PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

February 23, 2015

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi PSPTB imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya shahada ya
Ununuzi na ugavi.
Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 16 Februari 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha, ambaye aliwaasa wanafunzi hao wazingatie mafunzo hayo ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti watakazofanya kwa ajili ya kupata shahada ya juu ya ununuzi na ugavi. Aidha, alisisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia maadili katika kufanya utafiti, jambo ambalo ndio msingi na matakwa ya Bodi. wanafunzi wanatakiwa kufanya utafiti wao wenyewe na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine maana kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kujiamini, kuandika ripoti na kujieleza na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuandika, kujieleza na kutoa huduma bora kwa taifa, kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
New Picture (88) 
Mr. Godfred Mbanyi, Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akitoa neno katika ufunguzi wa semina ya utafiti iliyofanyika kwenye ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16/2/2015
New Picture (89)
Mkurugenzi wa mafunzo Mr. Godfred Mbanyi akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence TEsha kufungua semina ya utafiti katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam. Tarehe 16/02/2015
New Picture (90) 
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB na washiriki wa semina ya Utafiti iliyofanyika Katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16/2/2015.
New Picture (91)Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence Tesha(aliyeketi katikati), mwezeshaji wa semina Dr. Eli Tumsifu (aliyeketi kushoto) na Mr. Godfred Mbanyi Mkurugenzi wa mafunzo (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na washiriki wa semina
New Picture (92) 
Washiriki wa Semina ya utafiti wakimsikiliza mwezeshaji Dr. Eli Tumsifu toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwenye semina ya utafiti iliyofanyika katika ukumbi waTEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16-20 Februari 2015
New Picture (93) 
Dr. Eli Tumsifu akiwa na washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB ndani ya ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16-20 Februari 2015
New Picture (94) 
Washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. C. Tesha (aliyeketi katikati), Dr. Eli Tumsifu Mkufunzi wa semina (aliyeketi kushoto) na Mkurugenzi wa mafunzo wa PSPTB Mr. Godfred Mbanyi (aliyeketi kulia) wakati wa semina yautafiti iliyofnyika 16-20 Februari 2015 katika Ukumbi wa TEC Dar es Salaam.
 WATANZANIA ASILIMIA 7.11 HAPA NCHINI HAWANA KAZI

WATANZANIA ASILIMIA 7.11 HAPA NCHINI HAWANA KAZI

February 23, 2015
mah1
Mgeni rasmi kwenye mafunzo ya stadi za kazi na utambuzi wa fursa za kiuchumi zilizopo mkoa wa Lindi Naibu waziri wa kazi na ajira mhe.Dr. Makongo Mahanga (MB) amewataka vijana wa mkoa wa Lindi kuyageuza mafunzo watakayoyapata ya stadi za maisha sanjari na kuzitambua fursa  zilizopo ndani ya mkoa, waweze kujiajiri  na kujikomboa kiuchumi,wakati wa uzinduzi wa mafunzo  hayo ambapo jumla ya vijana 360 kutoka halmashauri sita zilizopo mkoani Lindi wameudhuria kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Mt.Kagwa
mah2
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza washiriki wa mafunzo ya stadi za maisha sambamba na kufahamu fursa za kiuchumu ambapo mpango wa kuendesha mafunzo hayo umebuniwa na yeye mwenyewe,mbele ya mgeni rasmi,wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
mah3
Vijana 360 kutoka kwenye wilaya za Kilwa,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Lindi Mjini na Vijijini ambao ni washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Mhe.Dr.Mkaongoro Mahanga hayupo pichani.
mah4
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza waandishi wa habari jambo mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
mah5
Katibu tawala wa mkoa wa LindiNdg.Abdlla Chikot akijadiliana jambo na wakuu wa wilaya  ya Kilwa kushoto mhe.Abdallah H. Ulega,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Liwale mhe. Ephrem Mmbaga,nje ya ukumbi wa mafunzo wa Mt. Kagwa Lindi.
mah6
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akitoa taarifa ya madhumuni ya ofisi ya mfuko kushiriki kwenye mafunzo hayo kwa waandishi wa habari,ambapo elimu ya faida na umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.(CHF) itatolewa hapo kesho kwa washiriki vijana..
…………………………………………………………………………………
Na .Mwandishi wetu-LINDI
 
NAIBU Waziri wa kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, amesema kuwa hali ya ukosefu wa ajira nchini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi uliofanyika mwaka 2006, jumla ya watu waliokuwa hawana kazi hapa nchini ni asilimia 11.7.
 
