HAIJAWAHI KUTOKEA: MAZISHI YA BILIONEA WA MAPENZI GARINI BUKOBA HISTORIA!

HAIJAWAHI KUTOKEA: MAZISHI YA BILIONEA WA MAPENZI GARINI BUKOBA HISTORIA!

November 25, 2014


Msafara wa magari kuelekea kwenye mazishi. Tukio hilo la mazishi lilijiri Jumamosi iliyopita katika Kijiji cha Kyaikailabwa, nje kidogo ya mji wa Bukoba ambapo siku hiyo, shughuli zote zilisimama kwa siku nzima kupisha tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi.
ACHANA na mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda kamili huu hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho, msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea kijiji cha Kyaikailabwa. 
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo. 
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni nyumbani. 
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini. 
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini.

RAIS KIKWETE APOKEA SALAMU ZA KHERI TOKA KWA RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI

November 25, 2014
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole  za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi  wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

DC,GAMBO AWATAKA WAUGUZI KUKOMESHA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA

November 25, 2014
NA SALUM MOHAMED,KOROGWE 
 MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, amewataka wauguzi Wilayani humo kutoa elimu kwa wazazi majumbani kujifungulia katika vituo vya afya lengo likiwa ni kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Akifungua kongamano la Chama Cha Wauguzi Tanzania (TAMA) hivi karibuni Wilayani humo, Gambo alisema kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto ni kutokana na wazazi wengi kutokuwa na elimu ya kuhudhuria vituo vya afya kutambua mwenendo wa mtoto tumboni.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiwalazimu kujifungulia katika sehemu ambazo sio za kutolea huduma na hivyo kuwataka kutoa elimu nyumba kwa nyumba jambo ambalo litasaidia kuwa na ada ya kuhudhuria vituo vya afya kila baada ya muda.

“Nashukuru kwa kupata nafasi hii adhimu ya kuzungumza nanyi natambua kuwa ni watu muhimu sana hasa suala zima la vifo vya mama na mtoto-----tutambue kuwa muko na nafasi ya kuelimisha jamii” alisema Gambo

“Wilayani kwetu hapa munatambua kuwa vifo vya mama na mtoto vimepungua kiasi ila tusibweteke kwani kuna kundi kubwa halina elimu ya kuhudhuria vituo vya afya wakati wa ujauzito na mwisho hujifungulia sehemu zisizo salama” alisema

Gambo aliwataka wauguzi hao kuwa na mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba kutoa elimu hiyo kwa wanawake  ili wakati wa ujauzito kuwa na utaratibu wa kuhudhuria vituo vya afya na madhara ya kujifungulia sehemu ambazo sio za kutolea huduma.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkunga na mwalimu chuo kikuu cha Canada, Angella Spencer, aliwataka wauguzi kuwa na kauli nzuri kwa wajawazito hasa wakati wa kujifungua.

Alisema wauguzi wako na nafasi kubwa ya kumfanya mzazi kujifungua kwa hali ya furaha baada ya kupata faraja na hivyo kuwataka kuzitumilia nafasi zao lengo likiwa ni kuwaweza wazazi katika mazingira ya  kujifungua salama.

“Ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto kwanza ni muuguzi kuhakikisha anampokea mzazi kwa furaha-----hii itamfanya kujisikia furaha hadi muda wa kujifungua” alisema Spencer

Alisema kama wauguzi wataifuata taaluma yao ni wazi kuwa vifo vya watoto wakati wa kujifungua vitapungua Tanzania sambamba na utoaji wa elimu ya kila mjamzito kuhudhuria kituo cha afya kwa utaratibu.



