MGAZA ASIFU JITIHADA ZA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA KUSAIDIA JAMII KWENYE MASUALA YA ELIMU

October 26, 2014

MKUU wa wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza amesifu juhudi zinazofanywa na Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) katika kusaidia sekta ya elimu wilayani humo lengo likiwa kupandisha juu taalumu hiyo kwenye shule mbalimbali kwa kuwawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira mazuri.

Mgaza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akipokea msaada wa
  mifuko 250 ya saruji iliyokuwa na thamani ya sh.milioni nne kutoka kwa mfuko huo wa Pensheni katika makabidhiano yaliyofanyika shule ya msingi Mwakikonge ya jamii ya kimasai wilayani humo.

Mfuko huo wa Pensheni ulitoa mifuko hivyo kwa ajili ya ujenzi wa

miundombinu kwenye shule tatu za msingi wilayani humo ambazo
zinakabiliwa na changamoto hiyo ambazo ni Mwakikonge mifuko 100,Mwakikoya mifuko 100 na Gonja Segoma mifuko 50.

Alisema juhudu hizo zinaonyesha kuwa namna gani mfuko huo ulivyokuwa
  na malengo makubwa ya kuhakikisha wanachangia maendeleo ya sekta hiyo hasa katika masuala ya ujenzi wa miundombinu jambo ambalo linasaidia kukuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hizo.

Aidha alisema kuwa wilaya hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha
kila shule inakuwa na miundombinu ya kutosha ikiwemo madarasa ilikuwawezesha wanafunzi kusoma kwa

Aliongeza kuwa shule hiyo ya Mwakikonge ina uhaba mkubwa wa

miundombinu ambayo ilijengwa kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuwasaidia jamii ya kimasai ili kuweza kupata elimu na kuwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jihudu hizo.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi mifuko hiyo,Afisa wa Fedha wa
  Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Samweli Haule alisema kuwa waliamua kutoka msaada huo ili kuchangia harakati za elimu wilayani humo kwa kuboresha miundombinu.

Aliongeza kuwa baada ya kutoa msaada huo matumaini yao makubwa ni
  kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora ambayo inaweza kuwainua kiwango cha ufaulu wao hasa katika mitihani yao ya mwisho.

Naye kwa upande wake,Afisa elimu Msingi wilayani Mkinga,Zakayo
  Mlenduka alisema msaada huo umewafikia wakati muafaka ambapo walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu na kuhaidi kuutumika kwenye matumizi yasiyokusudiwa.

Utoaji wa mifuko hiyo ya Saruji katika shule hizo unatokana na ombi
  ambalo liliwasilizwa kwenye mfuko wa PSPF na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantuma Mahiza kuwaomba wasaidia masuala ya ujenzi kwenye shule ya mwakikonge inayosomewa na jamii ya kimasai ili waweze kupata elimu bora.

PICHA NNE ZA RPC TANGA KASHAI AKIONYESHA NOTI BANDIA ZILIZOKAMATWA MKOANI TANGA HIVI KARIBUNI

October 26, 2014

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani hapa juzi amabo hawapo pichani  fedha bandia alizokamatwa nazo Khalid Ramadhani mkazi wa Makorora akiwa na noti bandia 11 kila noti moja ikiwa na thamani ya tsh.10,000 sawa n ash.110,000 na noti bandia nne za dola 100 ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alikiri kufanya biashara hiyo ya uuzaji wa noti hi


CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA 21 AMBAPO WAHITIMU 280 WATUNUKIWA STASHAHADA.

CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA 21 AMBAPO WAHITIMU 280 WATUNUKIWA STASHAHADA.

October 26, 2014

Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21. 04  
Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar wakifuatilia maadhimisho  hayo yaliyofanyika Chuoni, Mbweni.06 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali ya 21 yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Dkt. Abdalla Ismail Kanduru. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Serikali yapiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake

Serikali yapiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake

October 26, 2014

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonwa waliofuata huduma katikazahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru ,juzi  alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagionjwa wanaopita katik Hifadhi ya Taifa ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed1 
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo lake wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki mkoani Arusha juzi , kutokana  na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed2 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa muda mrefu.
unnamed3 
Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani Kilimanjaoro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema
Nyalandu alisema kasi ya ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.
“Kwa kaddri siku zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.
Aliwaagiza wakuu wa wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa  hadidu za rejea kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko huo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.
Alisema kwamba kwa msitu wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho alishauri  umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.
Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama nishati na kulinda misitu.
“Umemem ni nishati mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AKUTANA NA WASANII MLIMANI CITY

October 26, 2014

 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal, akiongea na wasanii na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Maadhimisho ya siku ya Wasanii Duniani wakati  akifungua kongamano  kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam jana, Hii ni  mara ya kwanza kwa tamasha hilo  kufanyika hapa nchini, .(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA.
 Naibu waziri wa Wizara ya  Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo , Juma Nkamia, alipokua akiongea na kumkaribisha mgeni rasmi  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal.
  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha wageni, (kulia) ni  Naibu waziri wa Wizara ya  Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo , Juma Nkamia.
 Msanii Aisha Mashauzi akitoa burudani katika Maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Wadau wa Sanaa
 Wanahabari wa katika engo ya kilammoja apate anacho kihitaji katika maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Wadau wakifatilia kwa makini mtanange huo.
   Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal, (katikati)  akimkabidhi Tuzo, Katibu wa chama cha Ushirika Tingatinga , Rashid Munyana, Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa Mlimani City, (kulia) na kushoto ni
Naibu waziri wa Wizara ya  Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo , Juma Nkamia.
 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal, (katikati)  akimkabidhi Tuzo, Katibu wa chama cha Ushirika Tingatinga,   Rashid Munyana, Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa Mlimani City, (kulia) na kushoto ni
Naibu waziri wa Wizara ya  Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo , Juma Nkamia.
  Katibu wa chama cha Ushirika Tingatinga,   Rashid Munyana (kushoto), akibusu Tuzo hiyo baada ya Kutunukiwa tuzo hiyo na
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal Daes Salaam jana katika Maadhimisho ya siku ya Wasanii Duniani iliyo fanyika katika ukumbi wa Milmani City jana (kulia) ni mgeni rasmi 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal.
    Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohammed Gharib Bilal, (kulia)  akimkabidhi Tuzo , Ofisa Habari Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Agnes Kimwaga,(kushoto)
 Staa wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platinum’ akifanya yake usiku huu Mlimani City akiwa na wacheza shoo wake.
Msanii Diamond Plutnams na kundi lake wakifanya mambo makubwa jukwaani wakati wa tamasha la siku ya  wasanii duniani  lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Wasanii wa Yamoto Bend wakitoa burudani katika Maadhimisho hayo ya siku ya wasanii Duniani.

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA JANA KWENYE MECHI YA STAND UNITED NA YANGA,SHINYANGA

October 26, 2014