DAVIS MOSHA AKUTANA NA WASANII WA MOSHI

September 24, 2015

Mh Davis Mosha akiwa na Mwenyekiti wa KDFAA Ndugu Msasu. 
Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya ccm Mh. Davis Mosha Amekutana na wasanii wa Filamu, Maigizo ya Jukwaani, Sarakasi na Muziki wa Mjini moshi. Wasanii hao wakiongozwa na Chama cha Wigizaji na wacheza filam Kilimanjaro (KDFAA)
Wasanii wakimsikiliza Mh. Davis Mosha wakati akizungumza nao Leo jioni.
Wasanii hao walioomba Mkutano na Mh. Davis Mosha leo katika ukumbi wa ccm Mkoa walipata fursa ya kuzungumza Changamoto zinazowakabili na Malengo yao kama wasanii wa Moshi na Mkoa Kilimanjaro. Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ukumbu huo mmoja wa Wasanii wa Muziki Ndugu Samwel Stephen aliweza kumuomba Mh. Davis Mosha awasaidie kupata studio ya kisasa na kuwapa wigo mpana wa kazi zao za muziki kuweza kupigwa katika Radio.
Mh. Davis Mosha akijibu hilo aliwahakikishia Kujenga Studio ya Kisasa itakayoanza kufanya kazi mapema Mwezi ujao chini ya Kampuni yake ya African Swahili Media sambamba na Kufungua kituo cha Redio na Tv.
Wasanii wa Filamu waliomba kuweza kusaidiwa kurekodi Tamthilia ambayo itaweza kurushwa katika Tv na waweze kujitangaza na kujiajiri kupitia sanaa hiyo lakini pia hawakusita kutoa kilio chao juu ya Wizi wa kazi zao unaofanywa na wasambazaji pamoja na Wasambazaji kutoka Dar es Salaam kuwanyonya na kusababisha kazi zao za Film kubaki nyumbani badala ya kwenda Sokoni. Pia waliweza kutoa malalamiko yao juu ya uongozi uliokuwepo madarakani katika ngazi ya ubunge na Udiwani kuwaahidi maramara ahadi ambazo hazitekelezeki.
Mh Davis Mosha akifafanua Jambo katika Mkutano na Wasanii Leo
Bwana Mosha aliweza kuwahakikishia Soko la uhakika la filam zao na pia ulinzi wa kazi zao kupitia vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya haki miliki na pia kuweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao. Na pia aligusia suala la wasanii wa Ngoma za asili juu ya kuhakikisha anaweka kituo cha sanaa na utalii ili kuweza kuwakutanisha wageni wanaokuja kupanda mlima na kufanya ni kituo cha kubuudika kupitia ngoma za asili na sehemu ya kujifunzi aTamaduni za Makabila mbalimbali ya Tanzania. LAkini pia aliwaasa wasanii kutumia sanaa yao kutoa elimu ya uchaguzi juu ya wananchi kutumia haki yao ya msingi katika kuchagua na wasifanye makosa watumie Mitaji yao ya Vitambulisho vya kupigia kura kuhakikisha wanachagua Kiongozi atakayeenda kufanya kazi na si mwanasiasa.


Mwenyekiti wa KDFAA akitoa shukrani zake kw Mh. Davis Mosha kwa Kukubali kuja kuwasikiliza. 
Akifunga Mkutano huo wa wasanii, Mwenyekiti wa Chama cha waigizaji na Filamu Ndugu Msasu alitoa shukrani za Dhati kwa Mh. Davis Mosha huku akimfananisha na Mkombozi ambaye amekuja kuwakomboa kutokana na Viongozi wengi kuwadharau wasaniii na kupelekea Sanaa ya Moshi kuzidi kushuka. Alitumia nafasi hiyo kuwaasa wasanii kutochezea nafasi waliyopata ambayo Mh. Davis Mosha ameonesha nia ya dhati ya kuweza kuwakomboa kupitia sanaa yao na wao basi waoneshe hitaji lao kwake kwa kuhakikisha wanafanya kazi nzuri katika sanaa

