WAZIRI MIGIRO AKABIDHI NAKALA ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA WALEMAVU, TAASISI ZA KIDNI NA ASASI ZA KIRAIA

March 16, 2015

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Watanzania wametakiwa kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika kuandika historia mpya ya nchi.

Hayo aliyasema leo Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Asha-Rose Migiro wakati akikabidhi katiba inayopendekezwa kwa makundi mbalimbali,Migiro amesema nchi itaandika historia mpya baada ya kupata katiba mpya.

Alisema wananchi wakisoma katiba kwa umakini kutasaidia kufikia matarajio katika kutengeneza ramani ya nchi kwa kuvuka miaka 50 ya katiba mpya.

Migiro amesema kuwa wamechapisha katiba inayopendekezwa kwa watu wenye ulemavu wa kuona kwa alama ya nukta nundu na baada ya kupita kwa katiba watapewa kwani ni haki yao kuwa nayo.

“Kujitokeza kwenu ni ishara ya kuunga mkono kwa katiba inayopendekezwa hivyo ni wajibu wenu kutoa elimu ili waweze kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura ya maoni”amesema Dk.Asha-Rose.

Aidha wamechapisha nakala hizo kwa herufi kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili nao waweze kusoma na kuelewa na kuweza kufanya maamuzi.

Migiro amesema wamechapisha nakala na kugawa kwa nchi nzima ambapo kila kata inapata nakala 300 na Zanzibar zinagaiwa chini ya ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

Baadhi ya wadau waliopokea nakala hizo wamesema watafikisha,lakini hawawezi kuwaamulia katika maamuzi yao
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015). Dkt. Turuka alipokea kwa niaba ya Makatibu Wakuu wenzake.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa mwakilishi wa Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam Sheikh Mussa Kundecha katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa mwakilishi wa Taasisi ya Mabohora Bw. Zainuddin Adamjee katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za kidini katika hafla fupi ya kugawa nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia katika hafla fupi ya kugawa nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana (Jumatatu, Machi 16, 2015). (Picha: Farida Khalfan, Wizara ya Katiba na Sheria)
CHADEMA KARATU YAVITENGA VIJIJI VINAVYOONGOZWA NA CCM KATIKA HUDUMA ZA MAENDELEO

CHADEMA KARATU YAVITENGA VIJIJI VINAVYOONGOZWA NA CCM KATIKA HUDUMA ZA MAENDELEO

March 16, 2015


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka mfereji wakati alipokagua mradi wa mashamba ya umwagiliaji ya vitunguu katika kijiji cha Mang’ola Barazani Wilayani Karatu wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha akihimiza na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo hata hivyo katika wilaya ya Karatu imeonekana kukwamishwa na Mbunge wa jimbo hilo Mchungaji  Israel Natse Chadema, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na madiwani kwa kuitenga baadhi ya miradi ambayo ipo katika vijiji ambavyo madiwani na wenyeviti wa vijiji wanatoka Chama cha Mapinduzi CCM ambapo wananchi wa kijiji hicho wamemlalamikia Kinana.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamekaa juu ya mti wakati walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara kijijini Mang’ola. 5 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kjiji cha Mang’ola.9 

TAMISEMI YATOA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA WAPYA

March 16, 2015

Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia akizungumza mapema leo katika siku ya kwanza ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba yanayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Bw. Zuberi Samataba.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini akitoa mada kuhusu kazi na majukumu ya Wakuu wa Wilaya katika semina hiyo iliyoanza leo tarehe 16 hadi 19 Machi 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja, ambaye pia ndiye mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma. UONGOZI Institute ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais inayoshughulikia mafunzo kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na kufanya utafiti na ushauri wa sera kwa serikali.
Mshiriki wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Shaban Kissu akichangia mada wakati wa mafunzo. Mada moja wapo zilizojadiliwa leo ni kuhusu mahusiano na mawasiliano baina ya serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda akizungumzia kuhusu changamoto mbali mbali za Wakuu wa Wilaya. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na maadili na sheria za kazi.
Baadhi ya wahudhuriaji wa kundi la Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba wakifuatilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mafunzo ya Wakuu wa Wilaya Wapya yanayoendelea mjini Dodoma.

