MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AKAGUA UKUMBI KABLA YA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM KUFANYIKA

MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AKAGUA UKUMBI KABLA YA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM KUFANYIKA

July 21, 2016

1Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre uliopo  mjini Dodoma ambapo ndipo mkutano mkuu maalum wa kuthibitisha  jina la Rais Dk John Pombe Magufuli kuwa  Mwenyekiti  mpya wa chama hicho baada ya kukabidhiwa na Mtangulizi wake Mh. Dk Jakaya Kikwete.
2Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akikagua matayarisho ya mkutano huo, kushoto ni Ndugu Rajab Luhwavi Naibu Katibu Mkuu Bara.
3
Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akizungumza na mjumbe wa kamati kuu Ndugu Mohamed Seif Khatib.
4Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akizungumza jambo wakati akikagua kumbi mbalimbali za Wageni Maalum, wanaomsikiliza kulia ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM na kusoho ni Nape Nnauye Katibu Mwenezi wa CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajab Luhwavi.
5Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akijaribu kipaza sauti huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia.
6
Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete akionyesha mandhali ya ukumbi na Nape Nnauye Katibu Mwenezi Taifa wa CCM wakati alipokuwa akikagua ukumbi huo.
7Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu Mwenezi Taifa CCM
8Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baadhi ya mambo kwa ajili ya matayarisho ya mkutano mkuu wa maalum wa CCM.
9Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mh. Dk. Jakaya Kikwete akiendelea kukagua ukumbi huo huku akiwa ameongozana na viongozi waandamizi wa Chama hicho.
WARSHA YA WADAU YA KUPITIA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA YAFANYIKA DAR ES SALAAM

WARSHA YA WADAU YA KUPITIA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA YAFANYIKA DAR ES SALAAM

July 21, 2016

s1 
Sehemu  ya wadau kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (hayupo pichani) katika Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira.
s2 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka AbdulWakil akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi (kushoto) mara baada ya kufungua Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira. Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Bw. Deogratius Paul.
s3 
Wana warsha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa Warsha katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na Mpiga Picha Wetu
TAIFA STARS KAMBINI AGOSTI MOSI, 2016

TAIFA STARS KAMBINI AGOSTI MOSI, 2016

July 21, 2016

mkwasaserena 
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Jumanne ya Julai 26, 2016 anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mkwasa maarufu kama Masters amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.
“Kikosi change kitakuwa na vijana wengi, mimi ni muumini mkubwa soka la vijana ambao baadhi niko nao na ambao nitawaita, lakini pia mara baada ya ligi kuanza, nitaangalia wengine kabla ya kuwa na program ya ratiba ijayo ya michuano mbalimbali ya kimataifa itakayotolewa na CAF na FIFA,” amesema Mkwasa.
Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili; Taifa Stars ina pointi moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NA CONGO JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NA CONGO JIJINI DAR ES SALAAM

July 21, 2016

C1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. 
C3 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akipokea zawadi ya Pambo kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem. Waziri Mwigulu alizungumza na Balozi huyo masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MJINI DODOMA LEO.

July 21, 2016

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016 pamoja na wajumbe wa mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais Dkt John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano unaotarajiwa kufanyika Julai 23,2016.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.
Mwenyekiti Mtarajiwa Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama cha CCM nje ya ukumbi wa ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mwenyekiti mtarajiwa,Rais Dkt Jonh Magufuli nje ya ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.

Wajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.
 ajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.

KATIBU MKUU SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA HABARI , UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

July 21, 2016
Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime, leo 21 Julai 2016, amefanya mazungumzo marefu na  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura ofisini kwa Naibu Waziri huyo. 

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Shirikisho aligusia mambo mbalimbali yakiwemo, sehemu za kufanyia kazi za sanaa ya muziki (kumbi), matatizo ya utekelezaji wa Hakimiliki, ukubwa wa kodi za vifaa vya kazi za muziki,  na mengine mengi ikiwemo kumkabidhi Naibu Waziri tafiti mbalimbali zilizofanywa zilizohusu menejimenti ya tasnia ya muziki. 

Mazungumzo haya yaliyochukua zaidi ya saa mbili, yalifikia kwa makubaliano kuwa kutakuwa na ukaribu zaidi kati ya Wizara na viongozi mbalimbali wa sanaa ili kuboresha mazingira ya utendaji wa kazi za sanaa.
DKT. REGINALD MENGI AMTUMIA UJUMBE MZITO WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA

DKT. REGINALD MENGI AMTUMIA UJUMBE MZITO WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA

July 21, 2016
Katika kufikia malengo ya Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi amemtumia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ujumbe kupitia kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama, ujumbe ambao anaamini kama ukifanyiwa kazi Tanzania itaweza kufikia malengo yake kwa haraka zaidi.
Dkt. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP alituma ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wakati ufunguzi wa Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji ambalo linafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, kongamano lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Alisema kuwa pamoja na serikali kufanya jitihada nyingi ili kuwashirikisha wananchi wake katika uwekezaji kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi lakini bado kuna changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza na zinahitaji kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kwa niaba ya TPSF ambapo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali mambo ambayo anaamini serikali ikiyafanyia kazi uchumi wa Tanzania utakua kwa kasi tofauti na sasa.(Picha na Modewjiblog)

"Serikali imekuwa ikitumia pesa kuwapeleka vijana kusoma nje lakini nikakutana na kijana mmoja akaniambia kasoma nje lakini bado hana ajira na alipelekwa kusomea digrii ya mambo ya mafuta na gesi,

"Nadhani ni vyema serikali ikabidili mwenendo wake na kuhakikisha vijana wote ambao wanapelekwa kusoma nje wakirudi nchini wapewe nafasi za kazi ili kulisaidia taifa kwa hiyo naomba utufikishie ujumbe kwa Waziri Mkuu ukienda Dodoma katika mkutano mkuu wa chama," alisema Dkt. Mengi.

Pia alisema nchi yetu imekuwa ikitegemea zaidi kilimo hivyo iwekeze katika kilimo na iache kuagiza nje bidhaa ambazo zinatengenezwa na vyakula ambavyo vinapatikana nchini lakini pia kuwapa vipaumbele wawekezaji wazawa na hata wanapokuja wageni ihakikishe na watanzania wanashiriki kikamilifu katika kuwekeza.

Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

"Nchi yetu kwa miaka mingi tunajulikana kuwa tunafanya zaidi kilimo na nadhani hapa kunahitaji ushirikishwaji mkubwa wa watanzania na tuache kulima nanasi na hapo hapo tunaagiza juisi ya nanasi nje ni muhimu watanzania watambue kuwa nchi yao ni tajiri na wakishiriki kikamilifu itafika mbali," alisema Dk. Mengi.

Kwa upande wa Waziri Mhagama ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lakini serikali inalifahamu hilo na wameanza kufanya mabadiliko ya sheria na sera wanazozitumia kwa sasa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba katika kongamano hilo pamoja na kujibu baadhi ya hoja alizotoa Dkt. Mengi.

"Serikali inalifahamu jambo hilo kama kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ili kuwasaidia Watanzania kukuza uchumi wao na wa taifa, kwa sasa tumeanza kufanya mabadiliko kwa baadhi ya sheria na sera na tutaendelea kuangalia ni wapi kunahitajika mabadiliko ili kila jambo lifanyike kwa faida ya watanzania wote," alisema Waziri Mhagama.

Akielezea kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa alisema malengo ya kongamano ni kubadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa serikali na sekta binafsi lakini pia kushirikisha mashirika ya nje ya nchi ili kuweza kupata njia bora ambayo itakwenda kutumika katika kuwashikirikisha watanzania wote ili kila mmoja ashiriki kukuza uchumi wa taifa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa akielezea malengo ya kongamano hilo la siku mbili.

Baadhi ya wageni waalikwa ambao wamehudhuria kongamano hilo la siku mbili.



Wageni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

KUELEKEA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM MJINI DODOMA, WAJUMBE KUTOKA MKOANI MWANZA WAELEZEA IMANI YAO.

July 21, 2016
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, akizungumzia maandalizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza, ambao tayari wameanza kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 23,2016 ambapo pamoja na mambo mengine pia Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatarajiwa kumpitisha kwa kura za ndiyo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, akipokea Uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoani Mwanza, wamesema wana imani kubwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ambaye anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Katibu Mwenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, ameyasema hayo hii leo, wakati akizungumzia maandalizi ya wajumbe hao ambao baadhi yao tayari wamewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 23 mwaka huu.

“Sisi wajumbe tunaotoka Mkoa wa Mwanza tunaamini kwamba anatosha (JPM) na yuko makini na chama chetu kitaendelea kuimarika zaidi akikabidhiwa uongozi. Amesema Mangelepa na kuwasihi viongozi wengine wa CCM kuanzia ngazi ya Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa, kuendelea kukiimarisha chama, ikiwemo kusimamia vizuri Ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge kama Rais Magufuli anavyosisitiza.

Ametanabaisha kwamba wananchi wakiwemo wanaccm, wanayo matumaini makubwa kwa Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi, na kwamba wapenda amani na maendeleo wanaochukia rushwa pamoja na ubadhirifu wanampenda sana.

Katika hatua nyingine Mangelepa amepuuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba hiyo inaashiria hofu waliyo nayo baada ya kukabidhiwa uongozi wa CCM kwa kuwa watakosa hoja za kuzungumza kisiasa.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

MAN UTD DORTMUND KUFUNGUA PAZIA LA MICHUANO YA ICC ITAKAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES

July 21, 2016



 Na Dotto Mwaibale

 IKIWA chini ya kocha wake mpya Mreno, Jose Mourinho, Manchester United wanatarajia kushuka dimbani jijini Shanghai, China kuwakabili Borrusia Dortmund siku ya Ijumaa Julai 22, 2016 mechi itakayopigwa saa tisa za alasiri kwa saa za hapa nyumbani kupitia ving’amuzi vya StarTimes.

