CCM YAMPA POLEPOLE VIATU VYA NAPE, MGOGOLO NAIBU KATIBU MKUU

CCM YAMPA POLEPOLE VIATU VYA NAPE, MGOGOLO NAIBU KATIBU MKUU

December 13, 2016
hum
Na Bashir Nkoromo, Dar

Chama Cha Cha Mapinduzi (CCM), leo kimeteua viongozi waandamizi watatu kuziba nafasi zilizokuwa wazi, kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya serikalini.
kijani
Uteuzi huo, umefuatia Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kikao chake, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli,  na kuridhia mapendekezo ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika juzi pia chini ya Dk. Magufuli.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, kupitia vikao hivyo, CCM imemteua Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
pole
Nape alisema, wapili ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga, kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi na Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Nape mwenyewe aliyeteuliwa kuwa Waziri.
 
Amesema, kupitia kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kilichofanyika leo, mambo kadhaa yaliyopendekezwa na Kamati Kuu, yamejadiliwa na kikao hicho cha NEC na yote yamepitishwa. Kusoma taarifa ya yooote, yaliyojiri katika kikao hicho cha NEC, sasa/BOFYA HAPA

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAINGIA MKATABA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

December 13, 2016
Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya.

JPM AOGOZA KIKAO CHA NEC LEO, IKULU

December 13, 2016
leooooooooooooooo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifungua kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 13, 2016. 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifungua kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 13, 2016. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, Katibu Mkuu wa CCM, .
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa hotuba ya utangulizi kumkaribisha Dk. Magufuli 
 Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa kikao hicho
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi aliyemaliza mda wake, Nape Nnauye akizunguza wakati wa kikao hicho. Picha zote na Bashir Nkoromo. PICHA NYINGI ZAIDI/>>BOFYA HAPA

UN Tanzania yawahamasisha Vijana kujiunga na fursa zilizopo katika malengo endelevu ya dunia

December 13, 2016
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez amewahamasisha vijana mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zilizopo katika malengo endelevu ya Dunia ilikuwezeshwa kimafunzo na mitaji zaidi. Akizungumza katika semina maalum ya FURSA 2016 kwa mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) na wadau wengine mbalimbali huku wananchi kutoka maeneo tofauti wamepata kuhudhuria, Bw. Alvaro amesema vijana na wananchi wanayo fursa ya kuchangamkia malengo hayo ya endelevu. 
“Tumeweza kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kuwafundisha vijana kuwa mabalozi wa malengo endelevu ya Dunia. Na zaidi ya vijana 10,000 kwa kufikiwa na elimu ya maendeleo endelevu. Ikiwemo Iringa, Kigoma Mbeya na mikoa mingine” amesema Bw. Alvaro. Aidha kwa upande wa washiriki wengine wakiwemo watoa mada wameweza kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio na namna ya kupata elimu ya kibiashara. 

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa elimu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini Dar.
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela akizungumza kwenye kongamano la Fursa 2016 kwa vijana liliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mtana, Millenium Towers.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo

WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 55 YA UHURU WAKABIDHIWA VYETI.

December 13, 2016


Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwemo Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Waandishi wa Habari wakishuka baada  ya kupanda mlima huo kwa siku sita.Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Witara (Mwenye fimbo mstari wa mbele) na Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ardhini (JWTZ) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipokea Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro walipofika katika lango la Marangu,Kippi akisalimiana na Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu.
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA.
Baadhi ya Washiriki wa changamoto ya upandaji Mlima Kilimanjaro baada ya kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Star Tv ,Ramadhan Mvungi baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. .
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwanadishi wa Habari wa Clouds Media Group ,Kilimanjaro na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini ,Dixon Busagaga baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi ,Arusha ,Zulfa Musa baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari akiwa ni miongoni mwa wasicha wawili waliofika kileleni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mtanzania ,Arusha,Eliya Mbonea baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima,Charles Ndagulla mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.

MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO.

December 13, 2016
Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers Network TBN, uliofanyika ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.

Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia. Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari


Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.

Kauli iliyowafurahisha wengi ni ile ya Waziri Nnauye aliyowakaribisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa tuzo kwa wanablogu kwa mwaka ujao 2017 akisema wanafanya kazi kubwa hivyo ni vyema kutambua mchango wao kupitia tuzo.

BMG inawapongeza wote waliofanikisha mkutano huo, ikiwemo Bank ya NMB kwa ufadhiri wake, NHIF, PSPF, Kampuni ya bia Serengeti, Cocacola na TANAPA. Kwa pamoja tuienzi kaulimbiu ya mkutano huo, "Mitandao ya Kijamii ni Ajira, Itumike kwa Manufaa".
Kutoka kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili, Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili na mjumbe wa kamati tendaji TBN, Klantz Mwantepele.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili.
Mwanablogu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wenzake.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda 
Wanablogu wakiendelea kutoa mawazo yao katika kuijenga TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Tazama HAPA na HAPA ujionee.