TANGA UWASA KUKABIDHI VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA KWA SHULE YA SEKONDARI MISALAI NA ZIRAI AMANI MUHEZA

March 16, 2015


MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASAMHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WIKI YA MAJI LEO

              
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji

                       NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)inatarajia kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa kwa shule ya sekondari za Misalai na Zirai zilizopo Tarafa ya Amani wilayani Muheza vyenye thamani ya milioni 1,110,00.
KUSHOTO NI KAIMU MENEJA WA HUDUMA KWA WATEJA WA MAMLAKA HIYO,ROGERS MACHAKU NA KULIA NI KAIMU AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA HIYO RAMADHANI NYAMBUKA WAKIFUATILIA KIKAO HICHO CHA WAANDISHI WA HABARI NA MKURUGENZI WA MAMLAKA HIYO

Vifaa hivyo ni kwa kutambua mchano wao mkubwa katika kuhifadhi chanzo cha maji cha Mto Zigi ambapo ili kuwa na Maendeleo endelevu kwa Muheza na Tanga ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa muda wote kwa kutunza mazingira.


Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji ambapo amesema kuwa mamlaka hiyo itamkabidhi Vifaa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Esterina Kilasi ili avikabidhi kwa wahusika.



WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO BAINA YAO NA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASA),MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA LEO
Alisema kuwa kuelekea maadhimisho hayo watafanya mikutano ya hadhara kwa kata sita za Jiji la Tanga ili kueleza shughuli wanazozifanya wateja wao na wajibu kwao ikiwemo kuwafafanulia haki zao kama wateja pamoja na kupata maoni yao katika kuboresha huduma wanazozitoa.

Aidha alisema kuwa katika wiki hiyo watazindua rasmi jengo jipya la huduma kwa wateja katika eneo la Pongwe ikiwa ni pamoja na kuzindua huduma ya malipo ya Ankara za maji kwa Tigo Pesa ambapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula.

Ameongeza kuwa sambamba na hilo wataendesha dawati maalumu katika ofisi kuu swahili kwa lengo la kuwahudumia wateja wenye madeni sugu pamoja na kuwapa njia rahisi ya kulipia madeni yao na wale watakaolipa watasamehewa ada ya kutejesha maji katika kipindi cha Machi 16 mwaka 22 mwaka huu.

MAHAKAMA TANGA YAZINDUA BODI YA PAROLE

March 16, 2015


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula Said Magalula amewataka wajumbe wa Bodi ya Paroli Mkoa  kutenda kazi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ili kutenda haki na kuepuka ushawishi wa namna yeyote katika kupokea na kuomba rushwa.

Hayo yamesemwa mapema siku ya alhamisi ya machi 12 mwaka huu wakati wa uzindua rasmi Bodi ya Parole Mkoa tukio lililofanyika katika ofisi za Magereza Mkoa.

 Lengo la Bodi hii ni  kuwajadili  wafungwa wenye sifa  za kuweza kuachiliwa huru baada ya kutimiza vigezo ambavyo vimeainishwa kwenye  sheria namba 25  ya Paroli ya mwaka 1994 na kufanyiwa mabadiliko mwaka 2002.

Sheria husika imeweza kuanisha ni aina gani ya makosa ambayo mfungwa anaweza kupata fursa ya kuingia kwenye mpango wa Paroli . Pamoja na makosa hayo mfungwa hawezi kuingizwa kwenye utaratibu wa Paroli endapo amepatikana na kosa la unyanyanyi wa siraha, madawa ya kulevya, kulawiti, kubaka na mauaji ya kukusudia.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa sheria ya parole tangu utekelezaji wake mwaka 2003, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishina Agustino Mboje amesema tayari wafungwa 331 wameshaachiliwa huru kwa utaratibu wa parole, wafungwa 305 wamemaliza vifungo vyao salama na wafungwa 26 bado wanaendelea na vifungo vyao kwa utaratibu huu.

Licha ya kuwepo na mpango huu wa kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani lakini bado wafungwa wengi wameshindwa kunufaika na utaratibu wa Paroli kutokana na kutotimiza masharti ya parole.

Sababu kubwa ni ukosefu wa nakala za hukumu kwa wakati na ukosefu wa elimu ya kutosha  kwa wanajamii kuhusu sheria hii na hivyo kupelekea maafisa wa Paroli  kuwa na ugumu wa kupata taarifa muhimu zinazowahusu wafungwa wananotarajiwa kunufaika na mpango huu.