Hayo yamebainisha leo na Naibu huyo, kwenye ufunguzi wa semina ya vijana mkoa wa Lindi, na kusema kuwa utafiti huo ulionyesha kuwa takribani asilimia 13.4 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 wa Tanzania hawana kazi kabisa.
 
Alisema ukosefu huo wa ajira kwa vijana ni kubwa zaidi asilimia 26.7 ukilinganisha na vijijini asilimia 7.9 ,imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutofikiwa kikamilifu kwa malengo ya nchi ya kuinua uchumi katika sekta za kilimo, uzalishaji na viwanda.
 
“Wimbi la vijana ambalo ni nguvu kazi ukimbilia mijini na hivyo kupunguza uzalishaji wenye tija kwenye sekta ya kilimo,hivyo kuchangia ongezeko la ukosefu wa ajira mijini sambamba na ongezeko la wafanya biashara wa sekta isiyo rasmi maarufu kwa jina la machinga..Kuendelea kupanuka kwa sekta isiyo rasmi kutoka asilimia 8.8 mwaka 1990/01 hadi asilimia 11.3 mwaka 2005 na kupungua kwa nguvu kazi katika sekta ya kilimo kutoka asilimia 83.7 hadi asilimia 74.6 ni dalili kuwa kuna uhamaji mkubwa wa nguvu kazi kutoka vijijini kwenda mijini.
 
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza, alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwawezesha vijana hao kupata ufahamu na uelewa wa nafasi yao katika jamii, wajibu wa kijana, haki zake na kuwajengea uwezo ambapo watapata stadi za namna ya kutambua fursa zilizowazunguka, na umuhimu wa  kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii hususani mfuko wa afya ya Jamii (CHF) kwani ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu.
 
Mahiza alisema, katika semina hiyo ya siku tano, vijana watapata fursa ya kupitishwa katika mambo mbalimbali, ambapo taasisi mbalimbali zitapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana kuhusu,usalama wa raia na mali zao, Katiba inayopendekezwa na kushiriki wa vijana katika kukuza uchumi.
 RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DAR ES SALAAM

February 23, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana baada ya kumkabidhi hati ya Chuo
Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu
jijini Dar es salaam ag2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati
ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23,
2015 Ikulu jijini Dar es salaam ag3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan
kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es
salaam ag4 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongeqa kwa furaha na
Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea
baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es
salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
ag6 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana tayari kwa  kumkabidhi hati ya Chuo
Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu
jijini Dar es salaam
PICHA NA IKULU
CHUO CHA BIASHARA DAR ES SALAAM (CBE) CHATOA MSAADA WA MASHUKA KWA AJILI YA WODI YA AKINAMAMA NA WATOTO KATIKA HOSPITALI KUU YA MANZIMMOJA

CHUO CHA BIASHARA DAR ES SALAAM (CBE) CHATOA MSAADA WA MASHUKA KWA AJILI YA WODI YA AKINAMAMA NA WATOTO KATIKA HOSPITALI KUU YA MANZIMMOJA

February 23, 2015

Mkuu wa Chuo cha Biashara cha Dar es Salaam Prof. Emanuel Amani Mjema akitoa maelezo kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo  katika hafla ya kukabidhi mashuka katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Zanzibar, kulia ni  Naibu  Mkuu wa Chuo hicho anaeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Dkt. Esther R. Mbise. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Mkuu wa Chuo cha CBE  Prof. Emanuel Amani Mjema akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi msaada wa mashuka uliotolewa na chuo hicho kwa ajili ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. cb4 
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Chuo cha CBE  na baadhi ya maafisa wa Hospitali  ya Mnazimmoja . (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis akiagana na Mkuu wa Chuo cha CBE baada ya kukabidhiwa mashuka kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto  Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

MWADUI FC BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL)

February 23, 2015

Timu ya Mwadui kutoka mjini Shinyanga jana imetawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuifunga timu ya African Sports ya jijini Tanga kwa bao 1 - 0, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Comlex Chamazi jijni Dar es alaam.
Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui ushindi katika mchezo huo wa fainali.
Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni 2.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/205.
Jumla ya timu nne zimepanda Ligi Kuu msimu ujao ambazo ni  Bingwa Mwadui FC, African Sports, Majimaji na Toto Africans.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)