POLISI YAIPONGEZA SGA SECURITY KWA KUIMARISHA MAFUNZO KWA ASKARI

POLISI YAIPONGEZA SGA SECURITY KWA KUIMARISHA MAFUNZO KWA ASKARI

March 24, 2017
Makampuni ya ulinzi yanayofanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam yametakiwa kutoa mafunzo ya kila mara kwa askari wake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazolikumba Jiji hilo kwa sasa. 

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni ya ulinzi ya SGA Security yaliyofayika katika makao makuu ya kampuni hiyo, Mbezi Beach. Mafunzo haya yaliandaliwa na Polisi Tanzania katika kuimarisha ufanisi wa askari katika makampuni binafsi. 

“Natoa rai kwa makampuni mengine ya ulinzi yaliyopo Mkoa wa Kinondoni yaige mfano mzuri kutoka SGA Security kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wao ili kuwaongezea maarifa yatakayowawezesha kufanya kazi kwa kujiamini na kwa uhakika,” alisema. 

Alisema jeshi la polisi liko tayari kutoa ushirikiano, msaada wa kitaalamu na ushauri pale itakapohitajika huku akiongeza kuwa jeshi hilo pekee haliwezi kumaliza kabisa uhalifu bila kushirikiana na wadau mablimbali yakiwemo makampuni kama SGA Security. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzan Kaganda akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na askari wa SGA Security wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni hiyo. 

“Aidha nawaasa kuzingatia taratibu na sheria za nchi tunapokuwa tukitimiza majukumu yetu ili kazi yetu iwe na tija kwa jamii tunayoihudumia na taifa kwa ujumla,” alisema na kuwaasa askari waliopata mafunzo kuyatumia vizuri kwa manufaa yao na kampuni kwa ujumla. 

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security -Tanzania, Eric Sambu, alisema mafunzo hayo ya mara kwa mara yamekuwa na manufaa makubwa kwa kampuni kwani wameweza kuwajengea askari wao uwezo mkubwa hivi kuwafanya wananchi waongeze imani kwao. 

Zaidi, Mkurungenzi Mtendaji alishukuru Polisi kuanzisha mchakato huu wa kutoa mafunzo wao wenyewe moja kwa moja hii ni ishara kuwa kazi zetu katika makampuni binafsi zinatambuliwa na Polisi wanatuchukulia kama wadau wao katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

 “Tumekuwa tukiendesha mafunzo haya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwani kazi zetu zinafanana kwa kuwa tupo ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao,” alisema. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP, Suzan Kaganda akikabidhi cheti kwa mmoja wa maaskari wa SGA Security wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo. 

Alisema katika siku tano za mafunzo askari hao waliweza kujifunza mada tofauti kama vile matumizi ya nguvu na silaha za moto, haki za binadamu, polisi jamii, uvunjifu wa haki za binadamu, huduma kwa wateja na uhusiano wa jamii, doria, eneo la tukio, usuluhishi wa migogoro na nguvu ya kukamata. 

“Tutaendelea kutoa mafunzo ya aina hii mara kwa mara kwa kuwa tayari tumeona matunda yake ili askari wetu kote nchini katika sehemu ambazo tunafanya kazi waendelee kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa weledi,” alisema.

 Kampuni ya SGA ni moja ya makampuni makubwa ya ulinzi Afrika Mashariki huku ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika ukanda huu na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 17000 huku ikiwa imewekeza vikamilifu katika rasilimali tofauti za shughuli za ulinzi na usalama. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda akipewa maelezo kuhusu chumba cha mawasiliano cha SGA Security kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Ufundi wa SGA-Tanzania Prochest Peter.  

SGA Security ni kampuni ya kwanza binafsi kusajiliwa nchini Tanzania mwaka 1984, kama Group Four Security baadae ikajulikana kama Security Group, baada ya zaidi ya miaka 32 ya shughuli na mafanikio Tanzania na 48 Afrika Mashariki, kampuni imeweza mpaka sasa kuajiri wafanyakazi takriban 5,000 nchini Tanzania na zaidi ya 18,500 katika kanda ya Afrika Mashariki, SGA Security ni moja ya waajiri kubwa katika eneo hilo. 

SGA Security ina uwakilishi wa kiasi kikubwa sana katika kila eneo la huduma ya usimamizi na usafirishaji wa pesa na vitu vyenye thamani na inatoa huduma hizi kwa zaidi ya Mabenki na Taasisi za Fedha 55 katika eneo la Afrika Mashariki, pia kwenye kutoa huduma za ulinzi kwa takribani mashirika 65 binafsi, kidiplomasia na NGO sekta katika eneo hilo.

 SGA Security imejikita zaidi pia katika ulinzi shirikishi kupitia teknolojia zaidi za kisasa kama Closed Circuit TV na Access Control, huduma za radio, Tracking ya magari na ufuatiliaji wa mizigo iwapo safarini (RFID).
WAZIRI MAKAMBA:RASIRILAMI ZA NCHI ZITUNZWE KWA FAIDA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO

WAZIRI MAKAMBA:RASIRILAMI ZA NCHI ZITUNZWE KWA FAIDA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO

March 24, 2017
KAM1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiandaa mti kwa ajili ya kuupanda ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya upandaji miti nchini. Zoezi hilo limefanyika leo katika Halmashauri ya mji Korogwe.
KAM2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe (hawapo pichani). Waziri Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na hifadhi ya mazingira kwa ujumla wake.
KAM3
Sehemu ya wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe wakimsikiliza Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi kutembelea Halmashauri hiyo, kusikiliza na kujionea changamoto za kimazingira na kuainisha namna bora ya kukabiliana nazo.
…………………………………………………………………………………..
Akizungumza katika katika ziara yake mkoani Tanga iliyoingia siku ya tano  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba amesema kuwa ni vema rasilimali za nchi hii zitunzwe kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.”hatuwezi kufanikiwa kama tutaharibu mazingira” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema ofisi yake ya imedhamiria kuchukua swala la mazingira kwa uzito wa kipee ikiwa ni pamoja na kuweka hifadhi ya mazingira katika mipango ya maendeleo.” Uwekezaji wote lazima uende sambamba na hifadhi ya mazingira”
Aidha, uongozi wa Halmashauri ya Mji Korogwe imetakiwa kuwachukua hatua kali wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kwa kutumia sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na ile ya maji ya mwaka 2009. Waziri Makamba amesema kuwa ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kuteua wakaguzi wa mazingira 200 ambao watapata mafunzo na kusambazwa katika Halmashauri mbali mbali nchini.
Pia Waziri Makamba amesema kuwa katika kikao kijacho cha Bunge Ofisi ya Makamu wa Rais itatoa waraka juu ya usimamizi na uchimbaji wa mchanga nchini pamoja na umiliki wa “Chain-saw” kwa lengo kuweka utaratibu utakaowezesha kutambua na kutoa vibali maalumu kwa shughuli hizo ili kulinda mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake maalumu ya kukagua shughuli mbalimbali za kimazingira nchini na hii leo amepokea  taarifa ya hali ya mazingira katika Halmashauri ya Mji Korogwe na Same.
Awali akimkaribisha Waziri Makamba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo Bw. Hillary Ngonyani amesema kuwa katika kutekeleza sheria ya mazingira zoezi la uzoaji na utupaji wa taka ngumu na taka maji umewekewa mkakati maalumu na kutekelezwa kikamilifu pia usafi wa mazingira umefanyika kwa kufanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kutoza faini kwa wananchi wasio na vyoo.
Bw. Ngonyani amebainisha kuwa wananchi wanaokiuka taratibu hizo hushtakiwa kwenye mabaraza ya kata na kupewa muda maalumu wa kujenga vyoo, kusisitizwa kuvitumia pia kuamriwa kusafisha mazingira yao chini ya uangalizi wa maafisa afya.
Aidha Bw. Ngonyani amesema kuwa wananchi wamekumbusha pia kutofanya shughuli za maendeleo kando ya mito na vyanzo vya maji ili kupunguza athari kwa mazingira, na kuunda kwa kamati za mazingira.
Katika hatua nyingine Bw. Ngonyani ameinisha changamoto zinazojitokeza katika Halmashauri ya Korogwe mji kuwa ni pamoja na Ukosefu wa wakaguzi wa Mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha vipindi vya mvua kubadilika na kuongezeka kwa joto.