 Maafisa wa Magereza wakimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Magalula Said Magalula
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akisaini kitabu cha wageni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kam. Augostino Mboje akitoa taarifa ya utekelezaji wa sheria ya Parole katika Mkoa wa Tanga
Baadhi ya wajumbe na Maafisa wa magereza wakati wa uzinduzi

FILIKUNJOME ATIMIZA AHADI YA UJENZI WA DARAJA MTO KITEWAKA JIMBONI KWAKE

March 16, 2015

 Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe wa pili   kushoto na viongozi wa Halmashauri  wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa  ajili ya  kujengwa kisasa baada ya  serikali  kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh miloni 240
 Mbunge  Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa  kisasa 

 Wannchi  wa  kijiji  cha Maholong'wa  wakimpongeza  mbunge  Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake
 Waumini  wa  kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa  wakimkabidhi zawadi mbali mbali mbunge Filikunjombe baada ya  kuwasaidia bati na  saruji  ya kutosha  kujenga kanisa  jipya
 Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa  wakiongozana na mbunge Filikunjombe  mwenye kofia
 Mbunge  Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya  kufika  kusaidia ujenzi  wa kanisa  hilo
 Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na  wanakijiji  wa Maholong;wa
 Mzee  wa  kanisa la E.A.G.T Maboga  Ezekia Mhagama  (kulia)akimwombea  dua  mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya  kutoa misaada  mbali mbali ya ujenzi na  kujitolea kinanda  kwa  kanisa  hilo vyote  vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11  wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maholong'wa
Mkurugenzi  Ludewa Bw Waziri akizungumza katika mkutano  wa mbunge Filikunjombe
 Wananchi  wa Maholong'wa wakimpokea mbunge  wao
 Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honoratus Mgaya  akiwahutubia  wananchi wa Maholong'wa

BREAKING NEWS: MABIBO HOSTEL INAUNGUA MOTO MUDA HUU!

March 16, 2015

Moto umeibuka katika hostel za chuo cha UDSM zilizoko Mabibo (Mabibo hostel) na bado unaendelea hadi sasa ila chanzo hakijajulikana.
Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho cha UDSM Bwana Gibson George amesema kuwa chanzo hakijajulikana na nini ila moto umesambaa maeneo mbalimbali ya hosteli hizo.
"Watu wa zimamoto tumewapigia mapema sana ila wamechelewa kufika hadi muda huu ndio wamefika, tumejaribu kuuzima moto na umepungua kidogo japo bado unaendelea kwa baadhi ya vyumba" alisema Waziri Mkuu huyo


Fire II

Imeripotiwa muda mfupi uliopita kuhusu tukio la moto katika Hostel za Mabibo ambapo wanaishi wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinasema kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme, hakuna taarifa ya mtu yoyote kuathirika na moto huo mpaka sasa.
Naendelea kufuatilia tukio hili, nitakufikishia taarifa yote muda wowote kuanzia sasa pamoja na picha zaidi.

Fire

Mabibo
IMG-20150316-WA0007
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com



WAHAMIAJI HARAMU 64 RAIA WA ETHIOPIA WAKAMATWA MKOANI DODOMA

March 16, 2015

Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wananchi limewakamata Wahamiaji haramu 64  raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi) katika Kijiji cha KIDOKA, Kata ya KIDOKA, Tarafa ya GOIMA, Wilaya ya na CHEMBA na Mkoa wa DODOMA, mmoja kati yao alikutwa akiwa amefariki dunia aliyetambuliwa kwa jina moja la TAJIRU anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 – 30. Watu hao walikuwa wakisafirishwa kwa Lori lenye namba za usajili T.353 AYW Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na OTHMAN YUNUS MTEKATEKA, miaka 45, na Mkazi wa ILALA Jangwani  jijini Dar es Salaam akitokea Moshi - Kilimanjaro kwenda mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Mnamo tarehe 14/03/2015 saa 01:00 asubuhi katika kijiji cha KIDOKA walionekana watu wengi wasiofahamika wakiwa wamejificha katika vichaka na mashamba ya watu. 
Watu hao walionekana dhaifu, walikuwa wakila mahindi mabichi na wengine wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa chakula na maji ya kunywa kwa ishara,  kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kiingereza wala Kiswahili. 

Kamanda MISIME amefafanua zaidi kwa kusema wanakijiji walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na Jeshi la Polisi, ndipo msako wa kuwakamata ulifanyika na kufanikia kuwakamata watu hao waliotambuliwa kuwa ni raia wa nchi ya ETHIOPIA ambao hawakuwa na vibali vya kuingia/kusafiria. Aidha katika msako huo alikamatwa dereva wa gari hilo aitwaye OTHMAN YUNUS MTEKATEKA, 45yrs na mkazi wa Ilala Jangwani jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa yeye ndiye aliyekuwa anawasafirisha watu hao akiwa na wenzake wanne ambao walitoweka baada ya gari kuharibika. 

