NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY ATEMBELEA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

March 10, 2016



Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika(kushoto)akimwongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kuwasilimia wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara yake ,Norway ni moja ya nchi zinazosaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini. 

Ujumbe uliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kutoka Norway na maafisa kutoka ubalozi wao nchini wakisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen (kulia)akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen na ujumbe wake wakipata maelezo ya mfano wa kuzalisha umeme unaotokana na chanzo kidogo cha maji. 
Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Chuo hicho akimpa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen maelezo kuhusiana na kozi yake. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo.Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

TPSF YAZINDUA MFUMO WA HABARI KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA WADOGO JIJINI DAR

March 10, 2016


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na mwenyekiti mtendaji wa IPP LTD Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakifuatilia uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Furaha mara baada ya uzinduzi huo. Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kupewa vyeti vya shukrani.
SPIKA JOB NDUGAI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

SPIKA JOB NDUGAI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

March 10, 2016


dug1

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
dug2
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunhgano wa Tanzania (hayupo pichani) mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
dug3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongea na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (hayupo pichani) leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
dug4
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani) mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
dug5
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) na ujumbe wake akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia ) na ujumbe wake mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
dug6
Baadhi ya ujumbe alifuatana nao Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakifuatilia mazungumzo yao leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. . 
dug7
Baadhi ya ujumbe alifuatana nao Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai wakifuatilia mazungumzo yao leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
dug8
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiongea na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
dug9
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiongea na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya mkutano uliofanyika kati ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es
Salaam.spi1
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) pamoja na  Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) na  Naibu Spika wa Bunge Mhe Dkt Tulia Ackson wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yaliyohusishwa na baadhi ya ujumbe toka nchi ya Vietnam na Tanzania leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATEMBELEA GEREZA BIHARAMULO PAMOJA NA ENEO LINAKOJENGWA GEREZA LA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATEMBELEA GEREZA BIHARAMULO PAMOJA NA ENEO LINAKOJENGWA GEREZA LA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA

March 10, 2016

cas1
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
cas2
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.
cas3
Mkuu wa Wilaya ya  Chato, Mhe. Shaban Ntarambe(kushoto) akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakielekea eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato mara baada ya Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasili Wilayani Chato kabla ya kuelekea Mkoani Kagera
cas4
Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
cas5
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
cas6
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akisaini katika kitabu cha Wageni alipotembelea Gereza la Wilaya ya Biharamulo katika ziara yake ya kikazi leo Machi 10, 2016.
cas7
Mkuu wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara yake ya kikazi.

MWAMOTO KUKUTANA NA WAZIRI MKUU KUKUMBUSHIA AHADI YA MAJI MJI WA ILULA ILIYOTOLEWA NA RAIS DR MAGUFULI

March 10, 2016


 mbunge  wa  Kilolo mkoani Iringa Bw  Venance Mwamoto akisalimiana na wananchi  wa Ilula  waliokuwa wakisubiri maji
Mwamoto akizungumza na meneja wa maji mji mdogo wa Ilula Bi Mvungi
 

 Mbunge wa Kilolo Bw  Venance Mwamoto (kushoto)  akisalimiana na mmoja kati ya  wazee wa mji wa Ilula  aliyetoka  kuchota maji
Mbunge  wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akisaidia  kufungulia maji    
 ……………………………………………………………………………………………………………………..
 Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa  jimbo la  Kilolo  Venance  Mwamoto ameahidi kuongozana na  wazee  wa mji  wa Ilula kwenda Dodoma kuonana na   waziri  mkuu Kassim Majaliwa  ili  kumfikishia ahadi ya  maji ya Rais Dr John Magufuli kwa
wananchi  wa mji  mdogo  wa Ilula .
 
Huku  akiwataka wananchi wa Ilula na Nyalumbu  kutomchagua mwaka 2020  iwapo atashindwa  kutekeleza ahadi ya maji katika mji  huo wa Ilula ndani ya  miaka  yake  mitano ya  ubunge.
 
Akizungumza  na  wananchi  wa kata ya  Nyalumbu na Ilula  wakati wa  mikutano yake ya  hadhara ya  kuwashukuru  wananchi  wake kwa kumchagua  kuwa mbunge wa  jimbo  hilo la Kilolo jana ,Mwamoto  alisema  kuwa  kero ya maji
katika  mji wa Ilula  imekuwa ya muda murefu   jambo ambalo hatataka   kuona   wananchi  hao  wakiendelea kutabika.
 
Alisema  kuwa   kero hiyo  ya maji imeanza  kuwasumbua  wananchi hao toka nchi ipate  uhuru  wake mwaka 1961  hadi  leo wapo katika mahangaiko ya maji na  baadhi ya  viongozi  wameendelea  kufanya udanganyifu  wa mradi huo
kama  ambavyo   mwaka 2010   viongozi  walivyomdanganya aliyekuwa makamu  wa Rais Dr Alli Mohamed  Shein  kwa  kupelekwa  kufungua  mradi wa maji ambao  viongozi  walimdanganya kwa  kujaza maji katika tanki
hilo  ili azindue mradi huo.
 
