WAKULIMA MKOANI IRINGA WATAKIWA KUTUMIA MBOLEA YA YARA INAYOZALISHWA NA KAMPUNI YA YARA TANZANIA

April 16, 2018

Afisa Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya Yara mkoa wa Iringa Dionis Tshonde akitoa maelezo kwa kiasi gani mbolea hiyo inawasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kuvuna mavuno mengi kwenye msimu mmoja
Uongozi wa timu ya Singida United ya mkoani Singida na wachezaji wa timu hiyo nao walifanikiwa kutembelea shamba darasa ambalo wanatumia mbolea ya kampuni ya Yara na kuwataka wakulima wa mkoani Iringa kulima kilimo bora kwa kutumia mbolea ambazo zinazalishwa na kampuni ya Yara iliyopo kulasini jijini Dar es salaam.


Shamba darasa ambalo lipo mkoani Iringa katika kata ya Ruaha manispaa ya Iringa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WAKULIMA wametakiwa kutumia kulima kilimo chenye tija kwa kufuata maelekezo ya wataalamu ili waweze kupata mazao bora.

Hayo yamesemwa na Afisa Kilimo Manispaa ya Iringa Bi.Happines Nnko wakati akizungumza na wakulima wa kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa katika shamba darasa ambalo wakulima wamelima kwa kufuata kanuni na taratibu za kilimo bora na kufanikiwa kustawisha mazao vizuri.

Hapinpines alisema kuwa wakulima wanapoteza nguvu,muda kulima kilimo sikichokuwa na tija kwa kutofuata kanuni za kilimo, mbegu bora na mborea za kupandia na kukuzia.

"Ninawaomba tuwatumie wataalamu wetu ili tuweze kulima kilimo chenye tija.Pia ninawaomba haya mliyoshauriwa na wataalamu kutoka kmpuni ya Mbolea Yara na Seed.co mkayafanyie kazi,lengo tunataka kuona kilimo kikimkwamua Mkulima na si kumdidimiza"

Akitoa Elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa kutumia Mbolea ya Yara Vespa Kwavava,amabae ni Mkulima katika eneo la Ipogolo kata ya Ruaha alisema kuwa hapo awali kabla hajaanza kutrumia Mbolea uzalishaji ulikuwa mdogo ,lakini kwa hivi sasa umeongezeka.

Ninawaomba wakulima wenzangu watumie mbolea na wataalamu ili wawaeze kupiga hatua katika uzalishaji na hatimae kujikwamua kimaisha kupitia kilimo.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Dionis Tshonde alisema kuwa wataendelea kutoa elimu ya kilimo bora kwa kushirikiana na wananachi ili kuhakikisha wanalima kilimo chenye faida kubwa kuliko wanavyofanya sasa wakulima wengi.

“Wananchi wengi wanapenda kulima lakini bado hawafuati taratibu na kanuni za kilimo bora hivyo atahakikisha kupitia kampuni ya Yara wanatoa elimu kwa wakulima ili kuwakomboa katika kilimo wanacholima kwa sasa hadi kufikia kulima kilimo cha kisasa na chenye faida” alisema
Tshonde aliwataka wakulima kutumia mbolea za kampuni ya Yara ambazo kwa sasa ndio imekuwa mkombozi wa wakulima kwa kuzalisha mazao mengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Mbolea za kampuni ya Yara zinavirubisho ambavyo vinasaidia mazoa kukuwa na kuzalisha mazao mengi ambayo yanakuwa faida kwa wakulima”

Tshonde alisema kuwa ukitumia mbolea ya kampuni Yara utapata faida kubwa kwa kuwa ukilima hekali moja unakuwa na uhakika wa kuvuna kati ya gunia 35 hadi 40 endapo mkulima atazingatia kanuni na taratibu za kilimo che tija.