MO AMPIKU DANGOTE MFANYABISHARA BORA AFRIKA

MO AMPIKU DANGOTE MFANYABISHARA BORA AFRIKA

September 24, 2015
MO dewji
Vinara wa biashara Afrika walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika picha ya pamoja. Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa, Helen Hai na Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika hoteli ya Four Seasons Hotel mjini New York.(Picha na African Business).
Na Mwandishi wetu, New York
MTANZANIA Bilionea Mohamed Dewji amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015).
Dewji maarufu kama Mo alikabidhiwa tuzo hizo usiku wa kuamkia jana mjini New York.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Tuzo hizo zimeandaliwa na jarida la African Business .
Pia katika tuzo hizo taasisi kadhaa zinazofanya vyema bara la Afrika zilitambulika. Taasisi hizo ni pamoja na kiwanda cha sementi cha Dangote , Guaranty Trust Bank, Abellon Clean Energy, Nigerian Stock Exchange na taasisi ya bima kwa masoko yanayochipukia ya BIMA.
Akielezwa wasifu wake katika hafla hiyo, Mo ameelezwa kama mfanyabiashara aliyefanikiwa kutokana na kuongeza kipato na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprise toka aitwae kutoka kwa baba yake.
Akiwa mtendaji wa kampuni hiyo, akiwa katika miaka ya 40 amefanya mabadiliko makubwa katika makampuni mbalimbali ya umma yaliyoshindwa kujiendesha katika sekta ya kilimo, viwanda na maeneo ya makazi na viwanda.
Uongozi wake uliwezesha kampuni hiyo ya MeTL kufanya makubwa kiasi cha kumfanya aingie katika jarida la Forbes la matajiri wa Afrika.
Majaji waliompa tuzo kwa mwaka huu walisema kwamba uongozi wake umewezesha biashara katika kampuni hiyo kuchupa kutoka dola za Marekani milioni 30 hadi bilioni 3.
Akipokea tuzo hizo Dewji alisema kwamba tuzo hiyo ni ishara muhimu kwa waafrika wote na uwakilishi wa uhakika wa vijana katika masuala ya ujasirimali.
DSC_0310
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji.
Tuzo ya Biashara ya Mwaka ilienda kwa kiwanda cha saruji cha Dangote kinachoongozwa na bilionea wa Afrika, Aliko Dangote.
Kiwanda hiki kilichopo Nigeria kimejipanga kusambaza uzalishaji katika nchi nyingine za Afrika, hatua ambayo imeifanya tuzo hiyo kuwa ya kwao.
Akipokea tuzo hiyo Aliko alisema amefurahishwa sana na tuzo hiyo ya thamani kubwa na kwamba imetolewa wakati ambapo kiwanda hicho kinatanua shughuli zake kuhakikisha ukombozi wa uchumi kwa nchi za Afrika unafanyika kwa dhati.
“Tunaamini katika Afrika. Tunaamini kwamba katika kuhakikisha kuna uwekezaji mkubwa wa miundombinu Afrika itaweza kusonga mbele katika uchumi wake”.
Daphne Mashile Nkosi, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya manganisi ya Kalagadi ya Afrika Kusini alipokea tuzo mwanamke bora katika biashara. Majaji walimpa tuzo hiyo kwa kuwa ameonesha mafanikio makubwa katika sekta ambayo kwa kawaida huendeshwa na wanaume.
Mdada huyo anatambulika kwa kuwezesha kupatikana kwa ajira 30,000 huko Northern Cape, na ni muasisi wa mgodi wa aina yake katika kipindi cha miaka 30.
Mfanyabiashara wa Zimbabwe, mjasiriamali, anayependa kusaidia watu wenye mahitaji Strive Masiyiwa alipata tuzo ya mafanikio katika maisha.
CPoF_XCWcAAyCO6
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipokea tuzo yake.
Strive ambaye ni mmoja wa waanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji kwa kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya simu Econet Wireless amepewa tuzo hiyo kwa mafanikio yake na pia kwa misaada mingi aliyotoa kwa vijana.
Masiyiwa ametumia utajiri wake kusomesha vijana zaidi ya laki moja wa Afrika katika kipindi cha miaka 20.
“Ni heshima kuu kupata nafasi ya kuthaminiwa na jarida lako, Ni heshima kuwa miongoni mwa marafiki… tafadhali endelezeni kazi hii njema,” alisema akizungumza kwa njia ya video.
Tuzo ya mfanyabiashara wa Mfano imeenda kwa Helen Hai, Mtendaji mkuu wa Made in Africa Initiative.
Tuzo hii kwa kawaida hutolewa kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuboresha hali ya ufanyaji biashara barani Afrika.
Helen ambaye ana asili ya China amewezesha mabadiliko makubwa katika biashara ya viatu ya Ethiopia baada ya kuanzisha kiwanda cha viatu cha Huajian Oktoba 2011 baada ya kuwa na mkutano na rais wa nchi hiyo Meles Zenawi mwaka huo huo.
Imeelezwa kuwa kiwanda hicho mara baada ya kuanzisha katika kipindi cha miezi sita tu waliweza kuongeza pato la mauzo ya nje ya nchi hiyo kwa mara mbili na katika kipindi cha miaka miwili kiliajiri waethiopia 4000.
Sasa hivi mdada huyo amefungua kiwanda cha nguo nchini Rwanda.
“Sekta binafsi haikuja Afrika kutoa msaada, tumekuja afrika kufanyabiashara. KLakini katika biashara tunatekeleza maelengo ya maendeleo. Nina imani kubwa na Afrika, naamini kupitia simulizi za mafanikio tunashawishi wengine kujiamini kutwaa uongozi na kuliwezesha bara hili kutambua fursa zake,” alisema Helen.
Guaranty Trust Bank, iliwashinda wengine kadhaa waliotajwa na kushinda tuzo ya utawala bora wakati Abellon Clean Energy ilipata tuzio ya ubinifu wakati Nigerian Stock Exchange ilipata tuzo ya urejeshaji kwa jamii faida ikiwa ni huduma bora za jamii.
Akizungumzia tuzo hizo ambazo ni za sab, Omar Ben Yedder alisema hafla hiyo imwezeshwa na Zenith Bank, GTBank, Agility na Cofina .
Washindi wa 2015
AFRICAN BUSINESS OF THE YEAR
-Dangote, Nigeria
BUSINESS LEADER OF THE YEAR
-Mohammed Dewji, CEO, Mohammed Enterprise, Tanzania
MOST OUTSTANDING WOMAN IN BUSINESS
-Daphne Mashile Nkosi, Executive Chairperson, Kalagadi Manganese, South Africa
AWARD FOR GOOD CORPORATE GOVERNANCE
-Guaranty Trust Bank, Nigeria
AWARD FOR BEST CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY
-The Nigerian Stock Exchange, Nigeria
AWARD FOR INNOVATION
-Abellon Clean Energy, Ghana
INSURANCE COMPANY & INITIATIVE OF THE YEAR
-BIMA ( bimamobile.com )
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
-Strive Masiyiwa
AFRICAN BUSINESS ICON
-Helen Hai
SWALA YA EID EL HAJJ KITAIFA YAFANYIKA MKOKOTONI

