VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI WAFURAHIA MAFUNZO YA URAGHABISHI

December 27, 2015



Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya uraghabishi  yaliyofanyika wilayani hapo
Na Krantz Mwantepele


“Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,” 
Hayo ni maneno ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Loliondo, mwezi Agosti  mwaka huu.
Alisema hayo kwa lengo la kufafanua dhana ya uwajibikaji kwa viongozi kama njia muhimu ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini katika wilaya yake.
Ni dhahiri kwamba viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maeneo husika. 
Kuna nafuu kwa watendaji wa kata na vijiji,  ambao ni waajiriwa wa serikali na hupewa kazi kutokana  na miongozo, lakini siyo kwa wenyeviti wa vijiji na madiwani, wakati mwingine hata wabunge.
Akielezea changamoto hiyo wakati wa mafunzo ya wenyeviti wa vijiji kupitia mradi wa Chukua Hatua yaliyofanyika Septemba mwaka huu na shirika mdau la CABUIPA, mwenyekiti wa kijiji cha Nyakafulu kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Salum Said amesema: 
“Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki, hakika sikufahamu vya kutosha kuhusu majukumu yangu mapya kama kiongozi. Na hii ni changamoto kubwa kwa wenyeviti wa vijiji karibu vyote vya wilaya yetu.” 
Yeye ni mmoja kati ya wenyeviti 200 wanaopatiwa mafunzo katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Simiyu. 
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, katika awamu ya kwanza ya mradi wa Chukua Hatua, nguvu kubwa iliwekwa katika kuwawezesha wananchi kuwachukulia hatua watendaji na viongozi wabadhirifu wa mali za umma. 
Wakati wananchi wakiwezeshwa kuwasimamia viongozi wao, viongozi hawakuwa wakiwezeshwa kutimiza majukumu yao kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi wao.  Hivyo, haja ya kutoa mafunzo kwa viongozi hao ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowachagua, ilikuwa lazima. 
Akielezea umuhimu wa kuwawezesha wenyeviti wa vijiji  wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wenyeviti na watendaji wa kata Julai 2015, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Jane Mutagurwa alisema:
“Kwa muda mrefu wenyeviti mmekuwa mkilalamika kusahaulika kwenye programu zetu za mafunzo, fursa ndio hii imekuja. Tunafahamu kwamba wenyeviti wetu mnakutana na changamoto nyingi za kiutendaji zinazotokana na uwelewa mdogo katika majukumu yenu, hasa kwa wale wanaoingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivyo mtumie mafunzo haya vizuri.” 

Pamoja na umuhimu wa mafunzo hayo kwa viongozi wa ngazi  ya kijiji na kata, bado imekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali kuwawezesha wenyeviti kujua majukumu yao. Na hii inatokana bajeti kuwa na vipaumbele vingine ambavyo halmashauri huwa wamejiwekea katika  kutimiza majukumu yao."
Kwa upande wa Ngorongoro, mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Arusha anaeleza:
“Tangu tulipofanya uchaguzi mwaka jana hatujawahi kutoa mafunzo kwa wenyeviti. Kwa hiyo tunaunga mkono mafunzo haya yanayotolewa na PALISEP yatasaidia sana kwenye kuwawezesha viongozi hawa na watendaji wetu,” 
Kutokana na hali hii, wenyeviti wamekuwa na changamoto za kuelewa mipaka ya majukumu yao, hivyo muda mwingine hujikuta kwenye mzozo na watendaji wa vijiji vyao.  Mwenyekiti anawajibika kwa mwananchi aliyemchagua, wakati mtendaji anawajibika kwa mkurugenzi aliyemwajiri.
Kutokana na tofauti hizo, mafunzo ya sasa ya wenyeviti na watendaji yanaendeshwa kwa pamoja kuwafanya waelewe mipaka yao ya kiutendaji, hivyo kuboresha utendaji wao. 

