Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi
wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa
Nchini.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera,
Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao
Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia
usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa
kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.