Akizungumzia juu ya habari hiyo njema kwa wapenda soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa michuano hiyo itakuwa ni ya kusisimua kutokana na orodha ndefu ya timu kubwa zitakazoshiriki kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich kwa uchache.

“Tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa watapata fursa ya kutazama timu zao katika mechi za awali kabla ya kuanza kwa ligi kuu mbalimbali duniani kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee. Mechi zote za michuano ya ICC itaonekana moja kwa moja kupitia chaneli ya World Football inayopatikana katika kifurushi cha Mambo kwa malipo ya shilingi 12000/- tu kwa mwezi. Michezo yote itakuwa ni yenye msisimko mkubwa kwani timu zinazoshiriki ni kubwa, nyingi zikiwa ni mabingwa katika ligi kuu zao, zina wachezaji nyota na kikubwa zaidi zingine hazikuwahi kukutana kabla.” Alisema Bi. Hanif

“Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kwani tunafahamu ya kuwa ni wapenzi wakubwa wa mchezo huu na siku zote StarTimes tunajitahidi kuwapatia kile wanachokipenda. Hii ni mara ya pili tunaonyesha moja kwa moja michuano hii kwani mwaka jana tulifanya hivyo ambapo timu ya Real Madrid waliibuka mabingwa. Hivyo basi mashabiki watakuwa na shauku kubwa ya kujua ni timu gani itakayoibuka mabingwa au kama utarudi kwa Real Madrid,” alisema na kumalizia Bi. Hanif kuwa, “Ni wajibu wetu kuhakikisha wanafikiwa na matangazo ya vipindi vizuri na kusisimua kama hivi kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu ambazo kila mtu atazimudu.”

Mchezo huo ni sehemu ya ufunguzi wa michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa almaarufu kama International Champions Cup au ICC itakayoanza kutimua vumbi Julai 22 na kumalizika Agosti 13, 2016 katika viwanja mbalimbali nchini Marekani, Ulaya, Australia na China.

Katika michuano hii wapenzi wa soka duniani watapat fursa kujionea kwa mara kwanza mechi ya watani wa jadi kutoka jiji la Manchester au unavyojulikana kama ‘Machester Derby’ miongoni mwa mashabiki wengi. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatatu ya Julai 25 jijini Beijing, China.

Mchezo huo utanogeshwa si tu na ushindani baina ya wachezaji au mashabiki bali safari hii ni makocha waliopewa vibarua vya kunoa vikosi hivyo, Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Ukiachana na mechi hiyo, pia macho ya mashabiki wengi yatakuwa yakisubiria kwa hamu kutazama mechi kali zitakazozikutanisha timu za, Real Madrid na  PSG,  Chelsea na Liverpool, Real Madrid na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Liverpool na Barcelona.

Kwa ujumla timu zitazoshiriki  michuano hii ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain (PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham Hotspurs, AC Millan, Inter Millan, Leicester City FC, Celtic FC, Atletico Madrid, Melbourne Victoria na South China.

WARSHA YA WADAU YA KUPITIA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA MAZINGIRA YAFANYIKA DAR ES SALAAM

July 21, 2016
 Sehemu  ya wadau kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (hayupo pichani) katika Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka AbdulWakil akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi (kushoto) mara baada ya kufungua Warsha ya kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira. Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Bw. Deogratius Paul
Wana warsha wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa Warsha katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam

MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMA LEO

MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMA LEO

July 21, 2016

1 
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete wakati akifungua kikao cha Kamati Kuu ya ya Halmashauri kuu ya  CCM kilichofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma kupendekeza jina la Mwenyekiti mpya wa CCM ambapo jina hilo litapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili kupelekwa kwenye mkutano mkuu   na kuthibitishwa katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
2Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete  akifungua kikao cha Kamati Kuu ya ya Halmashauri kuu ya  CCM kilichofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula na katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurrahman Kinana.
3 
Rais Dk John Pombe Magufuli kushoto pamoja na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete na viongozi wengine wakiimba wimbo maalum wa CCM wakati mkutano huo uliofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma
4
Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu William Lukuvi akizungumza na wajumbe wenzake Adam Kimbisa kushoto na Nape Nnauye Katibu Mwenezi wa CCM Taifa.
5
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Adam Kimbisa akuzungumza na wajumbe wenzake kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu Mwenyezi wa CCM Taifa, Mama Zakia Megji , William  Lukuvi na Mohamed Seif Khatib.
6
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa kamati kuu wakati alipowasili kuhudhuria katika mkutano huo.
7
Wajumbe wa Kamati Kuu Mzee Steven Wasira kulia na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka wakifurahia jambo kabla ya mkutano huo kuanza.
8 
Mjumbe wa Kamati kuu kutoka Zanzibar Sadifa Juma Khamis akizungumza na mjumbe mwenzake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ndugu Abdallah Bulembo kutoka kulia ni Jerry Silaa na Hussein Mwinyi.