BENKI YA NMB YAZINDUA HUDUMA MAALUM KWA WASTAAFU

BENKI YA NMB YAZINDUA HUDUMA MAALUM KWA WASTAAFU

October 16, 2023



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi – Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akizindua rasmi mpango maalumu kwaajili ya Wastaafu na Wastaafu watarajiwa wa Benki ya NMB uitwao NMB Hekima Plan, katika hafla maalum iliyofanyika katika Ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma. Watatu kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi na Mauzo wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wapili kushoto), mwakilishi wa Wastaafu, Mzee Martine Chiwaligo (wapili kulia), Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa benki hiyo, Aikansia Muro (kulia).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) katika picha ya pamoja na wageni waalikwa ambao ni Wastaafu na Wastaafu watarajiwa, baada ya kuzindua rasmi mpango maalumu wa NMB Hekima Plan katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

……………………………


Benki ya NMB imeanzisha mpango maalum wenye masuluhisho mahususi kwaajili ya kuwahudumia Wastaafu na Wastaafu watarajiwa unaoitwa NMB Hekima Plan wenye Kauli Mbiu “Staafu Kifahari”

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha Wastaafu na Wastaafu watarajiwa zaidi ya 400 jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwaandaa kukabiliana na changamoto za maisha baada ya ajira, Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali wa benki hiyo, Bi. Vicky Bishubo alieleza kuwa, masuluhisho yaliyomo kwenye NMB Hekima Plan ni pamoja na mikopo mbalimbali ikiwemo ile ya nyumba, ambapo mkopaji anaweza kupata hadi Tsh. bilioni 1.

Kupitia utaratibu huu, wastaafu watapewa pia elimu ya ustawi wa afya na usalama wa fedha zao huku wakionyeshwa fursa mbalimbali za uwekezaji. Lakini pia, NMB Hekima Plan ina bima za afya na mali za gharama nafuu na bei shindani sokoni.

Zipo pia Akaunti maalumu zisizokuwa na makato ya mwezi ambazo zinampa nafasi mstaafu kupata mkono wa pole wa hadi Tsh milioni 2 endapo yeye au mwenza wake atafariki na kumwezesha kupata kiasi kama hicho akipata ulemavu wa kudumu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa program hii, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako aliipongeza Benki ya NMB kwa kuja na utaratibu huu ambao lengo lake kubwa ni kusaidia kuenzi mchango mkubwa wa watumishi hawa katika ujenzi wa taifa.
- Advertisement -


Aliongeza kuwa pia ni suala la thamani na azma ya Serikali kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii na kuhakikisha kuwa Wastaafu si tu wanaishi maisha bora na ya Furaha, lakini pia kuhakikisha wanaendelea kuchangia juhudi za ujenzi wa taifa.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii na kuboresha mazingira ya uwekezaji nchni, ili wastaafu waweze kuchangamkia fursa zinazoletwa na taasisi za fedha kama huu mpango wa NMB Hekima Plan,” Prof Ndalichako alisema.

Akisisitiza umuhimu wa wastaafu kuwa na nidhamu ya fedha na matumizi ya pensheni zao, Waziri alibainisha kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali kuiimarisha sekta hiyo ni pamoja na kuboresha mifuko ya hifadhi ya jamii na utoaji wa huduma kwa ujumla.

Aidha, alisema uwekezaji unaofanywa kubuni masuluhisho ya kidijitali na Benki ya NMB yatasaidia si tu kuwahudumia wastaafu lakini pia upatikanaji wa huduma kwa watu wote na kuwasihi Wastaafu kuzingatia mafunzo na maarifa watakayopewa na wataalum ili waweze kuzikabili changamoto hizi. Zoezi la kutoa elimu litafanyika kwa Wastaafu litafanyika nchi nzima.

NIC KUENDELEA KUBORESHA NA KUBUNI HUDUMA MPYA ZA BIMA

NIC KUENDELEA KUBORESHA NA KUBUNI HUDUMA MPYA ZA BIMA

October 16, 2023








Na Sophia Kingimali

Shurika la Bima la taifa NIC katika kutimiza miaka 60 limesema litahakikisha linaendelea kuboresha huduma zake kwa kubuni huduma mpya lakini kushirikiana zaidi na jamii ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mmoja.

