MBUNGE RITTA KABATI AWAJENGEA KIVUKO WALEMAVU MKOANI IRINGA

October 25, 2017
 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho kwa chama cha walemavu mkoa wa Iringa.
 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikata upete  wa kuashiria kivuko kimezinduliwa rasmi
 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mmoja wa walemavu akipita katika kivuko hicho
Mmoja wa watu wenye ulemavu akipita kwenye kivuko hicho kuelekea kwenye ofisi zao za chama cha walemavu mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amewajengea kivuko walemavu katika ofisi yao kwa lengo la kuwarahisishia kufika ofisni hapo.

Akizungumza wakati wa kuzindua kivuko hicho Mb Kabati alisema kuwa lengo la kuwasaidia mara kwa mara watu wenye ulemavu ni kutokana kuwa kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.

“Unajua hakuna mtu aijua kesho yake hivyo usipowajali walemavu leo hata wewe kesho ukiwa mlemavu watu hawata wajali mimi binafsi nawajali sana walemavu kwa kuwa nao ni binadamu kama binadamu wengine” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa ametumia gharama zake binafsi kujenga kivuko hicho ambacho kitakuwa msaada kwa watu wote wenye ulemavu kufika ofisini kwa urahisi kabisa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Saizi naona mambo yatakuwa safi maana kila kitu naona kimetuwa bora na mafundi wamejenga vizuri na kivuko hiki naona ni imara sananaombeni na nyinyi mkitunze sana hiki kivuko” alisema Kabati

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha walemavu mkoa wa Iringa (CHAWATA) Rukia Makweta alimshukuru mbunge huyo kwa kuwajengea kivuko hicho maana kimewaondolea adhabu ya kudondoka dondoka wakati wanaingia ofisini kutokana na ubovu uliokuwepo

KAMPUNI YUA KILUWA INDUSTRIAL GROUP OF COMPANIES YAFANIKIWA KUANDAA KONGAMANO KUBWA LA UHAMASISHAJI WA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING CHINA

October 25, 2017


Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali wakati wa kufungua Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.Picha Ahmad Michuzi-China.

Balozi Kairuki ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies kwa kuthubutu na kuonesha juhudi kubwa za kutafuta na kuwahamasisha washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

Balozi Kairuki amesema kuwa,yeye yuko tayari kushiriki kwa pamoja kusaidia kuendelea kuwahamasisha Wawekezaji wa nchini China,kuja kuwekeza nchini Tanzania,ili kuhakkisha dhana ya Tanzania ya Viwanda inatimia na hatimaye nchi ya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

"Kwa kufanya hivyo sote kwa pamoja tutakuwa tunetekeleza kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda",alisema Balozi Kairuki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali waliojitokeza kushiriki Kongamano la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akipongezwa mara baada ya kutoa hotuba yake .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwalekeza jambo baadhi ya Wadau wenye nia ya Uwekezaji nchini Tanzania,mara baada ya Kongamano la uwekezaji wa Viwanda kumalizika.Kongamano hilo lilifanyika Oktoba 25,2017 katika moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing,mjini Beijing nchini China,ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini humo,Mh Mbelwa Kairuki.
Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Samataba akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yameulizwa na baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo la Uhamasishaji wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing mjini Beijing nchini China.Mh Semataba ambaye aliongozana na baddhi ya viongozi waandamizi wa Serikali mkoa wa Pwani,aliwahikikishia mazingira mazuri Washiriki hao wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalibali ikiwemo Viwanda,madini na kilimo na kuwa.

MAMBO 10 ANAYOTAKIWA KUWA NAYO MWANAUME KATIKA UMRI WA MIAKA 30

October 25, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Watanzania wana misemo mingi inayoendana na umri lengo likiwa ni kukumbushana katika kuwajibika na kujipanga katika maisha ya kawaida. Miongoni mwa misemo hiyo ni, ‘Ujana maji ya moto, fainali uzeeni.’ Msemo huu una maana kubwa kama ukiutafakari kwa makini, lakini kwa tafsiri ya haraka ni kwamba ujana ndio kipindi ambacho mtu huwa na nguvu za kutosha kufanya masuala tofauti yatakayomuwezesha kuishi vema uzeeni. Licha ya kuwa na nguvu hizo lakini huwa na changamoto kadhaa zinazomuandama ambapo kama asipokuwa makini atakuja kujuta akiwa uzeeni.
Mojawapo ya changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi ni kutokujua vitu gani vya kuweka kipaumbele katika wakati waliopo. Kulingana na umri waliokuwa nao huona kwamba muda unawatosha na hivyo kufanya masuala yasiyo na tija wala kujijengea misingi mizuri ya kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye. Kwa kuliona hilo, Jumia Travel imeona ni vema kukushirikisha wewe kama kijana wa kiume ni mambo gani ya msingi unatakiwa kuwa nayo ukiwa katika umri wa miaka 30.
  
