MAKAMBA AONGOZA UZINDUZI WA AZAM TV

December 05, 2013

 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB) akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na chaneli zisizopungua 50.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Tv, Rhys Torrington akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Azam Television jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
 Naibu waziri Januari Makamba akifuatilia maelezo ya awali ya Azam TV

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI YA RAIS KAZI UTUMISHI WA UMMA

December 05, 2013
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi, Kazi na Utumishi wa Umma,katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,(wa pili kulia)  Katibu Mkuu  Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee. 

 Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Ofisi ya Rais, Kazi,na Utumishi wa Umma,wakiwa katika cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi  hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KAMPENI MPYA YA KUZUIA MALARIA YA M-ZINDUKA

December 05, 2013
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wasanii wa muziki wa Kizazi kipya 'Bongo Flava', walioshiriki katika kuandaa wimbo wa M Zinduka unaohamasisha kushiriki katika kampeni mpya ya Malaria inayokwenda kwa jina la M Zinduka, baada ya kuizindua rasmi jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye  uzinduzi wa Kampeni ya Kuzuia Malaria inayojulikana kama ‘M-Zinduka’ inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom,  Tanzania House of Talents na Malaria  no more.  
 Wasanii hao wakiimba wimbo wao waliorekodi wa kampeni ya kuzuia malaria.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao.

MKE WA WAZIRI KUU AZINDUA KAMPENI YA "TUNAWEZA" TANGA

December 05, 2013
MKE WA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAMA TUNU PINDA AKIZUNDUA KAMPENI YA TANGA TUNAWEZA LEO ILIYORATIBIWA NA ASASI YA TREE HOPE.



ZIUNGENI MKONO TAASISI ZINAZOPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE NA WATOTO-TUNU PINDA.

December 05, 2013
Na Paskal Mbunga,Tanga.
 MKOA wa Tanga umehimizwa kuziunga mkono taasisi zinazopambana dhidi ya ukatili na unyanyasi kwa wanawake na watoto ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa.

Akizindua rasmi leo kampeni ya “Tunaweza Mkoa wa Tanga” inayoerndeshwa na asasi ya Tree of Hope ya jijini hapa, Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda alisema suala la ukatili wa kijinsia katika jamii yetu linaendelea kushika kasi na kuleta madhara mengi yakiwemo ulemavu mwilini, msongo wa mawazo, kuvunjia kwa ndoa ama kusababisha wanandoa kuathiriwa na magonjwa hatari, ukiwemo UKIMWI, na wakati mwingine vifo.


KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA.

December 05, 2013


1 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda bajaji tayari kwa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe Mwanjelwa jijini Mbeya akitokea ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, huku Nape Nnauye naye akijiandaa kuinga kwenye bajaji. Kinana akiongozana na Ujumbe wake pamoja na viongozi wa mkoa wa Mbeya na wilaya Jana wametumia usafiri huo ili kuonyesha kwamba Chama hicho ni chama cha wananchi wa kawaida ambao ni wafanyakazi na wakulima tofauti na wenzetu wanaojifanya wanawatetea lakini wanakuja na Helikopta na kuwachangisha michango ya fedha kisha wanatokomea zao. Katika msafara huo pia yupo Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa.2 
Msafara ukielekea kwenye mkutano 4 
Vijana wa Mwanjelwa wakiuzuia msafara wa Kinana wakati alipokuwa akielekea uwanja wa Luanda Nzovwe kwenye mkutano jambo lililofanya Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye watembeee kwa mguu

*WAZAZI NA WALEZI WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATA VITAMIN A

December 05, 2013


Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa utoaji matone ya vitamin A ya nyongeza kwa watoto walio katika umri wa Miezi 6 hadi mitano, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo.
***************************************************
Na Fatma Salum wa  THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG, 
Wazazi na Walezi wamesisitizwa kuwapeleka watoto wenye umri wa Miezi sita hadi miaka Mitano kupata matone ya vitamin A yanayotolewa kwenye vituo vya Huduma za afya Kote nchini.

Msisitizo huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Assey alisema  kuwa zoezi la utoaji matone ya vitamin A kwa watoto linalofayika mara mbili kwa mwaka kila mwezi juni na disemba huenda sanjari na utoaji wa dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano.