KONGAMANO LA MAADILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

March 20, 2017
 Naibu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano la maadili litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa kuanzia saa nne asubuhi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inatarajia kufanya kongamano  linalolenga maadili kwa Taifa nchini.

Kongamano hilo litafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa wizara hiyo,  Anastazia Wambura amesema ni wajibu  kwa kila mwanajamii kuthamini, kuenzi na kuendeleza maadili mema, mila na desturi zinazofaa.

“Serikali hususani wizara inajukumu la kutoa muelekeo na usimamizi kuhakikisha Taifa linaenzi na kuimarisha utambulisho wake na kujenga utamaduni huru na sio huria” alisemaWambura.

Aidha Wambura alisema kuna fursa ya kubaini, kuenzi na kukuza, kuhifadhi  na kurithisha utamaduni na sanaa vyenye kuzingatia na kuimarisha maadili, mila na desturi kwa kuleta maendeleo.

“Wananchi wamekuwa  wanaendelea kujihusisha  na shughuli mbalimbali za Kifani, Sanaa na utamaduni ikiwemo ngoma za asili, filamu, muziki, jando, unyago, matambiko, Sherehe na maadhimisho mbalimbali” alisemaWambura.

Ameongeza kuwa shughuli hizo ni halali ilimradi zifanywe  kwa kuzingatia sheria na kanuni na msingi wa asili yake, kwa maana kwamba kama jambo ni la faragha na usiri libaki kwenye uhalisia wake na kuhusisha rika jinsia na asili yake.


RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO-UBUNGO INTERCHANGE

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO-UBUNGO INTERCHANGE

March 20, 2017
BCU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
BC
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuzindua mitambo na magari yatakayotumika katika ujenzi wa makutano ya barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange) jijini Dar es Salaam.
BC 1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
BV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVVVVVVV
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwapungia wananchi mkono wakati wakielekea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa makutano ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi  wa ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BNU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BNUUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiwa ndani ya moja ya basi la DART wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
BVUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
VUKU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
NUUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiagana na wananchi wa Kivukoni hawapo pichani kabla ya kupanda Basi la Mwendokasi (DART) kuelekea Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi Mradi wa Makutano ya barabara za juu za Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVMM
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
VCC
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-Maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
BVN
Picha namba 19. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ndani ya basi la Mwendokasi wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam
BCC
 Baadhi ya Wananchi wakifatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam-PICHA NA IKULU
KUUNDWA KWA KAMATI YA KUCHUNGUZA SUALA LA KILICHOTOKEA CLOUDS MEDIA

KUUNDWA KWA KAMATI YA KUCHUNGUZA SUALA LA KILICHOTOKEA CLOUDS MEDIA

March 20, 2017
CZZZ
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano kuchunguza suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi pamoja na Ijumaa usiku.
Kamati hiyo imeundwa baada ya Waziri Nape kufanya ziara Clouds Media leo Jumatatu 20/03/2017 na kuzungumza na uongozi wa Clouds Media kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea ofisi hizo siku ya Ijumaa usiku akiwa na askari wenye silaha.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Dkt. Hassan Abbas Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Deodatusi Balile Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Ndg. Jesse Kwayu Mhariri Mtendaji Gazeti la Nipashe, Ndg. Mengida Johannes kutoka Wapo Redio pamoja Ndg. Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Baada ya kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kutoka pande zote mbili Wizara itasema hatua itakazochukua.  

Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

TANGA UWASA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA.

March 20, 2017
 Mtaalamu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Ramadhani Nyambuka akisistiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma kwa mteja wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Machi 22 mwaka huu
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo


 Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga( Tanga Uwasa) Ruluani Luambo akisistiza jambo wakati wa semina hiyo
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo
 Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Joachim Kapembe akiuliza swali kwenye semina hiyo kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo

 Waandishi wa Habari Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbali mbali

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu wiki ya kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 hadi Machi 22 mwaka huu kulia kwake ni Meneja Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka hiyo,Haika Ndalama

SOKO LA MBAO LIMESHUKA WILAYANI MUFINDI

March 20, 2017


 Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na
Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa
 Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi waliohudhulia mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.

Na Fredy Mgunda,Mufindi

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya nyingime.
“Ukienda mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara
Aidha wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa  kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na nguzo.
Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.
"Tunawaomba TRA mkatoe elimu kwa mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa  chini akuulizie nguzo 5 alafu awe na lisiti ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima hawa Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio kampuni" alisema Kenyatta

Akijibu hoja hiyo meneja msaidizi WA TRA mkoa WA iringa Mustapha Mkilamwenye alisema Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka WA uelimishaji.



Pia Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara hao kupata kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo check point.



"Ombi lenu tumelipokea hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka TRA mkoa au wilayani kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia tutatoa elimu ya matumizi ya mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti yako kwa wafanyabiashara" alisema



Kwa upande wake Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua kuwakutanisha wafanyabiashara na TRA kupata ufafanuzi WA kuombwa ushuru check point kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara hao Kuwa magari yako wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku tatu wakiombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.



"Mkutano huku ni mahususi kwa wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini mnakamatwa check point na mkiobwa ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio adui kwa sababu mufindi ndio chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA mbao" alisema Chumi



Meneja wa TRA wilayani ya Mufindi Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli tuhuma hizo na lawama tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za wafanyabiashara na kutatua matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge amekututanisha na tumewapa uelewa na sisi kama TRA tumewaambia mini cha kufanya kuondoa huo usumbufu"

Bi.Emmanuela Mtatifikolo Kaganda achukua fomu kugombea ubunge wa Bunge la Afrika mashariki

March 20, 2017

Bi.Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, mmoja wa wagombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki akikabidhiwa fomu na  Bw. Said Bakari wa  Idara ya Uhusiano wa kimataifa katika makao makuu ya CCM mtaa wa  Lumbumba jijini Dar es salaam.
Bi. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, mmoja wa wagombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki akitoka nje baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea nafasi hiyo makao makuu ya CCM mtaa wa  Lumbumba jijini Dar es salaam. Bi Kaganda alifika hapo akiwa peke yake na bila mbwembwe akiwa na imani kwamba dhamira yake ya kusimamia na kutetea maslahi ya kina mama na watoto katika jamii ni agenda yake itayomsimamia katika kinyang'anyiro hicho.