Hayo ameyasema leo Oktoba 16, 2023 mtendaji mkuu wa NIC Elirehema Doriye wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kilichowakutanisha na watendaji wakuu wa timu ya yanga na wachezaji.

Amesema maadhimisho ya miaka 60 ya shirika hilo yamekua ya manufaa makubwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima.




“Leo tunaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo tunajivunia mafanikio makubwa ambayo tumeyapa kwa kipindi chote lakini pia tumekuja na mikakati itakayosaidia katika kuandaa miaka mingine 60 ijayo”amesema Doliye.

Amesema moja ya vipaumbele ambavyo wameviweka ni kuhakikisha wanawekeza kwenye TEHAMA kwa kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni huduma ambazo zitabaki kwenye mioyo ya wateja kwani itakuwa kampuni ya kwanza kutumia akili bandia katika utendaji wake.

Amesema wataendelea kukuza biashara ndogo ndogo kwa kwa kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Doriye ameongeza kuwa kuunga mkono vipaumbele vya serikali ikiwemo katika sekta ya kilimo kwa kutoa Bima ya kilimo.

Sambamba na hayo Doriye amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo katika sekta ya Afya na mazingira.

“Hii ni Bima ya wanachi na tupo kwenye maazimisho ya miaka 60 lakini pia kuandaa miaka 60 ijayo tumejidhatiti kutoa elimu kwa wananchi lakini kushirikiana na wananchi hivyo tutakua na mabonanza mbalimbali ya michezo yatakayohusisha sekta binafsi na serikali wakiwemo waandishi wa habari”ameongeza Doriye.

Amesema wanatarajia pia kufanya mazungumzo ya kitaaluma ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kuandaa video yenye historia ya Bima.

Aidha Doriye ameongeza kuwa yote watakayoyafanya kama maazimisho ya miaka 60 watashirikiana na timu ya mpira wa miguu ya Yanga.

Nae,Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga Andre Mtine ameishukuru NIC na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kushirikia katika shughuli za kijamii ikiwa kama sehemu ya kutoa elimu.

“Sisi kama Yanga tunafurahia kuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya NIC kwani hii ni taasisi ya kwanza ya Bima na inafanya vizuri sana sisi tunaahidi kushirikiana nao”amesema mtine.
WAZIRI NDUMBARO AIAGIZA BMT ISIMAMIE MICHEZO KUONGEZA PATO LA TAIFA

WAZIRI NDUMBARO AIAGIZA BMT ISIMAMIE MICHEZO KUONGEZA PATO LA TAIFA

October 16, 2023




NA Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitasaidia kuongeza Pato la Taifa kupitia Sekta ya Michezo.

Mhe. Ndumbaro amesema hayo wakati wa kikao na Baraza hilo kilichofanyika Oktoba 16, 2023 jijini Dar es salaam ambapo ameliagiza lisaidie Vyama na Mashirikisho ya Michezo kupata ushirikiano na Vyama wenza nje ya nchi hatua itakayoviwezesha vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika Utawala na uendeshaji wa shughuli za Vyama hivyo.

“BMT pitieni muundo wa uendeshaji michezo kuanzia ngazi ya Mikoa hadi vijiji, michezo iwe ni biashara na ajira, ifike wakati Vilabu vijue idadi ya wanachama wao kwa kuzingatia jinsia ili iwasaidie kujua idadi ya waliyonayo na namna ya kuongeza wanachama wapya” amesema Mhe. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro ametumia nafasi hiyo kuviasa Vyama na Mashirikisho viepuke migogoro ya mara kwa mara badala yake vizingatie Katiba zinazoongoza na kuzingatia Utawala Bora.

Awali, Katibu Mtendaji wa Barza hilo Bi. Neema Msitha amesema Baraza limeendelea kupata mafanikio mbalimbali kwa Timu za Taifa kupitia ufadhili wa Serikali chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo kufika mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia kwa Timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 pamoja na Timu ya Walemavu.

Bi. Neema ameongeza kuwa kwa sasa Baraza hilo linatumia mfumo wa Kidigitali kusajili Vyama na Mashirikisho ambao umerahisisha gharama na muda wa kufanya Usajili.