SWALA YA EID EL HAJJ KITAIFA YAFANYIKA MKOKOTONI

September 24, 2015


1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A,palipofanyika Swala ya EID El Hajj iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Septemba 24, 2015.
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A,palipofanyika Swala ya EID El Hajj iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akijumuika na Viongozi mbali mbali na Waislamu  katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A,palipofanyika Swala ya Eid El Hajj iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi.
4
Viongozi mbali mbali na Waislamu  wakiwa katika Swala ya  Eid El Hajj katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A, iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi.
5
Akina mama wa Kijiji cha Mkokotoni na Vijiji Jirani walijumuika katika Swala ya  Eid El Hajj katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A, iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi.
6
Akina mama wakiwa katika kiwanja cha mpira  Kijiji cha Mkokotoni wakisikiliza Hotuba ya  Swala ya  Eid El Hajj iliyotolewa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi,baada ya kumalizika kwa ibada ya swala iliyoswaliwa leo kijijini hapo ikiwa ni kawaida ya swala za Eid  El Haji kuswaliwa katika Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba.
7
Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi,akitoa Khutba ya swala ya Eid El Hajj mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali waliojumuka  katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A,palipofanyika Ibada hiyo.
8
Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakisikiliza Khutba iliyotolewa leo na Sheikh Mmadi Shamata baada ya kuwaswalisha katika Swalaya Eid El Hajj iliyofanyika katika uwanja wa mpira Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja.
9
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya Watoto baada ya kumalizika kwa Ibada ya Swala ya EID El Hajj iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo katika Uwanja wa mpira wa Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja.
10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na baadhi ya Mashekhe wa Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja na Viongozi baada ya swala ya Eid El Hajj mazungumzo hayo yalifanyika leo katika ukumbi Ikulu ya Mkokotoni.
11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na Watoto Nabiel Mohammed (mwenye maiki) na Ahmed Mohammed wa kipindhi cha watoto katika (ZBC) Shirika la Utangazaji Zanzibar katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj,mahijiano yalifanyika leo katika Ikulu ya Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A Mkoa wa Kaskakazini Unguja,
[Picha zote na Ikulu.]