Na kwamba aliwapakia watu hao  tangu tarehe 12/03/2015 huko Moshi – Kilimanjaro kuwapeleka Mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya. Baada ya gari kuharibika tarehe 14/03/2015 saa 07:00 usiku katika Kijiji cha Kidoka waliwashusha na kuwapeleka porini kuwaficha kisha kuendelea kutengeneza gari na iliposhindikana waliwatelekeza porini na gari kulitelekeza kijijini.

Kamanda MISIME amewataja wahamiaji haramu hao 63 waliokamatwa kuwa ni:-

1.            FIWADO S/O ERIBALO,

2.            GANOLO S/O ABABA, 15YRS

3.            ABIRIHAM S/ RILE 27YRS

4.            DANIEL S/O AVERA, 25YRS

5.            ARABA S/O LOBE, 18YRS

6.            MEKSO S/O GETACHA, 20YRS

7.            MAMIRIS S/O DANXE, 20YRS

8.            GETACHAM  S/O HAFEBO, 25YRS

9.            MIRATU S/O ABINU, 21YRS

10.         SABSIBE YOHANAS, 18YRS

11.         ABIRIHAMU S/O HADARO, 25YRS

12.         ENDURE S/ SASIE, 18YRS

13.         KABABE S/O WORIW, 22YRS

14.         DANIEL S/O ABARE, 22YRS

15.         ADISE TRAGO, 26YRS

16.         GIRIMA S/O YOHANAS, 19YRS

17.         XILAHUN S/O ABEBE, 18YRS

18.         ESHETU S/O ABEBE, 18YRS

19.         ABEYINE S/O ERTIRO, 26YRS

20.         ENDIRAS S/O MAKANGO

21.         ABABE S/O ACHISO, 30YRS

22.         MISIGUNE S/O DALIKASO, 21YRS

23.         AYANO S/O MALASE, 30YRS

24.         DABADE MISHAMO 30YRS

25.         ERIMIAS S/O ABEBO @ MASORE, 18YRS

26.         ABIRIHAMU S/O ERISIMO, 20YRS

27.         BIRANU S/O ABASE, 25YRS

28.         EYASU S/O BEYENE, 26YRS

29.         KAZALA S/O QADIVE, 2OYRS

30.         ZAKADA S/O GIRIMA, 18YRS

31.         TSAGAYE S/O DESTA, 25YRS

32.         DAGINT S/O URIGO, 34YRS

33.         DAGAZA S/O MOLA, 25YRS

34.         MONAKU S/O ALUMU, 20YRS

35.         ALAMAYU S/O KIZIE, 26YRS

36.         BALAYME S/O WOLDE, 25YRS

37.         ZALALAMU S/O ZAWIDE, 18YRS

38.         FALAKA S/O ELKUCHE, 15YRS

39.         ANA S/O ERSIDO, 27YRS

40.         MALASA S/O TADASA, 22YRS

41.         ASHANAZI S/O MULUNA, 20YRS

42.         ASHANAZI S/O DESTA, 27YRS

43.         SALAMU S/O AYALA, 25YRS

44.         ARABA S/O LUBE, 28YRS

45.         DANIEL S/O TADASA, 22YRS

46.         MANI S/O SALAMU, 24YRS

47.         FANTU S/O LAILA, 28YRS

48.         MANAMU S/O NURYE, 23YRS

49.         NASIRU S/O ANULO, 24YRS

50.         DALALANG S/O ABRA, 20YRS

51.         DELELAG S/O FEKADU, 23YRS

52.         AHMAD S/O ELUSABO, 25YRS

53.         FEKADU S/O ERBALO, 25YRS

54.         GANURO S/O ABEBE, 25YRS

55.         WORKAZAM S/O TIRZE, 28YRS

56.         DANIEL S/O DETEBO, 22YRS

57.         CHARNAT S/O ABEBA, 22YRS

58.         TASHALA S/O BAYENE, 20YRS

59.         ASAUZU S/O DAGAZA, 27YRS

60.         SELAMU S/O WORKUNA, 2OYRS

61.         MEGISO S/O GETACHAU, 2OYRS

62.         TSAUGAYE S/O DETAMO, 15YRS

63.         FANTU S/O TASO, 22YRS.


Uchunguzi zaidi unaendelea ili kuwabaini wahusika wa mtandao huu wa usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha Kamanda MISIME anawashukuru wananchi wakazi wa kijiji cha Kidoka kwa ushirikiano waliouonyesha. Aidha ametoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kufichua wahalifu wanaofanya biashara haramu ya usafirishaji haramu wa Binadamu na madereva wasiwe na tamaa mbaya kufanya usafirishaji haramu wa binadamu.



Sehemu ya Wahamiaji haramu 64  raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi)