RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM

January 27, 2018

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa kusali pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  mara baada ya wote kwa pamoja kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli. Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika  katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
5
Wanakwaya  kutoka Chuo cha Ardhi jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika  katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
8
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta akihubiri katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli mara baada ya Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Nakala za CD ya kwaya kutoka Chuo cha Ardhi mara baada ya Ibada. Kushoto ni Mke wake Mama Janeth Magufuli akifurahia.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda mara baada ya kupewa na moja ya Waumini wa Kanisa hilo mara baada ya Ibada ya jumapili.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini wengine mara baada ya ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

UZINDUZI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KINONDONI ZAWAVUTIA WENGI.

January 27, 2018
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

WAVUVI WAASWA KUZINGATIA SHERIA,TARATIBU ZA UVUVI KUZILINDA RASILIMALI ZIWA VICTORIA

January 27, 2018
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayni Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo, Ulega aliwapongeza wavuvi hao kwa hatua hiyo walioichukua huku akikazia msimamo wa serikali wa kupambana na uvuvi halamu. Pamoja na kuwapongeza huko,Ulega aliwasisitiza wavuvi hao kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi ili kuzilinda rasilimali hiyo, ambayo ilikuwa inaelekea kutoweka.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa samaki, wazazi walikuwa wamebaki asilimia nne, wenye hadhi ya kuvuliwa kwa maana ya sentimita 50 hadi 85 wamebaki asilimia tatu na wachanga wamebaki asilimia 93, na kama uvuvi huu ungeendelea maana yake ziwa lingebaki jangwa," alisema Ulega

Waziri Ulega aliwataka wavuvi hao kununua nyavu zinazokubalika kwenye viwanda ambavyo vinauza nyavu hizo,  badala ya kuendelea kutumia nyavu zisizoruhusiwa kwani watapata hasara kwa kuteketezewa na wengine kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu, baadhi ya wavuvi waliamua kuzisalimisha nyavu hizo wenyewe bila shuruti. 


kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu baadhi us wavuvi waliamua kusalimisha nyavu  hizo wenyewe bila shuruti.

Alisema nyavu zinazokubalika kwa mujibu wa sheria, nyavu za dagaa zinatakiwa ziwe na milimita 8, nyavu za sangara inchi 6 hadi tisa na ndoano za sato inatakiwa zenyewe ziwe namba 4, hadi 12, hizi ndio zana sahihi zinazotakiwa kuonekana ziwani," alisema Lwekaza

Naye Benzi Nestory ambaye nimmoja wa wavuvi aliomba kupata muongozo wa sehemu sahihi ya kupata zana hizo haramu kwa haraka badala ya kuambiwa kwa mdomo kuwa nyavu hizo zinapatikana ili kuondokana na hasara wanazopata.

Kwa upande wake Joel Lusigwa alilalamikia upande wa faini Sh700000 kuwa kubwa wanayotozwa pindi wanapokutwa na kosa hivyo kuomba wapunguziwe ikilinganishwa na maeneo mengine ambayo wanatozwa faini kidogo. Hata hivyo waziri Ulega alisema licha ya kuwapo sheria nyingine zinazowakandamiza wavuvi lakini alisema faini hiyo ya Sh700000 ni pamoja faini ya kutokuwa na leseni na usajili ambayo ni Sh .200000 huku faini ya kuharibu mazingira ndani yaziwa ikiwa ni Sh .500000 ambazo hazitabadilishwa lengo ni kumtia uchungu mtuhumiwa.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akiongoza shughuli za kuteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 .Wavuvi wakisogeza  Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  eneo la kuchomea  baada ya kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi  katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

WAZIRI UMMY,MAKAMBA WASHUHUDIA MECHI BAINA YA COASTAL UNION NA POLISI DAR ZIKITOKA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1

January 27, 2018
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano  January Makamba akikagua timu wakati wa mechi ya Ligi Daraja la kwanza baina ya Coastal Union na Polisi dar uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano  January Makamba kulia akikagua timu wakati wa mechi ya Ligi Daraja la kwanza baina ya Coastal Union na Polisi dar uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union Steven Mguto
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akishiriki kwenye uhamasishaji wa nyimbo wakati timu ya Coastal Union ilipocheza na Polisi Dar kwenye mchezo uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akitokea kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano  January Makamba akizungumza na timu zote mbili kabla ya kuanza mchezo huo leo
 Waachezaji wa timu zote mbili wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo huo
 Kikosi cha timu ya Coastal Union ambacho kimeanza dhidi ya Polisi dar leo
 Kikosi cha timu ya Polisi Dar ambacho kimecheza dhidi ya Coastal Union leo

 Mchezaji wa timu ya Coastal Union kushoto akiwani mpira dhidi ya wa Polisi Dar katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.