SERIKALI KULINDA THAMANI YA SHILINGI KWA KUONGEZA THAMANI YA BIDHAA ZA NDANI

April 16, 2018


Na: WFM

Serikali imeeleza kuwa inalinda thamani ya Shilingi kwa kudhibiti mfumuko wa bei ya huduma na bidhaa, kuhamasisha usafirishaji na uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani nje ya nchi kupitia program ya “Export Credit Guarantee Scheme” na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za Kigeni.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Devotha Mathew Minja aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kulinda thamani ya Shilingi kwa kuwa wapo wamiliki wa majengo ambao wanapangisha majengo kwa kutumia fedha za kigeni kama vile Dola ya Kimarekani badala ya fedha ya Kitanzania hivyo kusababisha kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa matumizi ya fedha za kigeni sambamba na Shilingi ya Tanzania hapa nchini yanasimamiwa na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 (The Foreign Exchange Act, 1992), Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya Mwaka 2006 na Tamko la Serikali la mwaka 2007 kuhusu matumizi ya fedha za kigeni kulipia bidhaa na huduma katika soko la ndani.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa mwezi Desemba 2017, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alitoa tamko kwa umma kuwa kuanzia Januari Mosi, 2018 bei zote hapa nchini zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania zikijumuisha kodi ya nyumba za kuishi na ofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei ya vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

“Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, ambapo zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, visa kwa wageni na gharama za viwanja vya ndege na hoteli, hata hivyo wageni hao wanapaswa kutambuliwa kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa Kampuni”. Alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha aliongeza kuwa viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka bei hizo katika sarafu vinatakiwa kuwekwa wazi na visizidi vile vya soko, vilevile ni benki na maduka ya fedha za kigeni pekee ndiyo yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

Katika maswali ya nyongeza ya Mbunge huyo alitaka kujua sababu zinazofanya baadhi ya Taasisi kuendelea kupata na kutoa huduma kwa Dola, pia alihoji Serikali itapitia lini upya Sheria zake ili kuwa na sheria itakayozuia matumizi ya fedha za Kigeni kama ilivyo kwa nchi ya Afrika Kusini.

Dkt. Kijaji alisema kwa kuwa wajibu wa marekebisho na kupitisha Sheria ni wa Bunge hivyo basi, iwapo sheria iliyopo ina upungufu ni vema kukafanyika maboresho kupitia Bunge.

“Ikumbukwe kuwa katika misingi ya Uchumi mambo yanayosababisha kushuka au kudorora kwa thamani ya fedha yeyote duniani ni pamoja na Nakisi ya Urari wa Biashara ambapo kwa Serikali ya Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini” alisema Dkt. Kijaji.

Alibainisha kuwa Mfumuko wa bei na tofauti ya Msimu huchangia kushuka kwa thamani ya fedha ambapo Tanzania inaendelea kudhibiti mfumuko huo na Serikali tayari imefunga zaidi ya maduka 92 ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yameshindwa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kudhibiti maduka hayo kuwa kichaka cha kusafirisha fedha za Tanzania isivyo halali mambo ambayo yanaonesha juhudi za Serikali kuimarisha kwa kiwango kikubwa thamani ya shilingi.

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI MSAADA WA VITANDA KWA KITUO CHA AFYA

April 16, 2018
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria katika hafla ya kukabidhi vifaa na gari la kubebea wagonjwa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya katika jimbo hilo
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi vitanda kwa ajili ya kituo hicho
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kituo hicho

NA FREDY MGUNDA, MUFINDI


MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ametoa msaada wa vitanda kumi kwa kituo cha afya cha Ihongole kilichokuwa kinakabiliwa na upungufu wa vitanda katika wodi ya wazazi.

Akizungumza wakati kukabidhi vitanda hivyo sambamba na kukabidhi gari ndogo ya kubebea wagonjwa iliyotolewa na serikali, Chumi alisema kuwa msaada huo wa vitanda utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto katika kituo hicho cha afya ambacho kinachohudumia wakazi zaidi ya 20000 wa jimbo la Mafinga mjini.

Alisema kuwa ushirikiano katika kuondoa changamoto na kuchukulia mapungufu ndio njia pekee ya kuendelea kuinyanyua Mafinga hasa katika sekta ya afya ambayo imekuwa ikikabiliana na changomoto nyingi.

Chumi alisema kuwa msaada wa vitanda vimetolewa na mmoja wa wahisani wanaolisaidia jimbo la Mafinga kuondokana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya ambayo imekuwa na ikikabiliwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu bora.

Alisema changamoto za sekta ya afya katika jimbo hilo na wilaya ya Mufindi kwa ujumla zitakashughulikiwa kupitia serikali na wadau wake mbalimbali wanaotakiwa kujitokeza kuboresha huduma zake

Akizungumzia Gari hiyo ambayo imetolewa na Serikali Chumi alisema kuwa itatumika kubeba wagonjwa ambao watalazimika kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mafinga ambapo awali ilikuwa vigumu kwa wagonjwa pindi wakizidiwa kwenda kutibiwa.