CHADEMA WAMTAKA RAIS DK. MAGUFULI KUELEZA SABABU ZA KUTENGUA NAFASI YA UWAZIRI WA NAPE NNAUYE

March 24, 2017
 Makamu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kuwateuwa Lawrence Masha na Ezekia Wenje kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki pamoja na mambo mbalimbali yayoendelea nchini. Kulia ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.

MD KAYOMBO AKAGUA ENEO LITAKLOTUMIKA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE LA MANISPAA YA UBUNGO LILILOPO MKOANI MOROGORO

March 24, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Shamba litakaloandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane lililopo Mkoani Morogoro


Na Mathias Canal, Morogoro

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amefanya ukaguzi wa eneo kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ili kujiridhisha na kutoa maelekezo ya maandalizi kwa kufyeka majani yaliyopo katika eneo la JKT Mtaa wa Nanenane ikiwa ni hatua za ufanisi kwa ajili ya kuelekea Maonesho ya Nane Nane mwanzoni kwa mwezi Agosti.

Kayombo amesema kuwa lengo kuu la kuzuru kwanza ilikuwa ni kujionea eneo hilo sambamba na kuona hali ya utendaji kazi ili kuanza ufyekaji na kuanza kulima mazao ambayo yanakusudiwa kuoneshwa na Manispaa ya Ubungo.

Amesema kuwa katika utendaji wake amekusudia kwenda mwenyewe Field ili kuona hali ya utendaji ilivyo sio kupelekewa Taarifa pekee kwani kufanya hivyo Ukurugenzi alionao utakuwa hauna maana kama ataishia ofisini.

"Rais ametupa mamlaka makubwa ya kuwatumikia wananchi sasa kama tunakaa ofisi pekee nchi haiwezi kusonga mbele badala yake ili tuweze kuwa na mafanikio katika utendaji pamoja na Kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ni wazi kwamba tunapaswa kuzuru katika maeneo yote tunayoyaongoza" Alisema Kayombo

MD Kayombo amewapa maelekezo Afisa Kilimo na Afisa Mifugo na Uvuvi kuanza haraka iwezekanavyo usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Mita za Mraba 3600 ili kulima na kupanda mazao kusudiwa kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

Maelekezo mengine ni pamoja na kununua viuatilifu kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu na magonjwa, kuandaa mabango na kuainisha aina mbalimbali za malisho iliyooteshwa na kujenga bwawa la samaki.
Kayombo alisema kuwa eneo hilo limenunuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya Maonesho ya Nane Nane ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, Wafugaji na wavuvi kwa kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia na mbinu za kuongeza uzalishaji katika eneo la Uvuvi, Kilimo na Ufugaji.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Kaimu Afisa Kilimo wa Manispaa ya hiyo Ndg Salim Msuya amesema kuwa wanataraji kuanza kutekeleza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kujenga mabanda ya mifugo na sehemu za kusindika mazao ya mifugo, kuandaa mavazi rasmi kwa ajili ya washiriki wa Maonesho.

Mengine ni kukusanya bidhaa za mazao mbalimbali ya wafugaji, wakulima na wavuvi watakaoshiriki Maonesho hayo ya Kilimo Nane Nane kwa ajili ya kuyapeleka Morogoro.

Sambamba na hayo pia Msuya amesema kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kutengeneza matuta ya kuoteshea malisho, Kununua mbolea na kuweka kwenye eneo la malisho ya mifugo, kufunga maji katika eneo la malisho yatakayotumika kwa ajili ya umwagiliaji na mifugo itakayopelekwa wakati wa Maonesho.

Msuya ameeleza kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kuandaa mashimo katika matuta ya kuotesha miche, Vipande na Mbegu za malisho pamoja na kutayarisha eneo la kwa kusafisha eneolima na kufanya Layout ya eneo la kuchimba bwawa kwa ajili ya ufugaji samaki.