 Sehemu ya mashabiki wa soka mkoa wa Tanga wakifuatilia mchezo huo leo

SERIKALI YAMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUMALIZIA MAJENGO YA CHUO.

January 27, 2018
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo. 
aimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.
engo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA
Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara na CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya leo mkoani Humo.
NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.

“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja” alisema Bw. Simba.

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.

Kwa upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joachim Catherine amesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi Wa mabweni matatu yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo cha maafisa tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara.

Aidha Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati na upanuzi Wa madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw. Frolian Mbungu amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya apokee majengo kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha.

Aidha wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA TFF LEO

January 27, 2018
MAAMUZI YA KAMATI YA BODI YA LIGI KUU YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI KILICHOFANYIKA JANUARI 25, 2018 OFISI ZA TFF, UWANJA WA KUMBUKUMBU YA KARUME- DAR ES SALAAM
 
LIGI KUU YA VODACOM

Mechi namba 95 (Mbeya City 1 vs Kagera Sugar 1). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 1, 2018 jijini Mbeya, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu.

Kamati iliiagiza Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa waraka kwa wamiliki wa viwanja kuhakikisha timu zinaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi tu.

Mechi namba 100 (Tanzania Prisons 3 vs Mbeya City 2). Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Mwazurimo amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano), adhabu ambayo imezingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
 
Kocha Mwazurimo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) na Mwamuzi baada ya kumtolea lugha ya kashfa katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 14, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Pia klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwa madai alikataa kutoa penalti kwa timu hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Kamati imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha Mwamuzi wa mechi hiyo, Bw. Israel Nkongo na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua zaidi.

Mechi namba 103 (Majimaji 1 vs Azam 1). Klabu ya Azam FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kukataa wachezaji wake wakaguliwe ndani kwa madai kuwa chumba kimepuliziwa dawa katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 18, 2018 Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kitendo cha timu hiyo ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu. Pia klabu hiyo imeandikiwa barua ya kutakiwa kuthibitisha madai yake kuwa chumba hicho kilikuwa kimepuliziwa dawa.

Mechi namba 104 (Simba 4 vs Singida United 0).Mtunza Vifaa wa Singida United FC, Mussa Rajab amefungiwa mwezi mmoja na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mapumziko na kumlalamikia mwamuzi.

Kitendo alichofanya Mtunza Vifaa huyo katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 18, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kimekiuka Kanuni ya 14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Viongozi.

Mechi namba 106 (Mbao 0 vs Stand United 1). Klabu ya Stand United imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) kwa dakika sita, na pia kuchelewa kuingia uwanjani kwa dakika tisa katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 20, 2018 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Adhabu kwa klabu hiyo iliyokiuka Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu, imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 112 (Kagera Sugar 0 vs Simba 2). Suala la mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kumpiga shabiki baada ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 22, 2018 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kumalizika, limepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Mechi namba 44 Kundi A (African Lyon 2 v Friends Rangers 1). Mchezaji Almasi Mkinda wa Friends Rangers amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga ngumi mchezaji wa African Lyon katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 14, 2018 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) ya Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Nao wachezaji Mtoro Hamisi wa Friends Rangers, na Prosper Mushi wa African Lyon wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kupigana uwanjani. Adhabu imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Daktari wa Friends Rangers, Rajabu Shabani amefungiwa miezi mitatu na kupigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kuwatolea lugha ya matusi na dharau waamuzi wa mechi hiyo. Adhabu imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Viongozi.

Klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(10) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 45 Kundi A (JKT Tanzania 5 v African Lyon 1). Klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kukiuka Kanuni ya 14(13) kutokana na kugoma kuingia vyumbani katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 20, 2018 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko Mbweni jijini Dar es Salaam. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Nayo JKT Tanzania imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia eneo la kuchezea kushangilia ushindi. Klabu hiyo imeadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 41 Kundi B (JKT Mlale 1 v Mawenzi Market 0). Daktari wa Mawenzi, Novatus Ngowi amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kuwatolea waamuzi lugha isiyokuwa ya kiungwana katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 13, 2018 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Mechi namba 43 Kundi B (Mbeya Kwanza 0 vs KMC 0). Kocha wa Mbeya Kwanza, Maka Mwalwisi amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 13, 2018 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kumalizika akiwashambulia viongozi wa TFF akidai wanaandaa timu za kupanda Ligi Kuu, ndiyo maana waamuzi wananyonga haki yao ya kupata ushindi.
 