Mbali na msaada huo, mbunge huyo ambaye mbali na ahadi mbalimbali kwa wapiga kura wake, aliahidi kuboresha huduma za afya katika jimbo hilo amekwishatoa msaada vitanda, magodoro, viti vya kubeba wagonjwa na vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Mafinga.

Akipokea na kushukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa kituo cha Ihongole, Bernad Makupa alisema msaada huo wa vitanda na gari ya kubebea wagonjwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwahudumia wananchi katika vijiji mbalimbali vinavyopata huduma katika kituo hicho

Kwa niaba ya halmashauri ya Mafinga Mjini, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Charles Makoga alimshukuru Chumi kwa ushiriki wake katika kuchangia maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo kabla na baada ya kuingia madarakani na akamuomba endelee na moyo huo.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

April 16, 2018




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA KAMANDA WA MATUKIO BLOG 0715264202








Mjema akimpa pole mmoja wa akina mama aliyevuka katika daraja la hilo la muda linalohatarisha usalama wa wananchi wanaopita hapo.



Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.








Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.



Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi

maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.



Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.



Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake.

Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya watu.



Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo

la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.



Diwani wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.



Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.



Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa

serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.



Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha

maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.



Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja

la Ulongoni A.








Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja la Ulongoni A.



Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A

SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI MATUKIO YA UVUVI HARAMU NCHINI

April 16, 2018
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katikati akipanda moja kati ya mikoko ya miche 140,000 iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation
katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga kulia ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katikati akipanda moja kati ya mikoko ya miche 140,000 iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation
katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga kulia ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wa tatu kutoka kulia akiwa na Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia kushoto wakitembela kwenye ufukwe wa bahari ya hindi mara baada ya kupanda moja kati ya mikoko iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Foundation katika mikoa inazungukwa na bahari ya hindi ili kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi Jijini Tanga.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba katika akizungumza mara baada ya kupanda miti hiyo ya mikoko kushoto ni Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba kulia akimsikiliza kwa umakini Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia katikati aliyekuwa akieleza dhamira yao ya kusaidia upandaji wa miti hiyo ya mikoko
Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakipiga selfie na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji wa miti ya mikoko
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja na WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba mara baada ya kumalzika kwa zoezi la upandaji wa miti ya mikoko


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema serikali imefanikiwa kudhibiti matukio ya uvuvi haramu kwa zaidi ya asilimia 80 katika maeneo ya bahari na maziwa baada ya kuimarisha doria na ukaguzi wa samaki wanaovuliwa.

Aliyasema hayo wakati wa upandaji wa mikoko katika Pwani ya Bahari ya Hindi ambayo ilipandwa eneo la Mwambani Jijini Tanga chini ya Udhamini wa Mfuko wa Vodacom (Vodacom Faundation).

Alisema kuimarika kwa doria hizo kumesaidia wananachi kuwa na uelewa mpana kuhusu madhara ya uvuvi haramu na hivyo kuanz kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo ikiwemo ulinzi wa mazingira ya bahari ya hindi na rasilimali zake.

Waziri huyo alisema pamoja na jitihada za wizara katika kudhibiti fukwe za bahari zinasiendelee kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi lakini bado kuna maeneo mengi ambayo yanahitaji kuhifadhiwa kwa kupandwa miti ya mikoko.

Pamoja na hayo Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Vodacom Foundation kwa kuja na kampeni ya upandaji wa mikoko ili kuhifadhi mazingira ya bahari kwa kile alichosema kuwa kutasaidia kuboresha mazingira hayo.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Vodacom Foundation Rosalynn Mworia alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na chama cha skauti Tanzania waliamua kuja na kampeni hiyo upandaji wa mikoko ili kuhifadhi mazingira ya Fukwe.

Alisema kwamba kwa kuanzia kampeni hiyo wameanzia kwa mkoa wa Tanga na wanatarajia kuipeleka nchi nzima ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

MPINA AWATAKA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA PUNDA KUONGEZA BEI

April 16, 2018


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akikagua kiwanda cha kuchinja Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni leo. (Picha na Jumanne Mnyau)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akipokea maelezo ya usindikaji wa nyama Punda kutoka kwa mfanyakazi wa wa kiwanda cha kuchinja Punda cha Hua Cheng Limited Elizabeth Peter.(Picha na Jumanne Mnyau)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(mwenye miwani) akitembezwa katika kiwanda cha  kuchinja  Punda  cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma  alichokifungua  hivi karibuni na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho bwana Xun Long Go .(Picha na Jumanne Mnyau)
Na John Mapepele, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya kuchinja Punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao badala ya shilingi laki mbili ya sasa kwa punda mmoja ili kudhibiti utoroshaji wa mifugo nje ya nchi ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya mifugo elfu kumi inatoroshwa mipakani kwa siku kwenda nje ya nchi inakonunuliwa kwa bei ya juu.

