MAREFA NA KATIBU ZFA WAITWA KUHOJIWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

June 04, 2015

Na Abdallah Salum, ZANZIBAR
SIKU mbili baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa zinazowakabili maofisa sita wa shirikisho hilo, kadhia ya rushwa imetinga katika soka la Zanzibar.
Jana, Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, imewaita na kuwahoji waamuzi watatu wa mpira wa miguu pamoja na Katibu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali kufuatia taarifa kwamba wamehusika na kupokea hongo.
Watu hao wanadaiwa kujipatia shilingi 110,000 kwa njia ya rushwa ili waipe nafasi  ya tatu timu ya Chuo cha Utumishi wa Umma (IPA) kwenye mashindano ya vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu yaliyofanyika mwezi uliopita.
Mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma katika mamlaka hiyo Shuwekha Abdallah Omar, akiwa ofisini kwake Mnazi mmoja, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni waamuzi, Mzee Nuhu Ali, Abdulrahman Mahfoudh na  Mohammed  Ali  Mohammed.
Aidha amemtaja Katibu Mkuu wa ZFA Wilaya ya Mjini, Yahya Juma Ali.
Ofisa huyo alisema mamlaka yake iliwakamata watuhumiwa hao ndani ya ofisi ya ZFA iliyoko katika uwanja wa Amaan, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema  siku moja kabla ya kukamatwa kwao.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu Zanzibar (ZAHLIFE) Abdallah  Abdulrahman Mfaume, alisema jumuiya yao haijahusika na lolote kuhusiana na  rushwa katika mashindano hayo.
Hata hivyo, ametaka watu waliohusika na kadhia hiyo wachukuliwe hatua zinazostahiki.
Hadi mwandishi wa habari hizi akiondoka katika ofisi za ZAECA, watuhumiwa hao walikuwa wanaendelea kuhojiwa.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

June 04, 2015

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni ,
Seif Khatib. Picha na OMR
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
9
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
10 11 12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanachama wa CCM na wanahabari, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kuwania urais.
14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomy za kusaka wadhamini, mmoja kati ya vijana waliojitolea kusambaza fomu za kutafuta wadhamini, Saada Ilasi, baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.

WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA VIWANDA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WANAOKUSANYA TAARIFA ZA SENSA YA VIWANDA NCHINI.

June 04, 2015

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. Kushoto kwake ni Idd Mruke, Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mkoa wa Dodoma.
 Meneja wa Takwimu za Biashara na Utalii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambaye ni Msimamizi wa Sensa ya Viwanda nchini akiwaelezea waandishi wa habari leo mkoani Dodoma kuhusu vigezo vilivyotumika katika kuchagua sampuli ya viwanda vilivyochaguliwa kufanyiwa utafiti. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza nao leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. 

Na Veronica Kazimoto,
Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wasimamizi na wadadisi wanaokusanya taarifa za Sensa ya Viwanda inayoendelea hapa nchini.
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dododoma ambapo amesema ukusanyaji taarifa kwa nchi nzima umefikia wastani wa asilimia 80.5.
"Hadi kufikia tarehe 24 Mei, 2015 jumla ya viwanda vidogo 9,540 sawa na asilimia 82 pamoja na viwanda vya kati na vikubwa 1,158 sawa na asilimia 79 vilikamilika kukusanywa taarifa zake. Hii inafanya ukusanyaji Takwimu kwa nchi nzima kuwa wastani wa asilimia 80.5", amesema Dkt. Kigoda.
Aidha, Waziri Kigoda amesema licha ya mafaniko hayo, bado kuna kazi kubwa ya kukamilisha viwanda vilivyobaki ambavyo ni takriban 2,032 sawa na wastani wa asilimia 19.5.
"Hivyo, nawaasa wamiliki wote wa viwanda hususani katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Morogoro, Tabora, Kigoma na Manyara kutoa ushirikiano zaidi na wa kutosha kwa zoezi hili ili ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni, 2015, tuweze kuhitimisha", amesisitiza Dkt. Kigoda.
Waziri Abdallah Kigoda amesema lengo kuu la Sensa ya Viwanda ni kukusanya takwimu sahihi zinazohusu Sekta ya Viwanda nchini ambazo zitawezesha kupata viashiria sahihi vya uchumi pamoja na taarifa muhimu za viwanda kama vile orodha ya viwanda kimkoa, anuani na mahali vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa wamiliki.
Taarifa nyingine ni pamoja na  mwaka ambao viwanda hivyo vimeanza uzalishaji, shughuli kuu ya viwanda husika, idadi ya wafanyakazi, gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaji na gharama za uzalishaji.
Lengo lingine la Sensa ya Viwanda ni kupima na kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Viwanda ili kuiwezesha Serikali kuboresha sera na programu za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya Tanzania, 2025, Malengo ya MKUKUTA na Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
Jumla ya Wadadisi 198 wameajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kukusanya Takwimu na taarifa viwandani ambapo wanasimamiwa na Mameja Takwimu wa Mikoa, Watakwimu kutoka Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Maafisa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA, ONEL MALISA JIJINI DAR

June 04, 2015

Mwili wa Marehemu, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza tayari kwa zoezi la kuagwa Kijeshi katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye ameagwa leo Kijeshi Juni 04, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwa mazishi kwao Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiwa amesimama wakati mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ulipokuwa ukiwasili katika Viwanja vya Chuo Cha Maafisa Magereza Ukonga(katikati) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kulia) ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu.
Kiongozi Mwakilishi wa Wastaafu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka akitoa salaam za rambirambi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo kabla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu Onel Malisa.
Gadi Maalum ya Maafisa wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya paredi la kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini salaam mbalimbali za rambirambi zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa.
Umati wa ndugu na Jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.

TASWIRA MBALIMBALI ZA ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI FINLAND NA SWEDEN.

June 04, 2015

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzomna Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mahojiano na wanahabari jijini Helsinki, Finland.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Mari Kiviniemi, Waziri wa Masuala ya Nje wa Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa hashima yake jijini Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mabalozi wa sasa na wa zamani waliopata kuiwakilisha Finland nchini Tanzania
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Finlan
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyabiashara wa Finland pamoja na washirika wao wa Tanzania baada ya mkutano wao jijini Helsinki, Finland
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha METSO cha  kutengenezea vipuli vya mitambo ya gesi na mafuta katika jiji la Helsinki, Finland.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa Kitanzania aishiye Sweden Bw. Charles Njau alipomutana na  Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa katika tiu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia anaedeesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa 16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA  katika makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm

FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI KUZINDULIWA KESHO NA MAKAMU WA RAIS,DKT GHALIB BILAL.

June 04, 2015

KAIMU AFISA UHUSIANO WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA( TANGA UWASA) AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA MKURUGENZI WA MAMLAKA HIYO MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA LEO KATIKA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI LEO KUHUSU UZINDUZI WA FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI





MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA (TANGA UWASA) MHANNDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI UTAKAOFANYIKA KESHO NA MAKAMU WA RAIS DKT GHALIB BILAL
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA (TANGA UWASA) MHANNDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI UTAKAOFANYIKA KESHO NA MAKAMU WA RAIS DKT GHALIB BILAL



MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA (TANGA UWASA) MHANNDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA FILAMU YA MAMBA WA MTO ZIGI UTAKAOFANYIKA KESHO NA MAKAMU WA RAIS DKT GHALIB BILAL