Das mkoa wa Tanga akizungumza kwenye semina.

May 08, 2013
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga,Benedict Ole Kuyan akizungumza katika semina mkoani Morogoro jana ,Picha na Mpiga Picha wetu.

Tunakusikiliza mkuu

May 08, 2013
Waandishi wa habari wakifuatiliana semina mkoani Morogoro jana,katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga(Tanga Press Club)Hassani Hashim akifuatilia mjadala kwenye semina hiyo.

Semina Morogoro.

May 08, 2013
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto,Lucy Msofe akiwa na mmoja viongozi ambao aliambatana nao kutoka wilaya Lushoto,Picha na Mpiga Picha wetu.

Simba na Mgambo kupambana leo uwanja wa Taifa kuwania pointi tatu.

May 08, 2013
Kikosi cha timu ya Mgambo Shooting ambacho kitapambana na Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.

KOCHA Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga,Mohamed Kampira amesema timu yao imapania kupata matokeo mazuri katika mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi yao na Simba itakayochezwa leo saa kumi jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kampira alisema kikosi ambacho kitashuka kwenye dimba hilo hii leo kitakuwa chenye upinzani mkubwa kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kuelekea mechi hiyo .

Alisema licha ya kujiandaa kwa mechi hiyo lakini pia wao wamejiandaa katika mechi zao zilizosalia ili kuhakikisha wanachukua pointi tatu muhimu kwani lengo lao ni kumaliza ligi hiyo wakiwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo.

Blog hii inaitakia kilala heri Mgambo shooting kwenye mechi hiyo ili iweza kufanya vizuri kwani tunaamini uwezo wanao na nia pia wanayo hivyo wachezaji wahakikisha wanacheza kwa umakini mkubwa sana.

Mwisho.

Mashabiki Raha ya ushindi!

May 08, 2013
 
Mashabiki wa African Sports wakiwa na mabango wakiishangilia timu yao baada ya kutawadhwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mkoa wa Tanga,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga.

Raha ya Ubingwa kwa mashabiki wa African Sports.

May 08, 2013
MASHABIKI wa Wapenzi wa timu ya African Sports wakisherekea ubingwa wa timu hiyo mwishoni mwa wiki ambapo timu hiyo iliweza kufanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wapya mkoa wa Tanga,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga.
African Sports mabingwa wa soka Tanga.

African Sports mabingwa wa soka Tanga.

May 08, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU ya African Sports "Wanakimanumanu" mwishoni iliweza kufanikiwa kuwa mabingwa wa wapya wa mkoa wa Tanga baada ya kuibamiza Makorora Star mabao 5-0 ikiwa ni ligi ya mkoa wa Tanga mchezo uliochezwa uwanja wa soka Mkwakwani.

Licha ya African Sports kuwa mabingwa lakini bado wamesalia na michezo michache kwenye ligi hiyo kutokana na kuwa na wingi wa pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi hiyo ambapo mpaka sasa wamekwisha kujikusanyia pointi 54.

Furaha ya wanakimanumanu hao ilianza baada ya mchezaji wao James Mendy kupachika bao katika dakika ya 5 ambaye alitumia uzembe wa mabeki wa makorora waliokuwa wamezubaa langoni mwao wakishindwa kujua nini cha kufanya.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutokana na kila timu kuonekana kujipanga kwa ngwe hiyo ya mwisho kwa kufanya mashambulizi kwa zamu langoni mwa timu pinzani.

Wakionekana kujipanga na kupanga mashambulizi langoni mwa Makorora Star,African Sports waliweza kucheza kwa umakini na kucheza pasi fupifupi na ndefu na kuweza kukitawala kipindi hicho na kupelekea kuandika bao la pili dakika ya 47 kupitia Thabiti Mgoha ambaye alimalizia kazi iliyofanywa na Pera Ramadhani.

Baada ya kuingia mabao hayo langoni mwa Makorora Star nao waliweza kucharuka na kucheza kwa umakini huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini mlinda mlango wa African Sports Omari Jengo aliweza kupanchi mashuti yaliyokuwa yakielekezwa kwenye lango lao.

Wakiendeleza wimbi la mashambulizi ,African Sports waliweza kuongeza mabao mengine mawili kupitia dakika za 67 likifungwa na Shekue Salehe na bao la nne likifungwa na Mohamed Issa kwenye dakika ya 75 ambapo zilipoingia bao hizo ziliwafanya wapinzani wao kukata tamaa mapema na kucheza ilimradi mchezo umalizike.

Katika dakika ya 88 ya mchezo huo mchezaji Gidatu Akudae aliweza kuwainua mashabiki wa timu hiyo baada ya kuhitimisha karamu ya mabao langoni mwa Makorora kwa kupachika bao la tano ambapo alitumia uzembe wa mlinda mlango wa timu hiyo,Ally Salim kufunga bao hilo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo,Kocha Mkuu wa timu ya African Sports "Wanakimanumanu"Edmund Nyoni alisema wanamshukuru mungu kwa kuweza kuwa mabingwa na kuhaidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopo kwenye kikosi chake kabla ya kuanza mashindano ya mabingwa wa mikoa.

 Mwisho.

MIKOA YATAKIWA KUCHEZESHA COPA COCA-COLA WILAYANI

MIKOA YATAKIWA KUCHEZESHA COPA COCA-COLA WILAYANI

May 08, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.

Hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.

Vifaa na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania.

Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

          Mwisho.