“WAMBURA: TUZO IMENIPA MZUKA WA KUFANYA VIZURI MSIMU UJAO”

May 10, 2015
KIUNGO wa Timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura amesema kuwa tuzo ya uchezaji bora ya mwezi wa February aliyoipata imempa mzuka wa kuhakikisha anajipanga imara ili kuendelea kufanya vizuri.

Wambura ambaye alijiunga na Coastal Union katika drisha dogo akitokea klabu ya Kagera Sugar alisema hayo juzi mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo Vodacom.

Akizungumza jana, Wambura alisema kuwa anaamini uteuzi huo wa uchezaji bora uliofanywa na bodi ya Ligi kuu ulikuwa makini na ndio maana umeweza kumuwezesha kupata nafasi hiyo ambayo alikuwa akiiwaza kwa kipindi cha muda mrefu.

   “Tuzo hii imenipa hamasa ya kuhakikisha ninatumia vizuri nafasi yangu kama mchezaji lengo likiwa kuipa mafanikio timu yangu hasa katika harakati za kucheza ligi kuu kwa ufanisi mkubwa “Alisema Wambura.

Hata hivyo aliwataka wachezaji wengi kujituma na kucheza mechi kwa juhudi kubwa ili kuweza kupata nafasi za kuwawezesha kuonekana na kuchaguliwa kuwa wachezaji bora kama ilivyokuwa kwake.

MAMILIONI YA KOPA BAYPORT YAZIDI KUPATA WENYEWE

May 10, 2015
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.


                                              Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.
Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.


Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.



Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.

Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.
“Tunashukuru kuona Watanzania wenzetu wameendelea kupata urahisi wa huduma zetu za mikopo, maana anaweza kukopa mahala popote alipokuwapo, endapo ana kifaa kitachomuwezesha kuingia katika mtandao wetu wa www.kopabayport.co.tz, kama vile simu ya mkononi na kompyuta” alisema Cheyo.


Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania.

Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, alisema promosheni hiyo ya kopabayport ni nzuri kwa wateja na Watanzania wote wanaoweza kujikwamua kwa kupata mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kutoka Bayport.
“Sisi Bodi tunachoangalia ni kanuni na vigezo vya michezo ya kubahatisha kufuatwa, ikiwa ni upatikanaji wa washindi na namna walivyoweza kujiunga kwenye huduma hii ambayo kila mtu anaweza kuingia anapohitaji huduma yoyote,” alisema Abdulhussein.
Naye Meneja Huduma kwa Watejanwa Bayport Financial Services, Gladys John, aliwataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono Bayport kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali za mikopo isiyokuwa na amana wala dhamana, bila kusahau Kopa Bayport inayoendelea kutolewa kwa ajili ya kuwapongeza wanaomua kutumia huduma hiyo nzuri.
Wateja hao watatu waliojinyakulia sh Milioni moja kila mmoja, wanaungana na Hyasint Mbunda Songea, Phaustine Mbilinyi Dar es Salaam na Allen Bishubo Bukoba ambao walishinda katika droo ya mwezi wa nne, ambapo Bayport Financial Services, imeshawapatia fedha zao za ushindi. Click here to Reply, Reply to all, or Forward 5.64 GB (37%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 16 hours ago Details

LADY JAYDEE - GIVE ME LOVE FT. MAZET & DJ MAPHORISA (OFFICIAL VIDEO HD)

May 10, 2015
djide give me love
Finally Lady Jaydee's Give Me Love music video is out. The video was shot and directed by Nicky Campos on location in Johannesburg, South Africa. The Song was produced by Uhuru and features Mazet & DJ Maphorisa.This is the follow up single after the mega hit 'Forever ft Dabo' which has earned Jide multiple nominations in the upcoming Kili Music Awards, including 'Best Collaboration' and 'Best Female'. Other nods are from the prior releases 'Nasimama' and 'Historia' which both are competing for the 'Best Zouk Song' category. For more info please follow Lady Jaydee: Twitter: @jidejaydee Instagram: @jidejaydee Facebook: @ladyjaydee Enjoy the video below