KAIMU KATIBU MKUU UVCCM SHAKA HAMDU SHAKA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHE; ZELOTE STEPHEN ZELOTE

May 05, 2017
RC rukwa 2
Mhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe:Zelote Stephen Zelote wa kwanza kushoto akimpokea kaimu katibu mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipowasili ofisi za Mkoa kuzungumza Mambo mbali mbali ya kimaendelea pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2015.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akizungumza Mambo mbali mbali ya kimaendelea pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2015 pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen Zelote wa kwanza kulia.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe:Zelote Stephen Zelote wa kwanza kushoto akielezea jinsi ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyo tekelezwa katika mkoa wake kwa Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipowasili Mkoani hapo wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoan Rukwa.
Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe:Zelote Stephen Zelotemara baada ya kumaliza
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa NNE Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen Zelote wa nne kushoto pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Chama na Serikali  Mkoa wa Rukwa. (Picha na FAHADI SIRAJI)
SIKU YA WAKUNGA DUNIANI YAFANA DODOMA

SIKU YA WAKUNGA DUNIANI YAFANA DODOMA

May 05, 2017
ZA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza  Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama mkoani Dodoma Daktari Leah Kitundya wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha siku ya Wakunga Duniani ambapo Kitaifa imefanyika mjini Dodoma, katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ZA 1
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Hashina Begun akihutubia wakati wa kilele cha sherehe za Siku ya Wakunga Duniani zilizofanyika kitaoifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Julius K. Nyerere ,Chuo Cha Mipango ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. ZA 3 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  kwenye kilele cha siku ya Wakunga Duniani ambapo Kitaifa imefanyika mjini Dodoma ZA 4
Baadhi ya Wakunga wakirekodi hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha Siku ya Wangunga Duniani iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Julius K. Nyerere mjini Dodoma (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
……………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza halmashauri zote nchini zihakikishe zinajenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa afya hasa maeneo ya vijijini na kipaumbele kitolewe kwa wakunga ambao mara nyingi ndio wanatoa huduma za dharura kwa wanawake wajawazito na watoto.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani sherehe ambazo zimehudhuriwa na Mamia ya wakunga kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Makamu wa Rais amesema kuwa halmashauri zikijenga nyumba karibu na vituo vya kutolewa huduma za afya zitasaidia kupunguza matatizo ya mama na watoto wanaotaka kupata huduma za dharura ikilinganishwa na hali ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi wa afya hasa wakunga wanakaa mbali na maeneo yao ya kazi hivyo utoaji wa huduma za dharura kuwa duni.
Makamu wa Rais amewahimiza Wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ujenzi huo kikamilifu kama walivyoshughulikia matatizo ya madawati katika maeneo yao ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo yake ya kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi nchini.
Kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia wakunga na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto hizo ikiwemo uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa kada hiyo pamoja na kuongeza maradufu vifaa tiba,dawa na vitendanishi ili kuhakikisha wananchi kote nchini wanapata huduma bora za afya.
Amesema mpaka sasa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya nchini ni imefikia asilimia 83 hadi kufikia mwishoni mwa Marchi 2017.
Makamu wa Rais pia amewahimiza wakunga kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili na waache tabia ya kutoa lugha mbaya kwa wanawake wajawazito na wakunga watakaobainika kufanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia ipasavyo utoaji bora za afya kwa wananchi pamoja na kusimamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya kote nchini.
Amesema anaimani kubwa kuwa baada ya Serikali kuiongezea Wizara ya Afya bajeti kutoka bilioni zaidi ya 700 katika mwaka wa fedha za 2016/2017 hadi Trilioni Moja kwa mwaka wa fedha 2017/2018 inaonyesha wazi dhamira ya dhati ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa kiwango hali ya juu nchini ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Kauli mbinu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga mwaka huu ni Wakunga,Akina mama na Familia ni washirika wa Kudumu.(Midwives,Women and Families Partners)

HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA N/WAZIRI MPINA

May 05, 2017


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina anakumbuka siku yake ya kuzaliwa Leo.Heri ya siku ya Kuzaliwa Mhe. Mpina Mungu akupe Maisha Marefu.
LIGI KUU YA VODACOM BARA YANGA KESHO,SIMBA JUMAPILI MOTO KUWAKA

LIGI KUU YA VODACOM BARA YANGA KESHO,SIMBA JUMAPILI MOTO KUWAKA

May 05, 2017
Simba-VS-Yanga-manahodha-bongosoka
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.
Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na  mechi moja.
Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WAZIRI MWIGULU AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA YAKE KUJADILI UTEKELEZAJI WA BAJETI 2017/2018

WAZIRI MWIGULU AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA YAKE KUJADILI UTEKELEZAJI WA BAJETI 2017/2018

May 05, 2017
unnamed
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
 A
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake kabla ya kufungua Kikao Baraza hilo kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka Wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
A 1
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza katika Kikao kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga.
A 2
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake (hawapo pichani) kabla ya kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
A 3
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za Wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. A 4
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka  wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahaitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
A 6
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka  wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TFF, WILDAID WASAINI MAKUBALIANO KUPIGA VITA UJANGILI

