RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA

RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA

January 02, 2018
L (1) L (5)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa wafiwa alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 2, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki jana.
L (6)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 2, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki jana.
L (7)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli    akimfariji  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola  kwenye msiba wa  mkewe MarehemuKamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Gerezani Railyways Club jijinio Dar es salaam leo January 2, 2018
L (10)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  wanafamilia alipofika Gerezani Railways Club jijini Dar es salaam leo January 2, 2018  kwenye msiba wa Marehemu Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyekuwa mke wa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola aliyefariki jana.
PICHA NA IKULU

RAIS KARIA ASEMA ATAKAYEBAINIKA KUFANYA VITENDO VICHAFU LIGI DARAJA LA KWANZA HATAFUMBIWA MACHO ,TAKUKURU WASHIRIKISHWA

January 02, 2018
Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia amesema yeyote atakayebainika kufanya vitendo visivyo vya kiungwana kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza inayoendelea TFF haitasita kuwachukulia hatua.
Rais Karia alisema yapo malalamiko ambayo yanafanyiwa kazi yanayohusu michezo iliyohusisha Dodoma Fc vs Alliance na Biashara Mara vs Pamba ya Mwanza ambapo utaratibu utafuatwa na yeyote atakayebainika hatua dhidi yake zitachukuliwa.
Ameongeza kuwa tayari amemuagiza Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred kukutana na kamati ya Waamuzi ambao ndio wenye jukumu la masuala yote yanayohusu waamuzi ili kuangalia kama Waamuzi wanaotumika wana uwezo wa kuchezesha kwa kiasi gani.
Aidha Rais Karia amesema TFF inashirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) ili kudhibiti vitendo visivyo vya kiungwana na Taasisi hiyo itapatiwa ratiba ya mechi zote ili iweze kufuatilia kwa ukaribu.
Vilevile amesema TFF na Bodi ya Ligi wanashirikiana kwa karibu kuhakikisha anayeshinda ashinde kihalali kwa uwezo akitolea mfano namna mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa namna yanavyochezeshwa kwa haki na kuleta mvuto.
Amesema ni wakati wa kushirikiana kwa kila mmoja ili mpira uchezwe na kuondoa malalamiko ya kila wakati.

TANZANIA WENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA FIFA,INFANTINO KUONGOZA VIONGOZI FIFA,CAF.

January 02, 2018

Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Tanzania inataraji kuwa wenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa.
Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad Ahmad,Makamu wa Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa FIFA na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018
Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake
Nchi zitakazoshiriki ni Bahrain,Palestina,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE),Algeria,Burundi,Africa ya Kati,Ivory Coast,Mali,Morocco,Niger,Tunisia,Bermuda,Monserrat,St,Lucia,Us Virgin,Maldives,Congo na wenyeji Tanzania.
Akizungumzia Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia alisema TFF inajivunia kupata uwenyeji huo mkubwa wa mkutano wa FIFA na hiyo inachangiwa na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali ambayo yamezaa matunda.
Rais Karia ameongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa Serikali kupitia Wizara zake kuweza kutumia fursa hiyo ambayo inaweza kusaidia katika upande wa Uchumi.

DK. KIGWANGALLA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP KUANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UJANGILI WA TEMBO KATIKA HIFADHI YA RUAHA

January 02, 2018
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
.....................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.

Dk. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari 2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana  na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

ANZA MWAKA MPYA WA 2018 NA MALENGO HAYA

January 02, 2018

Na Jumia Travel Tanzania


Baada ya pilikapilika za msimu wa sikukuu na sherehe za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, huu ni muda muafaka kwako wa kujiwekea malengo mapya.

Malengo hutofautiana kulingana na kitu gani unataka kukifanikisha ndani ya kipindi cha muda fulani. Kwa mfano, kuacha kula aina ya vyakula fulani au vinywaji kutokana na kuvitumia kipindi cha sikukuu; kubana matumizi ili kukusanya kiasi fulani cha pesa; au kufanya mazoezi ya kutosha ili kurudia ile hali yako ya zamani kabla ya sikukuu, nakadhalika.