MPIGA CHAPA MKUU ASISITIZA KAMPUNI KUENDELEA KUJISAJILI

March 24, 2017
Mpigachapa Mkuu  wa Serikali,Cassian Chibogoyo akionesha waandishi wahabari (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake  rangi sahihi  ya bendera yaTaifa, kulia ni Afisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Shija. (NA MPIGA PICHA WETU)

Leonce Zimbandu

MPIGACHAPA Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo ameendelea kusisiti za na kuzitaka taasisi za serikali, binafsi za uchapishaji  kuendelea kujisajili katika ofisi hiyo na kuepuka usumbufu wa kubainika kwenye msako.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kutoridhishwa na kasi ya kampuni za uchapishaji zilizojitokeza tangu wito huo utolewe Februari 13, mwaka huu, kampuni 24 tayari zimejitokeza.

Chibogoyo  aliyasema hayo alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo  wakati akijibu swali kuhusu kampuni za uchapishaji zilizotii sharia kujisajili  bila shuruti.

Alisema amesikitishwa na mwitikio mdogo wa usajili wa kampuni na taasisi za uchapishaji, hivyo akiwa muungwana ameamua kutumia fursa ya  kuwakumbusha  watimize wajibu wao kisheria.

“Inawezekana katika mkutano wangu  sikueleweka vizuri lakini usajili unahusu kampuni binafsi na serikali kwa lengo la  kutambua shughuli zao na kuepuka kujificha,” alisema.

Alisema baada ya muda uliotolewa kukamilika na ofisi hiyo ikapata  taarifa kuwa ipo taasisi au kampuni inajihusisha na uchapishaji, Ofisi itachukua hatua ya kuifuatilia.

Hivyo kabla ya hali hiyo ya ufuataliaji, itakuwa busara kwa wachapishaji hao kujisajili  ndani ya siku tano zilizobaki tangu wito huo ulipotolewa. 

Aidha, alisema   ili kuondoa usumbufu kwa kampuni za uchapishaji za mikoani, zinaweza kujisajili kwa kupitia mtandao wa Ofisi ya Mpigachapa.

Alisema Wachapishaji   halali watakaojiorodhesha watakaribishwa na kupewa fursa ya kutoa mawazo ya kuiweka nchi mahali salama kupitia nyaraka.

Hatua hiyo imechukuliwa  ili kuendeleza vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka bandia kwa kuwasaka nyumba kwa nyumba, iwapo watashindwa kujitokeza na kujisajili kwa hiari.



DKT KEBWE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO

March 24, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao hicho kwa makini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki

Na Mathias Canal, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Morogoro.

Kikao hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika Katika Ukumbi wa JKT Nane Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli moja kimepitisha Agenda zote sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2016 sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2017 ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe ameitaka kamati inayoratibu shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi uaminifu kwa wananchi na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza uchumi nchini kupitia Kilimo.

Dkt Kebwe alisema kuwa TASO kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya Halmashauri zingine kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina weledi uliokusudiwa.

Sambamba na hayo pia amewasihi wadaiwa sugu kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kwani kufanya hivyo itaongeza ustawi na uimara wa Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na hatimaye Kilele chake kuwa na Tija kwa jamii.

Dkt Kebwe amewapongeza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya waliohudhuria katika kikao hicho ambapo alisema kuwa wanafanya kazi nzuri na kuonyesha ushirikiano imara katika Maandalizi hayo japo amesisitiza kuongezwa kwa jitihada za Maandalizi ili Maonesho hayo yawe na weledi na tija.

Sherehe za Maonesho ya Kilimo Nane Nane hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa kuwaelimisha watazamaji na hasa wakulima, wafugaji na wavuvi kujifunza na kupata uzoefu wa teknolojia na mbinu zinazotumika kuongeza uzalishaji katika eneo la kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Katika Maonesho hayo mambo muhimu hutawala ikiwa ni pamoja na kuonyesha mazao mbalimbali sambamba na mifugo mbalimbali kwenye mabanda.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewapongeza viongozi wote kwa namna ambavyo wanashiriki kuandaa Maonesho hayo huku akisema kuwa pamoja na Halmashauri ya Ubungo kuwa mpya na inaanza kushiriki katika Maonesho hayo kwa Mara ya kwanza atahakikisha kuwa maonesho yanakuwa na tija katika mabanda yote yanayoendelea kuandaliwa na Maafisa Kilimo, Uvuvi na Mifugaji.