Kupevuka kiakili. Ingawa suala la kupevuka kwa akili halihusiani na umri lakini kufikia umri wa miaka 30 kama mwanaume unatakiwa kuonyesha ukomavu wa akili wa hali ya juu. Hili huweza kupimwa kutokana na misimamo uliyonayo na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya masuala mbalimbali yanayoathiri maisha yako. Maisha hutofautiana kwani kuna wengine hupevuka kiakili wakiwa katika umri mdogo na wengine huwachukua muda. Kwa mfano, katika umri huu kushindwa kujua ni nini unakitaka katika maisha yako kinaweza kuibua wasiwasi kwa wazazi, ndugu au jamii nzima inayokuzunguka. 
Kuwa katika mahusiano ya kudumu. Kuna ule usemi unaosema, ‘Vunja mifupa kama meno bado ipo,’ ulijipatia umaarufu pia kupitia mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa bolingo, Samba Mapangala. Semi huwa zina maana tofauti kulingana na watu wataamua kuzitafsiri na kuzitumia kwa malengo gani. Lakini itapendeza kuzitumia katika njia zenye manufaa zaidi. Vijana wengi huubeba usemi huo na kuutafsiri kama ukiwa kijana pengine huwa ni fursa ya kujihusisha na mahusiano na wanawake tofauti tena kwa nyakati tofauti. Lengo, eti, ni kupata uzoefu na kupata mambo ya kuhadithia enzi za ujana wako zilikuwaje pindi uzeekapo. Kama unafanya hivyo unajiongopea. Kuwa na mahusiano ya kudumu na msichana mmoja hukupatia fursa mwanaume ya kutulia na kujipanga na maisha yako.    
Kuelimika (darasani au njia nyinginezo). Zipo njia nyingi za kujielimisha sio lazima mpaka upitie darasani na kupata astashahada, stashahada au shahada juu ya taaluma mbalimbali. Vipato na fursa hutofautiana katika kulifanikisha hilo, lakini kama unapata fursa hiyo ni vema kuitumia ipasavyo. Elimu pia hupatikana kwa njia ya mafunzo, semina, warsha au kufundishwa na watu wa kawaida ambapo fursa ni nyingi katika jamii inayokuzunguka. Zipo fursa za kujifunza katika jamii tunamoishi lakini watu hupuuzia tena zingine huwa ni bure kabisa. Mwanaume katika umri wa miaka 30 hakikisha unakuwa na elimu, ujuzi au ufahamu juu ya mambo tofauti ambayo yatakurahisishia katika kupata kipato kwa urahisi.

WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUMALIZA MGOGORO WA MPAKA WA HIFADHI YA NORTH UGALA NA VIJIJI JIRANI

October 25, 2017
NA HAMZA TEMBA- WMU- URAMBO, TABORA
Naibu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema Wizara yake itashirikiana na Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pamoja wa kumaliza mgogoro wa mpaka baina ya Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja wilayani Urambo .

Naibu Waziri Hasunga amesema hayo mkoani Tabora jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Akiwa mkoani humo alitembelea eneo lenye mgogoro, akafanya mkutano wa hadhara na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa ajili ya kutafuta majibu ya kutatua mgogoro huo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme, Mkazi wa Kijiji hicho, Ramadhan Rashid alisema wananchi wa vijiji hivyo wanailalamika Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu kwa kusogeza mpaka wa hifadhi hiyo hadi ndani ya ardhi ya vijiji wakati wa uwekaji wa vigingi vipya vya mpaka. Alisema eneo hilo ni la vijiji hivyo tangu mwaka 1988.