Mechi namba 47 Kundi B (Polisi Tanzania 0 vs Coastal Union 0). Klabu ya Polisi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na gari la washabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani, na kuzunguka uwanja wakati timu zikifanya mazoezi. Pia wakati wa mapumziko na baada ya mchezo kumalizika washabiki wa timu hiyo waliwafuata waamuzi na kutaka kuwapiga.
 
Vilevile washabiki wa timu hiyo walitoa lugha chafu kwa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 20, 2018 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
 
Mechi namba 44 Kundi C (Biashara United 2 vs Alliance Schools 0). Klabu ya Alliance Schools imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 13, 2018 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 45 Kundi C (JKT Oljoro 1 vs Dodoma FC 1). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Emmanuel Muga na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina wamepata alama za chini hivyo kukosa sifa ya kuendelea kuchezesha Ligi.

Hivyo, Kamati imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha waamuzi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi dhidi yao.

Mechi namba 47 Kundi C (Biashara United 1 vs Rhino Rangers 1). Daktari wa Viungo wa Rhino Rangers, Ahamad Mgongo na kipa Mohamed Ibrahim Salumu wa Rhino Rangers wamesimamishwa hadi suala lao la utovu wa nidhamu waliofanya litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Wamesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mbali ya kumpiga teke Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Mara, Mgongo pia wakati vurugu zikiendelea katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 21, 2018 Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma alimchapa kibao Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Athuman Rajabu.

Naye kipa Salumu baada ya kumuangusha kwa makusudi ndani ya eneo la hatari mchezaji wa Biashara United, na refa kuamuru adhabu ya penalti dhidi yake alimpiga ngumi kwa makusudi mchezaji huyo wa Biashara United. Baada ya vurugu kutulia Mwamuzi alimuonyesha kadi nyekundu. Lakini Kipa huyo baada ya kuamuliwa kutoka nje alimpiga Mwamuzi ngumi ya kisogoni.

Mechi namba 48 Kundi C (Transit Camp 0 vs Alliance Schools 3). Wachezaji Mohamed Suleiman Ussi, Khalid Mahmud Konobile, Abubakar Ramadhan na Victor William Alimwene wa Transit Camp wamepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumkimbilia Mwamuzi baada ya mechi kumalizika kwa lengo la kumfanyia vurugu kabla ya askari polisi kuingilia kati.

Walifanya kitendo hicho katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

LIGI DARAJA LA PILI

Mechi namba 21 Kundi C (The Mighty Elephant 2 v Burkina Faso 2).

Mchezaji Gideon Joram Richard wa The Mighty Elephant anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kitendo chake cha kwenda karibu na chumba cha waamuzi baada ya mechi na kuwakashfu kuwa ni mabwege katika mchezo huo uliofanyika Januari 15, 2018 Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

AJENDA 62/MSC/2018- MALALAMIKO YA DODOMA FC

Kamati imesikiliza malalamiko ya timu ya Dodoma FC dhidi ya JKT Oljoro katika mechi yao iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi. Malalamiko hayo yalikuwa na sehemu mbili; moja ni uhalali wa mchezaji wa JKT Oljoro, Haki Rubea kuwa hakuwa na leseni, na mbili ni kudai kuwa Mwamuzi na Mwamuzi Msaidizi Namba Moja walikataa bao lao halali.

Baada ya kupitia malalamiko hayo, Kamati imebaini kuwa Haki Rubea ni mchezaji wa JKT Oljoro mwenye leseni namba 961111011 iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hivyo ni mchezaji halali (qualified player). Vilevile Kamati haina mamlaka ya kukubali bao ambalo limekataliwa na Mwamuzi uwanjani. Hivyo, Kamati imetupa malalamiko ya Dodoma FC kwa hoja zote mbili.

 

Hata hivyo, Kamati imejiridhisha kuwa Kamishna wa mechi hiyo Paul Opiyo na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina walifanya makosa kumruhusu mchezaji huyo kucheza bila kuonyesha leseni yake, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(16) na 14(17) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

 

Kamati imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Emmanuel Muga na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua Zaidi.