MD Kayombo alisema kuwa kupitia Maonesho ya Kilimo mwaka huu 2017 wananchi watapata fursa ya kujifunza mbinu za ufugaji kwa kutumia mabanda bora, Uchanganyaji wa vyakula vya mifugo na ulishaji, Teknolojia bora ya ufugaji wa samaki wengi katika eneo dogo, Utotoleshaji vifaranga kwa kutumia incubator ya kienyeji na kisasa, Uhamilishaji wa samaki na Ng'ombe na teknolojia Nyinginezo.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho alizitaja changamoto za maandilizi za Maonesho ya Kilimo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa michango kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na kuchelewa kuthibitisha mialiko kwa wageni walioalikwa kutembelea Maonesho ya Kilimo Nane Nane.
HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI, MABALOZI NA KAMISHNA IKULU DAR ES SALAAM LEO

HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI, MABALOZI NA KAMISHNA IKULU DAR ES SALAAM LEO

March 24, 2017
MAG1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MAG3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG4
MAG5
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MAG6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba kabudi  baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA WA MABALOZI 6 WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA WA MABALOZI 6 WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

March 24, 2017


OZA
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Cyprus hapa nchini Andreas Panayiotou ambaye makazi yake yapo Muscat, Ikulu jijini Dar es Salaam.
OZA 1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Bangladesh hapa nchini Maj. Gen. Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir mwenye makazi yake Nairobi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
OZA 2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Bangladesh  hapa nchini Maj. Gen. Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir mwenye makazi yake Nairobi mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho  Ikulu jijini Dar es Salaam.
OZA 3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Nepal hapa nchini Amrit Bahadur  Rai ambaye makazi yake yapo Pretoria Afrika Kusini mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho  Ikulu jijini Dar es Salaam.
OZA 8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ecuador hapa nchini Benys Toscano Amores ambaye makazi yake yapo Addis Ababa nchini Ethiopia.
OZA 6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ecuador hapa nchini Benys Toscano Amores ambaye makazi yake yapo Addis Ababa nchini Ethiopia mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
OZA 7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa New Zealand hapa nchini Michael Gerrard Burrel ambaye makazi yake yapo Pretoria nchini Afrika Kusini.
OZA 5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Congo Brazaville hapa nchini  Guy Nestor Itoua ambaye makazi yake yapo Kigali nchini Rwanda. PICHA NA IKULU
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

March 24, 2017


NIS1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke na ujumbe wake, wawekezaji kutoka Denmark na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea Kilwa mkoani Lindi.
NIS2
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS3
Sehemu ya ujumbe kutoka Ujerumani na wawekezaji kutoka Denmark wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifafanua jambo katika kikao hicho.
NIS5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA UJENZI WA UKUTA WA OCEAN RAOD

March 24, 2017
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.) Maswa Mashariki akiongea na waandishi wa Habari baada ya ukaguzi wa ujenzi wa ukuta wa Ocear Road katika Barabara ya Baraka Obama Jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais  Bw. Richard Muyungi akiwasilisha taarifa utekelezaji wa ujenzi wa ukuta wa fukwe ya Ocean Road kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi malisili na Mazingira. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Sehemu ya ukuta wa fukwe ya Ocean Road kama unavyooneka katika picha ukiwa katika matengenezo.
Evelyn Mkokoi – Dar es Salaam
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira, imetembelea mradi wa ujenzi wa ukuta wa fukwe ya Ocean Road katika Barabara ya Barak Obama Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kukagua  mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi, unaoratibiwa na  Ofisi ya Makamu wa Rais.