Akizungumza leo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Kiwanda cha Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni, Waziri Mpina alisema bei hiyo haiendani na gharama halisi ya ufugaji wa Punda hali inayowafanya wafugaji kuwatorosha mifugo na kulikosesha taifa mapato makubwa.

Alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa inachukua kiasi cha miaka miwili ambapo gharama zake za ufugaji zinakuwa juu ukilinganisha na bei ya shilingi laki mbili anayouzwa kwa wenye viwanda vya punda nchini.

Aidha alisema kumekuwa na utoroshaji mkubwa wa mifugo wanaokadiriwa kufikia takribani 1,614,035 kwa mwaka unaofanyika kwenye mipaka ya nchi yetu ambapo takribani shilingi bilioni 32.28 zinapotea kama ushuru na takribani shilingi bilioni 24.21 zinapotea kutokana na kodi ya mapato ambayo ingelipwa kwa nyama ambayo ingeuzwa hapo nchini.

Aidha Mpina ameunda tume ya wataalam kutoka Wizarani kwa ajili ya kuja kufanya tathmini kama kiwanda hicho kimetimiza masharti yote yaliyotolewa na Serikali baada ya kukifungua Februari mosi mwaka huu ambapo alisema ikibainika kuwa kiwanda hakijakidhi masharti yaliyotolewa na Serikali kitachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kukifungia kufanya kazi zake.

Aliyataja baadhi ya masharti yaliyotolewa na Serikali wakati wa kukifunga kiwanda hicho Julai 2017 kuwa ni pamoja na kuwa na ranchi za punda, kuboresha kosaafu za Punda nchini, kuunda na kuingia mikataba na vikundi vya wafugaji wa Punda na kuwa na Punda wasiopungua mia tatu katika eneo la kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa ili kuwa kuhakikisha kwamba mifugo wanaangaliwa kwa wiki mbili kabla ya kuchinjwa ili wawe katika ubora wa kimataifa.

Waziri Mpina alisema uwekezaji wa aina hiyo wa kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ni moja ya vipaumbele vya wizara yake kwa sasa ili kuchochea kwa kasi kufanikisha azma ya Tanzania ya viwanda.

Aidha aliwahakikishia wawekezaji wa kiwanda hicho kuwa endapo watakuwa wamekamilisha masharti atawapa kibali cha kudumu ambapo pia atawaongezea idadi ya kuchinja Punda kutoka punda 20 wa sasa ili vijana wengi wapate ajira na kiwanda kiweze kuchangia zaidi katika mapato ya Serikali.

Mpina aliwahimiza wawekezaji hao kuhakikisha wanawasaidia wafugaji katika kuongeza uzalishaji, kupambana na maradhi, upatikanaji wa maji na malisho kwa mifugo.

Alisema idadi ya punda waliopo nchini ni 520,000 tu hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuongeza uzalishaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Xun Long Go alimshukuru Waziri Mpina kwa kufungua kiwanda hicho ambapo amesema hadi sasa kiwanda kimezalisha na kuuza tani 224 za nyama ya Punda kwenda nchini China na Vietinam ambapo pia tani 52 za ngozi ya Punda ilizalishwa na kuuzwa kuanzi mwezi Februari, 2018.

Alisema kiwanda hicho kimeajiri watanzania 55 ambapo hadi sasa kina punda 88 katika maeneo ya Chalinze na Zuzu mkoani Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Lucia Chacha aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni mbinu za kuwasaidia wafugaji kwa kuwapatia elimu bora zaidi ya ufufaji wa punda ili waweze kuwazalisha kwa wingi zaidi kuliko ilivyo sasa

Hivi sasa Tanzania ina viwanda viwili tu vya kuchinja na kuuza nyama ya punda ambavyo ni kiwanda cha Punda cha Huacheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma na Kiwanda cha Fang Hua kilichopo Shinyanga ambavyo vyote vimepewa kibali cha kuchinja Punda 20 kwa siku kila kimoja.