  UVUMI WA TAARIFA ZINAZOZUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) KUHUSU UWEPO WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAYAI, KATA YA GOBA, WILAYA YA UBUNGO MKOA WA DAR ES SALAAM

UVUMI WA TAARIFA ZINAZOZUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) KUHUSU UWEPO WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAYAI, KATA YA GOBA, WILAYA YA UBUNGO MKOA WA DAR ES SALAAM

October 16, 2023

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

Telegramu: “Mifugo”

Simu: 255 026 2322610

Tovuti:www.mifugouvuvi.go.tz

Baruapepe: ps@mifugo.go.tz

 

 

 

 

 

Mji wa Serikali Mtumba,

       S. L. P. 2870,

       DODOMA.

 

 
 


 

 

 

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Dar es Salaam, Oktoba 16, 2023

 

UVUMI WA TAARIFA ZINAZOZUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) KUHUSU UWEPO WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAYAI, KATA YA GOBA, WILAYA YA UBUNGO MKOA WA DAR ES SALAAM

 

Ndugu wanahabari,

 

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inakanusha taarifa za uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam ambazo zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii. Wizara inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa imefuatilia suala hilo kwa kina na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli, ni upotoshaji na hivyo kuitaka jamii  kuipuuza.

 

Ndugu wanahabari,

 

Kuanzia tarehe 12 Oktoba 2023 kumekuwa na picha ya mayai mengi na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam. Picha hiyo imeambatana na maneno “Serikali Hailali Kama alivyo Shetani Halali!! Wanajua kabisa Kwa sababu Shetani Halali kwa hiyo Kuna Mambo Mabaya atayatenda tu!! Kiwanda Cha mayai Goba Kwa wachina kimekamatwa Sasa hayo Mayai Yote Sijui yametagwa na Kuku Gani? Tusubiri yanayojiri, Usikie Technologia ilivyo hapo Ndiyo utakapojua Kwa nini kila Mtu Ana Kitambi”.

 

Taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu tasnia ya kuku nchini inayokuwa kwa kasi. Katika kufuatilia zaidi, Wizara imebaini kuwa picha hiyo ya mayai mengi iliyotumiwa ilionekana kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2016 na haikupigwa hapa nchini.

 

Ndugu wanahabari,

 

Vilevile, kuna kipande cha video (video clip) ya kijana anauza mayai ya kuchemsha ambayo yana viini viwili ambapo baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wanasema mayai haya yanatengenezwa viwandani na yanaweza kuwa hatarishi kwa afya ya binadamu. Mayai yenye viini viwili hayatengenezwi viwandani bali yanatagwa na kuku kama kawaida. Sababu zinazopelekea yai kuwa na viini viwili ni pamoja na:

 

(i)        Umri wa kuku, mara nyingi hutokea kwa kuku wanaoanza kutaga au wanaomalizia umri wa kutaga;

(ii)      Chakula: Wakipewa chakula chenye virutubisho vingi kuku huweza kuwa na mayai yenye viini viwili;

(iii)    Kuwasisimua kuku kwa mwanga (overphotostimulation);

(iv)    Aina ya kuku (genetic effects).

 

Ndugu wanahabari

 

Viini viwili kwenye kuku ni sawa na ilivyo mapacha kwa wanyama wengine. Kinachotekea hapa ni kuwa kampuni za vitotoleshi vya vifaranga hazipendelei kutumia mayai yenye viini viwili kwa kuwa mayai haya huwa mara nyingi hayaanguliwi, au hata yakianguliwa vifaranga vitakavyopatikana vinakuwa na uzito mdogo sana au vinakuwa na ulemavu. Hivyo, kampuni hizo huyabagua mayai yote yenye viini viwili na kuyauza kama mayai ya chakula kama ilivyoonekana kwenye kipande cha video. Nipende kuwatoa wasiwasi walaji wa mayai haya kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu. 

 

Ndugu wanahabari,

 

Naomba kumalizia kuwa uzushi uliojitokeza kutokana na kusambazwa kwa uwepo wa taarifa ya kiwanda cha kutengeneza mayai ni upotoshaji na unapaswa kupuuzwa. Serikali inafuatilia kwa kina aliyeanzisha uhalifu wa taarifa hii na akipatikana Sheria itachukua mkondo wake.