Afisa Programu wa CABUIPA, Michael Ikila anafafanua: “Tunawafundisha vitu sita muhimu; taratibu za uendeshaji serikali za mitaa, majukumu na haki za  wenyeviti wa vijiji, uwajibikaji na utawala bora,  mamlaka za vijiji, masuala ya fedha, ikiwamo uandaaji wa  bajeti na mawasiliano mazuri baina ya viongozi wa  vijiji.” 
Mada hizi ni kwa mujibu wa mwongozo wa wizara ya Tawala za Mikoa and Serikali za Mitaa (TAMISEMI). 
Majukumu mengine ya wenyeviti hawa ni pamoja na  kuhamasisha shughuli za maendeleo, utawala na  kuhakikisha usalama wa watu katika maeneo yao kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji. 
Kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro, hii ni mara ya kwanza kwa wenyeviti kufundishwa majukumu yao. Mwanzoni mafunzo haya yaliwalenga madiwani ambao kimsingi hawakuyapenda kwa sababu ya kutokuwapo kwa posho. Hivyo mafunzo yao yakaamishiwa kwa wenyeviti wa vijiji ambao walipokea mwaliko kwa furaha pasipo kudai posho.
“Mafunzo haya yatatusaidia kuboresha mahusiano na utendaji wetu. Mara kadhaa unakuta wenyeviti wanaingilia mipaka yetu ya kazi, hivyo kuathiri uhamasishaji wa shughuli za maendeleo. Na hii hutokea pale mwenyekiti mpya anapotaka kuwaonyesha wapigakura wake kwamba mwenzake aliyepita hakufanya kazi,” anaelezea mmoja wa watendaji wa kijiji aliyehudhuria mafunzo hayo.
Pamoja na changamoto hizo, bado washiriki ambao ni wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wamekiri kwamba mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kumaliza tofauti zinazojitokeza baina yao. 
Lakini si hivyo tu, viongozi wa wilaya wameonyesha kuunga mkono mafunzo hayo kwa kuwa yanasaidia kuhamasisha wananchi kutimiza majukumu yao.
Lakini pia viongozi hao walionyesha umuhimu wa kufikia wajumbe wengi zaidi ya halmashauri za serikali ya kijiji. Kwa mfano, wakati akizungumza na wakufunzi kwenye ofisi yake, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, alisema:
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ina jumla ya vijiji 117 vyenye wajumbe 2,925. Kwa mantiki hiyo, mafunzo haya yanayoendeshwa kupitia mradi wa Chukua Hatua yamefikia asilimia 4 tu ya wajumbe wanaounda uongozi wa serikali za vijiji, hivyo wengi bado wanahitaji mafunzo. Katika mazingira hayo, mkurugenzi alitoa ombi maalumu la kusaidiwa kuwawezesha wakufunzi 25 wa wilaya watakaotoa mafunzo kwa wajumbe wa halmashauri za vijiji hivyo. Gharama za wakufunzi hawa kuwafikia wajumbe wengine zitakuwa ni za serikali. 
Na huu ni ushirikiano unaotakiwa baina ya sekta ya umma na binafsi kwa kuwa ni jukumu letu sote kwa mustakabali wa maendeleo yetu. 

WAWEKEZAJI KATIKA MIGODI TANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAKAZI WAISHIO MAENEO HAYO ILI KUPUNGUZA MIGOGORO.

December 27, 2015


Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo.

Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.  Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini.  Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo.

Mgodi huo unazungukwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mwendakulima, Mwime na Chapurwa.  Lakini kutokana na hali halisi kumekuwa na kelele nyingi za manung’uniko toka kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo hayo kuachwa bila maendeleo yoyote wakati wageni wanachukua madini kwa kiwango ambacho hakijulikani.“Kitu kingine uwepo uwazi waweke uwazi katika haya masuala ya madini mapato wamepata kiasi gani wawekezaji na serikali yenyewe imepata kiasi gani, ikibidi hata kwa wale wananchi wanaozunguka mgodi huu au migodi mingine ya Tanzania. Waweze kuwa  wanawabandikia kwamba mwezi huu mgodi umeingiza kipato hiki na serikali imepata hiki angalau kidogo inaweza kupunguza manung’uniko. Kwa watanzania wengine ambao wanaishi sehemu ambapo hapana madini wapeleke hata kwenye magazeti matangazo ya mapato,” anafafanua mkazi wa Mwime.Haya yamejiri kwenye mda- halo uliondaliwa na waraghabishi wa Chukua Hatua toka kijiji cha Mwime. Ambapo wananchi walipata fursa yakuchangia mawazo kama madini ni laana ama neema. Katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika shule ya sekondari ya Mwendakulima washiriki toka kada mbalimbali za kijamii Kama wachungaji, mashekhe, wakulima, walimu, watendaji wa vijiji, wanafunzi na waandishi wa habari walipatafursa ya kuchangia mawazo yao kama madini ni laana ama neema. Mwanafunzi wa kike toka katika shule ya sekondari ya Mwendakulima yeye aliona kwamba madini yanaweza yakawa ni janga la mazingira pale aliposema kwamba, “Suluhisho jingine angalau wangebadilisha mfumo wa uchimbaji, kwa sababu mfumo wanaotumia ule yaani kadri siku zinavyokuja kutakuwa na janga kubwa sana, angalia udongo uliofika pale huku chini kuna nini.”   Ukiacha changamoto ya mazingira, suala jingine lililojitokeza ni athari zinazoletwa na kemikali mbalimbali ambapo mwalimu mraghabishi

