RC MPYA TANGA ATEMA CHECHE
Tangakumekuchablog
MKUU wa
Mkoa wa Tanga aliehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalula, amemtisha zigo la
migogoro ya ardhi aliyodai kufanya na watendaji wa Idara ya Mipango miji mbadala wake , Mwantumu Mahiza aliehamia
Tanga.
Akimkaribisha Leo ukumbi
wa ofisi ya mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa, Magalula alisema migogoro ya ardhi
inasababishwa na watendaji wa mipango miji na sio wananchi hivyo kumuachia zigo
hilo ambalo limekuwa likiwatesa wananchi.
Alisema Idara hiyo imekuwa
ikiwagombanisha wananchi wenyewe kwa wenyewe pasina sababu na linapobumbuluka hutoa
visingizio vya sheria na mwaka hivyo kumtaka kulivalia njuga ikiwa na pamoja na
kulikomesha.
“Mheshimiwa dada yangu Mwantumu
Mahiza karibu Tanga na niwaage watu wa Tanga kwa kusema kwaherini-----ila kuna
jambo moja ambalo niseme waziwazi pasina kuoneana haya kuwa Idara ya mipango
miji ni mabingwa wa kugombanisha wananchi” alisema Magalula na kuongeza
“Wao ndio wanaofanya hiyana kwa
kufanya mavirigisa na ujanja ujanja halafu husikilizia----pale linapobumbuluka
hukaa pembeni kisha kutoa vifungu vya sheria na mwaka baada ya watu kugombana
kuhamasiana” alisema
Alimtaka Mkuu huyo mpya kulikomesha
tatizo hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya
wananchi badala ya kufanya kazi za maendeleo wamekuwa wakipanga foleni ofisi za
mipango miji ambako ndiko kiini cha tatizo.
Akizungumza baada ya makabidhiano,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, alisema hatomuonea huruma kiongozi
yoyote katika kazi bila kujali cheo wala nasaba hivyo kuwataka kuwatumikia
wananchi kwa haki na uwazi.
Alisema yote ambayo ameelezwa na
mtangulizi wake atayafanyia kazi na yule ambaye amefanya madudu ajisafishe
kabla ya operesheni katika ofisi na idara hajaianza.
“Mheshimiwa Magalula changamoto na
kero zote ambazo umeniambia hapa mbele ya wakuu wa idara na watendaji ofisini
nimezipokea na niko tayari kwa lolote kwani uwezo ninao” alisema Mahiza
Alisema kinachotakiwa ni kufanya
kazi kwa uwazi na uwajibikaji ili kuwaletea maendeleo wananchi na kudai kuwa
yeyote ambaye ataonyesha ukiukwaji wa maadili ni vyema akajiengua mapema.
Mkuu wa Mkoa mpya wa Tanga, Mwantumu Mahiza, akizungumza
na wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara na
Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa
mara baada ya makabidhiano na mtangulizi wake aliehamishiwa Mkoa wa Katavi.
BARAZA LA VYUO VIKUU AFRIKA MASHARIK(IUCEA)KUWA NA MAONESHO YA VYUO VIKUU UGANDA
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki(EABC)Lilian Awinja akizungumza katika mkutano huo. |
Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini kwaajili kuuhabarisha umma. Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com |
Dk Shein Aendelea na Kampeni Zake na Kusema Ataendeleza Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Kuleta Maendeleo Zaidi kwa Wazanzibar katika Wananchi Wake na Elimu Bure Zanzibar.
Mgombea
Urais wa Zanzibar Kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana
na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Mpira Konde
Kisiwani Pemba kuendelea na Kampeni Kisiwani Pemba.
Mgombea
Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika
katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais
wa Zanzibar Dk Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira
Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama
wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili
katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa
Kampeni zake kisiwani Pemba.
