UBALOZI WA RWANDA NCHINI WAADHIMISHA SIKU KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI DHIDI YA WATUSI

May 24, 2017
 Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akiongozana na Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati wakiwasili kwenye Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji wa Kimbari dhidi ya Watusi yaliyotokea miaka 23 iliyopita huko nchini Rwanda.

Babalozi kutoka nchi mbali mbali wakiwasha mishumaa wakiongozwa na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura kwenye maaadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe Edzai Chimonyo akizungumza kwenye maadhimisho ya Mauaji ya Kimbari yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 23 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wageni waliohudhilia katika maadhimisho ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji wa Kimbari dhidi ya Watusi yaliyotokea miaka 23 iliyopita huko nchini Rwanda, yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani city, jijini Dar es salaam leo.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 23 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim  akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 13 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Nyimbo za mataifa mawili Tanzania na Rwanda zikiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbali nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

Sheikh Hamis Mtonga akiomba dua wakati wa kuanza maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbari ya nchini Rwanda leo
Lucky Vicent Wang’ara Juma la Elimu

Lucky Vicent Wang’ara Juma la Elimu

May 24, 2017
JU2 JU3Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akizungumza wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu katika Jiji la Arusha
JU4Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi. Eunice Tondi akisoma taarifa katika maadimisho ya juma la Elimu yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Arusha School jijini hapa.
JU5
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa(kwanza kushoto) akitembelea maonyesho wakati wa Juma la Elimu lililofanyika katika viwanja wa Arusha School.
JU6Wanafunzi wa shule mbalimbali pamoja na walimu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa sherehe za Juma la Elimu
JU7Katibu Tawala wa Wilaya David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi Kombe la Ushindi kwa kuwa nafasi ya kwanza kimkoa  kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent Bw. Innocent Mushi.
JU8Katibu Tawala wa Wilaya David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi cheti cha Ushindi kwa kuwa nafasi ya kwanza kiwilaya kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent Bw. Innocent Mushi.

NHIF YAZINDUA MPANGO WA MADAKTARI BINGWA GEITA

May 24, 2017


Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akielezea malengo ya kuwepo kwa madkatari Bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita wakati wa hafra fupi ya uzinduzi ambayo imefanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. 
Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya Akitoa utambulisho mbele ya mgeni Rasmi wakati wa Hafra fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Madaktari Bingwa.
Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine Gesimba  akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwaajili ya huduma ya afya kwenye Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Celestine Gesimba Shuka mia moja ambazo wametoa kama msaada kwa hosptali hiyo.
Mzee Peter Fulano ambaye ametokea Chato kwaajili ya kuja kufanyiwa Huduma ya afya akishukuru kwa huduma hiyo kuwepo Mkoani humo uku akiomba huduma hiyo kufika pia kwenye Wilaya ambazo zipo ndani ya Mkoa.
Bi,Mariam Walwa ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Geita akiomba kupatiwa nafasi na kipa umbele kwa wanawake kutokana na wao kuwa na majukumu mengi ya Kifamilia.
Meza Kuu ikifuatilia kile ambacho baadhi ya wananchi walikuwa wakikiomba.
Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya Rufaa na Madaktari Bingwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita  Brayn Mawala  akifafanua juu ya huduma ya afya kwenye Hospitali ya Mkoa.
Wodi ya wazee huduma zikiendelea.
Dr Mawala akimjulia hali moja kati ya wagonjwa ambao walikuwa kwenye hodi ya wazee.

MBEGU BORA ZA MHOGO ZINAHITAJIKA KUWANUSURU WAKULIMA WILAYANI CHATO MKOANI GEITA

May 24, 2017
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipandikilo kilichopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Lazaro Kagundulilo (kulia), akizungumza na wanahabari pamoja na  wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) na , Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), wilayani humo jana. Wataalamu hao wa kilimo wapo katika wilaya hiyo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa Mkoa wa Geita.



Maofisa ugani wakiangalia eneo ambalo patalimwa shamba dogo la mfano katika Kijiji cha Kibehe Kata ya Kigongo.
Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon (kulia),  akitoa maelezo kwa wanahabari wakati walipotembelea moja ya shamba la zao la mhogo lililokumbwa na ugonjwa wa batobato na michirizi ya kahawia wakati wa ziara hiyo katika Kijiji cha Ipandikilo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipandikilo kilichopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Lazaro Kagundulilo, akiwaonesha waandishi wa habari shina la mhogo lililoathiriwa na magonjwa.
Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF la nchini Kenya, Suleiman Okoth (kushoto), akiwaelekeza jambo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipandikilo, Clara Fidelis (kulia) na Ofisa Ugani wa Wilaya ya Chato, Charles Ntaki.
Shamba la mhogo lililoathiriwa na magonjwa.
Wanahabari wakitoka shambani.
Wakulima wa Kijiji cha Ipandikilo wakimenya mihogo tayari kwa kuianikwa kwa ajili ya unga wa ugari. Kutoka kulia ni Veronica Zakaria, Joyce Joseph na Teloza Lugiyege.
Shamba la mhogo linaloonekana kustawi vizuri lakini tayari limeathiriwa na magonjwa ya batobato na mchirizi kahawia.
Mkulima Andrew Misano akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu changamoto mbalimbali za kilimo cha mhogo.
Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon (kushoto), akizungumza na wakulima wa kijiji cha Ipandikilo kuhusu mbegu bora za mhogo.
Mjumbe wa Kijiji cha Idoselo, Majeshi Mussa akiwaonesha waandishi wa habari mtama ulioathirika kwa kukosa mvua.
UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SARPCCO

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SARPCCO

May 24, 2017
unnamed
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati anawasili katika ukumbi wa mikutano wa AICC kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO). Kulia ni Mkuu wa INTERPOL kanda ya Kusini Mubita Nawa.( Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
A
Katibu Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Tax akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika mkoani Arusha. IGP Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
A 1
Baadhi ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa heshima wakati wimbo wa taifa unapigwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania, Ernest Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
A 2
Katibu Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Taxi, akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
A 3
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa afrika (SARPCCO) baada ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika unaofanyika Mkoani Arusha. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
A 4
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,  IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa ameambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida (kushoto) na Mkuu wa jeshi la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine (kulia) wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.