RC MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

RC MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

June 28, 2016
Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Makonda alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila mwananchi alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lillilopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.


Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa Habari wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda amekuwa mgeni kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye maonyesho hayo.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda hilo na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

+AUDIO: SABABU ZA KUNDI LA MUZIKI LA PAYUS & MECRAS KUTOKA JIJINI MWANZA KUBADILI JINA.

June 28, 2016
Wakali wa wimbo wa Chausiku, Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza, ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Muziki la Payus & Pacras, wamebadili jina la kundi lao na sasa wanaitwa WAPANCRAS.

Sikiliza mahojiano ya wasanii hao ambapo msanii Mecras ameanza kwa kueleza sababu za kubadili jina la kundi lao kutoka Payus & Pacras hadi kuwa Wapancras huku msanii Mecras akiweka bayana chimbuko la jina hilo la Wapancras.
Bonyeza HAPA Kusikiliza au Bonyeza Play Hapo Chini


Msanii Payus
Msanii Mecras
Bonyeza Hapa Kujua Zaidi Au wacheck Wapancras 0742 182 836

KARIBU DUKA JIPYA LA JULIE ANGEL BRIDAL COURT UPATA BIDHAA MBALIMBALI

June 28, 2016









Duka Jipya la Julie Angel Bridal Court lililopo barabara 12 jijini Tanga imepatakana na Ofisi za Basi la Raha Leo Jengo Jipya juu ya Ghorofa ambalo halijamaliziwa katika Duka la Dawa na Saloon.
Wana kodisha,Kuuza na Kushona nguo za Wedding Gawn  ya Send Off,Wedding Accessories,Magauni ya Harusi za ain zote nay ale ya Send Off,Heleni,Cheni za Harusi na Bidhaa zote za harusi.
Lakini pia wanakodishya nguo za kipaimara,komunio na nguo za wasimamizi wa harusi.
Wanapatikana kwa simu namba 0658405045, 0712356844 na 0677013130 .
MAJALIWA AMWAKILISHA MAGUFULI MKUTANO WA SADC

MAJALIWA AMWAKILISHA MAGUFULI MKUTANO WA SADC

June 28, 2016


NAM1 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa  Viongozi  Wakuu wa  Nchi  na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm  mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAM2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma (wapili kulia)  kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi  na serikali wa  Jumuiya yaMaendeleo kusini mwa Afrika ( SADC ) kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli Juni 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA RAIS WA COMORO PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

June 28, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
                                     ………………………………………………
 Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusianona ushirikiano wa kihistoria  kati ya Tanzania  na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.
Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya  kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi
Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.RaisAzali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tanozinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii nakusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.
Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa  Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.
 Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka
nchini  JAPAN.
Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.
Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili  ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.

BALOZI SEIF AFUNGUA SEMINA YA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA ZANZIBAR

June 28, 2016



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifungua Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika katika ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na wa Pili kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia ya Rakgas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Kamal Ataya.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbali mbali zilizotolewa kwenye Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Mtaalamu wa utafiti na uchimbaji mafuta na gesi kutoka Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Osama Abdel akityoa mada kwenye semina ya mafuta na gesi ilitotolewa kwa wawakilishi wa Zanzibar.
Haiba ya ndani inavyoonekana ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar ukiwa katika matengenezo makubwa ili utoe huduma za kisasa.

Mrakibu Msaidizi wa Mafunzo { ASP } Juma Makame wa Pili kutoka kulia mwenye shati la drafti akimpatia maelezo Balozi Seif aliyepo kati kati juu ya harakati za kukamilika kwa matengenezo makubwa ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi hapo Kikwajuni Mjini Zanzibar.Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara  ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassan na nyuma ya ASP  Juma Makame ni Msimamizi wa ujenzi kutoka KMKM LCDR Hamad Masoud Khamis.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza akimueleza Balozi Seif hatua zinazofanywa za kuimarisha eneo la nje ya Ukumbi huo.Picha na – OMPR – ZNZ.

RAIS WA ZANZIBA DK.ALI MOHAMED SHEIN AWAAPISHA NAIBU KATIBU WAKUU LEO.

June 28, 2016

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein   akimuapisha Dk.Islam Seif Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo  Dk.Islam Seif Salum  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd,Hassan Abdulla Mitawi  kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Hassan Abdulla Mitawi  baada ya kumuapisha    kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd, Rafii Haji Makame kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Nd, Rafii Haji Makame baada ya kumuapisha   kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimwapisha  Nd, Rafii Haji Makame baada ya kumuapisha   kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Viongozi walioshiriki katika hafla ya kuwapishwa Watendaji katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika hafila iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,(kutoka kushoto) Mhe,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Haji Khamis,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Said Hassan Said na Mshauri wa Rais Utamaduni Mhe,Chimbeni Kheir
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid,(kulia) akifuatiwa na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi mhe,Hamad Rashid Mohamed,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo mhe,Rashid Ali Juma,pamoja na Viongozi wengine akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayuob Mohamed Mahmoud wakiwa katika hafla ya kuwapishwa Watendaji katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo Ikulu Mjini Unguja, 
[Picha na Ikulu.]{28/06/2016.

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

June 28, 2016

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Mwenyekiti waTimu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
 Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi ya kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu yaSimba na wapenzi wa timu ya Yanga Mhe. John Kadutu akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma uliolenga kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati ambapo kamati hiyo inaratibu maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu hizo itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kukusanya madawati yatakayo pelekwa katika Halmashauri zote nchini, kushoto ni Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia Ackson akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Kuahirisha shughuli za Bunge mapema leo.
( Pichazote na Frank Mvungi-Dodoma)