WAZIRI LUKUVI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA TANGA NA MANYARA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

February 07, 2017
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza  kwenye kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya kuumaliza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Dokta Joel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala 
Baadhi ya wenyeviti wa halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo
WAZIRI wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William  Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.

Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi
  kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake  mkoani hapa.

Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi
  ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

"Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya kazi
  hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji"Alisema Lukuvi.

Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo
  mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa  mara ya tatu na litakuwa la mwisho.

Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji

kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale
panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya kuuwongeza.

"Kama kuna viongozi wanamatakwa yao basi watambue hawatapata nafasi na
  tayari tulishapokea agizo kutoka Waziri Mkuu na kinachotakiwa hapa ni utekelezaji wa kumaliza mgogoro huo"Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela alisema jukumu kubwa
  lililopo mbele yao ni kutoa ushirikiano kwa timu iliyoundwa na Wizara hiyo na kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa wakati kama Waziri alivyoagiza.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera alisema lazima viongozi
  washirikiane kwa pamoja kutatua mgogoro huo ambao umekuwa ni tatizo kwa Wilaya hizo mbili na kupongeza hatua ya Serikali ya uhakiki upya hasa kwa kufuata GN ya namba 65 ya mwaka 1961 kama alivyoagiza Waziri Mkuu na si vinginevyo.

Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya
  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.

Majaliwa alisema katika ziara yake hiyo kuwa Aidha alisema baadhi ya
  viongozi wa kisiasa na Serikali kwa kutokuwa wa kweli mbele ya wananchi kuhusiana na mgogoro huo na wanajaribu kufanya maamuzi kwa ajili ya maslahi yao ya kujiaminisha mbele ya wananchi hao.

Alisema lazima ramani ya mwaka 1961 ifuatwe na viongozi waache kuwa na
  agenda zao za siri na kuwadanganya wananchi kwa kuanza kurudia kupima mpaka huo mara kwa mara bila ya kupata majibu sahihi ramani na huu ni muda wa kuwael3za ukweli wananchi

"Ramani ipo ya mwaka 1961 na najiuliza sana hivi hao wanaokuwa na
  tabia ya kurudia kupima pima mara mbili agenda yao ni nini,huu si udanganyifu kwa wananchi?"Alihoji Majaliwa.

Alisema kuananzia sasa GN itakayotumika ni ile namba 65 ya mwaka
  1961,zaidi wanachotakiwa wataalamu kukifanya ni kuimarisha mpaka huo kwa kuwashirikisha  viongozi wa Serikali,wanasiasa na wananchi ili kuweka mustakabali mzuri juu ya mpaka huo

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI

February 07, 2017
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akihutubia wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi ya takwimu za umaskini na namna bora ya kupima hali ya umaskini Afrika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akitoa hutuba yake.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Kanda ya Afrika Mashariki, Roland Van De Geer, akitsoma hutuba yake.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Repoa, Dk.Blandina Kilama, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtakwimu kutoka Menejimenti Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Tanzania Zanzibar, Mayasa Mwinyi akizungumza kwenye mkutano huo.
Taswira ya meza kuu.
Mkutano ukiendelea.
Taswira katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale

MATUMIZI  ya Takwimu rasmi katika kupanga maendeleo ya wananchi kwa nchi zinazoendelea yamekuwa hayaendi kwa kasi inayotakiwa kimataifa imefahamika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa Dar es Salaam leo wakati akisoma hutuba yake katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi ya takwimu za umaskini na namna bora ya kupima hali ya umaskini Afrika.

Alisema wakati dunia ikiendelea na utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo ya dunia ya mwaka 2030 yapatayo 17, shabaha 169 na viashiria 231 ni dhahiri kuwa matumizi ya takwimu rasmi katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake kila nchi haina budi kuyafanyia kazi ipasavyo.

"Kutokana na hali hiyo ndiyo maana Benki ya Dunia ikishirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeona umuhimu wa kuwa na mkutano huu wa kimataifa wa kukutanisha watakwimu, wachumi na fani nyingine za kitaalam kujadili kwa kina matumizi ya takwimu za hali ya umaskini na tafsiri yake kwa ujumla na nini kifanyike ili kuboresha zaidi tafsiri ya umaskini" alisema Dk. Chuwa.

Katika hatua nyingine Dk.Chuwa alitoa angalizo kwa kuwaomba wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuwa takwimu za hali ya umaskini pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya nchini zinatolewa na serikali hivyo zisitumike vibaya kuichafua nchi kuhusu hali ya umaskini.

Alisema iwapo itatokea kuwepo kwa matumizi mabaya sheria ya takwimu ya mwaka 2015 pamoja na kanuni zake tayari zimesainiwa zitachukua mkondo wake. 

Alisema Takwimu zitumike kwa lengo la kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi maskini wa Tanzania na kwa nchi zinazoendelea hususan kwa nchi zilizoko Kusini mwa Bara la Afrika.

Mgeni rasmi wa mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Benki ya Dunia, Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alisema ilikuweza kujenga Afrika lenye neema nilazima kuhakikisha kuwa bara hili linaondokana na umaskini na kuwataka wataalamu waliohudhuria mkutano huo  kutunganjia bora ya kupima umaskini.

Alisema ili kuendana na kasi ya dunia na utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo ya mwaka 2030 yapatayo 17 ni wazi ufanyaji takwimu na utafiti unapaswa kufanyika  ili kujua kiwango cha umaskini lakini pia aina ya umaskini uliopo.



RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI YA TANZANIA (CDF) PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

February 07, 2017


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza mara baada ya tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania pamoja na  Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza masuala mbalimbali mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja viongozi wengine wa Jeshi na Mabalozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza masuala mbalimbali mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja viongozi wengine wa Jeshi na Mabalozi Ikulu jijini Dar es Salaam.