DC HANDENI ASIFU JITIHADA ZA SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA HANDENI FREE TRADE DEVELOPMENT CHARITY

May 04, 2015
Mkuu wa wilaya ya Handeni,Husna Msangi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika akati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kwa ufadhili na shirika hilo,


Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga,Husna Msangi akizundua katiba ya shirika lisilokuwa la kiserikali la (Haftrade) juzi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wake katika kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika Tarafa ya Chanika wilayani
Handeni,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ,Ramadhani Diliwa,

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Husna Msangi akimpongeza Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalosaidia masuala la kijamii la (Haftrade) lenye makazi yake wilayani Handeni Hellen Makoni mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la vyumba viwili vya madarasa linalojengwa na shirika hilo kwenye kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika wilayani
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Husna Msangi amesifu jitihada zinazofanywa na shirika lisilokuwa la Kiserikali la (Handeni Free Trade Development Charity)  ni kuhakikisha wanapunguza umbali wa upatikanaji wa maji safi na salama uliopo sasa katika maeneo mengi  wilayani humo hadi kufikia umbali wa mita 400 ambao unatakiwa katika sera ya maji.
Ameyasema hayo jana wakati akilizindua  shirika hilo katika halfa
iliyo fanyika Kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika wilayani hapa
ambapo alisema kuwa shirika hilo limejikita kwenye mambo makuu manne ambayo ni Maji,Afya,Elimu na Mazingira.

Amesema kuwa hilo litaweze kufanikisha hayo likishirikiana kwa pamoja kati ya shirika hilo,serikali na wananchi katika kujenga miundombinu ya kuvunia maji ya mvua kama vile mabwawa ikiwemo uvunaji wa maji ya mvua kutoka kwenye mapaa ya nyumba na yale majengo ya serikali hali kadhalika na kuchimba visima virefu na vifupi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema licha ya hayo lakini pia litajikita kwenye suala la Afya ikiwemo kupambana na maradhi  yanayokuwa yakiwa andama wananchi kwa kujenga na kukarabati miundombinu katika vituo vya afya,Zahanati zilizopo maeneo yote yaliyopo wilayani humo pamoja na kutoa elimu ya afya ya jamii ya jinsi ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema kuwa pia shirika hilo litasaidia kwenye sekta ya elimu ili
kupambana kuondoa ujinga katika wilaya ya Handeni kwa kukarabati miundombinu katika shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo
.
Ambapo tayari shirika hilo kwa kushirikiana na wananchi wa kwamadule na maeneo mengine jirani wamekwisha anza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja.
Amesema kuwa hiyo itasaidia kupitia mpango wa elimu kwa walioikosa(MEMKWA) shirika hilo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali linakusudia kulipatia kundi hilo fursa ya elimu jambo ambalo litapunguza ujinga na umaskini kutoka ngazi ya familia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa wa Shirika hilo,Hellen Makoni anasema kuwa malengo yao ni kuwahamasisha na kuiunganisha jamii kuanzisha shughuli mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kuinua hali ya maisha kwa jamii kuanzia ngazi za familia.

Anasema kuwa pamoja na hivyo watashirikiana na mashirika mengine yasiokuwa ya kiserikali na kiserikali nay a kimataifa katika mapambana dhidi ya ujinga umaskini pamoja na maradhi ikiwemo kutilia mkazo juu ya shughuli za kijamii kwenye sekta za Maji, Afya, Huduma za Elimu na Mazingira kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao.

Mkurugenzi huyo anasema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watajitahidi kutoa misaada ya kijamii kwa wahanga wa majanga ya asili na yake yanayotokana na shughuli za kila siku zinazofanywa na jamii wakati yanapotokea.

Aidha anasema kuwa shirika hilo limeunga mkono agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa mifuko 100 ya saruji kwa wilaya ya Handeni kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo  lengo likiwa kuharakisha maendeleo ya elimu.

SEMINA YA USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012 YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

May 04, 2015

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo mafupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe akiwahutubia washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini Semina hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe (katikati) akiwa na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar na baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro. ( PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Na Veronica Kazimoto, Morogoro

Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni muhimu ili kila ngazi ya utawala iweze kuzipata, kuzielewa na kuzitumia takwimu zitokanazo na Sensa hiyo kwa ajili ya kutunga sera, kuandaa na kutathimini utekelezaji wa mipango ya maendeleo pamoja na kufanya maamuzi sahihi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe wakati akifungua Semina ya siku moja ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika mjini Morogoro.