Akiongea na waandishi wa Habari katika eneo la ujenzi wa ukuta huo, kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo (MB) Maswa Mashariki alisema kuwa kuwa, kamati inaishauri serikali kutumia vizuri  mahusiano ya nchi yetu na wahisani ili kuweza kupata pesa za kusaidia suala zima la kuhimili na kukabiliana na mbadiliko ya tabianchi.

Aidha, Mhe. Nyogo aliongeza kwa kusema kuwa Serikali nayo iongeze jitihada za kupambana na  kukabiliana na athari na hasara zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa elimu ya kulinda mazingira kwa umma.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Mhe Dk. Rafael Chegeni, alisema kuwa uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti ovyo kwa matumizi ya nishati ya mkaa ni mkubwa na ndiyo unaopelekea athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi, na nishati mbadala bado zinapatikana kwa gaharama za juu, na kushauri kuwa kuwe na mikakati kwa serikali na sekta husika ya kumsaidia mwanachi wa kawada kutunza mazingira aidha, kuwe na mkakati unaonekana na kusadia kuwa na upatikani wa haraka wa nishati mbadala.

Baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Dar es Salaam na Pwani, Mhe Hawa Mwaifunga alitaka kufahamu kuhusu mradi wa majiko banifu, utekelezaji wake na ugawaji wa majiko hayo kwani athari za mabadiliko ya tabia nchi yapo nchi nchi nzima.

Awali akiwasilisha ripoti ya utelelezaji wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi unaohusisha ujenzi wa ukuta wa ocean road, urejeshaji wa upandaji wa mikoko katika maeneo ya mbweni, daraja la salenda, ununio na ujenzi wa mitaro katika maeneo ya ilala Bungoni kata ya Buguruni, maeneo ya Mtoni katika Wilaya ya Temeke na katika maeneo ya chuo cha Mwalimu Nyerere KIgamboni, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi , alisema kuwa takribani kiasi cha dola milioni 500 zinahitajika kila mwaka nchini kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kusaidia mafunzo kwa wananchi katika ngazi za familia ili kuweza kukabilianda na janga hili la mabadiliko ya tabia nchi.

Aliongeza kwa kusema kuwa ujenzi huo wa ukuta wa ocean road utahusisha pia ujenzi wa njia za waendao kwa miguu, viti vya kumpuzikia, na taa.

Mradi wa ujenzi wa ukuta wa Ocean Rpoad unaoendelea kujengwa, umekalimika kwa asilimia 30% yenye urefu wa mita 820, kwa pande nyingine kwenda juu kwa urefu wa mita 2.5, na pande nyingine kwenda juu kwa urefu wa mita 4.

Mradi huo huo unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) , na kusimamiwa na shirika lingine la umoja wa maitaifa la Huduma kwa Miradi, (UNOPS) ambalo linasimamia miradi yote ya mabadiliko ya tabia nchi duniani. Mradi huo upo chini ya Uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Na ujenzi huo wa ukuta unafanywa na kampuni ya Dezo Civil Constractions ya jijjini Dar es Salaam

TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAKABIDHIWA BENDERA ,YAELEKEA UGANDA NA MATUMAINI YA KUREJEA NA MEDALI

March 24, 2017
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akikabidhi Bendera kwa manahodha wa timu ya taifa ya riadha kwa upande wa wanaume,Fabian Joseph (kushoto) na Magdalena Shauri (kulia)Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru (mwenye miwani) ,Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na kushoto ni Meneja wa timu ya taifa ya riadha Meta Petro.
Raisi wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akizungumza na wanariadha 28 wanaoelekea nchini Uganda kwa ajili ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru akitoa neno kwa wanariadha hao,Shirika la Hifadhi za Taifa ndilo limedhamini wanariadha hao ambao idadi yao katika ushiriki wa mbio hizo imevunja rekodi ya tangu mwaka 1991.
Baadhi ya wanariadha watakao iwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika jumapili hii.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Whilleam Gidabuday akizungumza wakati wa hafala hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanariadha wa timu ya taifa iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha.
Kikosi cha wanariadha 28 na viongozi 12 kitakachopeperusha Bendera ya Taifa nchini Uganda katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika yatakayofanyika Jumapili hii katika mji wa Entebe.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.