HIVI NDIVYO COASTAL UNION U-20 LEO WALIVYOIKALISHA MONGA STARS YA VYERU WILAYANI MKINGA,YAIPIGA 1-0

November 25, 2014
KIKOSI CHA U-20 CHA COASTAL UNION KIKIPASHA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO DHIDI YA MONGA STARS AMBAPO COASTAL UNION U-20 ILIIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 BAO HILO LILIFUNGWA NA ZAMIRU ISSA DAKIKA YA 36

MAKIPA YA KIKOSI CHA U-20 COASTAL UNION WAKIPASHA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO


KOCHA WA KIKOSI CHA U-20 YA COASTAL UNION,JOSEPH LAZARO AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION U-20 AMBACHO KILICHEZA NA MONGA STARS LEO NA KUWAFUNGA BAO 1-0

MWAMUZI WA MECHI HIYO,KASID KITENDO AKIWA NA WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO

KIKOSI CHA MONGA STARS KILICHOPIGWA KIMOJA NA COASTAL UNION U-20 LEO

KOCHA WA TIMU YA VIJANA YA COASTAL UNION U-20 JOSEPH LAZARO AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO LEO WAKATI WA MAPUMZIKO

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA WA PILI KUTOKA KULIA AKIFUATILIA MECHI HIYO NA VIONGOZI WENGINE WA TIMU HIYO WA KWANZA KULIA NI MENEJA WA TIMU YA COASTAL UNION AKIDA MACHAI NA KUSHOTO NI MJUMBE WA KAMATI YA USAJILI SALIM BAWAZIRI NA MWANACHAMA WA COASTAL UNION LEO


SHUHUDIA AJALI YA TOYOTA HAICE ILIYOUWA WATU TISA NA KUJERUHI WENGINE TISA SHINYANGA

November 25, 2014


Toyota haice yenye namba za usajili T761 CKD iliyokuwa ikitoka wilayani Kahama kuelekea mjni Shinyanga ikiwa imepinduka katika eneo la Buhangija manispaa ya Shinyanga na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine tisa,baada ya kupinduka mara tatu baada ya kuvuka tuta kisha kugonga daraja na kuangukia mtaroni,chanzo chake ni mwendo kasi ambapo dereva wa gari hilo Anwar Awadhi mkazi wa Lubaga Shinyanga aliruka na kukimbia.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
Gari likitolewa kwenye mtaro ni baada ya kuuwa watu tisa ambapo watano walikufa papo hapo .

Wananchi wakiwa eneo la tukio

WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUTOKA UBELGIJI WATEMBELEA MAENEO YA UWEKEZAJI BAGAMOYO

November 25, 2014


 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akiukaribisha ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ambao wametembelea mkoa wa Pwani kujionea fursa za uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akiongozana na ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ambao wametembelea mkoa wa Pwani kujionea fursa za uwekezaji.
  Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Mgeni Baruani akizungumza akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na Uongozi wa Mkaoa wa Pwani.
 Ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ukiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Otieno Igogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
 Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika mkutano huo.
 Ujumbwa wa Tanzania ukiwa katika mkutano huo.
  Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Ivan Korsak akizungumza katika mkutano huo.
 Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Ivan Korsak akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji na uongozi wa Mkoa wa Pwani waliofika kuangalia fursa za uwekezaji mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (kushoto) akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Shangwe Tamala akitoa mada kuhusu vivutio vya kitalii na maeneo ya uwekezaji katika mkoa wa Pwani.
 Ujembe wa Tanzania na Ubelgiji ukiwa katika mkutano huo.
Mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Jean-Christophe Van Acker akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji wakiwa mjini Bagamoyo wakiangalia maeneo ya uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akimkabidhi zawadi, mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Yvan De Coninck.
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Clara Ibinya akizungumza katika mkutano huo.
 Mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Jean-Christophe Van Acker akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa Mkoa wa Pwani na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji waliotembelea maeneo ya uwekezaji Bagamoyo mkoani Pwani.  
 Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Ivan Korsak akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
 Jean-Christophe Van Acker akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
 Nikki Martine Fedorowicz akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mko wa Pwani.
Jacques Delaunoit akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
 Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Otieno Igogo akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza. 
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (katikati) akiwaongoza wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji waliotembelea eneo la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Eneo la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani akito ufafanuzi kwa wawekezaji waliotembelea eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala.
 Eneo itakayojengwa Bandari Mpya ya Bagamoyo katika eneo la Mbegani.

Ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji wakitembelea eneo la 
Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji (EPZA) eneo la ekari 300 la Kamal Industrial Estate mjini Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuangalia maeneo ya uwekezaji.