MAMIA WAFUNGULIWA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI MWANZA

September 28, 2017
 Na George Binagi-GB Pazzo
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo waumini wa dini mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na kanisa la kanisa EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kukola.

Jana mamia ya wananchi walijitokeza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na kukutana na mlipuko mkubwa wa injili kutoka kwa watumishi wa Mungu akiwemo mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani chini ya huduma ya MORE International Ministry.

Aidha waimbaji Ambwene Mwasongwe, Mbilikimo Watatu, Samwel Lusekelo, Joseph Rwiza, Sam D, Havillah Gospel Singers na wengine wengi wameendelea kukonga nyoyo za wahudhuriaji kwenye mkutano huo.

“Maandalizi ya mkutano huu ni ya kuvutia, tuna majukwaa matatu makubwa, vyombo vya muziki wa injili vizuri na pia tunatoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo kwa wanaohudhuria mkutano huu”. Alisema Mchungaji Dkt.Kulola na kuwahimiza watu wote kufika kwenye mkutano huo ili wakutane na nguvu ya Mungu na kufunguliwa.


Mkutano huo ulianza juzi jumatano Septemba 27 na utafikia tamati jumapili Oktoba Mosi, 2017 katika Uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ambapo mamia ya wananchi waliokuwa wakiteswa na majini pamoja na magonjwa mbalimbali wanazidi kufunguliwa, na leo huduma ya maombezi inaanza mapema majira ya saa nne asubuhi na mkutano utaanza saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni.
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani akihubiri kwenye mkutano huo
Watumishi mbalimbali wakiendelea kutoa huduma ya maombezi jana ambapo zaidi ya 20 walifunguliwa mapepo huku wengine wengi wakiponywa magonjwa mbalimbali
Mwimbaji wa muziki wa injili Ambwene Mwasongwe kutoka Dar es salaam akihudumu kwenye mkutano ho
Baada ya ibada, kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kushirikiana na wachungaji kutoka Marekani lilitoa zawadi kwa wananchi
Tazama picha zaidi HAPA

WATANZANIA WANG'ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

September 28, 2017

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano hilo lililofanyika jana nchini Uganda.


 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ambae alishinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.  
Keki ikikatwa katika hafla hiyo

Na Mwandishi Wetu

Mwandishi wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ameshinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.

Kitabu alikuwa anachuana na waandishi kutoka nchi za Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Shindano hilo lilifanyika jana katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyoko nje kidogo ya jiji la Kampala.

"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga

September 28, 2017
Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe. Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO. Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. “Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi. Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema. Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

MBUNGE AZZA HILAL AWAPIGA JEKI WANAFUNZI WENYE ULEMAVU SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA SHINYANGA

September 28, 2017
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde
***

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO KUHUSU MAUDHUI NA KANUNI MPYA ZA HUDUMA YA UTANGAZAJI TANZANIA (TV, RADIO, BLOG, ONLINE TV

September 28, 2017

 Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers, Online Media) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

Kanuni  ziizojadiliwa ni maudhui yanayorushwa na vituo vya uatangazaji  vya Redio na Televisheni n maudhui mitandaoni (Online Content) Jumla ya vyombo vya habari 76 vilishiriki kwenye kikao hicho.

Wadau wamepewa wiki moja kuwasiliasha maoni yao kwenye kamati ya mashauriano ili yajadiliwe na kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresh kanuni. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wamiliki wa Wmiliki na wafanyakazi wa Vituo vya Televisheni na Radio wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza  kuhusu mambo mbalimbali waliyokubaliana katika kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

 Wadaui wa habari wakiwa katika kikao hicho



 Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group,  Nathan Rwehabura akichangia mada wakati wa kikao hicho, ambapo pia alilalamikia ada kubwa inayotozwa kwa mwaka wamiliki wa vituo vya tv ambayo ni dola 25,000 swa na sh/ mil/ 60

 Dina Chaali wa Chanel Ten akitafakari jambo katika kikao hicho
 Mkurugenzi Mstaafu wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze akifafanua jambo katika kiao hicho

 Wakili wa Jamii Forum Benedict akichangia mada wakati wa kikao hicho

  Mkuu wa Vipindi wa EAST AFRICA radio, Nasser Kingu akichangia mada wakati wa kikao




PROF. MAGHEMBE AONGOZA MAADHIMISHO YA 87 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

September 28, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata keki ya maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik (katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho hayo.

Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Muhimbili Yazindua Mwongozo wa Kuwahudumia Watoto Wachanga

September 28, 2017
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.

Muongozo huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo Afrika Kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata sehemu ambazo hakuna watalaam.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .

‘’ Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa hapa ni takribani 10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta mabadiliko makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.

Pia ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto mwenye vimelea vya bakteria.

Akiwasilisha mada kuhusu muongozo huo , Daktari wa watoto , Jullieth Cosmas ametaja sababu zinazochangia watoto wachanga kulazwa Hospitalini kuwa ni mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) mtoto kushindwa kupumua vizuri pindi anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia wakapi alipozaliwa na mtoto kuumia wakati akizaliwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
 Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
  Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.