Hivyo  alisema udanganyifu  huo hautapewa nafasi katika uongozi  wake wa miaka  mitano  lazima kero  hiyo imalizike na  wananchi hao  waweze kupata maji vinginevyo yupo tayari  kuongoza  wananchi  wake kumzuia waziri wa maji kupita Ilula kwenda jimboni kwake Njombe  iwapo  wananchi hao hawatatimiziwa ahadi yao ya maji  safi na salama .
 
Mbunge  huyo  alisema katika  kikao kijacho cha  bunge kinachoanza mwezi ujao ataomba  wananchi wa Ilula na Nyalumbu  kumteulia wazee watatu ama  wanne   ili kwenda nao bungeni Dodoma  kukutana na  waziri  mkuu ili
kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya  maji katika mji  huo wa Ilula
Pia  aliagiza mamlaka ya maji ya mji  mdogo wa Ilula  kuchunguza vema mradi wa maji uliopo kama umejengwa kwa kiwango ama chini ya kiwango maana amesema mradi mdogo  uliopo kwa  sasa  bado umekuwa na kero  kubwa ikiwa
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji  huku  akiwataka  wananchi kwa  upande  wao kutunza miundombinu ya maji.
Katika  hatua nyingine  mbunge Mwamoto  alimshauri meneja wa maji wa IRUWASA katika mji wa Ilula Teodolah Mvungi  kuangalia uwezekano wa  kuboresha kituo  cha maji eneo la Ilula  ili  kiweze  kunufaisha  wananchi  wengi
na  kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono
.
 

HAPPY BIRTH DAY MWANANZENGO WA 102.5 LAKE FM, RAHA YA ROCK CITY

March 10, 2016
Jana Machi 10,2016 ilikuwa ni Siku ya Kuzaliwa kwa Mkurugenzi wa 102.5 Lake Fm, Raha ya Rock City, Radio ya Wananzengo, Doreen Noni.
Zaidi Bonyeza HAPA

ZAIDI YA WASICHANA 500 JIJINI MWANZA WANUFAIKA NA MRADI WA BINTI BOX.

March 10, 2016
Wasichana wa Shule ya Sekondari Luchelele wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji toka DidaVitengeWear Foundation mara baada ya kupokea taulo za usafi (Pedi) na Elimu ya Usafi wa mwili na uzazi chini ya mradi wa Binti Box unaotekelezwa katika shule za Sekondari na Msingi kanda ya Ziwa.
Katika kusheherekea siku ya Wanawake Duniani Machi 08,2016, taasisi ya kusaidia wanawake na wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza, DidaVitengeWear Foundation, Imefanikisha kugawa taulo za usafi zaidi ya 2,000 kwa wasichana zaidi ya 600 wa shule ya msingi Igombe na Shule ya Sekondari ya Luchelele zote za Jijini Mwanza kupitia mradi wa kuwasaidia Mabinti kufikia malengo yao, ujulikanao kama ‘Binti Box’.  

Hatua hiyo pia imefikiwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya taasisi hiyo pamoja na Mtandao wa Wanawake jijini Mwanza wa ‘Women Roundtable’, na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mh.Stanslaus Mabula, Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoani Mwanza Zawadi Kiteto na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mkoani Mwanza Mh.Maria Kangoye Ndila 

Binti Box ni mradi ulioanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike waliopevuka kubaki shule na kuimarisha mahudhuria ya wasichana shuleni kwa kuwapatia vifaa vya usafi vitakavyowasaidia wakati wa siku zao za hedhi. Wasichana wengi hasa wa vijijini hukosa kwenda shule kwa siku 5 mpaka 7 kwa mwezi kwa sababu ya kukosa vifaa vya usafi wakati wa mzunguko wa hedhi, hivyo mradi huu kwa upande wa kanda ya ziwa ni mkombozi kwa mabinti wengi kuhudhuria shule na kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

Akiongea wakati wa kugawa taulo hizo za usafi mashuleni, Bi. Khadija Liganga, Mratibu wa Mradi na Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation, alieleza kwamba, elimu ya wasichana ni jambo la msingi katika jitihada za kuleta maendeleo kwa nchi masikini kwa sababu mafaniko ya wanawake hasa katika elimu inamaanika kuwa na faida ya muda mrefu na huenda mbali Zaidi katika kuinua uchumi wa jamii na nchi.

“Kuna sababu nyingi zinazochangia kudumaa kwa ustawi wa elimu ya mtoto wa kike hasa wale wa vijijini, tatizo la ukosefu wa vifaa vya usafi kwa mabinti wakati wa hedhi kwa kila mwezi nayo imeibuka kuwa ni tatizo sugu linalofumbiwa macho na wadau wengi wa maendeleo katika nchi zinazoendelea na Tanzania ikiwemo. Wasichana hawa hujawa na uwoga na kuhofia kupoteza thamani yao na utu wao wawapo shuleni au mbele za watu na kuwafanya wasihudhurie darasani au kutokwenda shule na matokeo yake wengi huacha shule,” amesema Bi. Khadija Liganga  

Bi.Khadija aliendelea kusema kwamba “Baada ya kutembelea baadhi ya shule zilizo pembezoni na miji tumegundua tatizo ni kubwa, tukapata uwelewa wa kutosha na tukaona ni vyema badala ya kuandaa makongamano ya wanawake wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Dunaini 2016, kwanini tusiguse eneo ambalo ndio chimbuko la ukandamizaji wa maendeleo ya Mwanamke, ambalo ni Elimu. Ndipo tukaja na huu mradi utakaokuwa endelevu wa ‘Binti Box’ kwa lengo la kutoa taulo za usafi kwa mabinti wa shule za msingi na sekondari pamoja na elimu ya usafi wakati wa siku za hedhi”

“Tungependa kuwashukuru watu wote pamoja na taasisi mbalimbali kwa mchango wa o wa maboksi ya taulo za usafi. Huu ni mwanzo tu, huku mipango ikiwa ni kuongeza uwezo wa mradi kuweza kutoa huduma hii kwa shule za sekondari na msingi katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, tuko tayari kushirikiana na watu binafsi au taasisi yoyote katika kumkomboa mtoto wa kike” alisema Bi. Khadija Liganga

Lengo la Mradi wa Binti Box ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia taulo za usafi wasichana wa sekondari na shule za msingi waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mwanza na Mara. Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation ambae pia ni Mratibu wa Mradi wa Binti Box akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum Vijana mkoa wa Mwanza kupitia CCM, Mh. Maria Kangoye Ndila (Katikati) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Mwanza Mh. Zawadi Kiteto (Kushoto), wakati wa utekelezaji wa mradi wa kugawa taulo za usafi kwa Mabinti wa Shule ya Msingi Igombe.
Mkufunzi wa Afya ya Uzazi ambae pia ni muuguzi msaidizi kutoka kituo cha Afya cha Makongoro akitoa elimu ya usafi wa mwili na kuepuka mimba za utoto kwa wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Igombe chini ya mradi wa Binti Box ulioandaliwa na DidaVitengeWear Foundation kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jijini Mwanza.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupewa vifaa vya usafi vitakavyowasaidia katika mzunguko wao wa kila mwezi na kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana na kutumia vifaa visivyo salama.
Kushoto ni Bi. Khadija Liganga Mkurugenzi wa taasisi ya kusaidia wanawake na maendeleo ya wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza, DidaVitengeWear Foundation akihimiza jambo juu matumizi mazuri ya vifaa vya usafi kwa wasichana wa shule ya sekondari ya Bujora (hawapo pichani), Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana mkoa wa Mwanza, Bi. Maria Kangoye Ndila ambae aliungana katika mradi huo kuwasaidia mabinti walio shuleni.
Mabinti wa shule ya sekondari ya Bujora iliyopo Wilayani Magu mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa taulo za usafi toka taasisi ya DidaVitengeWear Foundation.

BENKI YA CRDB YAIKOPESHA MANISPAA YA TEMEKE BIL.19.6

March 10, 2016

Na Mwandishi Wetu

MANISPAA ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, imepokea mkopo wa sh bilioni 19.6 kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi wa maeneo yatakayobomolewa ili kupisha mpango wa maendeleo na ustawi jiji.

Mkopo huo utakaolipwa kwa miaka sita una lengo la kufanikisha mradi mkubwa wa ujenzi na uboreshaji miundombinu ya jiji uitwao Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP).

Akizungumza na ujumbe wa viongozi na madiwani wa wilaya ya Temeke ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei iliyotoa mkopo huo alisema wanaunga mkono hatua za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali Kuu na Tamisemi. 

Alisema fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 81.63 ujenzi wa masoko ya kisasa, vituo vya mabasi ya kisasa, upimaji wa viwanja 2,000 eneo al Kijichi na kuweka huduma za msingi, ujenzi wa mifereji ya mvua kilometa 22.4, dampo la kisasa eneo la Kisarawe na madaraja yanayounganisha kata mbalimbali.

“Tumetoa mikopo ya maendeleo kama huu kwenye halmashauri za Mwanza, Magu, Kinondoni, Mbeya na Mji wa Bukoba ambapo jumla ya sh trilioni tatu ambazo ni karibu sawa na bajeti ya maendeleo inayotengwa na serikali ambayo ni sh trilioni saba,” alisema Dk. Kimei.

Mjema aliwaonya watendaji wanaohusika na mradi huo kutoongeza majina ya wanaotakiwa kulipwa huku akisisitiza kwamba watakaobainika kuhujumu mradi huo na kutumia isivyostahili mkopo huo, watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP). (Picha ha Francis Dande)
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP).
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Temeke.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa benki hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Saugata Bandyopadhya.
 Meya wa Manispaa  ya Temeke, Abdallah Chaurembo (kulia), Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Photidas Kagimbo (wa pili kulia), wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa tatu kushto, akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema mfano wa hundi yenye thamani ya Shs. Bilioni 19.6 kwa ajili ya uboresha wa miundombinu katika Mamlaka zaSerikali za Mitaa za Jijini la Dar es Salaam.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akibadilishana hati na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. 
RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) LEO

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) LEO

March 10, 2016

bt1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
bt7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016 Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.
bt8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akiwa kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao  makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016