 

Asanteni kwa kunisikiliza

 

Imetolewa na

Prof. Hezron Emmanuel Nonga

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo,

Wizara ya Mifugo na Uvuvi,

Simu: 0767238174

Barua pepe: hezron.nonga@mifugo.go.tz

Shirika la JHPIEGO laendesha mbio za hisani kuchangisha fedha za ujenzi wa wodi ya watoto njiti

October 16, 2023

 

Shirika la JHPIEGO Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Molles limeendesha mbio za hisani za 'Miles For Mothers' ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya Kwimba mkoani Mwanza.

Mbio hizo za kilomita tano, na kilomita kumi zimefanyika Jumapili Oktoba 15, 2025 katika Jiji la Mwanza na Jiji la Dar es salaam ambapo lengo ni kukusanya kiasi cha shilingi milioni 150 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa mbio hizo, Mganga Mkuu Mkoa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha zaidi huduma za mama na mtoto hususani kwa watoto njiti na hivyo kuokoa maisha ya watoto hao.

Amesema jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO pamoja na taasisi ya Doris Mollel zitasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma za watoto njiti katika Wilaya ya Kwimba huku mkakati ukiwa ni huduma hizo kupatikana kila wilaya.

Naye Mshauri Mwandamizi wa shughuli za utekelezaji wa mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAH, Dkt. Riziki Ponsiano amesema fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizo zitasaidia kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo hadi kukamilika litagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akizungumza kwa ni baya ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Mohamed Mtulyakwaku amesema ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya Kwimba utaondoa adha iliyopo ikiwemo kuwasafirisha umbali mrefu hadi Hospitali ya Kanda Bugando.

Katika mbio hizo, washindi wa kilomita tano na kumi wamekabidhiwa medali na vyeti kama sehemu ya kutambua ushiriki wao katika jitihada za kuokoa maisha ya mama na mtoto hususani watoto njiti.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Washiriki wakijiandaa na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizofanyika jijini Mwanza.
Mmoja wa wakimbiaji wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikimbiza upepo jijini Mwanza.
Washiriki wakikimbiza upepo kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizofanyika jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikata upepo jijini Mwanza.
Mshiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' akikata upepo.
Mmoja wa washiriki wa mbio za 'Miles For Mothers' akikimbiza upepo.
Washiriki wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' 2023 jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea na mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizoandaliwa na shirika la JHPIEGO kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Mollel ili kushangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiendelea na mbipo za hisani za 'Miles For Mothers'.
Washirikiwa wakiwa kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zenye lengo la kushangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiwa kwenye mbio za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo katika mbio za hisani za 'Miles For Mothers' zilizoandaliwa na shirika la JHPIEGO kwa kushirikiana na taasisi ya Doris Molles ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Wilaya Kwimba.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers'.
Washiriki wakiwa kwenye mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Washiriki wakiendelea kukimbiza upepo.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa washindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' umbali wa kilomita tano, jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (wa tatu kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' umbali wa kilomita tano jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba, Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba- Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba, Mohamed Mtulyakwaku (kushoto) akikabidhi cheti kwa mshindi wa mbio za hisani za 'Miles For Mothers' jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Washindi wa mbio za kilomita tano na kilomita kumi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

Umati Mkubwa Wa Samia Tishio Kwa Upinzani 2025

October 16, 2023

 * Azoa mafuriko ya watu kwenye ziara zake mikoani


* Abomoa ngome ya Lissu Mkoa wa Singida

Na Mwandishi Wetu, Singida

Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka kuwa tishio kubwa kwa vyama vya upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025 kutokana na umati mkubwa wa watu anaovutia katika ziara zake za mikoani.

Popote aendapo kwenye ziara zake za mikoani, Rais Samia amekuwa analakiwa na umati mkubwa wa watu na kuwafanya wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini kutabiri kuwa Rais Samia atashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Kada mbalimbali za wananchi, ikiwemo madereva vijana wa bodaboda, kina Kama Lishe, wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wamekuwa wanajitokeza kwa wingi kupokea Rais Samia kwa umati ambao haujawahi kutokea.