Naye, Mkuu wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Peter Maiga alisema hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1956 ikiwa na hekta 165,282 huku mipaka yake halisi ikiwa haijabadilishwa. Alisema zoezi la uwekaji wa vigingi vipya vya mpaka lilizingatia mipaka halisi kwa kutumia mfumo wa GPS.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Urambo, Magreth Sitta akizungumza kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo kwenye mkutano huo, alisema idadi ya wananchi inaongezeka huku maeneo yakiwa hayaongezeki hivyo akaiomba Serikali ione uwezekano wa kuwaongezea wananchi maeneo ya kulima na kuendeshea maisha yao.

Akijibu malalamiko na maombi ya wananchi hao wa Urambo, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutatua kero za wananchi sambamba na kuwaletea maendeleo.

“Baada ya kukagua eneo hili na kusikiliza pande zote, tunaenda kukaa pamoja na Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Ardhi tuangalie ramani zote zilizopo, Matangazo ya Serikali (GN) na taarifa mbalimbali ili tujiridhishe ni ipi mipaka halali tufikie ufumbuzi wa mwisho, migogoro ya namna hii haiwezi kuisha bila kushirikisha wizara hizi.

“Nawaagiza watendaji wangu kwenye taasisi mshirikiane na wananchi muwaelimishe na mzuie wasiendelee na uharibifu hadi hapo tutakapopata suluhu ya mgogoro huu”. alisema Naibu Waziri Hasunga.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo aliwataka wananchi wa vijiji hivyo kujiepusha na vitendo vya kuingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi. “Mkiingiza mifugo tukaikuta tutaitaifisha kwa mujibu wa sheria” alisema Naibu Waziri Hasunga.  

Aidha aliwataka wananchi hao kujikita kwenye shughuli za ufugaji nyuki kibiashara kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji. “Asali ina soko zuri duniani kwa sasa, bei yake ni nzuri, kila mtu afuge tuchangie uchumi wa taifa letu” alisema Hasunga.

Naibu Waziri Hasunga ataendelea na ziara yake ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi katika mikoa wa Katavi, Rukwa na Songwe.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kangeme kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana. Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo
 Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kulia) akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (katikati) akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kigwa (kushoto) kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana. Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo
WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI WAKUTANA NA REA NA WAZIRI WA NISHATI

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI WAKUTANA NA REA NA WAZIRI WA NISHATI

October 25, 2017
IMGL8951
Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Medard Kalemani (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu upatikanaji/ukusanyaji wa fedha za miradi ya REA katika kipindi cha robo mwaka katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
IMGL8959
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Boniface Gissima (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu upatikanaji/ukusanyaji wa fedha za miradi ya REA katika kipindi cha robo mwaka katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
IMGL9010
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Dotto Biteko akiongoza kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na watendaji kutoka Wizara ya nishati walioongozwa na Waziri wa nishati, Mheshimiwa, Medard Kalemani wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu upatikanaji/ukusanyaji wa fedha za miradi ya REA katika kipindi cha robo mwaka kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
IMGL9147
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa karagwe, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (katikati)akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na watendaji kutoka Wizara ya nishati walioongozwa na Waziri wa nishati, Mheshimiwa, Medard Kalemani wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu upatikanaji/ukusanyaji wa fedha za miradi ya REA katika kipindi cha robo mwaka kilichofanyika leo Mjini Dodoma. Wengine ni Wajumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Chonga Mheshimiwa, Juma khatib (kushoto) na Mbunge wa Musoma Mjini Mheshimiwa,Vedastus Manyinyi (kulia).
JNIA-TBIII LINATARAJIA KUKAMILIKA DESEMBA 2018 NA KUANZA KUTUMIA MFUMO WA E-VISA

JNIA-TBIII LINATARAJIA KUKAMILIKA DESEMBA 2018 NA KUANZA KUTUMIA MFUMO WA E-VISA

October 25, 2017
viza
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada ya kuwasili.
viza1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
ziara6
Bw. Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini.
…………………
TBIII kutumia e-visa
Na Mwandishi Wetu
JENGO la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji wake.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo ambayo ni rahisi na haraka.
“Tayari mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa haraka kwani itatumia mtandao,”  amesema Bw. Mbise.
Hata hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege nyingi za nje ya nchi.
“Hizi mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine zilikuwa chache.” amesema Mbise.
Naye Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.
“Nimegundua kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi Nditiye.
Hata hivyo, amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar, South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.