"Ni matumaini yangu kwamba, ninyi nyote mliokusanyika hapa  mtazitumia vizuri takwimu hizi ili ziwasaidie katika kuweka vipaumbele vya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa mkoa wa Morogoro", amesema Dkt. Rutengwe.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisistiza kuwa ni wajibu wa kila Ofisa wa Serikali mkoani Morogoro kuhakikisha takwimu zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 zinakuwa msingi wa mipango  ya maendeleo na kuwa kigezo cha kufanya maamuzi katika kuweka mstakabali wa mkoa wa Morogoro.

Nae  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, amesema lengo la Semina hiyo ni kuwaelimisha wadau katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri juu ya matumizi ya takwimu za Sensa ya Watu ili waweze kuzitumia katika kupanga na kutathmini program mbalimbali za maendeleo katika ngazi husika.

"Dumuni lingine la Semina hii ni kuhamasisha matumizi ya takwimu rasmi katika shughuli zetu za kikazi, ili lengo la kutumia takwimu za Sensa kuboresha maisha ya Mtanzania liweze kutimia", amesema Kwesigabo.

Kwesigabo amefafanua kua Semina hiyo ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi itasaidia kujua ni maeneo yapi mkoa wa Morogoro umepiga hatua na maeneo ambayo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuweza kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa.

Jumla ya washiriki mia moja na kumi (110) kutoka ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote mkoani Morogoro wameshiriki katika Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kwa lengo la kupata elimu juu ya matumizi ya takwimu zinazotokana na Sensa hiyo.
UMOJA WA ULAYA, UN; TUTAPIGANIA UHURU WA HABARI SIKU ZOTE

UMOJA WA ULAYA, UN; TUTAPIGANIA UHURU WA HABARI SIKU ZOTE

May 04, 2015
IMG_0062
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.  
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.  
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.  
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo. Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo.Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.  
Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu akifuatilia mijadala katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu wakifuatilia mijadala katika mkutano huo.Mwanahabari na Bloga, Majid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo. Mwanahabari na Bloga, Maggid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza. Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.  
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza jana mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Sebregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari.
"...Tulifanya hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Sebregondi.
Alisema kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti mawasiliano.
Alisema vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kujifunza zaidi.
Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia na faragha.

Kasi ya Utekelezaji miradi ya NHC Mtwara yafurahisha bodi ya shirika hilo

May 04, 2015

Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akielekeza jambo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amesifu kasi ya ujezi wa nyumba hizo unaozingatia viwango na muda na akawataka wafanyakazi wa NHC kuchapa kazi ili kufikia malengo yao waliyojiwekea. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi, wa pili ni Eliaisa Keenja wa NHC, Meneja wa NHC mkoa wa Mtwara, Joseph John na Injinia wa mradi huo Leonard Kazoba.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Baadhi ya Nyumba za gharama nafuu Masasi zilizoko mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akiendelea na ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Baadhi ya Nyumba za gharama nafuu Masasi zilizoko mkoani Mtwara.
Baadhi ya Nyumba za gharama nafuu Masasi zilizoko mkoani Mtwara.
Baadhi ya Nyumba za gharama nafuu Masasi zilizoko mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akitoa maelekezo kwa menejimenti na wafanyakazi wa Shirika hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akiendelea na ziara yake katika mradi wa nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akiendelea na ziara yake katika mradi wa nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akiendelea na ziara yake katika mradi wa nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Mojawapo ya majengo katika nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Mojawapo ya majengo katika nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Mojawapo ya majengo katika nyumba za ghorofa za NHC Shangani Apartments zilizopo katika eneo la Shangani mjini Mtwara, nyumba hizo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika

MAMBO YA MBELEZZ JAY Z NA BEYONCE KATIKA PAMBANO LA MAYWEATHER

May 04, 2015

MGOMO BARIDI, TANGA

May 04, 2015


 Abiria wa mabasi ya Mikoani kituo cha Kange Tanga wakiwa wameduwaa na kutojua cha kufanya baada ya madereva wa mabasi kugoma leo asubuhi na taarifa za hivi punde ni kuwa madereva wamekubali kuondosha magari kuelekea Mikoani.




DAKIKA 90, COASTAL UNION YAITANDIKA STEND UNITED MABAO 3------------1

May 04, 2015


 Mchezaji wa Stend United, Hamis Shengo akijaribu kumtoka mchezaji wa Coastal Union Joseph Mahundi wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom) leo katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.


 Mchezaji wa Stend United Pitter Mutambuzi akimiliki mpira na kujaribu kuwatoka wachezaji wa Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom) uliochezwa leokatika uwanja wa Mkwakwani.

Mchezaji wa Stend United akimdhibiti kiungo wa Coastal Union, Abdulhalim Humuod wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom) uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani.
Kiungo wa Coastal Union, Abdulhalim Homuod, akimtoka beki wa Stend United, Gisege Mathias wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom) uliochezwa Leo  katika uwanja wa Mkwakwani,Picha kwa hisani ya tangakumekucha