Ingawa bado ni mapema na Rais Samia mwenyewe hajatangaza hadharani kuwa atagombea urais 2025, lakini Rais Samia anaonekana kwa sasa kuwa ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika vyama vyote vya siasa nchini na ni turufu kubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na sasa katikati ya Tanzania kwenye mkoa wa Singida, Rais Samia amekuwa anavutia umati mkubwa wa wananchi wenye shauku ya kumuona, huku wakimshangilia.

Umati mkubwa wa maelfu ya watu umekuwa ukijaza viwanja vya mipira, mikutano ya hadhara na hata barabarani Rais Samia anaposimama kuwasalimia wananchi.

Akiwa mkoani Singida jana ambayo zamani ilikuwa ni ngome ya Tundu Lissu wa Chadema, Rais Samia amepokelewa na maelfu ya wananchi katika kijii anachotokea Lissu, kwenye kata ya Mahambe.

Wananchi hao waliongozwa na Suleiman Mohamed, Mzee wa kijiji anachotokea Lissu, Jackson Mghwai Muro, Baba Mdogo wa Lissu na Thomas Kongoro, Baba Mkubwa wa Lissu.

Wazee hao walitangaza hadharani kumuunga mkono Rais Samia kwa kuleta maendeleo makubwa kwenye kjiji chao tangu alipoingia madarakani na kumkemea mtoto wao Tundu Lissu kwa kufanya siasa za mfarakano na kutumia lugha za matusi na kejeli dhidi ya viongozi wa nchi, kinyume na utamaduni wa Tanzania.

Wananchi wengi wameonesha kuvutiwa na uongozi mahiri wa Rais Samia tangu aliposhika madaraka Machi 2021 baada ya kifo cha Rais John Magufuli.

Akiwa Rais wa kwanza mwanamke wa Afrika Mashariki, Rais Samia ameliongoza taifa kwa ushupavu mkubwa kwenye kipindi cha mpito baada ya kutokea kifo cha Rais wa kwanza nchini akiwa madarakani.

Pia, Rais Samia alishika uongozi wakati nchi imekumbwa na janga hatari la COVID-19 na akaonesha ujasiri mkubwa kukabiliana na changamoto hiyo ya dunia huku akiwashangaza watu wengi kwa uongozi wake usiotetereka.

Kwenye uongozi wa Rais Samia, siyo tu aliendeleza bali aliongeza kasi ya miradi yote mikubwa ya maendeleo aliyoikuta chini ya Magufuli, ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR, ujenzi wa bwawa la umeme la JNHPP, ununuzi wa ndege za ATCL, ujenzi wa barabara, vivuko na madaraja ikiwemo daraja la Kigongo-Busisi la Mwanza.

Pamoja na yote hayo, Rais Samia ameongeza kasi ya ujenzi wa shule, zahanati, hospitali na miradi ya maji kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu tupate uhuru.

Rais Samia pia ameagiza Serikali yake iwekeze kwenye sekta ya Kilimo kwa kuongeza bajeti maradufu na kuvunja rekodi nchini ili kuwafikia wananchi wa chini.

Zaidi ya hayo, Rais Samia amepanua uwanja wa demokrasia, uhuru na haki nchini na kuimarisha mahusiano ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa, pamoja na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Alipoingia tu madarakani, Rais Samia aliagiza kuwa Serikali ikamilishe majadiliano na wawekezaji wa nje ambao wanapanga kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata gesi asilia (LNG) mkoani Lindi, mradi ambao utaingiza uwekezaji kutoka nje wa zaidi ya shilingi trilioni 100.

"Kwa kweli kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2025, sisi wapinzani tumekubali yaishe. Rais Samia hana mshindani, atashinda kwa kishindo kutokana na kuwekeza pesa nyingi za serikali kwenye sekta zinazowagusa wananchi moja kwa moja kama elimu, afya, maji, umeme na miundombinu. Sisi upinzani tunajipanga kwa 2030, kwani utafiti wetu wa ndani unaonesha kuwa Rais Samia atashinda kwa kishindo 2025," alisema kiongozi mmoja wa Chadema mkoani Singida kwa sharti la kutotajwa jina.