KILIMANJARO MARATHON 2018 YAZINDULIWA RASMI DAR

October 25, 2017
Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Chama Cha Riadha Tanzania, wadhamini na waandaaji.
Akizindua mbio hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Mh. Dk. Harrison Mwakyembe alisema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na kuwataka waandaaji wa mbio nyingine kuiga mfano huu.
“Tunataka kuwaibua kina Felix Simbu wengine na hili linawezekana tu kupitia mbio kubwa kama Kilimanjaro Marathon. Nimefahamishwa kuwa Simbu pia alitokana na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya nyuma...sisi kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia malengo haya,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Executive Solutions Ltd, Aggrey Marealle akitambulisha meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 jijini Dar es Salaam.
Alishukuru pia wadhamini wengine ambao ni Tigo-21km, Grand Malt 5km na wale wa meza za maji ambao ni pamoja na First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement na KNAUF Gypsum.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis alisema wanajivunia kudhamini mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinakuwa kwa kasi kubwa mwaka hadi mwakana hii inawapa moyo na ari ya kuendelea kuwa wadhamini.
Alisema udhamini huu katika mbio za kilometa 42 na 5 kupitia Grand Malt, pamoja na mambo mengine unalenga kuibua vipaji zaidi katika riadha na kuwataka washiriki kujiandaa vizuri. “Inabidi tujiamini zaidi kwani siku moja wimbo wa Taifa wa Tanzania utapigwa katika mbio maarufu duniani,” alisema.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe akitoa hotuba wakati wa uzinduzi rasmi Mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alitoa rai kwa washiriki kuhakikisha wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu dakika za mwisho na kutoa mfano wa mwaka huu ambapo namba za ushiriki zilikwisha kutokana na watu wengi zaidi kujitokeza. “Tumeshazungumza na waandaaji ili kuwepo na namba za kutosha mwakani,” alisema.
Alisema ujumbe mkuu wa Kilimanjaro Premium Lager kwa mbio za mwakani ni ‘Kunywa kistaarabu usiendeshe ukiwa umekunywa’.”Najua wengi tungependa kufurahia kili zetu baridi baada ya mashindano lakini tunywe kwa ustaarabu,” alisema huku akiongeza kuwa zawadi kwa mshindi wa kilometa 42 ni milioni 4 kwa mwanaume na mwanamke na jumla ya zawadi ni milioni 20 kwa washindi wote.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis akizungumza kuhusu udhamini wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitakazofanyika mwakani Machi 4 mkoani Kilimanjaro. Kushoto Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli na Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe.
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,,Henry Kinabo alisema, “Tuna furaha kuwa sehemu ya mbio hizi kwa mara nyingine. Hizi ni mbio ambazo zinawaleta pamoja wanariadha wakubwa na watu kutoka Nyanja mbalimbali kusherekea michezo, kufurahi, kukuza utamaduni, utalii na pia kwa afya bora,” alisema.
Alisema Tigo, inayodhamini mbio za kilometa 21, itatoa jumla ya Milioni 11 kama zawadi huku msindi wa kwanza wa kiume na kike wakijinyakulia milioni 2 kila mmoja wa pili milioni 1 wakati wa tatu watapokwa Tsh 650,00o huku Katia ya 500,000 na 100,000 zikienda kwa washindi kuanzai wan ne hadi wa 10 pamoja za medali za ushiriki kwa kila atakayemaliza mbio.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa TBL anayesimamia kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro, alisema mbio za Kilometa 5 zinazodhaminiwa na Grand Malt zinakuwa mwaka hadi mwaka na kuwavutia watu wengi zaidi wakiwemo watoto, vijana na watu wazima. “Tumeandaa shughuli mbalimbali za kusisimua kwa ajili ya washiriki kwa hivyo tujiandikishe mapema na tukumbuke kunywa Grand malt kwa kuwa ni kinywaji chenye afya hasa kwa wanariadha,” alisema.
Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media na kuratibiwa na Executive Solutions. Wadau wengine muhimu ni, Chama Cha Riadha Tanzania, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro Marathon Club, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,vilabu vya jogging na Jeshi la Polisi.
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo (kulia) akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanga kutoa huduma mwakani katika mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitazofanyika mwakani machi 4 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

RAIS MHE.DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI TATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

October 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akijitambulisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitazama vitabu alivyokabidhiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiwa amesimama wakati wa nyimbo za Mataifa ya China na Tanzania zikipigwa katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uholanzi hapa nchini  Jeroen Verheul Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Uholanzi hapa nchini  Jeroen Verheul mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAHAKAMA ZA WATOTO PASUA KICHWA