Kukurahisishia baadhi ya malengo ambayo unaweza kujiwekea mwanzo huu wa mwaka, Jumia Travel imemekukusanyia malengo yafuatayo machache ambayo yanaweza kukufaa endapo utayazingatia.

Punguza muda wa kuangalia luninga, soma zaidi vitabu. Kuna faida nyingi za kusoma vitabu kuliko watu wanavyofikiria kama vile kuongeza maarifa juu ya masuala mbalimbali, kupata ujuzi pamoja na kuburudisha. Kwa mujibu wa wataalamu kusoma vitabu huimarisha afya ya akili yako pamoja na kukuongezea namna ya kuwasiliana na kuwaelewa watu. Hivyo basi, kama ulikuwa unatumia muda mwingi zaidi kutazama luninga basi jaribu kuutumia pia kwa kusoma vitabu.

Lala mapema. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha hatari ya kupata magonjwa kama vile kisukari, ugonjwa wa moyo, utapiamlo na msongo wa mawazo. Mwaka huu mpya jaribu kujiwekea utaratibu wa kulala mapema, weka kengele ya kukumbusha na hakikisha unaizingitia ili angalau ulale masaa 7 au 8.


Jaribu kuwa mbali na simu yako. Nadhani unaweza kuwa umeona mara kadhaa namna simu ya mkononi inavyowafanya watu kutokuwa makini au kuutoa muda wao kikamilifu katika baadhi ya shuguli. Unaweza kukuta kwenye kusanyiko la familia au kikao na mtu muhimu lakini simu inakuwa chanzo cha kuondoa umakini. Jaribu kulidhibiti hilo kwa kuizima kila unapokutana na watu muhimu au tukio kwa kipindi cha muda fulani au hata siku nzima pia kama ikiwezekana.


Weka akiba. Hakuna jambo ambalo lina changamoto kama kujiwekea akiba ya fedha. Wengi wetu hatujui namna ya kudhibiti matumizi ya pesa tunazozipata. Tunajikuta tunaweka hifadhi ya pesa baada ya matumizi kitu ambacho sio sahihi. Inashauriwa kwamba weka akiba ya fedha kwanza ndipo utumie kiasi kilichobakia. Na hakikisha unajitahidi kutumia kiasi ambacho umekwishajiwekea bajeti ili usiitumie akiba uliyojiwekea.


Punguza muda unaoutumia mitandaoni. Ni vizuri kutumia muda mtandaoni kwani unakupatia fursa ya kupata taarifa, maarifa pamoja na kujuana na watu tofauti. Lakini kutumia muda mwingi huko kunaweza kuwa na madhara kwako bila ya kutarajia. Wataalamu wamegundua kwamba kutumia muda mwingi mitandaoni kunaweza kuathiri afya ya akili yako, wanadai kwamba kunaweza kupelekea mtu kutojiamini kutokana na yale yanayoendelea mitandaoni.

Punguza madeni. Mwaka huu ufanye usiwe na madeni mengi yasiyo na tija ambayo hunyonya fedha zako na kukufanya kutotimiza malengo yako. Hakikisha kwamba unamaliza kulipa madeni uliyonayo ili uwe huru kifedha. Haukatazwi kukopa na ni jambo la busara wakati mwingine kwani hukuwezesha kufanikisha jambo ambalo hauna uwezo nalo kwa wakati uliopo. Lakini hakikisha unakopa kwa ajili ya jambo la maendeleo na siyo starehe.


Tumia muda zaidi na familia yako. Inawezekana mwaka ulioisha haukupata muda wa kutosha wa kutumia pamoja na familia yako badala yake ulikuwa umetingwa na kazi au marafiki. Wengi wetu huwa tunagundua ni jambo jema kutumia muda na familia hususani kwenye kipindi cha sikukuu. Unaweza kulibadili hilo kwa kujiwekea malengo mapema. Unaweza kupanga labda kila baada ya mwezi mmoja, miezi mitatu au minne.