SWALA YA IDD EL HAJI ILIVYOFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

September 24, 2015

 Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Waislam wa Tanzania leo waliungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji.
 Sheikh Nurudin Kishki alitohotuba baada ya swala hiyo.
 Sheikh  Othman Dishi akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika swala.
 Wanawake na watoto wakiwa kwenye swala hiyo.

WAIMBAJI NYIMBO ZA INJILI WAAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI

September 24, 2015

 Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ofisi za  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha kuombea amani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama  kuhusiana na kushiriki katika tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. Kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu akizungumza leo jijini Dar es Salaam jinsi tamasha la kuombea Amani ambapo wasanii hao watakavyo tumbuiza katika tamasha hilolitakalofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa taifa. Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) naMwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira. 
Kutoka kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili  Mathar Mwaipaja akizungumza na waandishi wa habari kuwa watu wote wajitokeze katika Tamasha hilo la kuombea amani na kuwa viingilio vyake kuwa sio vikubwa sana kwa watu wazima ni shilingi elfu tatu na watoto shilingi elfu moja pamoja na VIP  ni shilingi elfu tano.
Baadhi ya waandishi waliohudhulia katika katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam leo.
WASANII wa nyimbo za Injili wajitokeza katika  kuzungumzia Tamasha  la kuombea amani litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es  Salaam Oktoba 4 Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema wamejiandaa vizuli katika ulinzi pamoja na vyombo vya mziki vitakavyo tumika kutumbuizia siku hiyo.
Pia amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moja la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.

TBL YADHAMINI MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA NCHINI

September 24, 2015

 Ofisa Uhusiano wa TBL Doris Malulu, akizungumza na wadau wafanyabiashara wa vinywaji vyao katika semina ya biashara Dar es Salaam jana,ambao wanafadhiliwa na TBL.(kulia) ni Mkufunzi Msimamizi Taasisi ya washauri wa Biashara (TAPBDS CO LTD) Joseph Migunda
 Sehemu ya Wafanya biashara wakisikiliza kwa makini wakati semina hiyo ya jinsi ya kuendesha biashara.ya vinywaji vyao
  Mkufunzi Msimamizi Taasisi ya washauri wa Biashara (TAPBDS CO LTD) Joseph Migunda akiendesha mafunzo hayo
 Ofisa Uhusiano wa TBL Doris Malulu, akizungumza na wadau wa biashara (pichani hawapo) ambao wanafadhiliwa na TBL wakati wa semina ya kuboresha biashara.vinywaji vyao
 Mshauri wa Biashara, Nyainja Manyama, akizungumza na wafanya Biashara mbalimbali (pichani hawapo) wakati wa semina hiyo iliyo fanyika Dar es Salaam
 Mshauri wa Biashara, Nyainja Manyama, akizungumza na wafanya Biashara mbalimbali (pichani hawapo) wakati wa semina hiyo iliyo fanyika Dar es Salaam
 Mshauri wa Biashara, Nyainja Manyama, akizungumza na wafanya Biashara mbalimbali (pichani hawapo) wakati wa semina hiyo iliyo fanyika Dar es Salaam
Maofisa wa TBLK wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara hao