October 25, 2017

KUTOKUWA na uwakilishi wa kisheria katika mahakama za watoto wanaokinzana na sheria, kimekuwa kikwazo kikubwa kupata haki ambayo wanastahiki kupatiwa. Jambo hili limesababisha watoto wengi kuhukumiwa kutumikia adhabu mbalimbali.
Hali hiyo pia imesababisha maumivu makubwa kwa jamii hasa baada ya ndugu na jamaa zao kulazimika kuwa kizuizini kutokana na makosa mbalimbali ambayo huenda ametenda, anatuhumiwa au amesingiziwa.
Uwepo wa changamoto hiyo kubwa kwa watoto umekipelekea Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla) mkoani Tanga, kutoa elimu juu ya namna ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto walio katika ukinzani na sheria kwa wadau wake kwenye masuala ya watoto walio katika ukinzani na sheria.
Licha ya kutoa elimu hiyo, chama hicho pia kinatoa msaada wa kisheria kwa watoto walio katika ukinzani na sheria kwa kuwapatia wanasheria wa kuwawakilisha mahakamani kupitia mpango wake wa Pro bono.
Kupitia mpango wake huu wa Pro bono, Tawla iliwezesha kumpatia msaada wa kisheria mtoto, Sophia John Komba (17) ambaye alituhumiwa na kosa la mauaji ya kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya Nguvumali na  Raskazone. Mtoto Sophia aliwekwa kizuizini tangu Januari mwaka huu katika kituo cha mahabusu ya watoto.
Binti huyo ambaye ni mtahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne, alitakiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu lakini alishindwa kwenda shule kutokana na kukabiliana kesi ambayo yeye na baba yake mzazi zinawakabili.
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake mkoani Tanga (Tawla), Mwanasheria Latifa Mwabondo,(Pichani Juu) anasema Tawla  kupitia mradi wake wa utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto na wanawake waliokuwa katika ukinzani na sheria, aliembelea  mahabusu ya watoto ili kuweza kujua idadi ya watoto walio katika ukinzani na sheria na kujua makosa yanayowakabili ili kuwapatia msaada wa kisheria.

Shirika la Hakizetu lazindua awamu ya pili ya mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia Manispaa ya Ilemela

October 25, 2017
Binagi Media Group
Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake, Hakizetu lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, limezindua mradi ujulikanao kama “Kila Mtu Aishi Vyema Kuanzia Sasa” awamu ya pili (Living Better Today Project  phase II), lengo ikiwa ni kutokomeza ukatili katika jamii.

Mradi huo umelenga kufanya kazi katika Kata mbili za Ibungiro na Nyamanoro katika Manispaa ya Ilemela ambapo vikundi mbalimbali vya kijamii vitaundwa hadi katika ngazi ya jamii na wanafunzi wa sekondari katika shule za Mwanza Baptis na Ibungiro na kujengewa uwezo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa elimu ya kujikinga na ukatili wa kijinsia katika jamii.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa mradi huo, Afisa Miradi wa shirika la Hakizetu, Gervas  Evodius alisema awamu ya kwanza ya mradi huo iliwafikia wananchi 2,400 katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana hivyo awamu ya pili matarajio ni kuwafikia wananchi 300 ambao watakuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.

Alisema mradi umelenga kufanya kazi zaidi katika ngazi za jamii/ familia ambapo kuna mzizi wa ukatili kwa wasichana na wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni na kwamba matarajio ni kutatua changamoto hiyo katika jamii.

Evodius alisema ni wakati mwafaka kwa wanajamii kuungana pamoja ili kutokomeza ndoa na mimba za utotoni pamoja kila aina ya ukatili wanaokumbana nao wasichana na wanawake kwani ni jukumu la kila mmoja kuwakinga.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Cunegunda Ngereja alisema shirika linatoa elimu pamoja na kuwawezesha kiuchumi wahanga wa ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo kuwawezesha kiujasiriamli ili kuondokana na umaskini kwani umaskini na ukatili katika jamii huchangia mimba na ndoa za utotoni.

Alisema wanashirikiana na wadau mbalimbali kupitia vikao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha mtoto wa kike na wanamke wanakua salama katika jamii.