Tabasamu, kutana na watu zaidi! Kuwa na furaha ni chaguo lako. Changamoto kwenye maisha lazima zitakuwepo, lakini ni chaguo lako aidha kuziruhusu zikuathiri au la. Jumia Travel inaamini kwamba mwaka huu mpya ufanye uwe wa pekee kwa kubadili mtazamo juu ya maisha yako, kutana zaidi na watu, badilishana mawazo, huwezi kufahamu kwani kwa kuzungumza zaidi na watu kunaweza kukufungulia milango ya fursa kwenye maisha yako!


Heri ya mwaka mpya 2018 na uwe wenye mafanikio tele kwako!

MAMIA WAMZIKA MKE WA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI MKOANI TANGA

January 02, 2018
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwa nyumbani kwa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi mkoani Tanga,Burhan Yakub ambaye alifiwa na mkewe wakati wa mazishi ambayo yamefanyika leo Makaburi ya Magomeni Jijini Tanga
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mke wa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga wakilipeleka makaburini tayari kwa ajili ya maziko
 Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani eneo la Magomeni Jijini Tanga
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakiwa msibani leo katikati mwenye tisheti ya mistari ni Mwandishi Mwandamizi wa ITV na Radio One mkoani Tanga,William Mngazija kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga,Hassan Hashim
 Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Burhan Yakub kushoto ambaye amefiwa na mkewe akiwa na ndugu jamaa wakati wa msiba huo nyumbani kwake eneo la magomeni Jijini Tanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akiingia kwenye eneo la Msiba leo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiwa eneo la msibani Magomeni Jijini Tanga kulia ni Katibu Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Tanga,Lupasio Kapange

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akisalimiana na wananchi waliokuwepo msibani mara baada ya kuwasili
Wananchi wakifukia mwili wa aliyekuwa mke wa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoani Tanga,Burhan Yakub
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi wakati wa mazishi hayo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga,Hassan Hashimn akiteta jambo na wandishi wa habari mkoani Tanga wakati wa msiba huo

POLEPOLE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUMUAGA MWANAHABARI JUSTINE LIMONGA

January 02, 2018
 Waombolezaji na wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari wa Uhuru FM, Justine Limonga, wakati ukiwasili Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa kabla ya kufanyika mazishi yake Makaburi ya Saku yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
 Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mwanahabari, Justine Limonga.
 Waombolezaji wakisubiri kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu kwenda eneo maalumu ilipo kufanyika ibada hiyo.
 Familia ya marehemu ikiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, ikitoa burudani.
 Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda, akitoa mahubiri.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Ibada ikiendelea
 Mwanamuziki Nguri, John Kitime akizungumzia jinsi alivyomfahamu marehemu Limonga.
 Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Mwani Nyangasa, akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas, akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Mbunge wa zamani wa Temeke, Abbas Mtemvu akimzungumzia marehemu Limonga.
 Mbunge wa Mbagala,  Issa Mangungu, akizungumza.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akizungumza katika ibada hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali, akiwapa pole wafiwa.


Mwanamuziki nguri, Hussein Jumbe, akiimba wimbo maalumu aliomtungia mwanahabari Justine Limonga.

Dotto Mwaibale na Kulwa Mwaibale

Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ameongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanahabari, Justine Limonga iliyofanyika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akizungumza katika ibada hiyo, Polepole alisema CCM na tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa bado akitegemewa.

"Tumempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akitegemewa kama chama tutaangalia namna ya kuisaidia familia yake," alisema Polepole.

Mkurugenzi wa Nduvini Auto Garage, Alhaji Ahmed Msangi alizungumza jinsi alivyomfahamu marehemu ambapo aliahidi kampuni yake kwa kipindi hiki cha kufunguliwa kwa shule itawanunulia vifaa vya shule, sare na kuwalipia karo wakati wakisubiri kukaa na familia kuona namna ya kuwazesha watoto hao kielimu.

Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali alisema kifo cha mwanahabari huyo aliyekuwa mwajiriwa wao kimeacha pengo kubwa ambalo halitazibika.

Alisema Limonga alikuwa mhariri na mbunifu na aliweza kuongoza vipindi mbalimbali ambavyo vilipendwa na wasikilizaji wa Uhuru FM ambapo aliahidi stahiki zote za marehemu kama mwajiriwa zitapatikana kwa wakati.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, siasa wanamuziki na wanahabari na wananchi iligubikwa na majonzi na baadhi ya watu kushindwa kujizuia kulia.

Akitoa mahubiri kwenye ibada hiyo Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda alisema mwenzetu Limonga amemaliza kazi ya hapa duniani je sisi tuliobakia tumejiandaeje?

Mbunda alisema kila mtu anapaswa kujitafakari maisha yake ya kiroho kabla ya kifo na hivyo ndivyo Mungu wetu anavyohitaji.

Limonga alifariki dunia Desemba 30, mwaka jana katika Hospitali ya TMJ alikolazwa akitibiwa na ameacha mjane na watoto wawili ambapo mazishi yake yamefanyika leo katika Makaburi ya Saku yaliyopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

DK. MNDOLWA AKABIDHIWA RASMI OFISI LEO, AAHIDI KUUNDA KAMATI KUTAFUTA UFUMBUZI DHIDI YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI KATIKA JAMII YA KITANZANIA

January 02, 2018

 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Seif Shabani Mohamed alipowasili Makamo Makuu ya Jumuiya hiyo kwa ajili ya makabidhiano hayo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa  akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Najma Giga wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Mndolwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Makamu Menyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar. 
 Bulembo akiendelea kukabidhi nyaraka
 Dk. Mndolwa na Bulembo wakisaini nyaraka za makabidhiano
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania  Zanzibar  Abdallah Haj Haidar na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed wakisaini nyaraka upande wa mashahidi
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi
 Dk Mndolwa na Bulembo wakifurahia jambo baada ya makabidhiano ya ofisi
Watumishi wa Jumuiya ya Wazazi Makao Makuu wakiwa kazini wakati wa makabidhiano hayo ya ofisi baina ya Dk Mndolwa na Bulembo PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

HABARI KAMILI
Na Bashir Nkoromo
Mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda Kamati ya  kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi tatizo la kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.

Dk. Mndolwa ametoa ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.

"Katika hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa. Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika kulifanyika kazi.

Kwa hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk Mndoldwa.

Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya kuwa ombaomba.

"Jumuiya hii ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.

Akimzungumzia Bulembo, Dk Mndolwa amesema, alikuwa kiongozi bora ambaye ameisaidia kwa kiasi kikubwa Jumuiya ya Wazazi, na kwamba katika jitihada zake ameiboresha Jumuia hiyo kwa karibu asilimia tisini.

"Nimejifunza mambo mengi kwa Bulembo, mojawapo ni uvumilivu, huyu ni mvumilivu kiasi kwamba itanibidi kuiga uvumilivu wake ili na mimi nistaafu kwenye Jumuiya hii nikiwa safi kama yeye," Alisema Dk. Mndolwa.

Kwa Upande wake Bulembo aliwataka viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kuthamini sana Waaandishi wa habari kwa kuwapa ushirikiano kila unapohitajika na kwamba yupo tayari kutoa ushauri pale utakapohitaji.

Aliwaasa viongozi wapya kuendeleza mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita huku wakiachana na mabaya yaliyofanyika wakati huo.

"Namna nzuri ya kuongoza ni kuwa karibu na unaowaongoza, msikae nao mbali mnaowaongoza na ikiwa kutakuwa na jambo miongozi mwenu viongozi ambalo haliendendi vizuri utatuzi wake uwe kwenye vikao si kwingineko", Alisema Bulembo.