WAISLAMU WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWASAIDIA WENZAO WASIO NA UWEZO

September 24, 2015


Waumini wa dini ya Kislaamu Mkoani Tanga wakiwa kwenye ghafla ya kuchinja ng’ombe  hamsini waliotolewa na wahisani REFSO  kutoka nchini Uturuki  kwa ajili ya siku kuu hiyo





Waislamu nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuwasaidia waumini wasio jiweza katika kutekeleza ibada tukufu ya Eid –el  Haj,inayoambatana na kuchinja ili wote wawe miongoni mwa waliopata razi za Mwenyezi Mungu.
Wito huo ulitolewa jana kwenye ghafla ya kuchinja ng’ombe  hamsini waliotolewa na wahisani REFSO  kutoka nchini Uturuki  kwa ajili ya siku kuu hiyo na Mwenyekiti wa Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Mkoa Tanga(Tampro), Nyumbwe Mwariko ambapo alisema jambo hilo ni kheri kwa umma wa kiislam na wameipokea kama changamoto.
Mwariko akiwa katika shughuli hiyo katika  viwanja Neema Jijini Tanga alisema kuwa tangu mwaka 2010 wahisan hao kutoka Uturuki wamekuwa mstari wa mbele kuwajali waislam wasiojiweza hapa nchini na kushirikiana nao katika ibada hiyo na kutoa idadi kubwa ya ng’ombe kwa mikoa kumi nchi nzima .
Aidha alisema ndani ya nchi yetu hususan mkoa wwetu wa Tanga wapo watu waliokuwa na uwezo mkubwa lakini kwa kutokuthamini umoja,mapenzi ,mshikamano kwa umma wa kiislam kumepelekea kujenga matabaka.
 “Niseme hakuna waislam Mwenyezi Mungu aliowaruzuku, ni kutokuwa na imani ndani ya mioyo yao na kusababisha kutowajali wale wasiojaaliwa” alisema Mwariko.
Hata hivyo alisema chama hicho  kwa kushirikiana na REFSO ya nchini Uturuki wamejipanga kutekeleza ibada hiyo kila mwaka kwa ufanisi zaidi ili kuwasaidia waislam wote wasiojiweza mkoa mzima wa Tanga kwa siku hiyo adhwimu ya Eid El haji.

Serikali ya CCM Yaahidi Kuweka Umeme Vijiji Vyote Tanzania Ndani ya Miaka Miwili Madarakani

September 24, 2015


Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. Baadhi ya ahadi aliyoitoa Bi. Samia ni pamoja na upimaji wa ardhi ya vijiji na wilaya ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa wafugaji na wakulima.  
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano mdogo wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Kilindi, Tanga.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa chama hicho, Bi. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Chemba. Miongoni mwa ahadi kwa wakazi wa eneo hilo alizozitoa ni kushughulikia migogoro ya ardhi suala la ukame na huduma za maji.
Kutoka kulia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akiserebuka na baadhi ya viongozi na makada wa CCM walioongozana kwenye kampeni za mgombea mwenza Wilaya ya Kilindi.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita kwa wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akionesha nakala ya ilani ya chama hicho kwa wananchi kabla ya kumkabidhi, mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akionesha kwa wananchi nakala ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho mara baada ya kukabidhiwa na mgombea mwenza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akimtambulisha mmoja wa wagombea wa udiwani CCM katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Ummy Mwalimu (kushoto) na Mahadhi Juma wakijadili jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza. 

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi kunadi ilani ya CCM.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama juu ya kisiki kuweza kumshuhudia mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili Jimbo la Kilindi.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu kwa heshima na vijana wa UVCCM mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Kiteto ambapo alifanya mikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto kabla ya kuanzamikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kiteto kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Manyara. Katika ahadi zake alisema ndani ya miaka miwili baada ya kuingia madarakani watahakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vya Tanzania.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian John (kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na WanaCCM na Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Chemba, Wilaya ya Chemba.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni humo.
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Chemba, Juma Nkamia (kulia) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa chama hicho, Bi. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Chemba. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa hadhara Jimbo la Chemba.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Chemba kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Wilaya ya Chemba. Picha zote na www.thehabari.com.