Paul Chui wa shule ya msingi Mwime alisema,  “Kwa kweli kutokana na sera  ya elimu, bado tunafundisha elimu kwa kuzingatia sera ya elimu. Hivyo kwa mimi kama mwalimu najitahidi sana kuwaelekeza wanafunzi kuhusu suala zima la athari za kemikali kama vile sunlight pamoja na mekyuri.”  Wakati washirki wengine waliojitokeza wao walielezea tatizo la kiungozi na mikataba mibaya. Katika kuelezea tatizo hilo walielezea usiri uliopo kwenye mikatabana hivyo kushauri wananchi kuhusisha siasa na mali zao  kwa kuhakikisha kwamba wakati wa kupiga kura ni wakati sahihi wa kudhibiti maliasili za umma kwa kuchagua viongozi wanaofaa.  Mapungufu katika sera pamoja na sheria za madini ni moja ya sababu zilizotajwa kufanya  madini yaonekane laana kwa wananchi wanaozunguka migodi hiyo.
 Katika maelezo yake kwa washiriki, George Kingi ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Mwime alisema, “Kuna mapungufu kwenye sheria zetu hata ungemweka leo mwingine hata kila siku kama sheria  hujaiboreshwa bado unarudi kulekule kwa hiyo suala la sheria lifanyiwe marekebisho. Kingine ni sera.  Sera kama haisemi Mwime waachiwe  asilimia fulani, hata ungemleta mwingine kesho na mwingine atakwamishwa na sera ambayo haisemi wanamwendakulima mbaki na nini.”  Katika hili ushauri uliotolewa ni wa kukaa vikao wananchi wanatakiwa kutoogopa na wanapokaa kwenye vikao kweli wasema.

Kwa kuwa kama kuna watu wa kupiga  kelele kule juu sheria na sera zibadilishwe na zikabadilishwa basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama anavyomalizia George,  “Ukishabadilisha sheria na sera hata maji Mwime unayapata hata gari unaletewa si sera inasema uletewe gari kama sera haisemiutaletewa gari?” Akitoa majumuisho ya mdahalo huo uliondaliwa na waraghabishi walimu na wakulima Toka kijiji cha Mwime, mwenyekiti Maimuna Said alisema  “Madini sio laana lakini viongozi wenyewe ni laana kwa sababu hawatendi haki ipasavyo kulingana na katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania. Hii ni neema toka kwa Mungu.”   Suala jingine ambalo limejitokeza katika mdahalo huo ni wananchi kutokuwa na furaha jinsi ambavyo serikali haiwashirikishi katika  kufanya maamuzi muhimu yanayohusu mustakabali wa maeneo yao. Hivyo ili madini yasiwe laana ni muhimu sana kwa serikali kuwashirikisha wananch toka hatua za mwanzo.

Lakini pia suala zima la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.  “Kuna haja kubwa ya kutolewa elimu hususani elimu ya uraia. Watu kwanza watambue haki zao, mtu akishatambua haki zake kuna kuwa na uwezekano wa yeye kuzidai, lakini kama watu bado hawatapata elimu hiyo ni kwamba watu watakuwa wananung’unika tu pembeni. Lakni hajui aanzie wapi na hajui aishie wapi,” anafafanua Maalim Daudi Athman Imamu wa Masjid Noor Nyandekwa.
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com

Tigo yagawa simu 200 kwenye “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” Rufiji

December 27, 2015
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na kushoto kwake ni  Dkt. Flora Myamba Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA.


Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”



Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya vyeti watakavyopewa kinamama  walioshinda shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.  




 Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”





Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.


Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.



  

  • Itashirikana na  REPOA, CARE INTERNATIONAL & KIDOGO KIDOGO

Rufiji, Desemba 23, 2015: Tigo imetoa simu za mkononi 200 ambazo zitasambazwa kwa wanawake maskini ambao hawana uwezo wa kununua simu katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, lengo kuu likiwa ni kuziba pengo la kijinsia katika umiliki wa simu Tanzania.
Usambazaji wa simu hizo upo chini ya programu inayojulikana, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” utafanyika kwa kushirikiana na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.  
Akizungumzia zoezi hilo Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, alisema kwamba mtazamo wa Tigo uko kwenye sera za kampuni ya kuwawezesha watu walio na kipato duni ndani ya jamii katika kuzipata simu za mkononi.
“Tigo  inadhamiria kuboresha muunganisho wa simu za mkononi nchini Tanzania  hususani miongoni mwa wanawake  ambao kimsingi wana uwezo mdogo wa kupata simu,” alisema Bi.Thomas na kuongeza, “Ni matumaini yetu kwamba  kwa kusambaza simu hizi kwa wanawake maskini katika wilaya ya Rufiji, Tigo itakuwa imechangia kupunguza  pengo la kijinsia katika umiliki wa simu nchini.”
 Thomas alisema kwamba Tigo imewekeza zaidi ya dola 30,000 ambazo zitatumika kusambaza  pamoja na kuangalia tathmini ya matokeo ya mradi. Aliongeza kwamba washirika watatu REPOA, CARE International na KIDOGO KIDOGO kwa pamoja wataongoza utekelezaji huo wa usambazaji wa simu kwa kutoa laini ya simu pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya mradi.
“Pengo lililopo la kijinsia katika kuifikia teknolojia ya simu linaweza kukwaza Tanzania katika mchakato wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika kukuza usawa kijinsia na kuwawezesha wanwake nchini na ndio maana Tigo inachukua hatua za kuunga mkono mradi huu,” alisema Bi.Thomas.
 Kwa mujibu wa Bi. Thomas mradi huo unalenga kuwanufaisha watu 500 katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 na inakuwa ni mara ya pili kwa Tigo  kusambaza simu za mkononi kwenye mkoa huo kwani mara ya kwanza ilikuwa amwaka 2014. 


WATOTO WA WAHADHIRI WA UDSM WAJUMUIKA PAMOJA KWENYE 'GET TOGETHER' YA NGUVU

December 27, 2015

Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu. Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha maana watu walikuwa wanakumbushana mambo ya miaka ya 90 kwani kipindi hicho walikuwa wadogo.
Watoto wakiendelea kucheza wakati wa party ya watoto walioishi chuoni hapo kipindi wazazi wao bado ni waalimu katika chuo cha UDSM
Full Happy kwa kila tu aliyefika katika Party hiyo.
Watoto wa wahadhiri wa UDSM wakibadilishana mawazo kwenye party ya kuwaunganisha pamoja kama wanafamilia wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Hakika watoto walikuwa waki-enjoy vya kutosha maana hakuna aliyeboreka kwani kulikuwa na kila aina ya michezo kwa watoto wa rika zote.

Baadhi ya watoto wakiwa wametokelezea kwenye ukodak.

Baadhi ya watoto walioishi Chuoni UDSM wakiangalia vitabu pamoja na kununua vitabu hii ikiwa ni kundeleza utamaduni wa kujisomea.
Hakika ilikuwa shangwe kwa watoto walioishi chuoni hapo wakati wazazi wao ni wahadhiri chuoni hapo
Hivi ni Baadhi ya vitabu vilivyokuwa vinauzwa wakati wa Party hiyo iliyofanyika chuoni hapo.
Muda wa kuserebuka ulifika sasa kila mtu akaanza kuonesha umahiri wake kwenye kulisakata Rhumba.
Watoto wa Chuo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza party yao.