Taswira
ya wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia CCM katika
viwanja vya mpira Konde Pemba kama inavyooneka Mwanachama huyu wa CCM
akishangilia akiwa na picha ya Mgombea Urais wa CCM Dk Shein.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad
akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo
Zanzibar katika kipindi chake Dk Shein cha miaka mitano na kuwataka
kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar
katika sekta mbalimbali za Jamii
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.
Katibu
wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu
akiwahutubia Wananchi wa Konde katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea
Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika katika uwanja wa mpira Konde
Kisiwani Pemba.
LOWASSA APOKELEWA KWA KISHINDO MJINI BUKOBA LEO
Umati
wa Wananchi wa Mji wa Bukoba ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Aghakhan
kuhudhulia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,
leo Septemba 19, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi Bukoba waliofika
kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye
Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadhi ya wagombea wa Udiwani
wa vyama vinavyouda UKAWA, kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera
zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera
leo Septemba 19, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mmoja wa wadau wa
Mabadiliko, Prof. Azaveli Rwaitama, katika Mkutano wa Kampeni,
uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo
Septemba 19, 2015.
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza, Mh. Ezeckiel Wenje
akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba,
Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Mke wa
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred
Lwakatare, akimuombea Mumewe Kura kwa Wananchi wa Mji wa Bukoba, wakati
wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,
uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo
Septemba 19, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimpongeza Mke wa Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, mara baada ya
kuzungumza na Wananchi wa Bukoba.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare,
akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba,
Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Waziri
Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano
wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Aliekuwa
Meya Mji wa Bukoba, Anatory Amani akizungumza kwenye Mkutano wa Kampeni
za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NCHINI LAFANA
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni
wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi katika Kongamano la Wajasiriamali
Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures
Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana).wa kwanza kushoto
ni Meneja Msaidizi wa Mfuko huo Bi Matilda Nyallu.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni
wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (katikati) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi katika Kongamano la Wajasiriamali
Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa
Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini
Dar es Salaam leo (jana).
Wafanyakazi wa Mfuko wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF wakiwa katika Banda la Mfuko huo wakati katika Kongamano la
Wajasiriamali Wanawake nchini kabla ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of Women
Entrepreneures Tanzania (VoWET) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa
kwanza kulia ni Meneja wa Mpango wa
Uchangiaji wa Hiari kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP
Media, Reginald Mengi akizindua Kampuni ya Voice of Women Entrepreneures
Tanzania (VoWET) katika Kongamano la Wanawake Wajasiriamali nchini
lililofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida
Waziri
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media,
Reginald Mengi akimlisha keki Rais wa VoWET nchini Bi. Mahida Waziri katika Kongamano
la Wanawake Wajasiriamali nchini mara baada ya uzinduzi wa Kampuni ya Voice of
Women Entrepreneures Tanzania. (Picha na
Benjamin Sawe)
MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU (CCM) YUSUF MANJI AZINDUA KAMPENI ZAKE DAR ES SALAAM LEO
Kiongozi
wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia (kulia),
akimtambulisha Yusuf Manji katika uzinduzi huo.
Mgombea
nafasi ya udiwani Kata ya Mbagala Kuu kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Yusuf Manji (kushoto), akihutubia wananchi na makada wa chama
hicho katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika eneo la Kichemuchemu
Kaskazini Dar es Salaam leo jioni.
Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia, akihutubia katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Mchumi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Urio akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Kada wa CCM, Godbertha Kinyondo akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
Makada wa CCM wakiserebuka
Vijana wa hamasa wa CCM wakiwa kazini.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Michango mbalimbali ikitolewa.
Umati ukimsikiliza Yusuf Manji.
Mkazi wa eneo hilo, Sharifa Ali akimueleza Manji kuhusu kero ya kutokuwa na soko.
Dogo
akihubia kwenye uzinduzi huo. Dogo huyo alisema wana CCM wanapaswa
kumchagua Magufuli kuwa Rais, Mbunge Mangungu na Diwani Manji.
Chipukizi wakifanya vitu vyao.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Yusuf Manji (kulia) akifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)