TFF, WILDAID WASAINI MAKUBALIANO KUPIGA VITA UJANGILI

May 05, 2017
images

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya kupigania uhai wa maisha ya wanyama wa mbugani ya Wildaid Alhamisi Mei 4, mwaka huu kwa pamoja wamesaini makubaliano ya vita dhidi ya ujangili.
Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam kati ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mwakilishi wa taasisi hiyo, Lily Massa.
Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema kwamba, “Hii ni sehemu nyingine ya TFF kujihusisha na shughuli za kijamii licha ya kuwa na majukumu ya kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu katika kukuza na kuendesha mashindano.”
Malinzi amesema TFF inaendeleza utamaduni wa shughuli mbalimbali za jamii kwani hata kwa Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Tenga enzi za utawala wake akiwa kiongozi mkuu wa mpira wa miguu, alifanya hivyo katika kampeni za kupinga maambukizi mapya ya UKIMWI.
“Wengi mtakumbuka kuwa kulikuwa pia na vita vya kupigania afya za watoto na kupigania uhai wao pia kampeni za amani ambazo mpira wa miguu umetumika kuelimisha,” amesema.
Kwa hatua hii ya sasa, Rais Malinzi amesema kwamba TFF, inaingia makubaliano hayo na kuiteua timu ya taifa ya vijana Tanzania maarufu kama Serengeti Boys kusimama kidete kupinga uwindaji haramu wa wanyama mbugani kwa kuwa ni hazina kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wa Mwakilishi wa WildAid, Lily Massa, alishukuru kuingia kwa makubalino hayo akisema kwamba ndoto zao za kupiga vita uwindaji haramu na ujangili, itafanikiwa.
“Tunashukuru kuingia programu hii na ninaamini Mungu atatusaidia,” amesema Massa ambaye taasisi yake iko karibu kila nchi yenye wanyama wa mbugani.
Katika hatua nyingine, Rais Malinzi aliitakia kila la kheri Serengeti Boys ambayo kwa sasa inajiandaa kuingia Gabon kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Mei 14, mwaka huu ambako Serengeti Boys ambayo iko Kundi B itakuwa Libreville – Mji Mkuu wa Gabon. Timu nyingine za Kundi B ni Mali, Niger na Angola

MUONEKANO WA JIJI LA TANGA ENEO LA BARABARA YA TAIFA ROAD MCHANA HUU

May 05, 2017
 Muonekano wa barabara ya Taifa Road Jijini Tanga leo mchana  inavyoonekana


Muonekano wa barabara ya Taifa Road inayoelekea wilayani Pangani kama inavyoonekena mchana huu
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA TENGERU-SAKINA, ARUSHA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA TENGERU-SAKINA, ARUSHA

May 05, 2017
as1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
as2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
as3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
as4 as5
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
as6

LORI LADONDOKA NA KUFUNGA BARABARA KARIBU NA DARAJA LA WAMI

May 05, 2017

 ABIRIA na Wananchi wakiwa na askari wakiangalia namna lori lilivyoanguka na kuziba barabara ya kuelekea Mto Wami na kusababisha usumbufu kwa abiria waliokuwa wakitumia barabara hiyo kwa safari zao


ABIRIA wakiangalia namna lori lilivyoanguka na kuziba barabara ya kuelekea Mto Wami na kusababisha usumbufu kwa abiria waliokuwa wakitumia barabara hiyo kwa safari zao

 Lori likiwa limeanguka kwenye barabara ya kuelekea mto Wami leo na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaoitumia barabara hiyo

HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA N/WAZIRI MPINA

May 05, 2017
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina anakumbuka siku yake ya kuzaliwa Leo.Heri ya siku ya Kuzaliwa Mhe. Mpina Mungu akupe Maisha Marefu.

DC KASESELA ATOA WIKI MBILI KUFANYIKA MIKUTANO YA HADHARA KATA MLANDEGE

May 05, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Iringa kama Naibu Meya Joseph Lyata na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati wakisikiza hoja za wananchi wa Kata ya mlandege

Na Fredy Mgunda, Iringa

Watendaji wa kata ya mlandege wamepewe wiki mbili kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya kila mitaa ili kupunguza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka viongozi kufanya kazi kwa umakini na kuitisha mikutano ya hadhara kwa wakati ili kupunguza kero zinazowakabili.

"Wananchi wa Kata hii wanakero nyingi ambazo viongozi wa Kata mnaweza kuzitatua sio lazima zinifikie mimi huku,nawaombeni sana viongozi fanyeni kazi la sivyo nitawachukulia hatua mara moja"alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa kata ya mlandege haina changamoto nyingi ili changamoto hizo zinasababishwa na viongozi wa Kata kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa wakati.

Aidha Kasesela alisema kuwa ataendelea kutatua kero zote kwa wananchi kwa kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi na ameletwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa wananchi.

Kero nyingine zilizokuwa hapa Kata ya mlandege zitatatuliwa wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa atazitatuwa kulingana na mipango iliyopo  serikalini.
Kasesela alimuomba mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuzipeleka bungeni baadhi kero ambazo zipo juu ya uwezo wao kama kero ya maji,ardhi na swala Mipangomiji.

Kwa upande wake mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati alisema kuwa ameyapokea na anayapeleka bungeni kuyatatua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi wa kero za wananchi.

"Nimekuja hapa kwenye mkutano hadhara kuzichukua kero hizi ili nizipeleke sehemu husika na mimi nitafanya kazi kwa kujituma ili kuisaidia Manispaa ya Iringa kuwa na maendeleo ya haraka sana"alisema Kabati

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa dr mafwele alisema kuwa amezisikia kero zote na atazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili kuboresha maisha ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
.