Mmoja wa washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Mwanasheria Akram Salim, alisema wanajamii wanapaswa kuelewa kwamba ukatili wa kijinsia katika jamii umepitwa na wakati hivyo ni vyema kuwa na mtazamo chanya wa kutambua kuwa kujihusisha na ukatili wa kijinsia ni kuvunja sheria za nchi.


Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkudi katika Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, Salum Heri alisema baadhi ya watoto wa kike hukumbana na ukatili wakiwa nyumbani ikiwa ni pamoja mbimba za utotoni kutoka kwa watu wa karibu na hivyo sheria kushindwa kuchukua mkondo wake kutokana na kesi za aina hiyo kumalizwa kifamilia ambapo alitoa rai kwa shirika la Hakizetu kuendelea kuwasaidia kielimu na kiujasiriamli wasichana waliokumbana na ukatili wa aina hiyo ili kuwaondoa kwenye utegemezi katika jamii.

DC KASESELA, MBUNGE PETTER MSIGWA NA RITTA KABATI KUUPAMBA UZINDUZI WA ALBAMU YA DR TUMAINI MSOWOYA

October 25, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili DR Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall Iringa mjini.

Sambamba na kasesela wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo ni Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupita chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma na  wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.

Akizungumza na blog hii DR Msowoya alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.

“Naenda Iringa kurudisha shukrani zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya kuimba niliyoanza ”

Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.

“Kazi hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.

Lakini Meneja wa Dr Msowoya Smart Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.

Alizitaja kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka Iringa mjini.

Baadhi ya waimbaji ni  Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.

Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi,  Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.

“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi nab ado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.

Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.

Historia
Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.
“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.


SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA NGUVU KWENYE TASNIA YA FILAMU

October 25, 2017


 MSANII wa filamu nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Paparazi Intertaiment,Simon Mwapagata maarufu Rado akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Jumamosi oct 28 mwaka huu kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanga (TD FAA),Mohamed Majuto na kulia ni Katibu wa Chama hicho,Raphael Kiango
 MSANII wa filamu nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Paparazi Intertaiment,Simon Mwapagata maarufu Rado akiwaonyeshawaandishi wa habari mkoani Tanga kava la filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Jumamosi oct 28 mwaka huu kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanga (TD FAA),Mohamed Majuto na kulia ni Katibu wa Chama hicho,Raphael Kiango
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Nyumbani iliyopo Jijini Tanga
SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imeshauriwa kuwekeza nguvu kwenye tasnia ya filamu za kitanzania ambazo zinaweza kusaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumia kwa kutoa ajira kama itakavyokuwa kwenye viwanda.
Ushauri huo ulitolewa na Msanii muigizaji wa tasnia ya Filamu hapa nchini maarufu kama (Bongo Muvi) Saimon Mwapagata “Rado”ambapo alisema kutokana na uwepo wa soko kubwa la filamu linaweza kusaidia kuajiri vijana wengi wa kitanzania.

Alisema iwapo tasnia hiyo ikitiliwa mkazo na kuwepo kwa usimamizi makini ambao utaweza kusaidia wasanii kuweza kupata mafanikio kitendo ambacho kitawawezesha kulipa kodi na kuinua uchumi wa nchini.

Sanjari na hayo lakini msanii huyo ambaye yupo jijini Tanga alisema atazinduzi wa filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Juma mosi oct 28 mwaka huu.

Alisema uwepo wa tasnia hiyo ni sawa na kiwanda kisichokuwa na hasara iwapo watawekewa mazingira mazuri ikiwemo kudhibiti matapeli wanaoihujumu tasnia hiyo hali inayosababisha waandaaji wa filamu hizo kukosa haki zao za msingi za mauzo na kuisababishia serikali kukosa mapato kupitia tasnia hiyo.

“Tunamuona Rais wetu anavyohangaika na uchumi wa viwanda lakini amesahau kuwa tasnia ya filamu ni viwanda visivyokuwa na hasara na ikiwa atahakikishia haki zetu za msingi na kudhibiti walaghai ninaimani Serikali inaweza kuvuna mapato mengi kupitia filamu na kutengeneza ajira nyingi”Alisema.

Aidha alisema filamu hiyo alikwisha ionyesha Mlimani City lakini kutokana na ubora wake na maombi ya watu wengi ameamua kuonyesha Jijini hapa ambapo anatarajia Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kuwa Mgeni rasmi.