani Arusha*
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiwa Ufaransa, amefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Samwel W Shelukindo. Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini Tanzania. Pamoja na mambo mwingine wamejadiliana Yafuatayo:-
1. Mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha
2. Kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha (Fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Arusha )
3. Kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo yupo katika ziara ya mafunzo nchini Ufaransa pamoja na mafunzo hayo amekua akiutangaza mkoa wa Arusha kama kitovu cha utalii nchini Tanzania.
1 2

Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo

June 13, 2017


Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyo na Soko la hisa la Dar es salaam (Dar Es Salaam stock Exchange ) na kuanzia sasa itauza hisa zake kwa umma na kubadili jina lake kuwa Maxcom Africa PLC Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya  uzinduzi wa uuzaji wa  hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia )  akikata utepe wa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC anayeshuhudia ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.


Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia )  akionesha nembo ya jina jipya Maxcom Africa PLC  kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za kampuni hiyo kushoto kwake ni  Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam
waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa mapema leo.
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC.Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa mapema leo katika hafla ya uzinduzi zilizofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.